Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #3,521
Binamu Muziki bado haujatutendea haki Friday, 21 January 2011 20:37
Minael Msuya
MSANII maarufu wa bongo katika tasnia ya muziki nchini Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana F.A, Binamu amesema serikali ikizingatia utaratibu wa soko katika masuala ya muziki itasaidia kuitangaza Tanzania katika nchi nyingine.
Mwana F.A ambaye alijinyakulia tuzo ya msanii bora wa miondoko ya hip hop ya Kilimanjaro 2003, kufuatia kibao chake cha ‘Alikufa kwa ngoma' kufanya vizuri, anasema pamoja na ukongwe wa muziki wa kizazi kipya bado haujawekewa mazingira ya kuwanufaisha wasanii wake.
Akizungumza na starehe Mwana F.A anasema muziki ulianza zamani lakini sasa unatumika katika siasa na kwamba bado mazingira ya soko katika tasinia hiyo hayajaboreshwa.
"Muziki ulianza tangu zamani na ulikuwa unapokelewa na watu wachache sana lakini sasa hivi unatumiwa hadi kwemye siasa, viongozi wanatakiwa kuboresha mazingira mazuri ya kuuzia ili tuweze kupata faida kwa sababu mimi nasema mziki kwangu ni maisha," anasema.
Mwana F.A anasema pia viongozi wakiboresha mazingira ya soko itasaidia kuitangaza nchi katika nchi zingine duniani na kuwa itakuza uchumi wake vizuri.
Aidha Mwana F.A anasema anajaribu kuangalia soko la kimataifa ili kuimarisha sekta hiyo ambapo ataanzana nchi ya Kenya na Uganda na Tanzania ambako anatarajia kufanya kazi na wasanii mahiri kama , Wyre, Amin, Jose Chameleon na Navio.

PRINT