Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

Kama Muhadzabe, swala nawapa kipondo/

Wanauliza umepigaje, Misso wa Missondo/

Kwa rhymes za kibabe, sibaki nyuma kama kondo/

Ma Rapa wa mazabe, nawaangusha kama kimondo/

Tungo hapa ni nyingi/ wametema bungo hadi madingi/ Mvumbo mlinda misingi/ kutegemea ungo ni upimbi/

Amani kwa wafuasi wanaowakilisha Hip Hop Logo/

Mziki wenye chakula cha nafsi usiopendwa na madogo/

Wanaotaka za kudansi huku wamepaka mkorogo/

Wakinisikia wana wasi wasi kama wapo choo cha magogo/
 
Haonekani kila mahali, nyumbani mpaka kwenye kazi/

Baba mama maswali, mpaka marafiki uswazi/

Rabda kapata ajali, au kauwawa na majambazi/

Kumbe anapakwa asali, na kupikiwa wali nazi/

20231129_000354.jpg
 
Alishashikwa kwenye msako, wa dili za kiharamia/

Daima akichukua chako, namba atakubadilishia/

Hakuwa na Upako, wala elimu ya Biblia/

Ila akaona hapo, ndio pa kukimbilia/

Yaani bila noma, akavamia kwenye Dini/

Akajenga boma, na akapata waumini/

Akaenda kwa Sangoma, akapewa pete za majini/

Akikugusa ona, lazima utaanguka chini/

Akaaminika, na wengi kondoo/

Akasifika, kuwa Nabii ni soo/

Pesa akashika, akawa ndio jogoo/

Na jioni ikifika, mwana anapoza koo/
JamiiForums-772586512.jpg
 
Aliaminika na Taasisi, ya Dini afundishe Madrasa/

Za Mtume Hadithi, na kuiepuka anasa/

Mshahara tukampa sisi, kila mwezi tulijipapasa/

Ili iwe rahisi, watoto elimu kuipata/

Akafundisha watoto, pamoja na wadada/

Wasiingie kwenye moto, wafate Ibada/

Kumbe aliomba joto, na akapewa msaada/

Leo ni changamoto, amekimbilia Kibada/

Hakufata ya Kitabu, ona amejishusha ngazi/

Vya kwenye nikabu, kataka kuviona wazi/

Alifundisha ustaarabu, ambao hakuufanyia kazi/

Kabla ya Allah hisabu, atubu na kumuomba radhi/
20231128_213741.jpg
 
Mjini mnajisahau, kisa mna visenti vya ofa/

Mnajiona mmependa dau, mkimiliki Tv na sofa/

Tukiwafata hamna angalau, mnatuona malofa/

Vipi unidharau, wakati kijijini namiliki ghorofa/
20231129_000411.jpg
 
Sisi ndio wale tuliopitia shida na majanga/ nyota wakaiba kwa waganga/ wakatupa miba na kusema karanga/ riziki wakaziba kwa manyanga/

Niamini tumepitia magumu/ tuliowaamini walitupa sumu/ hata nifanye nini walilaumu/ ila dakika ya tisini shida hazikudumu/

Sasa hivi wanapiga magoti kama sio/ baada ya ya kuona noti hazina mbio/ wanadai sapoti hawa vihio/ nawaongoza ka remote wananisikiliza ka' redio/

Ukiniona nasafisha koo ujue sitaki ushauri/ acha nitumie doo nilikotoka sio kuzuri/ ajabu wanaomba poo walioniombea kaburi/
Ungana nami kwenye show, au kapige tunguri/

Ukinifata fata nilipo, chukua tahadhari/

Maana "na hapa ipo", kama Dotto Magari/
 
Happy New year Kwa ma-snitch na majembe
Niko nimepoa beach na juisi ya maembe
Kuna Wana hapa JF Wana akili za Milembe
Wengine n mashoga na mashati ya vitenge
Ndo maana unakuta dume lina post za vijembe
Sishangai mamba kwenye msafara kuona kenge/

Ni mwaka wa tatu sasa tangu alipokufa Magu
Wamekuja wenye gubu sasa wanatupa tabu
Mwakani ni uchaguzi najua watacheza rafu
Mshindi ni yuleyule hawezi kipewa CUF/

Happy New year 2024 [emoji91]
 
Happy New year Kwa ma-snitch na majembe
Niko nimepoa beach na juisi ya maembe
Kuna Wana hapa JF Wana akili za Milembe
Wengine n mashoga na mashati ya vitenge
Ndo maana unakuta dume lina post za vijembe
Sishangai mamba kwenye msafara kuona kenge/

Ni mwaka wa tatu sasa tangu alipokufa Magu
Wamekuja wenye gubu sasa wanatupa tabu
Mwakani ni uchaguzi najua watacheza rafu
Mshindi ni yuleyule hawezi kipew CUF/

Happy New year 2024 [emoji91]
Red black happy new year 🎉
 
Zile hips na haga, kidume nilifika/

Nikahisi nikimpataga, chaga zitavunjika/

Sio hadithi hii zaga, ni wazi imekamilika/

Miss Lady kama Gaga, alivyo umbika/

Nikazama Dm Insta, nikamueleza matatizo yangu/

Kunikubali hakusita, akataka location chimbo langu/

Muda ulipofika, akataka nauli nimtumie/

Nikatuma nusu saa ilipopita, ikabidi anipigie/
1697610849-picsay.jpg
 
Tushapitia matendo, ya umaskini wa kutupwa/

Tukatengwa na warembo, kama buti la kuchumpa/

Siku hizi tunachinja tu tembo, sio bata life ni supa/

Wanafki wamesahau matendo, nembo wanazitupa/

Naonanyesha umahiri, kwa vina vya kimalenga/

Ukikosa akili, unaweza sema nimekulenga/

Wanashindwa kuhimili, Rap si maigizo ya Senga/

Mvumbo ni Muhimili, haina kuvishana vilemba/

Wengi ni nabii Titto, ndio maana wanashindwa kunifesi/

Kwenye Game hawana wito, hivyo hii ni kesi/

Kitambo kama Bito, na nazidi kuonekana mtesi/

Tatizo naandika vitu vizito, kwa watu wepesi/

Namwaga upupu nipo kazini, madogo nawakanda/

Watupu na wanajiamini, kama dem mwenye msambwanda/
 
Mwaka huu ni wangu kuwapa mistari kwenzi

Utazani nimetoa ndagu nilivo tajiri wa tenzi

Toka Dar hadi Marangu Ka makonda na uenezi

Ni zaidi ya mtoto wa Dandu ntapokufa mnienzi

Niite Langa au Messi, Manju nisiye na mfano

Jiite PAC au BIG Ila huniwezi Kwa michano

Nakubalika kitaa kama hayati John Pombe

Nyota yangu inang'aa kama Yanga na makombe

Mi ndo mkali wa jukwaa Wana acheni mazonge

Ntawafundisha Sanaa sio kilimo cha mkonge

Mi ndo bingwa freestyle hakuna wa kunisogelea

Ukibishana na Mimi hukawii kupotea
 
ACHIA JALA Rmx

Begi limejaa manoti/ nimekuona nyingine zipo kwenye koti/ nyumbani unasubiriwa na marost/ na una Ghorofa kama Joti/ So Achia jala/

Siwezi kuku handle kama shost/ kwa sasa mimi ndio remote/ achia noti/ acha ubishi nitakuvunja goti/ empty siondoki/ maana natembelea choki/ so usilete ufala/

Nina fikra kama paka mwenye njaa/

Nilipotoka mashaka yamenipa ushujaa/

Ndio maana nipo hapa kuzisaka chapaa/

Sijali ulipozipata ila hizi ni zangu jamaa/

Nishazisaka kwenye mgodi/ mikosi ikapiga hodi/ biashara nikashindwa Kodi/ mzigo sikuweza ku afford/ nikaomba sana God/ leo pesa unaichezea road/ ACHIA JALA

Hizi pesa unakwenda kuchezea/

Maisha yamesha kunyookea/

Mimi nataka kufuta fedhea/

Hivyo achia jala fala utapotea/

Kisu na hii Baretta ndio mtaji uliobaki/

So ukileta za kuleta nitakupeleka mbele ya haki/
 
AChia jala 2

Majibu;

Unajisifu una gundu na bado unafanya ukora/ unanifuata macho mekundu ili kunipora/

Piga risasi usoni mwangu na sikuitii ving'ora/ nishayachoka maisha yangu hivyo kupumzika ni bora/

Unapagawa na hizi noti unadhani ninastarehe/

Huliwezi hili koti hata nikisema ulipokee/

Wewe una marafiki/ wanaokujali/ una amani moyoni/

Mimi wote masnitch/ kisa hizi mali, nawindwa mpaka ndotoni/

Kisa mkuu wa Idara/ hiki cheo nimetoa ndugu kafara/ mke sitakiwi kumlala/ shetani tushafunga ndoa ya mitaala/

Kariakoo nina biashara, Temeke Kino na Ilala, ukiona msafara/ wangu kwenye barabara/ unaweza ukajiona fala/

Ila hizi pesa kwangu ni chungu zaidi ya shubiri/ sisaidii walio wangu hata dawa wakisubiri/ alikufa baba yangu kwa kukosa tiba Muhimbili, masharti kwangu napaswa kuyakabili/

Ili niishi/ vipi unapata ushawishi/ unazitaka kwa ubishi/ na kukomaa kama Shishi?/ Ukichukua hazikubakishi/ hivyo tuliza dishi/

Haya ma Range na majumba/ yasifanye u change mwanayumba/ omba Mwenyezi akupe Vumba/ halali ule enzi na sio kubumba/

Nayatamani maisha yako/ unayatamani yangu kisa vitita/

Sio kila aliye mbele yako/ anafurahi kukupita/
 
Noma. Hii ina audio yake?
 
Back
Top Bottom