INAUZWA Miche ya kisasa ya matunda inauzwa

INAUZWA Miche ya kisasa ya matunda inauzwa

3.Asilimia kubwa ya miche yetu ni ya kisasa(zaidi ya 90%),nikiwa na maana kuwa imefanyiwa budding na mingine grafting, ni miche michache sana ambayo ni ya asili mfano,Ukwaju,Zaituni,Tende n.k
Hivyo basi,kigezo cha kwanza tunachokitumia kujua kama Mche wetu wa kisasa aina ya Muembe(mfano)utastawi,tunaangalia je, Bagamoyo ipo.miembe ya asili inayostawi?.Kama jibu ni ndio,basi mche wetu wa muembe uliofanyiwa grafting nao pia utaleta matokeo mazuri.
Sababu grafting ni muunganiko wa mche wa asili na mche wa kisasa.
Hivyo basi,kwa Bagamoyo miche ambayo itakuletea matokeo ni kama Embe,Minazi,Citrus zote(chungwa,chenza,ndimu,limao,balungi),Parachichi,Papai,passion
Na budding ni nini?
 
Mie natamani ungekuwa dar, ukatembelea shambani kwangu, ulione ndio mengine yasogee.

Shamba lipo mkuranga(lubambawe.)
Huduma ya kutembelewa shambani ipo,na huwa inaambatana na kufanyiwa layout pamoja na kupandiwa miche na team yetu.
Huduma hii ina malipo kama utaihitaji nitakuunganisha na kiongozi wa team akupe muongozo
 
Na budding ni nini?
Ni kitendo cha kupandikiza sehemu ya mche mmoja kwenye mche mwingine(Yote iwe ya jamii moja)
Sijui kama nimekupa maelezo ya kukutosheleza mkuu.
jaribu google pia unaweza pata maelezo na picha
 
Kila siku nitatoa kwa uchache maelezo muhimu ya awali ya miche yetu ya matunda inayopatikana kwenye bustani yetu iliyopo ndani ya chuo kikuu cha kilimo SUA

Karibuni,Lily loves you all[emoji7]
Kasoro mimi tu.. Usinilavu pliizii[emoji23]
 
Hii miche inaanza kuzaa ikiwa na urefu wa kuanzia 50-80cm.
Kadri unavyovuma matunda,mche unazidi kurefuka,kimo kinaongezeka.

Kuna aina mbili za mizizi.
Fibrous.Hii inatokea kwenye miche/mimea ya Mono.
Taproot,inatokea kwenye miche/mimea ya Dicot
Nadhani mpaka hapo utakuwa umeelewa miziz ya papai iko kwenye kundi gani mkuu(Tulisoma kwenye sayansi ya darasa la sita)
Haina ukomo wa kuzaa?
 
Nimesoma uzi woote, nimeng'amua changamoto moja,
Kuna watu waliwahi kununua miche(sio kwako) na haijaleta matokeo(mavuno)

Je nyinyi sasa mnatusaidia vipi wateja wenu likitokea suala kama hilo?

Maana kununua miche ya miembe/mipapai ya heka 3-10 halafu zote zikafeli mie si nitakufa kwa kihoro. [emoji854]
 
Huduma ya kutembelewa shambani ipo,na huwa inaambatana na kufanyiwa layout pamoja na kupandiwa miche na team yetu.
Huduma hii ina malipo kama utaihitaji nitakuunganisha na kiongozi wa team akupe muongozo
Gharama ni kiasi gani?
 
Ni kitendo cha kupandikiza sehemu ya mche mmoja kwenye mche mwingine(Yote iwe ya jamii moja)
Sijui kama nimekupa maelezo ya kukutosheleza mkuu.
jaribu google pia unaweza pata maelezo na picha
Miche yote ni ya kiasili ama ya kisasa?
 
Niko Krt nahitaji ila naomba kujua kama miche ypte hii inastawi karatu

Kama ndivyo miche inayofaa huko ni
parachichi,Makadamia,Passion,komamanga,papai,embe,stafeli,fenesi etc
 
Nina eno langu 2000 sqm nataka niwe na kila mche uliotaja na bado niwe na sehemu ya kahawa ba jussi Joe unaweza e kunifanyia upembui yakinifu na mpangilio Niko Tegeta
Tuna aina tofauti tofauti 45 za miche na kila siku tunaongeza aina mpya kulingana na upatikanaji wa mbegu.
Nadhani ungekuwa specific utahitaji miche aina gani ,tuanzie hapo
 
tuna embe aina 7.
aina mbili tu ndio zikienyeji(dodo na bolibo)
aina 5 ni za kisasa na zinaanza kutoa maua kuanzia miezi 4 na kuanza kuzaa baada ya miezi 7-8.Hapo muembe utatoa matunda mawili mpaka manne na wengi huwa wanayajoa sababu bado mti haujawa stable kubeba tunda.

Hii uliyouliza pia ni moja kati ya embe za kisasa.
Hizi za kienyeji(bolibo na dodo) zinachukua muda gani kuzaa..

Hizi za kisasa zinakoma muda gani kuzaa(kusimama kutoa mazao) nimesikia baada ya muda fulani haizai tena.
 
Hizi za kienyeji(bolibo na dodo) zinachukua muda gani kuzaa..

Hizi za kisasa zinakoma muda gani kuzaa(kusimama kutoa mazao) nimesikia baada ya muda fulani haizai tena.
bolibo na dodo baada ya miaka 3
Kinachotokea ni kuwa baada ya miaka kadhaa mche utaanza kupunguza rate ya kutoa matunda.Hapo inabidi mkulima/mmiliki ufanye prunning,weka mbolea,mwagilia maji ya kutosha,baada ya hapo mti wako utaanza kutoa matawi kwa upya na matunda .Ukifika Horticulture utaweza kuona sample ya mti ambayo imefanyiwa prunning na kuanza kuzaa tena baada ya muda.

Lakini pia hakuna mche wa ambao utazaa milele mkuu,lazima utafika umri mti utachoka.
 
IMG_20210107_141126_061.jpg
 
Back
Top Bottom