Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #2,101
MSANII nyota wa muziki wa Injili nchini, Boniface Mwaitege amekiri kuwepo kwa baadhi ya wasanii ambao wamekuwa na tabia ya kutoa taarifa mbaya kwa lengo la kuwachafulia wengine wakiwa na lengo la kuharibu heshima waliyojijengea kwa jamii.
Akizungumza na Starehe msanii huyo ambaye aliwahi kutamba na kibao chake cha kwanza cha �Utanitambuaje� anabainisha kwamba kitendo kama hicho kinachofanywa na baadhi ya wasanii hakimpendezi Mungu kwani ni kuchafuliana tu majina.
�Kitendo cha baadhi ya wasanii, kutoa taarifa ambazo sio sahihi kwa watu na watu hao ..huzisambaza bila kufanya uchunguzi ni kuchafuliana majina tu na si kingine,�anasema Mwaitege
Anaongeza kuwa, mbali na kuwachafua wasanii pia huathiri mashabiki hususani wanaoishi vijijini ambao wengi wao hawajui kutofautisha gazeti la udaku na �siriazi�.
�Hivyo wanapoipata taarifa kama hiyo, imevumishwa kwenye vyombo vya habari anaichukua kama ilivyo na kuanza kuifanyia kazi na matokeo yake anakata tamaa ya kukusikiliza,� anasema
Pia anafafanua kuwa, kitendo hicho kinapoteza mashabiki kwa wasanii kwasababu wao ndiyo wanaowafanya wasanii kupata chochote, hivyo anaposikia taarifa mbaya kutoka kwako anapunguza ushabiki kwako.
�Hususani wanaoishi maeneo ya vijijini, ambapo wanaweza wakakuona hauko siriazi na kazi unayoifanya, kumbe ni hujuma tu! zinazofanywa na baadhi ya wasanii kwa lengo la kukushushia kiwango,� anasema
Msanii huyo anaongeza kwa kuwataka wale wote wanaopokea taarifa mbaya za uvumi kutoka kwa wasanii, bila kufanyia uchunguzi ni kubeba mzigo wa lawama kwa watu, na kwamba wasipoangalia na kuwa makini wataendelea kupokea taarifa za majungu bila kujijua.