Eti mnajifanya mnarap hivi nyinyi mnaijua rap? / rap tunafanya sisi kina nanii japo hatupati mshiko chap chap /
Rap imekupiga kanzu, ukiforce utaonekana kavu/
Rap sio vitisho wala mipasho kuifanya yahitaji nyenzo, mabishoo acheni rap sikilizeni rege ya senzo/
Mistari yangu zaidi ya koleo inawatoa jasho, na ndio maana hutaki leo una
Takakeisho/
]Nyie wote maboya kama mnabisha njooni niwatie ndani ya kapu /
Mi ni boya hunikosi katika bahari ya rap, bila mimi hufiki popote hata kama mkononi una map/
Boya niko hapa kuwanusuru fake mcees msizame, nishike vizuri nimebeba pumzi zenu msidate/
Boya nishasimama sioni wavuvi wakunikalia, hiki kina kirefu kwa mbizi mnajiongopea/
Mashua zenu mbovu zishatoboka, hamuwezi zuia matundu ya maji kwa bazoka/
Uliyeanzisha uzi wewe ni kolo kama nanii anayeamini ili ufanikiwe lazima uende shule ukasome fasihi / au nakosea kama yule nanii aliyesema historia huwa haijurudii? / hahaha nacheka kifala kama mbwa alotokwa na manii.
cheka kifala ntakutoa kafara niwe bosi, yani nakugeuza kua mleta hela ukiwa upo ndani ya box/
Shule haina maana yeyote katika maisha zaidi ya fix, maswali ya kipuuzi kukomoana eti utafute thamani ya x/
Ticha wa hesabu nakuheshimu niache wala usinifosi, usitumie ghadhabu kwenye mambo yako ya kiofisi/
Nataka vitu laini kama somo la civics, na sio huo uhaini wa kunipa hesabu za matrix/
By the way kuanzia ulipo si sawa na kubakia ulipo Nikise 'chini hapana' ina maana fanya unyanyuke / me ni mkushi zaidi yako ukichukia karibu nikupaushe.
African - Japanese
african japanese mi ni mjeda waulize Vietnamese, natisha kama alqaida naogopeka kama jinamizi/
We ni mkushi na ndio maana flow zako zimekaa ki bush, mi ndo
Scars nazika marapa wabishi/
Mi ni kero kama kunguni walioko kitandani, yaani kiboko ya wahuni hadi maaskofu makanisani/
Siuliki kwa muarobaini, wala dawa yeyote ya hospitalini/