Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Yanga, JKT Ruvu 'ligwaride' Uhuru leo


na Juma Kasesa


amka2.gif
TIMU ya soka ya Yanga leo inashuka Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuvaana na Maafande wa JKT Ruvu, katika mechi ya kirafiki kujiandaa na mzunguko wa pili Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa. Yanga iliyo chini ya Kocha Mserbia, Kostadin Papic inacheza mechi hiyo ya kirafiki ikiwa ni ya tatu, baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 katika mechi ya kwanza dhidi ya Azam FC, kabla ya kuzinduka na kuitandika AFC Leopard ya Kenya bao 1-0.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo Louis Sendeu, Papic amepanga kushusha kikosi kizima cha timu hiyo, ili kuweza kupima uwezo wa kila mchezaji ikiwa ni maandalizi ya kusaka kikosi cha kwanza ambacho kitaweza kuwapokonya ubingwa wa Ligi hiyo 'Wekundu wa Msimbazi' Simba na kufanya vema katika michuano ya kimataifa.
Sendeu alisema, mchezo wa leo ni kati ya mechi tisa ambazo Papic amepanga timu hiyo icheze ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kunguruma Januari 15 mwakani na michuano ya kimataifa, ambako Yanga inatarajia kucheza Kombe la Shirikisho.
Alivitaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni mzunguko sh 2,000, Jukwaa la Kijani sh 3,000, Jukwaa Kuu sh 5,000, na VIP sh 7,000.
 
Gumbo ampa 'tano' Jan Poulsen


na Juma Kasesa


amka2.gif
KIUNGO wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba, Rashidi Gumbo, amempongeza Kocha Mkuu wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Jan Poulsen kwa kumteua katika kikosi cha timu hiyo kinachojiwinda na michuano ya Ukanda wa bonde la mto Nile 'Nile Basin' inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 5-17 mwakani mjini Cairo Misri. Gumbo ambaye ni mara yake pili kuitwa Stars, mara ya kwanza ikiwa mwaka jana na Kocha aliyemaliza mkataba wake, Mbrazil Marcio Maximo kabla ya kutemwa na kuitwa tena juzi akichukua nafasi ya Henry Joseph Shindika anayekabiliwa na matatizo ya kifamilia.
Akizungumza kwa njia simu kutoka mjini Zanzibar, ambako yupo na kikosi cha Simba ambacho kimepiga kambi, Gumbo alisema, amepokea uteuzi wa Poulsen kama changamoto kwake ya kujituma zaidi ili kukuza kipaji chake na kujitangaza kimataifa kupitia michuano hiyo.
Alisema, anaamini anaweza kuvaa viatu vya Shindika, ili kuisaidia Stars katika michuano hiyo na kumuonyesha kocha Poulsen kuwa hakufanya makosa kumwita.
Alitoa wito kwa wachezaji wenzake kumpa ushirikiano ili kuiletea mafanikio timu hiyo.
Alisema, anatarajia kutua jijini kujiunga na kambi ya Stars baada ya kupata ruhusa kwa uongozi wake wa Simba.
 
Stars wapigwa darasa
DORIS MALIYAGA
KOCHA wa Taifa Stars Sylivester Marsh jana Jumatatu aliwaweka darasani nyota wake kabla ya kuanza mazoezi rasmi leo huku akisisitiza kuwa kikosi hicho ni cha mafanikio.

Marsh ambaye ndiye atakuwa akikifundisha kikosi hicho kwa siku zote hapa nchini hadi Januari 3 watakapoungana na Jan Paulsen huko Misri.

Ameliambia Mwanaspoti kuwa wameanza kwa darasa ili kuwaweka sawa kinadharia kabla ya vitendo ili kujitambua na kuelekezana malengo ya timu na TFF kushiriki michuano hiyo..

��Tunawaweka kwanza darasani na kesho [leo] ndiyo tutaanza kwa vitendo, tumeanza kuelekezana kila mmoja ajue majukumu yake na hasa baada ya wageni kuongezwa ambao ilikuwa ni lazima tukutane nao.��

Marsh alikisifu kikosi hicho na kusema; ��Ni cha mafanikio kulingana na mazingira ya kipindi tulichonacho ,tunahitaji wachezaji wa aina gani ndiyo maana tumewaongeza hao na kwa walioachwa si kama ndiyo mwisho wataitwa kwa mara nyingine.

��Banka mgonjwa anatakiwa kutibiwa, Thomas Ulimwengu anamajukumu katika klabu yake huko Sweden na wengine tumewapumzisha kama ulivyoona kwa Jeryson Tegete mashindano yaliyoisha.��
 
Mtibwa Sugar yaitambia Majimaji Uhai Cup


na Juma Kasesa


amka2.gif
TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar chini ya miaka 20, jana ilianza kwa kishindo mashindano ya 'Uhai Cup' baada ya kuichapa Majimaji ya Songea 'Wanalizombe' mabao 4-0, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam. Katika mechi hiyo iliyokuwa ya upande mmoja, kwa Mtibwa kutawala kwa takriban dakika zote 90, mchezaji Michael Mgimwa aliibuka shujaa baada ya kuifungia timu yake mabao yote manne.
Mtibwa waliandika bao la kwanza dakika ya 24 baada mabeki wa Majimaji kuzembea kuokoa hatari langoni mwao na mfungaji kuunasa na kuujaza wavuni, kabla ya kupachika la pili dakika ya 54, huku akifunga la tatu dakika ya 74 na la nne dakika ya 80.
Katika mechi nyingine iliyopigwa juzi jioni, Wekundu wa Msimbazi Simba ya jijini Dar es Salaam waliitafuna Toto Africa ya Mwanza kwa mabao 3-1.
Bao la kwanza la washindi lilifungwa dakika ya 14 na Haruna Athuman, kabla ya Edward Christopher kupachika la pili dakika 44 na kudumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili, Simba ilianza kwa kishindo mchezo huo ambao waliutawala katika kila idara na kuandika bao la tatu dakika ya 67 kwa njia ya penalty, baada ya Haruna Athumani kuangushwa na mabeki wa Toto katika eneo hatari na Ramadhani Yahaya kufunga penalti hiyo, kabla ya Toto kupata la kufutia machozi dakika ya 75, likifungwa na Sebastian Bahati.
Katika mechi nyingine, Yanga ilibanwa mbavu na African Lyon na kujikuta ikilazimishwa sare ya bila kufungana.



h.sep3.gif


juu
 
Kova aahidi ulinzi mzito Cheka vs Maugo


na Samia Mussa


amka2.gif
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna (DCP), Suleiman Kova, ameahidi kutoa ushirikiano siku ya pambano lisilo la ubingwa kati ya Francis Cheka na Mada Maugo litakalofanyika Januari mosi ukumbi wa PTA jijini. Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Mratibu wa pambano hilo Kaike Silaji, alisema mbali ya Kova kuwa ni mgeni rasmi siku hiyo, ameahidi kutoa ushikiano wa kutosha ambako kutakuwa na askari polisi zaidi ya 100, ambao watahakikisha kuna usalama wa kutosha katika pambano hilo.
Silaji alisema kuwa anawahakikishia mashabiki na wadau wa mchezo huo kuwa, suala la ulinzi katika pambano hilo limezingatiwa, ambako kutakuwa na walinzi wasiopungua 50 kutoka kampuni ya ulinzi ya Aurola.
'Nawahakikishia wapenzi wote wanaotarajia kufika siku hiyo kwamba usalama utakuwa ni wa hali ya juu, hakuna mtu yeyote atakayeleta fujo kutokana na ulinzi utakaokuwepo siku hiyo, kwa hiyo watu wajitokeze kwa wingi kuangalia pambano hilo la kukata na shoka,'� alisema Kaike.
Mbali ya hilo, mratibu huyo aliongeza kuwa amerejea Jiji la Morogoro kwa ajili ya kushughulikia vipimo vya afya vya Cheka, ikiwa ni maandalizi ya pambano hilo ambapo mpinzani wake Maugo tayari alishapima na yuko salama kwa pambano.
 
Tisa kuiwakilisha Temeke masumbwi Taifa


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MABONDIA tisa wa ngumi za ridhaa wanatarajiwa kuiwakilisha Wilaya ya Temeke katika mashindano ya wazi ya ubingwa wa taifa yaliyopangwa kufanyika Februari 26 hadi Machi 5 mwakani jijini, Dar e Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Ngumi za Ridhaa Wilaya ya Temeke (TEABA), Said Omari 'Gogopoa', Kamati ya Utendaji ndiyo iliyofanya uteuzi wa majina hayo.
Omari alisema mabondia hao wanatoka katika klabu mbalimbali wilayani humo ambazo zilishiriki mashindano ya wazi ya ngumi za ridhaa katika ukumbi wa Amana Ilala jijini Dar es Salaam, Desemba 15 hadi 20 mwaka huu.
Omari aliwataja mabondia hao na klabu zao kwenye mabano kuwa ni Seif Ramadhan kilo 60, (Keko), Thomas Benson kilo 56 (Mji Mpya), Mohamed Mnolokela kilo 52 na Salum Mrwanda kilo 56 (Mtoni).
Wengine ni Rashid Mohamed kilo 60 na Joseph Timoth kilo 49 (Keko), Chuki Mohamed kilo 64 (Mtoni), Ismail Isack kilo 56 (Davis Corner), na George Constantino kilo 52 (Polisi).
Alisema, ili timu hiyo iweze kukaa kambini, wamepeleka maombi ya kudhaminiwa kwa wadau mbalimbali wa michezo ikiwemo kampuni inayozalisha maziwa ya Cowbell ambayo iliwapa udhamini alisimia 100 kwenye mashindano yaliyomalizika hivi karibuni.
Omari alitoa wito kwa kampuni na taasisi mbalimbali, kuunga mkono kauli ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi na Mkuu wa Kitengo cha Maabara ya Uchunguzi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, (SACP), Jamal Rwambow, ambaye aliziomba taasisi hizo, kuona umuhimu wa kukuza vipaji vya mabondia wa ngumi za ridhaa, wakati akifunga mashindano hayo.
Rwambow aliipongeza kampuni inayozalisha maziwa ya Cowbell, kwa moyo walionao katika kuendeleza na kukuza vipaji vya mabondia wa ridhaa nchini.
 
Imewekwa:: 2010-12-28 02:31:00
Congo yakimbilia Dar es Salaam
ABDULRAHMAN SHERIFF, MOMBASA
MABINGWA wa Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza nchini Kenya, Congo United ya hapa itapiga kambi ya mazoezi kwa wiki mbili jijini Dar es Salaam kwa matayarisho ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) msimu wa Mwaka 2011.

Meneja wa timu hiyo, Aref Baghazally aliiambia Mwanaspoti mjini hapa kuwa Congo itaondoka mjini Mombasa Januari 17 na itacheza mechi tatu za kirafiki na Simba, Yanga na Azam. Alisema wakati wa kurudi Mombasa, watajaribu kucheza mchezo mnmoja na timu ya mseto ya Tanga.

Congo United ilianzishwa miaka mitatu iliyopita ambapo walianza kushinda ubingwa wa Ligi ya Mkoa wa Pwani mwaka 2008, wakashinda Ligi ya Taifa Daraja la Pili Mwaka jana na mwaka huu wakashinda Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza.


Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
 
Msechu kupeleka 'Hasira Hasara' Bilicanas Jumapili


na Khadija Kalili


amka2.gif
MSHINDI wa pili katika shindano la Tusker Project Fame Peter 2010, Peter Msechu, Jumapili hii atalindima ndani ya ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas katika usiku wa Bongo Stars Nite. Msechu ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha 'Hasira Hasara', katika onyesho la siku hiyo kukiwa bado kuna mashamsham ya kusherehekea mwaka mpya 2011, atatambulisha kibao chake cha 'Majaribu' ambacho amemshirikisha msanii nyota wa kuchana mistari Joh Makini 'Mwamba wa Kaskazini', ambapo kiingilio siku hiyo kitakuwa ni sh. 5,000.
Nyota ya Msechu ilianza kung'ara mwaka 2009 aliposhiriki na kuibuka mshindi wa pili katika shindano la kusaka vipaji hapa nchini la Bongo Star Seach (BSS), linaloratibiwa na Kampuni ya Benchmark Production.
Mbali ya kung'ara na nyimbo zake, Msechu pia ni mahiri katika kuimba nyimbo za 'kukopi' na kucheza muziki, hasa katika miondoko ya Kilingala.
Aidha, kwa mujibu wa ratiba ya Club Bilicanas leo Alhamisi ni usiku maalumu wa kina dada 'Ladies Nite'.
 
Kevin wa BBA, TID wafunika Bills


na Andrew Chale


amka2.gif
MASHABIKI wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake, usiku wa kuamkia jana walipagawishwa na shoo kali iliyoangushwa na msanii Khaleed Mohamed 'TID' ndani ya ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas. Shoo hiyo ya aina yake, ilikuwa maalum kwa ajili ya utambulisho wa albamu mpya ya msanii huyo aliyoipa jina la 'Sifai' huku ikisindikizwa na wasanii nyota Bongo sambamba na mshindi wa kwanza wa Big Brother Revolution, 2009, Kevin Pam.
TID ambaye hupiga shoo kila Jumanne ndani ya ukumbi huo, alifanya kweli wakati wa utambulisho wake huku akikonga nyoyo za mashabiki kwa vibao vyake vipya na vya zamani.
Hata hivyo, mashabiki walionekana kuchizika baada ya TID kuimba wimbo wake wa 'Zeze' huku akiwa na 'shemeji' Kevin jukwaani na kufanya burudani ya aina yake pale alipoingiza maneno ya nyimbo zake.
Kevin ambaye ni raia wa Nigeria, aliyevishana pete na aliyekuwa mshiriki wa Tanzania, Elizabeth Gupta, ana vipaji lukuki ikiwemo uimbaji na utangazaji, aliweza kupagawisha mashabiki kwa kuwaimbisha kwa kibwagizo cha 'Bongo' na mashabiki wakiitikia 'Dar es Salaam' kwa shangwe.
Mbali na Kevin, msanii mwingine aliyepagawisha ni Banana Zoro (kwa nyimbo za 'live' huku akisindikizwa na Top Band), Jafarai, Sam wa Ukweli, Albert Mangwea, Judith Wambura 'Lady Jaydee' na wacheza shoo mahiri.
Uzinduzi wa albamu hiyo ya 'Sifai' kwa TID, unakuwa ni wa nne.
Baadhi ya nyimbo zilizomo ni pamoja na 'Sweetie', Only Me' na 'Dada'.
 
Shameless aionya Yanga
DORIS MALIYAGA
KIUNGO wa Ethiopia Shameles Gordo amewaonya Yanga kuwa wasiizarau Dedebit ambayo watakayokutana nayo mwishoni mwa Januari kwa sababu ni timu iliyo na mafanikio kwenye Ligi ya kwao.

Yanga inakumba na Dedebits katika mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho ikianzia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Shemeles anayeichezea Awasa City ya huko alizua gumzo kwenye michuano ya chalenji iliyomalizika hivikaribuni jijini Dar es Salaam,

��Dedebit ni timu nzuri ina usumbufu sana kwenye Ligi yetu wasipoangalia watawafunga kwa sababu wanacheza mpira wa kutumia sana akili.
 
Mgao wawalostisha wasanii


na Zainab Mlimbila


amka2.gif
MGAO wa umeme unaoendelea nchini kwa sasa umezidi kupigiwa kelele na wadau wa sekta mbalimbali wakiwemo wasanii kutokana na kuathiri kazi zao za kila siku. Kilio hicho kilitolewa hivi karibuni na mmiliki wa studio ya Ngoma Record, Tuddy Thomas, ambaye pia ni muandaaji wa muziki jijini Dar es Salaam.
Tuddy alisema, mgao unaoendelea hivi sasa umeathiri mwenendo mzima wa uandaaji wa kazi za wasanii ambao walikuwa warekodiwe kazi zao mwishoni mwa mwaka huu, jambo linalowafanya wasubiri hadi mwakani.
'Kuna baadhi ya wasanii ambao ilikuwa watengenezewe kazi zao mwaka huu, lakini hawatatengenezewa; itawabidi wasubiri mpaka mwakani na hii ni kutokana na mgao unaoendelea hivi sasa,'� alisema Tuddy.
Aliongeza kuwa mgao uliopo hivi sasa umefanya kazi kuwa ngumu, kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu, si kwa upande wake tu bali anaamini hata kwa watu wengine.
Ngoma Record ni studio inayokuja juu kwa sasa, kutokana na nyimbo bora ilizoziandaa ambazo zinakimbiza katika chati mbalimbali jijini Dar es Salaam na nje ya nchi.
Wasanii ambao nyimbo zao zinafanya vizuri katika chati mbalimbali na zimetayarishwa Ngoma Record ni Mwasiti na 'Kisa siyo pombe'; Amini na 'Ndio unikimbie'; na Linex na wimbo wake wa 'Mama Halima'.
 
Naibu Waziri ataka Stars iendeleze raha

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 30th December 2010 @ 06:54 Imesomwa na watu: 91; Jumla ya maoni: 0


12_10_ez4c30.jpg

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto), akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa Stars alipowatembelea katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Mto Nile kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. (Picha na Yusuf Badi).



WACHEZAJI wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars wametakiwa kutetea hadhi ya taifa kwa kushinda michuano ya Mto Nile kama walivyofanya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika katikati ya mwezi huu.

Wito huo ulitolewa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dk. Fenella Mukangara wakati alipowatembelea wachezaji hao kwenye mazoezi katika Uwanja wa Uhuru.

Fenella aliwataka wachezaji hao kutambua kuwa walililetea heshima kubwa taifa kwa kushinda kombe hilo na hivyo wanalo jukumu la kutetea heshima hiyo kwa manufaa yao na taifa kiujumla.

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ilitwaa Kombe hilo kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 16.

Naibu Waziri Fenella Alisema kuwa kujituma na kucheza kwa bidii ndio itakuwa siri kubwa ya mafanikio kwao na kuongeza kuwa serikali ipo nyuma yao kuhakikisha kuwa hilo linafanikiwa.

Alisema kuwa ni vyema wakatambua kuwa wapo kazini na wanafanya kazi pengine kubwa zaidi kwa kuwa wao wanawakilisha nchi katika ngazi za kimataifa hivyo aliwataka kutambua kuwa wanalo jukumu kubwa mbele yao.

Alisisitiza kuwa serikali kupitia watendaji wake wataendelea kuwatembelea mara kwa mara kwa lengo la kufahamu changamoto zinazowakabili na kuzitatua.

" Najua mimi binafsi naona juhudi zenu katika soka na kama mpenda michezo natambua
namna ambavyo mnajitahidi kuiwakilisha nchi katika kona mbalimbali ya dunia, sasa nina matumaini kuwa katika michuano hii ya Mto Nile kwenu ni kama mnateremka na mtafanya
vema," alisema.

Taifa Stars inatarajiwa kwenda Cairo Januari 2 ambapo Januari 5 itacheza na wenyeji Misri katika michuano hiyo inayoshirikisha nchi za Kenya, Rwanda, Burundi, Kongo, Eritrea, Ethiopia, Sudan na Burundi.

Michuano hiyo ina lengo la kuhamasisha nchi zilizopo kwenye bonde la mto huo kutunza vyanzo vya maji kwa vizazi vijavyo.

Stars itacheza na Sudan Januari 11 na baadaye itamenyana na Kenya Januari 14 na kumaliza kampeni hizo dhidi ya Uganda Januari 17.
 
Naibu Waziri ataka Stars iendeleze raha

Imeandikwa na Evance Ng’ingo; Tarehe: 30th December 2010 @ 06:54 Imesomwa na watu: 91; Jumla ya maoni: 0


12_10_ez4c30.jpg

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto), akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa Stars alipowatembelea katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Mto Nile kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. (Picha na Yusuf Badi).



WACHEZAJI wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars wametakiwa kutetea hadhi ya taifa kwa kushinda michuano ya Mto Nile kama walivyofanya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika katikati ya mwezi huu.

Wito huo ulitolewa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dk. Fenella Mukangara wakati alipowatembelea wachezaji hao kwenye mazoezi katika Uwanja wa Uhuru.

Fenella aliwataka wachezaji hao kutambua kuwa walililetea heshima kubwa taifa kwa kushinda kombe hilo na hivyo wanalo jukumu la kutetea heshima hiyo kwa manufaa yao na taifa kiujumla.

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ilitwaa Kombe hilo kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 16.

Naibu Waziri Fenella Alisema kuwa kujituma na kucheza kwa bidii ndio itakuwa siri kubwa ya mafanikio kwao na kuongeza kuwa serikali ipo nyuma yao kuhakikisha kuwa hilo linafanikiwa.

Alisema kuwa ni vyema wakatambua kuwa wapo kazini na wanafanya kazi pengine kubwa zaidi kwa kuwa wao wanawakilisha nchi katika ngazi za kimataifa hivyo aliwataka kutambua kuwa wanalo jukumu kubwa mbele yao.

Alisisitiza kuwa serikali kupitia watendaji wake wataendelea kuwatembelea mara kwa mara kwa lengo la kufahamu changamoto zinazowakabili na kuzitatua.

“ Najua mimi binafsi naona juhudi zenu katika soka na kama mpenda michezo natambua
namna ambavyo mnajitahidi kuiwakilisha nchi katika kona mbalimbali ya dunia, sasa nina matumaini kuwa katika michuano hii ya Mto Nile kwenu ni kama mnateremka na mtafanya
vema,” alisema.

Taifa Stars inatarajiwa kwenda Cairo Januari 2 ambapo Januari 5 itacheza na wenyeji Misri katika michuano hiyo inayoshirikisha nchi za Kenya, Rwanda, Burundi, Kongo, Eritrea, Ethiopia, Sudan na Burundi.

Michuano hiyo ina lengo la kuhamasisha nchi zilizopo kwenye bonde la mto huo kutunza vyanzo vya maji kwa vizazi vijavyo.

Stars itacheza na Sudan Januari 11 na baadaye itamenyana na Kenya Januari 14 na kumaliza kampeni hizo dhidi ya Uganda Januari 17.
 
Baba wa Mariga apanga timu Simba
DORIS MALIYAGA
NOAH Wanyama ambaye ni baba wa kiungo wa Inter Milan ya Italia, Mc Donald Mariga amemwambia kocha wa Simba Patrick Phiri kama anataka kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa apange kikosi walichoanza nacho kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya FC Leopard ya Kenya.

Kikosi hicho kilikuwa na Juma Kaseja,Salum Kanon, Juma Nyoso, Jerry Santo, Ally Shiboli, Mbwana Samatta, Abdulhalim Humud, Aziz Gilla, Juma Jabu, Shija Mkina na Nico Nyagawa na akasema kama watashirikiana vilivyo watashangaza kwenye Ligi ya Mabingwa.

Wanyama ambaye ni kocha wa FC Leopard "Kikosi hicho ndicho kitamfaa kina ubora japo wanachoka haraka na ulinzi pia ufanyiwe marekebisho lakini cha pili kilikuwa na makosa mengi sana,

��alisema Wanyama akizungumzia kikosi cha pili ambacho waliongezeka Amir Maftah, Rashid Gumbo, Hillary Echessa, Mohamed Banka, Meshack Abel, Kelvin Chale, Mussa Mgosi na Ally Mustapha �Barthez�.


 
Matangalu amkimbia kocha Kagera
OLIVER ALBERT
BEKI Antony Matangalu ameapa kuwa harudi tena kuichezea Kagera Sugar kutokana na mizengwe anayofanyiwa na viongozi wa timu hiyo akiwemo Kocha Mkuu Jackson Mayanja lakini kocha msaidizi Mlage Kabange amedai mchezaji huyo hana nidhamu.

Matangalu ambaye pia aliwahi kuichezea Simba msimu uliopita aliimbia Mwanaspoti kuwa amechoshwa na mizengwe ya baadhi ya viongozi wa timu hiyo na kocha hivyo ameamua ajiondoe.

"Mimi sirudi kuichezea tena Kagera kwenye mzunguko wa pili kwani nimechoka na mizengwe ya viongozi na yule kocha hivyo siwezi kuvumilia bora nikae nyumbani tu.��

��Wao wanasema sina nidhamu, mara nimezoea mjini hivyo siwezi kukaa kijijini mambo yote hayo yanatoka wapi, halafu wanasema wamenisimamisha lakini barua hawajanipa hadi leo hivyo siwaelewi.

��Kabla hata dirisha dogo halijaanza niliwaambia nipeni barua yangu nitafute timu nyingine hawataki wananizungusha tu hadi dirisha dogo limefungwa, hivyo siwaelewi, mimi sirudi tena kwanza mkataba wangu unamalizika ligi ikiisha,�� alisema Matangalu.

Lakini Kabange alisema; "Aseme ukweli wala si kwamba wana tofauti na kocha yeye ndio ana matatizo, hataki mazoezi, akiitwa kambini anachelewa kuja kwa wakati, hivyo uongozi uliamua kumsimamisha na barua walishapeleka hadi shirikisho la soka (TFF)."


 
Ulimboka: Poulsen ameniwekea namba
MWANDISHI WETU
MSHAMBULIAJI mpya wa Majimaji ya Songea, Ulimboka Mwakingwe anatua rasmi leo mjini humo tayari kuanza kazi na amesisitiza kuwa namba yake ipo kwenye timu ya Taifa Stars iliyopo chini ya Jan Poulsen.
Ulimboka amesajiliwa na timu hiyo katika dirisha dogo lililofungwa mwezi Novemba na amesisitiza kuwa anataka kuweka rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kuripoti kambini kabla ya safari ya kwenda Msumbiji Desemba 30.
"Nimepania kufanya mambo makubwa sana katika mzunguko wa pili, ndio maana nimekuwa nikifanya maandalizi makubwa sana ndani ya miezi karibu sita na nitafanya kazi ya ukweli kila mtu ataiona Uwanjani,"alisisitiza.
"Mimi siyo mtu wa kuongea nitafanya kazi uwanjani na nakuhakikishia namba yangu ipo Taifa Stars, nipeni muda tu mtaona mambo yangu. Naamini sana kiwango changu na nikiwa fiti najiona kabisa, hakuna kitu kinachoweza kunizuia kufanya ninachotaka, ndio maana nataka nitulie kabisa."
 
Phiri ‘alilia' nyota wake Stars

Imeandikwa na Issa Yussuf, Zanzibar; Tarehe: 29th December 2010 @ 23:59


KOCHA wa Simba, Patrick Phiri ameendelea ‘kuwalilia' nyota wake waliopo kwenye kambi ya timu ya Taifa, Taifa Stars na kutaka waachiwe ili waungane na wenzao kwenye kambi ya mazoezi Zanzibar.

Simba ipo Zanzibar ikijiandaa na michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari 2, na pia ikijifua kwa ajili ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana, Phiri alisema anahitaji wachezaji wake wanne waliopo kwenye kikosi cha Stars ili waende sambamba na wenzao.

Wachezaji wa Simba waliopo kwenye kambi ya Stars inayojiandaa na michuano maalumu ya mto Nile ni Juma Kaseja, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Ali Ahmed ‘Shiboli' na Rashid Gumbo.

"Zanzibar ni mahali pazuri kwa mazoezi, na tunaendelea vizuri na tunatarajia kufanya vizuri, lakini tumeomba turudishiwe wachezaji wetu mpaka leo kimya, hatujui kama wataruhusiwa au, tungependa tuwe nao wote kwenye mazoezi,"alisema.

"Wanasema kukosekana kwa wachezaji wanne kwenye kambi ya mazoezi Zanzibar hakutaathiri kwenye mashindano yajayo, lakini mara zote ni vizuri kuwa nao pamoja," alisema Phiri.

Tangu kuitwa kwa wachezaji wa Stars kwenye kambi hiyo, uongozi wa Simba na Yanga umekuwa ukipinga na kutaka wachezaji wake kwa madai kuwa TFF inavuruga Programu zao ikizingatia kuwa michuano hiyo haikuwepo kwenye ratiba.

Hata hivyo Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Sunday Kayuni alisema hajapata taarifa rasmi za klabu hizo kutaka wachezaji wake.

Stars inatarajiwa kuondoka nchini kwenda Cairo, Misri Januari 2 kwa ajili ya michuano hiyo itakayoanza Januari 5 ambapo itafungua dimba na wenyeji Misri.

 
Mgosi atetea viatu vya Yanga
OLIVER ALBERT
MSHAMBULIAJI wa Simba, Mussa Hassan Mgosi mwishoni mwa wiki alijikuta katika wakati mgumu mbele ya mashabiki wake kutokana kuvaa na viatu vya rangi ya njano lakini yeye amejitetea.

Simba ilicheza na AFC Leopards Jumamosi na kushinda mabao 2-0 lakini kitendo cha Mgosi kuvaa viatu vya njano ambavyo ni vya rangi ya Yanga kiliwakera mashabiki ambapo .

Mgosi aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ally Ahmed Shiboli, huku mashabiki wakitegemea mabao mengi zaidi lakini ikawa kinyume huku kwavile alikuwa akikosa mabao huku viungo wakimpa pasi ndefu ambazo alishindwa kuziwahi na wakati mwingine akipewa pasi nzuri na kushindwa kumalizia.

Mashabiki hao walisimama na kuanza kumwambia mchezaji huyo avue kwanza viatu alivyovaa kwani ndivyo vilivyokuwa vikimletea nuksi. "Viatu.. viatu hivyo.. vua wewe nani kakwambia uvae hivyo na ndio maana unakosa mabao hovyo," walisikika mashabiki hao pindi mchezaji huyo alipopoteza mpira au akikosa goli.

Baada ya mchezo huo mashabiki hao walimwambia mchezaji huyo asirudie tena kuvaa viatu vya njano na kumuacha Mgosi akiangua kicheko, lakini akaiambia Mwanaspoti kuwa ;

"Sioni kama viatu vinachangia kukosa magoli , ile ni hali ya mchezo tu siku nyingine unafunga na siku nyingine hufungi."
 
Yanga iache kuwa ombaomba
UFA umeibuka katika klabu ya soka ya Yanga kufuatia wachezaji wa Yanga kugomea mazoezi wiki iliyopita na kwa madai mbalimbali ya fedha.

Sakata hili limeibuka wakati kukikwa kuna taarifa za kuwepo kwa mvutano katika uongozi wa timu hiyo.

Hata hivyo, kutokana na fitna za chinichini zilizokuwa zinaendelea kwa muda mrefu ndio maana haikuwa ajabu kuona kilichotokea.

Bahati mbaya mvutano huu ulioibuka umeturudisha kulekule kwenye katika klabu hizi.

Tunapenda kutahadharisha kuwa hatuna upande katika mgogoro huu lakini tumeonya mara nyingi utegemezi wa klabu ya Yanga ndio chanzo cha matatizo haya.

Ukiacha umasikini uliotanda katika klabu hizi, viongozi wake kukosa uadilifu ndio vinarudisha maendeleo ya klabu hizi.

Mgogoro wa klabu wa Yanga kwa kiasi kikubwa umechangiwa na watu kuigeuza `shamba la bibi' kwa nia ya kujisafishia njia kisiasa, kuchuma fedha na kufanya biashara.

Sio siri tena, mgogoro wa Yanga umetokana na uongozi wa klabu kukosa mikakati ya kuinua klabu hiyo kiuchumi na badala yake kumtegemea zaidi mdhamini wa klabu hiyo, Yussuf Manji.

Mgomo huu wa wachezaji umeibuka karibuni baada ya viongozi wa klabu kuwa katika mgogoro na Manji.

Manji, ambaye alitoa mapendekezo mbalimbali katika uongozi lakini pia hivi karibuni aliandika barua kuhoji matumizi ya Sh. milioni 100 alizokopesha klabu hiyo kwenye masuala ya ufadhili.

Fedha hizo inasadikiwa zimesababisha kutoelewana kwa viongozi katika klabu hiyo.

Hali hii haikubaliki kutokana na ukweli kuwa katika siku za usoni inaweza kusababisha uvunjaji wa amani kama ilivyotokea mwaka 1976, Yanga ilipomeguka na kupelekea Pan African kuzaliwa.

Ni ukweli usiofichika kuwa mashabiki wa soka wanapenda kuona klabua Yanga inapiga hatua ndani ya nje ya uwanja.

Ni vyema sasa uongozi wa Yanga ukakaa na wanachama na wa kujadili kwa akina uendeshaji na hata taarifa za mapato na matumuzi.

Hali iliyopo sasa ni hakuna kinachoeleweka kinachoendelea katika klabu ya yanga.

Ni kweli Manji analipa makocha, wachezaji na hata amekarabati jengo la klabu lakini sasa viongozi wa Yanga wanatumia rasilmali hizi.

Uongozi wa klabu unatakiwa kutumia rasilmali zake kuendeleza klabu lakini badala ya Yanga uawa ombaomba.

Ikumbukwe mwanzoni mwaka huu, Manji aligoma kuwasaidia kwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kucheza na Lupopo wakachangiwa na wadau mbalimbali dola zisizodi 5000 ili kufanikisha safari hiyo kutokana na klabu kutokuwa na kitu.

Ndio maana badala ya Yanga kusonga mbele inakuwa ile ile ya mwaka '47.

Mkanganyiko kama huu haupaswi kutokea katika kipindi ambacho nchi yetu iko katika harakati kubwa za kuendesha soka letu kisasa.

Utaratibu wa sasa wa udhamini wa Manji na Yanga hauna tija na ndio maana kinachoonekana ni nguvu nyingi zinaelekezwa na ndio maana umetokea mgomo kutokana na viongozi kutotumia rasilimali vizuri.

Klabu hizi kubwa za Simba na Yanga zimekuwa zikikumbatia watu wanaojiita wadhamini au wafadhili tangu miaka ya 1970 lakini matokeo yake wamekuwa wakizitumia kama ngazi ya kufanikisha ndoto zao za kisiasa au kibiashara na kuziacha bila uwezo wa kujiendesha.

Mageuzi kwa mfano ya Yanga yanatakiwa yawe katika kutumia rasilmali zake vizuri na kuachana na kupigia magoti wafadhili.

Pia kuhakikisha zinawekwa katiba ambazo zinasaidia kuwepo uwajibikaji kwa viongozi wanaovunja katiba kwa kukwepa kuitisha mikutano, kuficha taarifa za mapato na matumizi ya fedha na hata kukwepa kuitisha uchaguzi.

Ndio maana baada ya mgomo huu, viongozi wa yanga wanatakiwa kutafakari kwa makini mustakabali wa klabu hiyo na ajenda lazima iwez kuipeleka kujitegemea.
 

Ligi Vijana: JKT Ruvu 2- Kagera Sugar 0


Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 29th December 2010 @ 23:40


TIMU ya vijana ya JKT Ruvu jana iliiadhibu timu ya Kagera Sugar mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi ya Vijana chini ya miaka 20 uliochezwa kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam.

Katika mchezo huo JKT ilionekana kuutawala zaidi ambapo dakika ya 11 mchezaji wake Suleiman Bofu aliiandikia timu yake hiyo bao la kwanza baada ya kuwatoka wachezaji wa Kagera Sugar kabla ya kufunga.

Mchezaji wa JKT Mohamed Amza dakika ya 21 alitumia vyema nafasi aliyopewa ya kupiga mpira wa adhabu ambapo aliachia shuti la mbali lililompita kipa wa JKT Husein Rashen na kujaa wavuni.




Katika mchezo huo wa jana ambao pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Vijana na Michezo Dk. Fellen Mukangara pamoja na wadau wengine wa michezo, Kagera Sugar ilijitahidi kushambulia bila ya mafanikio.

Mchezaji wake Said Kabenga alipiga shuti kali dakika ya 32 na likagonga mwamba na pia mchezaji mwingine Judson Kanywea naye alibakia na kipa na kupiga shuti lililotoka nje.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom