kasimba123
JF-Expert Member
- Apr 18, 2010
- 1,753
- 816
nakumbuka niliporudi nyumbani baada ya miaka miwili toka ughaibuni mwanangu kipindi hicho anamiaka mitatu niliitumia likizo yangu kucheza naye muda mwingi kwa kumtengenezea magari ya maboksi na kumnunulia magari ya midori kisha kucheza pamoja kwakweli kipindi nilichoondoka kurudi ughaibuni zikuweza amini pale nilipomuona anatoa machozi ya kuninililia na kila mara alikuwa anamlazimisha mama yake anipigie simu ili niongee naye hadi niliporudi nyumbani baada ya kumaliza mwaka mwingine mmoja siku hiyo nakumbuka aliponiona ndani ya uwanja wa ndege sehemu ya kusubiria mizigo alimcholopoka mama yake na kunikimbilia ndani sitakaa nisahau hii na kwakweli imenifanya niishi naye kwa upendo na sasa anajisikia huru zaidi kuongea na mimi kuliko rafiki yake yeyote yule kwenye huu umri wake wa miaka 15