Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

Mvumbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
3,489
Reaction score
12,137
Kwanza nawapa salamu, nazingatia itifaki/
Nadhani Mvumbo mnamfahamu, kwenye mistari mimi ndiye chaki/
Naandika zaidi ya kalamu, mwana Hip hop kindaki ndaki/
Ma mc's wa Jamii Forums, karibuni nyuma msibaki/
Leo mitandaoni ukisema usome, habari zimejaa ukakasi/
Huku Kiba anasema UNIKOME, huku Idriss akaripoti Polisi/
Huku Kigwa kavunja ngome, Le M'bebez kapiga pasi/
Haya yasikufanye ulale ukorome, pambana watoto wasile nyasi.
 
Dah napenda sana Hip Hop flow ni kali homie [emoji91]mm ni mshabiki tu mzee siunajua kunadika tu hiyo mistari ni talanta wengine tumeumbwa kushabikia tu. [emoji22]
Hapo mkuu nimekupata, ni kweli Hip Hop iko poa/
Japo Marapa wanashuka fasta, kama chupi ya changudoa/
Misingi hawataki kuifuata, wanaishia kujipodoa/
Tayari Mvumbo nipo hapa, mistari nakohoa/
 
Kwanza nawapa salamu, nazingatia itifaki/
Nadhani Mvumbo mnamfahamu, kwenye mistari mimi ndiye chaki/
Naandika zaidi ya kalamu, mwana Hip hop kindaki ndaki/
Ma mc's wa Jamii Forum, karibuni nyuma msibaki/
Leo mitandaoni ukisema usome, habari zimejaa ukakasi/
Huku Kiba anasema UNIKOME, huku Idriss akaripoti Polisi/
Huku Kigwa kavunja ngome, Le M'bebez kapiga pasi/
Haya yasikufanye ulale ukorome, pambana watoto wasile nyasi.
oiii mwana nimeingia, wito wako kuusikia
salam napkea na gwala nakugea,
naona verse yako1 wabana pua wamekimbia,
Rusha mawe hewani, weka bitini ukumbini
uone wanyama wanavyo inuka toka chini.
Piga chini Chibu kiba wakala wa shetani, wadau wa vilingeni,
kutwa kutumia majini, ili waendelee kutamba mjini
NGoja nkumegee jambo nafanya hapa, boya hawezi elewa lazima atoke kapa,
niko nyuma ya keyboard napiga na kugonga code,
Dunia ina code utataka zipigie HODI
 
Ngumu kumeza si zamoto, ila laini wang mamito/

Karibu jamvini bebito, nikupe kiss za upendo/

Leo hata zaidi ya kesho, hata family iwe special/

Asante wang financial, kwa penzi lako zito/

Services balaa zako, kitandani feni UNO/

Mashallah we mtoto, pia huna mfano/

Nitakupenda kaa kichaa, ila langu we tulizo/
Ngumu kumezaa
 
Akhsante mwana kwa kuja, nathamini wako uwezo/
Ni kweli Hip Hop haiwezi chuja, sio hao wavaa milegezo/
Ona siri zimevuja, kwamba wanafanyiana michezo/
Waambie waendelee kuzuga, ila tukitimba ni maombolezo/
 
Hii sio mada/ ya siasa au anasa/ ili watoto wachangie/
huwezi ona makada/ warembo wa kisasa/ wanataka za "njoo ubambie"/
Hakuna ada/ ila vipi wajaze kurasa/ lazima wakimbie/
Juu kama KISHADA/ Mvumbo nawanyanyasa/ ni vipi niwahurumie/
Nachoma dawa/ nakohoa nipo sawa/ wanapagawa wanaandika mashudu/
Hawana power/ nawanawa hawa chawa/ nawachinja kibudu/
 
Ngumu kumeza si zamoto, ila laini wang mamito/

Karibu jamvini bebito, nikupe kiss za upendo/

Leo hata zaidi ya kesho, hata family iwe special/

Asante wang financial, kwa penzi lako zito/

Services balaa zako, kitandani feni UNO/

Mashallah we mtoto, pia huna mfano/

Nitakupenda kaa kichaa, ila langu we tulizo/
Babe wangu huyoo, uko vizuri kila sekta nitaki nini tena, nnachotaka napata!

I love you babe kichwaaa[emoji3] [emoji3]
 
Flow za kitoto bado magasho wamechochora/
Ma mc tunakuchora na izo style za kikora/
Tunakulock ka Jesus na u_king tunapora/
usijaribu kupima huu ni moto wa kombora

Ya gundu ndo nishatua/
Machoko wamefua/
Wanajua/
Nisipo kill napasua/
K mnato natanua/
Rinda natatua/
Ile kiganster kila kitu nakamua
 
Mistari inaririka kichwani/
Iwaingie kwenu maskioni/
Nitakayonena muyatilie maanani/
Mi ndiye wenu fanani/
Mambo yamebadilika sio kama zamani/
Sasa hivi kwenye shida hata ndugu huwaoni/
Wengine watakupita bila soni/
Watajifanya hawakuoni/
Usife moyo zidi kupambana/
Usimsahau wako maulana/
Ukipata zidisha sala sana/
Azidi kukujali zake nyingi baraka/
Shukran kutega sikio,ujaliwe heri na fanaka.
 
Natamani niwashe moto, ila goto ni sawa na kuvunja mayai/
Japo ni changamoto, mtoto unapo jimwambafai/
Umeingia lile chaka linaloogopeka/
umeingia chaka unalotamani kujiteka/
umeingia chaka ambalo una bunduki na unatetemeka/
umeingia chaka ambalo ukitoka wanakucheka/
Mvumbo atakutenda, hana tofauti na gaidi/
Rabda Mungu akikupenda, ila usiombe akupende zaidi/
 
Mistari inaririka kichwani/
Iwaingie kwenu maskioni/
Nitakayonena muyatilie maanani/
Mi ndiye wenu fanani/
Mambo yamebadilika sio kama zamani/
Sasa hivi kwenye shida hata ndugu huwaoni/
Wengine watakupita bila soni/
Watajifanya hawakuoni/
Usife moyo zidi kupambana/
Usimsahau wako maulana/
Ukipata zidisha sala sana/
Azidi kukujali zake nyingi baraka/
Shukran kutega sikio,ujaliwe heri na fanaka.
Maneno yako ya busara, hakika jamii umeipa somo/
Ukikaza utakuwa kinara, japo game ni ya Promo/
Zama tena maabara, leta vitu wafunge midomo/
Kukata tamaa ni hasara, najua hujafika kikomo/
 
Life ni kubattle/na usiogope kuishi gheto/ogopa watoto warito/ufunge ndoa na punyeto/usijeishia kula msoto/usijifanye we mnato/na usiogope changamoto/ujana maji ya moto/piga kazi isiwe majuto.
The Gt/ umeandika sahihi/ na si tuu umewasihi/ bali ni kama unabii/ wanapaswa kutii/ haswa watoto wa karne hii/ naamini ukiongeza bidii/ itakuelewa jamii/ na kufikia level hii/
 
dah mmenishinda tabia, naona mmemaliza kila kitu/
nimefungua uzi kichwakichwa, ghafla nkakutana na vitu vigumu/
ngoja nmfikishie wife nyanya, nirudi kulisukuma hili gurudumu/
Ni kweli hujasema uongo/ hizi ladha ngumu kama gongo/ watoto wanaziona sifongo/ na wakijaribu wanatema nyongo/ nikighani nawashtua ka' vumbi la Kongo/
 
Back
Top Bottom