Michezo haramu katika mikopo chechefu. Je, Martin Masese anapata wapi taarifa nyeti kama hizi?

Aisee hapa wana sheria ndio wangetupa majibu sahihi
Itakuwa kuna loopholes kwenye hiyo mikataba ya mikopo
 
Katika notisi ya kesi zinazotarajiwa kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa, leo, Aprili 23 mbele ya majaji watatu; Jaji Mkuye, Jaji Mwampashi na Jaji Muruke,
Mbele ya waheshimiwa majaji hao, itasikilizwa kesi ya madai baina ya EQUITY BANK dhidi ya kampuni ya STATE OIL (T) Ltd (mali ya Nilesh Suchak);

STATE OIL (T) Ltd walikopa $26 milioni (zaidi ya TZS 67.1 bilioni) EQUITY BANK na kukataa kulipa deni hilo. Wakakimbilia mahakamani. Kesi wakashinda.Kesi ya Biashara Na. 25 ya mwaka 2021, tarehe ya kusikilizwa ilikuwa Agosti 4, 2023, na tarehe ya hukumu Novemba 3, 2023. Jaji alikuwa Nangela, J.


EQUITY BANK (T) LTD wakakata rufaa mahakama ya rufaa, kesi inaendelea muda huu Mahakama ya Rufaa Tanzania (The Court of Appeal of Tanzania).

Mbele ya majaji hao pia, jumatatu ijayo, 29/04/2024 itasikilizwa kesi nyingine ya rufaa baina ya EXIM BANK dhidi ya THEM & FIVE B Hotel and Tours LTD.

Jumanne, 30/04/2024 mbele ya majaji hao kesi nyingine ya madai baina ya EQUITY BANK itasikilizwa dhidi ya kampuni ya usafirishaji ya Nas Hauliers LtdNas Hauliers Ltd; walikopa na kukataa kulipa $16 milioni za EQUITY BANK. Wakakimbilia mahakamani. wakapewa ushindi dhidi ya EQUITY BANK (T) Ltd.

Jaji Deo John Nangela aliandika hukumu ndefu ya kurasa 164 19/04/2023 akiwapa ushindi Nas Hauliers Ltd katika COMMERCIAL CASE NO. 105 OF 2021
Huu mwendelezo unaohusu ile mikopo chechefu ambayo kampuni kubwa za mafuta, usafirishaji na kilimo inachukua na kuingia mitini bila kurejesha.Hizo kampuni zikidaiwa fedha hizo, wanakimbilia mahakamani, na mahakama zinatoa hukumu kuwapa ushindi.

Benki zinabaki na hasara kubwa bila mitaji.NB; kama upo Dar es Salaam, unaweza kufika Mahakama ya Rufaa (The Court of Appeal of Tanzania), ukasikiliza mwenendo wa kesi hiyo.Martin Maranja Masese, MMM.
 
Kuna pdf za kesi zao online. Wasomi mtufanyie uchambuzi.


Jamaa wanakopesheka hela nyingi sana, mamilioni ya madola, yaani ni maB na maB na mabB
 

Attachments

Yaani ufisadi wa kupanga kabisa. yaan wanakopa mabilioni kisha serikali ndio inalipa kutokana na dhamana ya letter of credit. Wenyewe wanaenda kwa majaji wao wanajuana wanashinda. Hao ndio waliyosherekea kufa magufuli. Sasa hii kitu iko nje sio siri mama ajue wananchi wanataka fedha zao. Kama hawawezi tusisikie eti mama mitano tena. Tunataka kiongozi wa kuwashika hawa fisadi na kuwabana walipe fedha za umma.
 
HUwezi tembelea jamhuri ya kujitegemea ya X ukakosa bandiko la mmm mzee wa spana
 
Yaani mabenki yanatakiwa kuwadhibiti na kuwawajibisha mameneja na wakurugenzi wao kwa kuwahusisha na mikopo chechefu. Kwa nini benki itoe mabilioni kwa kampuni haina uwezo kulipa au imepanga kutorudisha deni.
 
Hata mimi nimeshindwa kuunganisha dots hapa. Najua ni kweli nchi yetu ina namna nyingi za upigaji lakini kwa hili nimeshindwa kuona kama kuna mantiki.
 
Vijana kama wewe wana mchango mdogo sana kwa Taifa!
 
Katafute judgement upate ufahamu!
 
Kuna wajanja wanajua tusiyoyajua mwanya kidogo tu anapigia humohumo
Kabla ya kuibuliwa bungeni uliijua ESCROW ? Kwa hiyo tusibishe
Comment yako nimeipenda niya kiungwana sana...na katika maisha sio kila kitu nicha kubisha ni bora ukasoma andiko na kutulia ili uzidi kujionea na kusikia mengi kwani nyuma ya pazia kuna mambo mengi sana huwa yanaendelea ila kama haupo kwenye system huwezi kuyajua kamwe na ndio pale sasa walio kwenye system wakiyaleta hapa tunaanza kuwabishia me huwa ni mfuatilia mzuri sana wa taarifa na hupenda pia kuwa kimyaaa tu kusubiri matokeo yake.
 
Rais Samia ndiye aliyelalama na mikopo chechefu, naye pia humwamini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…