Wake up skiza hizi fasihi, stanza za digrii mtaani nabii/
Kutoka chugga chalii, mwenye upendo utii na bidii/
Kipenzi wa mama, mamama jua limezama/
Muda hausimami ulishavuka ujana, yote umemalizana/
Busara ka za jo na anna, saint asiye na laana/
Move on tafuta na bwana, nishamove on nakula ujana/
Naijua leo sikumbuki jana, nkiwaza kesho sioni maana/
Zaidi michezo ya kut*ana, kichwa changu kigumu/
Kama pusha marijuana, sijawahi kuacha ndumu/
Cha mapinduzi kidumu, chama nilijua utakwama/
Penzi limekua sumu, mipasho skendo na drama/
Naspit ukweli humu, humu kugumu/
Kama dent mwenye room, aliyekosa boom/
Hana uhakika wa milo, max ana uhakika wa zero/
Kimajukumu nipo active, mood inafanya niwe selective/
Selective na story za uongo, nani kampenda nani/
Wakikutana hawaendani, usiamuamini mbongo/
Vita zishapigana kumjua muongo, Hakuna aliyeshinda/
Mtaani wanauza mirinda, humu wanaiponda coca/
Nimeshachoka naropoka, walio unique wapeni maua/
Mnawajua wavimbe bichwa, komwe litawaumbua/
Askari kijana smart niliyepitia depo, nipo kama sipo/
Nipo poa cool and good, Arusha is my hood/
Usiniulize kuhusu dar-lini, niulize nitamiliki car-lini/
Learn the difference, mtoto wa mjini swagga za kijanja/
Mjanja najua mshamba, hachekwi akiomba namba/
Flow classic and intelligent, kichwani nna vyombo/
Konyagi sio sahani na mabakuli, k vant mlevi nguli/
Nalewa napiga na puli, sijaona yoyote mzuri/
Mzuri kama miss, eyes haziwezi niongopea/
Internet never forget misy, jf pm mipicha ya kushea/
Tunza hiyo kitu mamy, K Ina thamani haina spea/
Mitandao imejaa umbea, fundi wa kupandisha stimu/
Mtundu kungwi na tena mwalimu, hanna tu posho/
Fundi midondoko 40bars michosho, fundi sishikiki/
Fundi sio wa pikipiki, mapikipiki yamaha au mahonda/
Najua kupenda najua kusifia, najua na kuponda/
Nipo real sio fake, P funk majani kwenye mdundo/
ashasadiki hiki kipaji mantiki mpangilio na muundoo