INAUZWA Miche ya kisasa ya matunda inauzwa

Apple zinastawi zaidi na kutoa matunda mazuri kwa ardhi ya aina gani mkuu, na pia mikoa ipi inafaa kupanda Apple
Apple hustawi kwenye mikoa yenye joto la wastani,mvua ya kutosha,ardhi yenye rutuba ya kutosha.
Mikoa ambayo inafaa kwa apple ni kama Mbeya,Arusha,Iringa,Morogoro(baadhi ya wilaya),Tanga na mikoa /wilaya zenye hali ya hewa kama hiyo.
 
Sipendi ligi, sitakanyaga tena kwenye huu uzi
 
Comment yake imenikatisha tamaa. Naomba wiki ijayo nitumie miche mi3 ya varieties tofauti tofauti za parachichi.
 
Comment yake imenikatisha tamaa. Naomba wiki ijayo nitumie miche mi3 ya varieties tofauti tofauti za parachichi.
Usikate tamaa boss,nilianza kuona mwenda anaokwenda nao sio rafiki.
Kuhusu odder yako ya next week,hakuna shida.Ukiwa tayari utanijulisha ili nikutumie.
Asante kwa kuendelea kuniamini katika kukuhudumia na kupata kilicho bora.
 
Sawa, pia unakumbuka order yangu ya apple? Au moro haiwezekani kupatikana.
 
Basi utaniunganishia na hizo parachichi. Nitumie invoice [emoji1649] 3 hass moja na varieties nyingine na apple [emoji519] 4
sawa,kuhusu apple nitakuunganisha na Agent wetu yuko Dar,yeye ana apple pia.Nadhani nitakuwa nimekurahisishia zaidi
Unaonaje?
 
You mean yeye anazo kwenye kitalu hapa Dar? Au anaagiza somewhere...kama anazo hapa Dar you'd better provide me with his physical address nikachukue
 
You mean yeye anazo kwenye kitalu hapa Dar? Au anaagiza somewhere...kama anazo hapa Dar you'd better provide me with his physical address nikachukue
ana kitalu cha apple.Nakutumia namba yake akupe direction
 
Mkuu dawa gani ya kuzuia majani kujikunyata kwenye mche?
 
Mna Agent/partners Arusha reliable,atakaeweza kunishauri na kunisimamia kwa karibu kwa Mimi ninayeanza bustani ya mbogamboga na matunda?

"Be Humble"
 
Mkuu dawa gani ya kuzuia majani kujikunyata kwenye mche?
Changamoto hii husababishwa na wadudu ambayo wanafyonza utomvu wa mche.Na hawa wadudu wanauwezo wa kuhama kutoka mche mmoja kwenda mwingine.Hivyo hatua ya kwanza

1.Hakikisha unatoa majani /mche uliopata madhara tayari.

2.Eneo lako liwe safi muda wote,toa magugu yote

3.Tafuta fungicides ambayo ina content ya copper au sulpher,hakikisha wanakupa maelekezo ya wakati unaofaa kupulizia hiyo dawa

4.Epuka kumwagilia majani ya mche(kama inawezekana)

5.weka mbolea ya organic,ina kiwango kikubwa cha N

6.Wakati mwingine pia tatizo hili huweza kusabaishwa na jua kali,hivyo usimwagilie wakati wa jua,hakikisha unatandaza majani ili kutunza unyevu kwenye mche.

Pole kwa changamoto hii
 
Mna Agent/partners Arusha reliable,atakaeweza kunishauri na kunisimamia kwa karibu kwa Mimi ninayeanza bustani ya mbogamboga na matunda?

"Be Humble"
Kwa bahati mbaya Arusha hatuna agent.Lakini ukifika wakati unahitaji msaada,utanitafuta ili nikuunganishe na mtaalamu wa mbogamboga.Nina amini atakusaidia hatua kwa hatua hata kama mtakuwa mikoa tofauti.
 
Dada hauna brach dar ...kwq maana wengine tunstaka miche michache..

Kwa hyo kutuma kwenye bas itatugharimu sana..
 
Dada wilaya ya manyoni hapa nishauri aina ya matunda yanayoweza stawi fresh kutokana na hali ya hewa ya hapa
 
Dada wilaya ya manyoni hapa nishauri aina ya matunda yanayoweza stawi fresh kutokana na hali ya hewa ya hapa
Hali ya hewa ya Manyoni(Singida) haina tofauti sana na Dom.
Hivyo nina amini matunda yanayostawi Dom yatastawi pia Manyoni.
Huko unaweza kupanda miembe,tende,limao/ndimu,papai,pera,passion,komamanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…