Michano/Hiphop/Freestyle

Michano/Hiphop/Freestyle

naona ulinikimbia comrade me ndo masta wa vina/mistari yako yakuibia ingekua samaki basi imechina

hip hop iko mbele si tuko nyuma tunasukuma/walio kuja na vihere here nimewagaragaza bila huruma

comrade nawakimbiza mpaka boda/wana shtuka hawana viza wamekwama dubai wanaliwa kiboga
 
Daima wananiwazia, nianguke kwenye hii kabumbu/
Ila bado nipo juu naning'inia, zaidi ya mfuko wa pumbu/
Na kila ninapoingia, wanazo kumbukumbu/
Maana nimesha waharibia, game nimeibeba kama nundu/
Haina upinzani, kama bunge la sasa/
Ingia kwenye ramani, uchezee vitasa/
Uweke mpira kwapani, ukanisemee kwa Mambosasa/
Natawala hii fani, so usisogee kama ni garasa/
 
asante' mungu umenipa nguvu na heshima/ukanipa na uhuru ili nijitawale kama china'

walio nita yatima sasa wapo kimya/nimewavalia miwani nawaona makima

tena umenifanya maarufu sasa/nilie kua mtumwa umenipiga msasa

leo napendeza zaidi ya wale walio nibeza/si walinicheka eti sijui kingereza wanashangaa natembelea arteza
 
Game imejaa mamluki, na beki zishaluzi/
Thread kama ina mikuki, wanauogopa huu uzi/
MMU hawabanduki, wawapate akina Suzi/
Hawajui nazijua chupi, zaidi kitovu na mavuz*/
Nipo mjini kitambo, zaidi ya Bus za Uda/
Nisharekebisha mipango, Mungu anipe nini Macmuga/
Wakuda/ huu ndio muda/ wa kutoa ushuhuda/ ya kwamba budah/ nishavamia mbuga/
Haina kuzuga/ navuruga/ Dar mpaka Chugga/ haina husda/ kama nina Kisuga/
Natema vina, kama nimemeza Kamusi/
Kinguvu naichukua Heshima, singoji ishara za Mamajusi/
 
Comrade kwenye mapenzi nina stashahada/sichagui mademu nagonga mpaka makahaba

demu kama hawezi game namchapisha raba/nawapa mapenzi motomoto mpaka nafanyiwa ibada

pisi kali leo naivua bikini/ show kali nazama mpaka chumvini/vidole vya nini..?
 
Nakohoa madini kila verse, kama mchanga wa Makinikia/
Ma Mc's nawapa stress, wanabaki kunichukia/
Kimenuka ka' kinyesi, waache wabane pua/
Mistari yao mepesi, zaidi ya mzigo wa mabua/
Hizi Rhymes kama zinanidai, maana zinakuja kila wakati/
Watoto wanao jimwambafai, kwa Mvumbo hawana bahati/
Wanachezea umeme/ wamepotea hapa ndiyo penye/ napokea wenye genye/
Nina vocal zenye upako, zaidi ya Millard Ayo/
Kipaji siyo matako, kila mtu awe nayo/
 
Kabla ya hii mijengo, na hizi fedha/
Hip Hop ilikuwa ndiyo lengo, na walisema naweza/
Ila watu wa kitengo, bila pesa ngoma hawawezi cheza/
Sikuwa Tembo, kusema Wasafi watanitengeza/
Na baba aliacha pengo, kabla sijajiweza/
Nikabadili Engo, kipaji nikakitelekeza/
Mungu hakunipinga, nashukuru akanitoa Selo/
Siku hizi na change mandinga, kama na change kapelo/
So msikate tamaa, bora mkate mitaa/
Msidate na chapaa/ na msimfuate njaa/
Msipate kichaa/ mkate ni wa Jah/ msinate na U star/ MSINIFATE MTAKAA/
 
siku hiz Hip hop haina radha kaka/from Now trap tumewakamata/
dj play the beat uone tunavyo nata/
hawa rapper sasa vichwa kapa/tz sijaona rapper wote taka taka.

I remember nilimwambia mama nikikua atakula bata/she trusted me' look now anakula anachotaka/
 
Ujumbe wa leo ni kwamba ukicheza na Kazi ujue unabeti na Maisha/ni bora ubeti na kanji akipita na mkwanja ndio imeisha/mpira dakika 90 mwana tandaza mikeka/ mikeka imechanika hasira za nini Sepa/Maisha leo ni kazi tuu huwez pata kirahisi/Heshima Pesa siku hz sura hailipi /pesa sabun ya rohi sometime inatia uchizi/pesa inauza rohi shuda zinapokuwa mtiti/
 
bado underground mna flow mbichi/mnapiga round kutafuta kiki/mi natoa hit/verse zinawakata kama machete kule kibiti
nabado nasifiwa na mashabiki/they told me nimekua mkali na fly kama ninja

kwa hii mistari bro huwezi pinga/hip-pop now ni ya kijinga/na trap imekua kinga
na bado tuna fight ili game tulikuze ili young trappers waje wajifunze/
 
Hapa ni chimbo usilete zako story,ukizingua wahuni tunapandisha moli/utachapwa kama mdori
maisha kama tolori sukuma ukipata pesa unywe mtori/si ndo wahazabe kwenye pori hatutaki utani/
Dj play the beat tupate burudani i`ts so funny..
 
Kila nikipita hapa nataman rap battle,
Ko naihitaj straight sio njia za mkato,
Aje mmoja twende macho kwa macho,
Ziwe true rhymes na sio mipasho pasho,
 
Ninapotimba kama Bundi, watoto wanaona uchuro/
Nina mistari ya kiufundi, waambie Hip sio Danguro/
Wanachamba kama Diva, hawazingatii Itifaki/
Waambie mawe yameiva, na kuni zimebaki/
Mvumbo kwenye Game, zaidi ya teja na makushabu/
So ninapotimba sehemu, watoto wanashika adabu/
Hizo sifa kem kem, pelekeni kwenye taarabu/
Huku hakuna mambo ya kidemu, so msijifiche na nikabu.
 
Hii jf sasa imekua ya kipuuzi,ukipost kidogo mods wanakuja kufuta uzi/
sijui wanafikiria nini au ndio kujifanya wajuzi na kutuonatuoa si ni kama mbuzi/
hazija pita dakika nimepost thread wao na kiherehere chao wakadelete/ningemjua mmiliki haki ya mungu ninge mchoma na kibiriti.
 
Mb zetu tumezitoa kafara japo humu ndani mods wanatuona si mafala/
sasa bora kushinda fb maana jf sasa hivi ni kama jalala/mods hawapo makini wanafanya kazi kama wamelala
sijui nichuki binafsi maana nyuzi mnazofuta nina wasi wasi/
hii kitu imekua so nasty hadi nakosa mood nashinda snapchat
 
Mods kuweni makini msiwe na kiherehere kama wavaa bikini/
sijui mnajua kama mnatukera lakini au mawazo yenu yote yapo chini/
vitu mnafanya kipumbavu au ndio kwamba mnatuendesha kimabavu/
sasa kama mnaiendesha jf ki dictator nawatuma mkamwambie jf creator asizani kuwa ametuteka.
 
Leo nimemkumbuka mzee wenger, mpira piga pasi usipige chenga/arteta anatualibia timu wachezaji wamekua kama mrenda
matokeo ya ovyo na siku zinazidi kwenda/na kama haiwezi timu ni bora ange surrender
Cheki aubameyang anavyocheza kwa uoga, willian anakimbia kama boga/ama kweli mwaka huu kombe letu litakua uyoga
 
life lime kuwa gumu pande zote, sio wapinzani wala watawala tunaisoma namba wote
mzungu yuko wapi adondoshe pochi niokote, natamani nihame nchi ila nakumbuka maisha nipopote
mwaka huu bidhaa zimepanda bei hali ngumu chalinze hadi osterbey
 
Nimejikuta natabasam the way Comrade boy alivyowaka
Yaan ni full kutema shit washapata wanachotaka
Kama naona mods vile mwana wanavyomsaka
Ila kidume be kushinda snap kikwetu sio lakha
 
Nikipata pesa basi me na wahuni ni mwendo wa gambe/
mwendo wakukesha na wala hatuhitaji wapambe/
tunaishi Maisha ya kimafia japo tupo bongo
mambo ya mademu niku take easy so why uanzishe mlolongo/sasa we zingua tukutoe tongo tongo/kisha tukufanye chongo
ndipo utakapo jua wahuni ni wa moto hawakuumbwa na udongo
 
Back
Top Bottom