Mvumbo
JF-Expert Member
- Aug 20, 2015
- 3,489
- 12,137
- Thread starter
- #561
Hawataki u starehe, na usipate kushiba/yo yo yoh
yote nayopitia ni kwasababu sina noti
maadui wamekua wengi kuliko machizi boti
mi husubiri tajiri ale ndipo nikombe sahani
Fid alisema bila hela hupati rafiki maishani
na ghetto sina taa mwezi ndo hunipa nuru
najilinda nisilale njaa kwa uji wa sukari guru
wadeni wangu wameniziba mdomo ili nisiwadai
watesi wangu wameziba promo nionekane sifai
Ila haina noma! haina homa! sikia
nipeni nafasi niendelee kupaza kwenye microphone
mistari yangu ni ya kipekee Ka mtende jangwani
Kisa ni Wakipekee, kama samaki asie na mwiba/
Maisha yasikunyookee, kila pande wanaziba/
Ili wakae waongee, siku wakisikia umeiba/
Iwe cheko/ zisake hata wakuone mental/ usishike beto/ kabebe hata pareto/ heshima ni kesho/ na wewe ni special/
Zisake kama una marejesho/ ipo siku itakuwa mpeto/ watashikwa na mchecheto/ wakikuona kina Mobetto/ na kukusaka mpaka geto/
Acha leo Wakipekee, waonyeshe kukuchukia/
Ila wajue paka mzee, hawezi kupotea njia/