3.Asilimia kubwa ya miche yetu ni ya kisasa(zaidi ya 90%),nikiwa na maana kuwa imefanyiwa budding na mingine grafting, ni miche michache sana ambayo ni ya asili mfano,Ukwaju,Zaituni,Tende n.k
Hivyo basi,kigezo cha kwanza tunachokitumia kujua kama Mche wetu wa kisasa aina ya Muembe(mfano)utastawi,tunaangalia je, Bagamoyo ipo.miembe ya asili inayostawi?.Kama jibu ni ndio,basi mche wetu wa muembe uliofanyiwa grafting nao pia utaleta matokeo mazuri.
Sababu grafting ni muunganiko wa mche wa asili na mche wa kisasa.
Hivyo basi,kwa Bagamoyo miche ambayo itakuletea matokeo ni kama Embe,Minazi,Citrus zote(chungwa,chenza,ndimu,limao,balungi),Parachichi,Papai,passion