Kwanza hongera kwa hatua hiyo mkuu.
Pili,kuhusu aina ya mbegu nzuri ya mihogo,nikushauri uonane au upate ushauri wa kina kutoka kwa mtaalamu wa kilimo waliobase kwenye mazao.,kitengo chetu(Horticulture) tuna deal na miche/kilimo cha matunda.
Lakini kama eneo lako lina rutuba/mbolea,hakuna haja ya kuongeza mbolea ila kama itabidi kufanya hivyo,basi tumia mbolea ya samadi
tatu,minazi tunayo,Na mbegu tuliyonayo sasa ni African tall,bei ni sh 7000,discount ipo endapo utahitaji miche kuanzia 50.
nne,miche ya embe ipo na tuna aina zifuatazo
1.Kent
2.Alphonso
3.Dodo
4,Embe tang
5.Tommy
6.Red indian
7.Apple mango
Mche wa embe ni sh 2000
tano, tuna aina mbili za migomba
A.Migomba ambayo ndizi zake ni kwaajili ya tunda(Mtwike,Kimalindi,Kisukari)
B.Migomba ambayo ndizi zake ni kwa ajili ya chakula(mzuzu,mshale,M/tembo,Jamaica,Uganda green,William)
Migomba,mche sh 3500