Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

Mwana hayupo kwa ajili ya kuponda, wala mengi kueleza/
Bali hum tag Mahondaw, na kuandika INAPENDEZA/
Watakuja kukupa muongozo ndio slogan ya smart, kila post anapita hatakama ya magumashi/

Namkubali hana shobo yuko stable kama jina lake, wenye akili robo walianzisha uzi kumpaka tope/

Nawaza jibu sipati, Kama mahondaw kweli anatoka na smart basi mchizi anabahati/

Sina wivu nawatakia kila la heri, waishi kwa amani bila kuibiana penseli/

Wahuni tumezidisha ugumu, eti ndio sababu hatuna mademu/

Tunajikaza kisabuni sote tusongeshe gurudumu, ukitaka mademu wakali nenda mmu/
 
Hauna haja ya kutoka nduki, mkuu Injili ya Gheto/
Bali hakikisha hawainuki, wanao ku snitch na kufuata upepo/
wasivamie Tempo/ warudi Depo/ tukiwaona hatuna mchecheto/ kama tumemuona Mobetto/ Mvumbo sina mbeleko/ wananiogopa kama Meko/ Ukonga na Keko/ kote mpaka Soweto/

Ukonga mpaka keko, hakuna tofauti na central/

Hayo yote magereza lingine lipo kariakoo, Usiishi kimakengeza Mvumbo huko utabebeshwa ndoo/

Wezi na vibaka wakaba koo, ni washenzi ila kwa pale wanaomba poo/

Lazaro nimeamka mlidhani nimekufa, na sanda nishatupa niko kucheki uefa/
 
Eti mnajifanya mnarap hivi nyinyi mnaijua rap? / rap tunafanya sisi kina nanii japo hatupati mshiko chap chap /
Rap imekupiga kanzu, ukiforce utaonekana kavu/

Rap sio vitisho wala mipasho kuifanya yahitaji nyenzo, mabishoo acheni rap sikilizeni rege ya senzo/

Mistari yangu zaidi ya koleo inawatoa jasho, na ndio maana hutaki leo una Takakeisho/

]Nyie wote maboya kama mnabisha njooni niwatie ndani ya kapu /
Mi ni boya hunikosi katika bahari ya rap, bila mimi hufiki popote hata kama mkononi una map/

Boya niko hapa kuwanusuru fake mcees msizame, nishike vizuri nimebeba pumzi zenu msidate/

Boya nishasimama sioni wavuvi wakunikalia, hiki kina kirefu kwa mbizi mnajiongopea/

Mashua zenu mbovu zishatoboka, hamuwezi zuia matundu ya maji kwa bazoka/

Uliyeanzisha uzi wewe ni kolo kama nanii anayeamini ili ufanikiwe lazima uende shule ukasome fasihi / au nakosea kama yule nanii aliyesema historia huwa haijurudii? / hahaha nacheka kifala kama mbwa alotokwa na manii.

cheka kifala ntakutoa kafara niwe bosi, yani nakugeuza kua mleta hela ukiwa upo ndani ya box/

Shule haina maana yeyote katika maisha zaidi ya fix, maswali ya kipuuzi kukomoana eti utafute thamani ya x/

Ticha wa hesabu nakuheshimu niache wala usinifosi, usitumie ghadhabu kwenye mambo yako ya kiofisi/

Nataka vitu laini kama somo la civics, na sio huo uhaini wa kunipa hesabu za matrix/

By the way kuanzia ulipo si sawa na kubakia ulipo Nikise 'chini hapana' ina maana fanya unyanyuke / me ni mkushi zaidi yako ukichukia karibu nikupaushe.

African - Japanese

african japanese mi ni mjeda waulize Vietnamese, natisha kama alqaida naogopeka kama jinamizi/

We ni mkushi na ndio maana flow zako zimekaa ki bush, mi ndo Scars nazika marapa wabishi/

Mi ni kero kama kunguni walioko kitandani, yaani kiboko ya wahuni hadi maaskofu makanisani/

Siuliki kwa muarobaini, wala dawa yeyote ya hospitalini/
 
Unanifundisha nisnichi niwin bila ya jasho
Wakati mwenyewe umefeli na mwalimu mkuu mamaako
Kidole kwa triger, nawakili ma niga/
Nakupa pole we twiga, leo umeingia chaka la tiger/

Mwalimu mkuu mama yangu hicho ndicho nacho lingia, maana nawakimbiza machangu kwenye somo la jiografia/

Ukileta shobo nakupa dole litakalokupa faida, usiwe na akiri robo namaanisha dole gumba kwenye usajili wa nida/
 
Kwanza naipokea tano, kisha naweka mkono juu kama Mandela/
Na lile swali la kwenye mabano, nalifungua zaidi ya umbrella/
Masela hatutoki, kwa sababu kenge wameunga tela/
Na pia tayari kimaisha tupo Konki, ya nini tuuze sura ndio tupate hela/

Mi sina nyota ya umangi sa kivipi niuze sura?, hayo mambo waachie matozi wale wavaa kaptura/

Uchaguzi ndo huo jiandaeni kupiga kura, mi niko kwenye danguro nawacheki mademu wenye chura/

Habari mbaya kwa masharobaro watumia beauty camera, unaficha uhalisia wa uso wako kisa ashura?/


Kimaisha wahuni tupo konki, japo kuna masnich tayari washatoa koki, mchezo dakika tisini tusiwe na paniki/

tusijiangushe chini kutegemea huruma ya refa, tukaze buti tutashinda hata kwa dakika za nyongeza/

Japo kosi lipo pungufu lakini mpira hatuja poteza, kadi nyekundu walizopewa wachezaji wetu upande wa pili zime wa favor/
 
Mvumbo usilale utavunda utakua mvundo, mc mwenye machale nadunda ndani ya tungo/

Wanga hamniwezi maana sikuizi nalala na nyundo, jikanyageni nyie washenzi muone navyozichana hizo nyungo/

Wezi kueni makini nyuma ya mlango nimeifadhi nondo, natoa rai mapema kabla sijashusha kipondo/


Nawapiga kwa mistari mlale vizuri vizuri, yaani kama lwakatale kwenye upepo wa kisulisuli/
 
Hola hola hola!
Attention plz we nanii hii nayo unaiita rap au ngonjera za kina nanii? / acha niteme semi mpaka nukta kama nanii / nikiwapiga risasi za tenzi semeni maji kama braza nanii / mkifa mkabaki sita semeni basi kama mtemi mkwawa wananii /

Dan dana boyz mnataka kufanya mitundo huru na mimi nanii? / hahaha kaeni kando nisije nika spit fire words kama masihi / mawaki kama nyie hatuwashirikishi kwenye dili zetu za nanii / ulifikiri nini wewe nanii? Aaa nilikuwa namaanisha dili za kupiga puli nanii hahaha

Hola hola zimekua nyingi sasa mpaka zinakera, mistari yako mibovu kama yanga ya mwinyi zahera/

Umepewa shavu na mchomvu au said fella?, nakushauri achana na rap tafuta hela/

Ukinipiga risasi sifi kifuani nina vesti, mi ndo rap mkufunzi niliemtoa kanyewest/

Mistari yako ina bleed mwana inakupasa uipe pedi, mimi kwako ni zaidi usijiulize utapasuka head/

Wewe ni masihi mteule wa bwana mwingi wa upendo, nina swali kidogo naomba unipe muongozo, hivi uliazeje kumuonjesha utamu wako rose mhando?

Piga dana dana mi kauzu nakupiga ana kwa ana, mi na udhu wanga hamnigusi maana nalindwa na maulana/
 
Hii sio mada/ ya siasa au anasa/ ili watoto wachangie/
huwezi ona makada/ warembo wa kisasa/ wanataka za "njoo ubambie"/
Hakuna ada/ ila vipi wajaze kurasa/ lazima wakimbie/
Juu kama KISHADA/ Mvumbo nawanyanyasa/ ni vipi niwahurumie/
Nachoma dawa/ nakohoa nipo sawa/ wanapagawa wanaandika mashudu/
Hawana power/ nawanawa hawa chawa/ nawachinja kibudu/

Hii sio mada ya vimada, au umbea kwa kina dada/

Piga chini ukuda jaribu kwenda na muda, mmenisikia nyie matozi wapaka poda?

Mvumbo usiwahurumie we wakanyagie, nakupa mistari uwapigie ukichoka niambie/
 
Hauna haja ya kutoka nduki, mkuu Injili ya Gheto/
Bali hakikisha hawainuki, wanao ku snitch na kufuata upepo/
wasivamie Tempo/ warudi Depo/ tukiwaona hatuna mchecheto/ kama tumemuona Mobetto/ Mvumbo sina mbeleko/ wananiogopa kama Meko/ Ukonga na Keko/ kote mpaka Soweto/
Natoka ndukiii/
Kuwawahi wale washika bunduki feki/
Arsenane qudadaadekii/
Mashabiki wake wamenuna mwezi mzima hawacheki/
Unaanzaje kucheka wakati matokeo hupati/

Ndukiiii [emoji125][emoji125][emoji125]
 
Natoka ndukiii/
Kuwawahi wale washika bunduki feki/
Arsenane qudadaadekii/
Mashabiki wake wamenuna mwezi mzima hawacheki/
Unaanzaje kucheka wakati matokeo hupati/

Ndukiiii [emoji125][emoji125][emoji125]

Toka nduki mi mbishi natoka jasho, mi ni beki matata kisiki kama juma nyoso/

Arsenal wa mipasho kama masaubwire mzee wa papaso, nawalevya kama castle kisha nawaachia alosto/
 
Naona Ma mc's wengi mmefika, mnaonyesha uwezo wa kughani/
Nikiwasoma Mvumbo nafarijika, najihisi nipo nyumbani/
Sasa naleta mada mtawajibika, kuijibu kwa vina mzani/
Usiogope majibu kuandika, hakuna atakae kupandisha mahakamani/


Mada ya leo


Siku hizi mademu kila kona, wahuni tunapanda dau/
Kuna wale walioshona, na wale vimbaumbau/
Naanza na wale Singida Dodoma, wakikatiza lazima paka alie nyau/
Huko nyuma utakoma, mpaka jina unaweza kujisahau/
Huko Insta wanaleta noma, mapicha picha zaidi ya pilau/
Mtima wanachoma, na hawana madharau/
Narudi kwa wale wembamba, ama flat screen/
Hawa wanashika namba, kwenye jembe na mpini/
Hawana mambo ya kishamba, wanabadili style kama nini/
Wanaweza wasikufunge kamba, na ukajikuta umebadili dini/

Najua tunasaka pesa, ila mapenzi ni kama mshipi/
Haya bila kupepesa, kamata Mic sema chaguo lako ni lipi/
 
Nipe nikibandike,nipe nikibandue chanda tatu nizipue/
Nipeeee,kinachotoa maviiii/
Nipeeee kinacholia pwiiiiii/
[emoji2211][emoji2211][emoji2211][emoji2211][emoji2211][emoji2211] ndukiiii
 
Utani ukipitiliza dharau huibuka, Mvumbo kaza acha kubabaika/

Nafurahi kuona hip hop inatangazwa jf, taarabu na bana pua ni zaidi ya kichefuchefu/
Wana wanaflow kali kinoma wanatoa punch za maana [emoji23][emoji23][emoji23] rap battle hii [emoji119][emoji91]
 
Nachana kama koo lina viwembe, najiuliza nameza vipi/
Naficha mikono nisiwapige zachembe, sasa wanaolia nimewapiga na ipi?/
Waambie mvumbo ni kimbembe, zaidi ya Sir Chippy/
Watoto wamezoea tende, wanalalamika Hip Hop hailipi/
Mimi ndiyo Basata, wa Hii game ewe Mtanza/
Ukizingua nakuibukia fasta, zaidi ya bao la kwanza/
 
Hii sio mada ya vimada, au umbea kwa kina dada/

Piga chini ukuda jaribu kwenda na muda, mmenisikia nyie matozi wapaka poda?

Mvumbo usiwahurumie we wakanyagie, nakupa mistari uwapigie ukichoka niambie/
Hakika sina huruma nao, maana sioni wanachoimba/
Ama zangu ama zao, wamevamia chaka la Simba/
Mvumbo sina ubaya nao, ila waelewe hii siyo Sindimba/
Na wanaponiona Baba yao, wanapaswa kuchimba/
 
Mvumbo usilale utavunda utakua mvundo, mc mwenye machale nadunda ndani ya tungo/

Wanga hamniwezi maana sikuizi nalala na nyundo, jikanyageni nyie washenzi muone navyozichana hizo nyungo/

Wezi kueni makini nyuma ya mlango nimeifadhi nondo, natoa rai mapema kabla sijashusha kipondo/


Nawapiga kwa mistari mlale vizuri vizuri, yaani kama lwakatale kwenye upepo wa kisulisuli/
Mvumbo siku hizi silali, wachawi wananiita Bundi/
Wakija mkononi nina pombe kali, pembeni dem akinionyesha ufundi/
Na mtoto akilala chali, muhuni nahamia kwenye mirungi/
Nakesha kama sadali, maafande wanakuta vishungi/
 
Sisi tuko High, Na wao Wapo Low

Wacha niji Dai, Jesus Saves Bro

Zamani nilikua mdhambi, am Now Born Again

Kwa Shetani nimenyea kambi, Yesu kanilipia madeni
 
Wanasema rhymes nakohoa, kama AK Forty Seven/
Ngoma sitaki kutoa, watanipanga na madogo kwenye Top ten/
Ambao viduku wakinyoa, wanajiona tayari wapo Heaven/
Vocal zao za kidada poa/ Mvumbo napigia masturbation/
 
Back
Top Bottom