Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Serikali yafagilia kozi ya FIFA


Na Zahoro Mlanzi

SERIKALI imeifagilia kozi inayoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ya uandaaji wa matukio iliyofungiliwa jana, Dar es Salaam.
Programu hiyo imeingizwa katika kalenda ya FIFA mwaka huu na ilizinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Vijana na Michezo, Emmanuel Nchimbi ambayo inashirikisha Makatibu wa klabu, Mameneja wa Uwanja na Wadhamini wa soka.

Kabla hajafungua kozi hiyo, Nchimbi aliizungumzia program hiyo baada ya kupata muktasari kutoka kwa Ofisa Maendeleo wa FIFA, Ashford Mamelod juu kozi hiyo na kusema itafungua njia ya kutatua migogoro ya mara kwa mara ndani ya klabu nchini.

"Siku zote serikali itaendelea kujipanga kuinua soka na kama baada ya kozi hiyo timu zikijipanga vizuri katika kuandaa matukio kama michezo ya kirafiki, Ligi Kuu na mingine hakika mapato yatakuwa makubwa," alisema Nchimbi.

Alisema mafunzo yatakayotolewa ni lazima yafanyiwe kazi na si kuyaacha katika mabegi yao waliyokuja nayo, kama vitendo vitafanyika hakika migogoro haitakuwepo kwani kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.

Waziri huyo alisema kutokuwa na elimu ya uandaaji wa matukio ndiyo chanzo cha migogoro inayotokea katika klabu mbalimbali nchini, lakini aliongeza kozi hiyo itasaidia kuondoa migogoro hiyo.

Kabla ya Nchimbi kuzungumza, Mamelod alielezea juu ya umuhimu wa kozi hiyo, ambapo alisema itasaidia klabu kuandaa mechi vizuri huku zikijua usalama wa mashabiki, tiketi na mambo mengine yanayohusu mechi jinsi inavyotakiwa kuandaliwa.

Alisema kozi hiyo ndiyo imezinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam na sasa itaendelea kufanyika katika nchi wanachama wa FIFA na kwamba ana imani Tanzania, itakuwa ya kwanza kupata maendeleo ya soka kupitia programu hiyo.

Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga aliishukuru FIFA kwa kuleta kozi hiyo kwa mara ya kwanza nchini na kwamba itasaidia kuzikomboa klabu katika janga la kupata mapato madogo.
 
Wasanii watunga nyimbo kunadi Kili Music Awards


Na Elizabeth Mayemba

WASHINDI wa Tuzo za Kilimanjaro Music Awards wa mwaka jana, wametunga wimbo wa pamoja ambao utaanza kurushwa kwenye vituo vya televisheni na
redio kwa ajili ya kunadi tuzo za mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Geoege Kavishe alisema tuzo za mwaka huu zimeboreshwa kwa hali ya juu na mchakato wa kupata nyimbo bora unafanywa na watu maalumu ambao wameweka rekodi za kazi zote zilizofanywa na wasanii mwaka jana.

"Mwaka jana tuzo hizi za muziki zilifanyiwa mabadiliko makubwa, ambayo yataendelezwa na kuboreshwa zaidi mwaka huu, mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia katika hatua mbalimbali," alisema Kavishe.

Alisema hatua mojawapo ni Academy yenye mkusanyiko wa wadau wa muziki 100 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimaye kupata wateule wa vinyang'anyiro mbalimbali na kwamba utaratibu huo haujabadilika ambao mwaka huu utafanyika Februari 12 na 13 mwaka huu.

Pia majaji watakuwa na kazi moja kubwa ya kuhakiki uteuzi wa wateule uliofanywa na Academy hiyo, ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi na kwamba wao hutumia zaidi vigezo halali vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka jana.
 
Barca, Milan zaongoza kwa pointi nne Tuesday, 25 January 2011 00:07

MADRID, Hispania
BARCELONA na AC Milan zote zimeshinda na kuendelea kuongoza ligi za Hispania na Italia kwa pointi nne, huku Pep Guardiola akiweka historia ya kushinda mechi 14 mfululizo za La Liga.

Vinara Barcelona wameendeleeza wimbi la ushindi kwa kushinda mechi14, wakati waliposhinda 3-0 dhidi ya Racing Santander, kabla ya washindi wa pili Real Madrid kupunguza tofauti ya pointi na kubaki nne waliposhinda 1-0 dhidi ya Real Mallorca juzi Jumapili. Mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema alianzishwa kwenye mchezo huo na kocha Jose Mourinho na kuifungia Real bao pekee na goli lake la pili msimu huu.

Pedro, Lionel Messi na Andres Iniesta walifunga kwa Barca wakati vijana hao wa Pep Guardiola wakifikia rekodi ya kushinda mechi 14, waliyowahi kuweka chini ya Frank Rijkaard wakati walipotwaa taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa msimu wa 2005-6.

Mshambuliaji wa Italia, Giuseppe Rossi alifunga mabao mawili kwa Villarreal iliposhinda 2-1 dhidi ya Real Sociedad na kupanda hadi nafasi za tatu juu ya Valencia, wakiwa nyuma kwa pointi tisa kwa Real. Valencia ilichapa Malaga 4-3 Jumamosi.

Nchini Italia, AC Milan wameendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi nne baada ya kupata bao la zawadi kwa kujifunga na lile Zlatan Ibrahimovic walipotoka kifua mbele kwa 2-0 dhidi ya Cesena, huku Napoli nayo ikiendelea kukimbilia usukani kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Bari.

AS Roma imepanda hadi nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Cagliari, lakini majirani zao Lazio walipoteza nyumbani kwa kulala 3-1 kutoka kwa Bologna.

Mabingwa watetezi, Inter Milan walipokea kipigo cha kwanza cha mabao 3-1kutoka kwa Udinese tangu alipoanza kufundishwa na Leonardo kwenye michezo sita na kuwafanya wabaki nafasi ya tano wakiwa nyuma kwa pointi tisa kwa vinara.

 
Kaseja akiri kukosea Tuesday, 25 January 2011 00:13

Clara Alphonce
Kipa wa Simba, Juma Kaseja amekiri kufanya makosa yaliyosababishwa wakafungwa na Azam, lakini hamewataka mashabiki wasitafute mchawi kwa matokeo hayo zaidi ya kujipanga upya.

Simba ilifungwa mabao 3ñ2 na Azam FC juzi Jumapili huku magoli mawili yakifungwa kutokana na Kaseja kutokea mipira na kuwafanya mashabiki kudai kuwa amefungwa kizembe na ikibidi apumzike kudaka.

Kaseja alisema kuwa kupoteza mchezo wao dhidi ya Azam hakuna mtu ambaye hajaumia kwani ulikuwa ni mchezo muhimu, lakini siku zote mtu anafungwa kutokana na makosa waliyoyafanya wao katika mchezo huo ndio uliwapa Azam ushindi.

''Najua mengi yataongelewa, lakini hata mimi sijafurahia kufungwa ila kinachotakiwa Wanasimba wote tuelekeze mawazo yetu katika michezo ijayo kwani tukikaa na kujadili mchezo uliopita utafanya tufanye vibaya hata katika michezo iliyopita'' alisema.

Alisema sio wao pekee ndio walifanya makosa kwani hata Azam nao walifanya makosa ndio maana walipata magoli mawili japo kwa kweli wao walikuwa wakicheza chini ya kiwango japo aliongeza kuwa siku hazifanani juzi mpira haukuwa wao.

Hata hivyo aliongeza kuwa kufungwa na Azam katika mchezo wa kwanza hakujawakatisha moyo ya kuchukua ubingwa kwani bado michezo 11 ambayo wataitumia vizuri kuakikisha hawarudii makosa.

Timu hiyo ya Simba inaondoka kesho kwenda visiwa vya Comoro kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa Januari 29.
 
Mwape awapa raha Yanga

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 25th January 2011 @ 08:10

DAVIES Mwape jana alifunga mabao yaliyoipa Yanga ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Dodoma katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabao hayo ambayo moja alifunga kila kipindi yamemfanya aanze kuonesha umuhimu wake uliomfanya Kocha Mserbia Kostadin Papic kumsajili kwenye dirisha dogo mwezi uliopita aimarishe safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Mabao hayo ya jana yanamfanya afikishe mabao matano katika mechi mbili alizocheza, ambapo ya kwanza ilikuwa Ijumaa iliyopita alipopachika mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-1, ambao Yanga iliupata dhidi ya AFC Arusha.

Mwape raia wa Zambia sasa ameanza kuwapa tumbo joto washambuliaji wa Tanzania wanaofukuzia ufungaji bora katika ligi hiyo, ambapo anayeongoza ni Gaudence Mwaikimba wa Kagera Sugar mwenye mabao nane na Mrisho Ngasa wa Azam mwenye mabao saba.

Jerry Tegete wa Yanga anashika nafasi ya tatu akiwa na mabao sita, huku Mussa Mgosi wa Simba na Revocatus Maliwa wa Ruvu Shooting wenyewe wakiwa na mabao matano mkononi sawa na Mwape.

Kutokana na ushindi huo wa jana, Yanga sasa imefikisha pointi 31 na kuendelea kuongoza ligi hiyo ikiwa mbele kwa pointi nne dhidi ya mtani wake wa jadi Simba ambaye anashika nafasi ya pili baada ya juzi kufungwa mabao 3-2 na Azam katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.

Katika mchezo wa jana Polisi ilijitahidi kucheza kwa nguvu na kuwabana washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Tegete, Idd Mbaga na Mwape, lakini safu yao ya ushambuliaji yenyewe ilishindwa kutumia nafasi ilizozipata.

Baada ya kosakosa za hapa na pale, yanga ilipata bao la kuongoza dakika ya 43 mfungaji akiwa Mwape kwa shuti lililompita kipa Salum Kondo.

Washambuliaji wa Yanga waliendelea kuliandama lango la Polisi Dodoma inayonolewa na Kocha John Simkoko, lakini umaliziaji ulikuwa dhaifu.

John Kanakamfumu, Elias Mashaka na Salmin Kissy wa Polisi walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini nao walishindwa kuzitumia. Mwape alifunga bao la pili dakika ya 80 kwa shuti la mbali, lililoibua shangwe kwa mashabiki wa Yanga waliokuwa wakiimba wakitaja jina lake.

Mchezo huo uliingia dosari katikati ya kipindi cha pili baada ya mchezaji wa Polisi Elias Maftah kuzimia uwanjani baada ya kuanguka katika harakati za kuokoa mpira, hivyo kulazimika kupatiwa huduma ya kwanza na kisha kukimbizwa hospitali.

Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic ambaye jana alikaa benchi pamoja na Kocha Msaidizi Fred Minziro ambaye alikuwa hamtaki, alisema baada ya mchezo kuwa ulikuwa mzuri na kwamba vijana wake walicheza mchezo wa kuvutia.

Kwa upande wake Simkoko alisema vijana wake walicheza vizuri, lakini bahati haikuwa yao na watajipanga kwa michezo mingine.

Wakati huohuo, katika tukio la kushangaza jana mwamuzi wa akiba alikuwa akibadilisha wachezaji kwa kutumia karatasi badala ya vibao kama ilivyozoeleka.

Tukio hilo lilifanya kila wakati mchezaji alipokuwa akitaka kuingia uwanjani mashabiki kuzomea huku wakiimba: "TFF TFF", ambalo ni Shirikisho la Soka Tanzania.

Licha ya karatasi hizo kutoonekana namba zake kwa mashabiki, lakini pia hata wachezaji wenyewe walikuwa hawazioni na kushindwa kutambua kwa haraka nani anayetoka.
 
TSA hatuna taarifa Tuesday, 25 January 2011 00:12

Imani Makongoro
CHAMA cha Kuogelea Tanzania (TSA) kimesema kuwa kinasubili barua kutoka Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ili kujua kinatakiwa kupeleka waogeleaji wangapi katika mashindano ya Michezo ya Afrika (All Africa Game).

Michezo hiyo ambayo ufanyika kila baada ya miaka minne imepangwa kufanyika mapema mwezi Septemba mjini Maputo, Msumbiji na kushirikisha wanamichezo mbalimbali kutoka nchi za bara la Afrika ikiwamo Tanzania.

Tanzania ambayo imeanza kushiriki katika mashindano hayo miaka 46 iliyopita na kufanikiwa kutwaa medali 22 ikiongozwa na Ethiopia yenye Medali 1065, itawakilishwa na wanamichezo ya Riadha, Kuogelea, Ngumi, Mpira wa Meza, Paralimpiki na mingine mingi.

Katibu Mkuu wa TSA, Noel Kiunsi, aliiambia Mwananchi kuwa wao wanasubili barua ya TOC ili waweze kuandaa timu ya mchezo huo kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo makubwa.

"Hatuna taarifa kutoka TOC, ila mashindano tunajua yapo, sisi hatuna fedha kwa ajili ya timu kushiriki mashindano hayo, endapo tukiambiwa tupeleke majina ya washiriki wakati wowote kwenye kamati ya Olimpiki basi tutapeleka.

"
Michezo ya Afrika, Olimpiki na ile ya Jumuiya ya Madola sisi haituhusu hivyo hatuwezi kuisemea, tunaweza kuisemea Fina kwa kuwa inatuhusu, hivyo tunasubili taarifa tu," alisema Kiunsi.

Hata hivyo hivi karibuni TOC walivitaka vyama kutafuta wadhamini kwa ajili ya michezo ya Afrika wakidai kuwa hakuna fungu linalotoka Umoja wa Afrika (AU) ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo kwa ajili ya maandalizi ya michezo hiyo.

Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, alisema kuwa wao wamepeleka bajeti yao Serikalini hivyo wanasubili jibu.
 
Wachezaji Azam wapongezwa kwa Sh10mil
Tuesday, 25 January 2011 00:09

Doris Maliyaga
UONGOZI wa Azam FC, umewazawadia nyota wake milioni 10 kama zawadi ya ushindi baada ya kuwafunga mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Bara Simba katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa.

Mbali na fedha hizo, uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa nusu ya mapato ya mlangoni, yatakwenda kwa wachezaji. Azam FC kwa mara ya kwanza iliifunga Simba mabao 3-2.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Said Mohamed ameliambia Mwananchi kuwa, wachezaji hao watapewa pesa hizo mapema.

ëíTumewapa milioni 10, kama motisha itakayowaongezea hamasa ya kufanya vizuri katika mechi nyingine zijazo, lakini pia watapata nusu ya pesa za mapato zilizopatikana Uwanjani katika mchezo huo,ííalisema Mohamed ambaye timu yake inashinda kwa mara ya kwanza na mechi ya mzunguko wa pili baada ya kupoteza kwa Kagera Sugar.

Kocha wake mkuu, Stewart Hall alisema kuwa: "Azam iliyoifunga Simba ni ile ile, tumeshinda kwa sababu timu iliingia ikiwa inajiamini ikicheza mchezo mzuri.íí

"Hata hivyo bado tuanendelea kuiandaa ili icheze kitimu zaidi na ushinda kwa ajili ya mechi nyingine zijazo,íí alisema Hall ambaye pia ni kocha wa timu ya Taifa ya ëZanzibar Heroesí.


 
Kaseja awaomba radhi mashabiki Simba

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 24th January 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 353; Jumla ya maoni: 1


01_11_0t0tyx.jpg

Juma Kaseja





KIPA mahiri nchini Juma Kaseja amesema tukio la timu yake ya Simba kufungwa mabao 3-2 na Azam FC katika Ligi Kuu Tanzania Bara juzi limemnyima raha na kuwaomba mashabiki wamsamehe kwa kosa alilofanya ambalo lilizaa bao la tatu kwa Azam.

Akizungumza jana, Kaseja alisema hata yeye hapendi kufungwa, lakini soka ndivyo lilivyo na kuwaomba mashabiki wake kuwa wavumilivu kipindi hiki kigumu.

"Daima nimekuwa mstari wa mbele kucheza kwa nguvu zote kuitetea Simba, kuna wakati nilicheza hata nikiwa mgonjwa yote kuhakikisha Simba inashinda.

"Mimi ni mwanadamu, nilifanya kosa la kibinadamu nilikuwa katika harakati za kutaka kuhakikisha sifungwi, ndipo nikawahi kutoka langoni nikapishana na mpira.

"Yapo mambo mengi yanasemwa sasa, si mazuri, yanakatisha tamaa, naomba mashabiki wa Simba wanielewe na nawaomba radhi kwa kosa la kimchezo nililofanya," alisema Kaseja.

Kaseja alifanya kosa lililozaa bao la tatu dakika ya 54 kwa Azam baada ya kutaka kuuwahi
mpira wa juu ambao beki Juma Nyoso alikuwa akiuwania na mshambuliaji John Bocco, lakini baada ya Kaseja kutokea na kuliacha lango wazi Bocco aliinua mpira juu na kutinga wavuni.

Kabla ya hapo mshambuliaji Mrisho Ngasa wa Azam naye alifunga bao la pili dakika ya 23 baada ya kumpiga chenga Kaseja aliyekuwa ametoka langoni.

"Nimehuzunishwa sana na matokeo mechi ya Azam, kama kuna mtu aliumia basi mimi ilikuwa zaidi, lakini sina jinsi soka ndiyo ilivyo," alisema kipa huyo ambaye Desemba mwaka jana aliibuka Kipa Bora wa michuano ya Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

 
Terry: Chelsea can still win the title




9 comments »

Updated Jan 24, 2011 7:29 PM ET
Chelsea captain John Terry has refused to concede the Barclays Premier League title to Manchester United.
The Blues were convincing 4-0 winners over Bolton at the Reebok Stadium, with Didier Drogba, Florent Malouda, Nicolas Anelka and Ramires getting the goals.


The result leaves Carlo Ancelotti's team seven points behind leaders Manchester United having played a game more.
But the current champions have yet to face United - and Terry believes wins in those two matches could prove decisive in the title race.
The England defender told Sky Sports: "In the past we've never given up.
"Manchester United are playing well at the moment and getting the right results, maybe getting a bit of luck too.
"But things can change and if we can win both games against them we'll be right back in it."
Terry continued: "Away from home, at times we have shown very good form this season but tonight everything went really well for us.
"Didier got us off to good start with probably the best goal of this season so far and we worked really hard all over the park. We stopped Bolton playing and it worked for us."
Ramires' goal was his first for the club and Terry added: "The lads are delighted for him.
"He has settled in well and although he is still struggling with the language he's a good lad who works really hard. He's found his feet now and hopefully he can keep going."
Drogba, whose goal was a long-range swerving effort which flew over Bolton goalkeeper Jussi Jaskelainen, said: "I was in a good position to have a good so I took my chance - I had the confidence to try.
"You have to try if you want to score and the manager said 'shoot if you have a chance'. Maybe I have been thinking too much about things before."
On another title, the Ivory Coast international striker added: "I think it would be the best achievement in my six years here - but we have to think of the next game.
"It's good we are playing Manchester United twice - but we will have to win all our games and see what happens."
 
Ngassa aliongoza kuchezewa rafu
Tuesday, 25 January 2011 00:10

Calvin Kiwia
LICHA ya mabingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, kufungwa na Azam FC mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Wekundu hao wa Msimbazi waliongoza kwa kucheza rafu na kufika langoni mwa Azam.

Mshambuliaji Mrisho Ngassa wa Azam FC aliongoza kwa kuchezewa rafu nyingi na mabeki wa Simba akiwa amechezewa rafu tisa kati ya 17 walizocheza wekundu hao.

Pamoja na kufungwa huko Simba waliongoza kwa kufika langoni mwa Azam wakifika mara 19 na kufanikiwa kupata kona 10 ambazo hazikuwasaidia kusawazisha mabao hayo.

Azam kwa upande wao, walifika langoni kwa Simba mara 14 na kupata kona tatu ambazo bado hazikuwa na faida kwao.

Simba iliweza kutoa mipira nje ya uwanja mara 27 wakati Azam ilitoa mara 21, beki wa Simba Amir Maftar aliongoza kwa kutoa mipira nje akiwa ametoa mara 11 dhidi ya 27 walizotoa Wekundu hao.

Viungo wa Azam, Abubakar Salum 'Sure', Ramadhan Chombo na Ibrahim Mwaipopo walishirikiana vema kwenye safu ya kiungo ya Azam na kuifanya timu hiyo kupiga pasi 39 bila kuguswa na mchezaji wa Simba.

Winga wa kushoto wa Azam Jamal Mnyate aliongoza kwa kuotea akiwa ameotea mara tatu huku John Boko akiwa ameotea mara mbili wakati wapinzani wao Simba waliotea mara mbili.
 
Nchimbi awapa somo viongozi wa soka Dar es Salaam

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 24th January 2011 @ 23:50

VIONGOZI wa soka nchini wametakiwa kutumia vema mafunzo ya uandaaji wa matukio ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati akifungua semina ya uandaaji wa matukio iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Nchimbi alisema mafunzo hayo yanasaidia kuimarisha uwezo wa klabu na vyama vya soka kujua namna ya kuendesha sekta hiyo kiumakini.

Alisema elimu hiyo pia inawawezesha kujua namna ya kuendesha michuano mbalimbali wanayoiandaa na hivyo kuzuia kero mbalimbali kujitokeza.

Alisema mafunzo hayo yanawapatia uwezo wa kufahamu namna ya kujiongezea kipato kwa kuwa yanawapatia mbinu za kuandaa matukio kiutaalamu zaidi.

Pia aliwataka wadhamini wa michezo nchini kuhakikisha kuwa katika bajeti zao wanatenga fungu maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa viongozi wa soka kuhusiana na elimu ya uendeshaji na uandaaji wa matukio.

Naye msimamizi wa shughuli za Fifa kwa kanda ya Kusini mwa Afrika, Ashford Mamelodi alisema mafunzo hayo ni ya kwanza na ya aina yake kwa Afrika na Dunia nzima kiujumla.

Alisema suala la namna ya kuandaa matukio hususan ya soka ni muhimu kwa kuwa kwa muda mrefu baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikizikabili klabu nyingi hasa za Afrika ni namna ya kuendesha matukio kama hayo.

Naye Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema mafunzo hayo ya siku nne yamewashirikisha wadau wa soka 30 kutoka ndani na nje ya nchi.

Alisema wanafundishwa masuala ya namna ya kuandaa matukio kuanzia masuala ya protokali, namna ya kuvihudumia vyombo vya habari, wachezaji, viongozi na masuala mengine muhimu.

 
Mashindano ya gofu Nahodha kusogezwa mbele

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 24th January 2011 @ 23:45


MASHINDNO ya gofu ya Mwezi Januari ambayo yameshindwa kufanyika mwezi huu yamesogeza mbele mashindano ya Nahodha kwenye klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu wa gofu klabuni hapo Lawrence Pangani mashindano ya mwezi Januari sasa yamepangwa kufanyika Februari 12 ambayo awali ilikuwa yafanyike mashindano ya Nahodha.

Kutokana na mabadiliko hayo mashindano ya Nahodha ambayo awali yalikuwa yafanyike tarehe hiyo yamesogezwa mbele kwa wiki moja.

Pangani alisema kusogezwa mbele kwa mashindano ya Januari kuna lengo la kuwapa muda wa kutosha kujiandaa wadhamini wa mashindano hayo kampuni ya Zantel.

Itakuwa ni mwezi wa tatu kwa Zantel tangu kuanza kudhamini mashindano hayo ya kila mwezi baada ya kufanya hivyo mwezi Novemba na Desemba mwaka jana na washindi kuzoa zawadi nono ikiwa pamoja na simu za mkononi aina ya blackberry.

Pangani alisema mashindano ya Nahodha yatafanyika kwa siku mbili Februari 19 na 20 kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa viongozi wa gofu klabuni hapo Februari 23.

Mashindano ya nahodha yanafanyika kwa heshima ya nahodha anayemaliza muda wake
ambaye kwa sasa ni Joseph Tango.

Tango alisema mabadiliko hayo ni mazuri kwani ni vema kufanya mashindano yake siku ya mwisho kabla ya uchaguzi ili kufunga vema utawala wake.

Uchaguzi mkuu wa kamati ya gofu klabuni hapo hufanyika kila baada ya mwaka mmoja.
 
Berbatov, Van Persie, Gomez, Fabiano wazee wa tatu
Tuesday, 25 January 2011 00:08

PARIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Dimitar Berbatov aliongoza ufungaji wa mabao Ulaya pamoja na Arsenal, Robin van Persie, Mario Gomez wa Bayern Munich na Luis Fabiano wa Sevilla.

Nyota huyo wa Bulgaria, Berbatov alifunga kwa mara ya tatu magoli matatu katika mechi moja msimu huu waliposhinda 5-0 kwenye Old Trafford dhidi ya Birmingham na kumfanya kufikisha magoli 18, na kuiweka United kileleni mwa Ligi Kuu.

Wakati nyota huyo akiendela kupaa kwenye ufungaji nayo United imezidi rekodi yake ya kutokufungwa mechi 21hadi sasa.

"Dimitar anaelekea kufunga mabao 20 msimu huu jambo ambalo ni muhimu kwetu," alisema bosi wa United, Sir Alex Ferguson.

Mabao hayo matatu ya Berbatov yanamfanya kufikia rekodi ya Ruud van Nistelrooy aliyoiweka alipokuwa akicheza hapo msimu wa 2002-2003 alipofunga mara tatu mabao tatu katika msimu.

Bado mara mbili tu amvunje rekodi iliyowekwa kwenye Ligi Kuu ya kufunga mabao matatu katika mechi tano msimu mzima na mkongwe Alan Shearer mwaka 1995-1996.

Mchezaji Denis Law ndiye anayeshikiria rekodi ya kufunga mara saba mabao watatu katika msimu moja kwa United ilipokuwa ikishiriki Ligi Daraja la kwanza msimu wa 1963-64.

"Dimitar anauwezo wa kutimiza lengo lake," alisema Ferguson. "Wachezaji wengine wanatakiwa kufikiri pia. Ni wachezaji wanaocheza naye. Ni mchezaji wa kiwango cha pekee."

Van Persie kwa sasa ameshafunga mabao sita katika ligi baada ya muda mrefu wa kusumbuliwa na majeruhi, Jumamosi alipofunga mabao matatu waliposhinda 3-0 dhidi Wigan na kuifanya Arsenal kuisogelea United.

Mholanzi huyo nusura afunge bao la nne, lakini alikosa penalti.
Van Persie amerudi kwenye kiwango chake baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu akisumbuliwa na tatizo la kifundo cha mguu, lakini kocha Arsene Wenger amesisitiza mshambuliaji huyo asitegemee kucheza kila mechi.

"Amerudi kwenye kiwango chake," alisema Wenger. "Kwa sasa yupo fiti na mwepesi.

"Ni jambo zuri kuwa naye, lakini tunawachezaji wengi majeruhi hivyo ni kazi yetu kuhakisha tunamtunza na aendelee kuwa fiti hadi mwisho wa msimu na tutakuwa tukimtumia kwenye michezo muhimu zaidi kwetu.

Nchini Ujerumani, Gomez amepanda kileleni kwa wafungaji akiwa na mabao 15, baada ya kufunga magoli matatu na kuisaidia Bayern Munich kuishinda 5-1 dhidi ya Kaiserslautern hata hivyo mabingwa hao watetezi wamebaki nyuma kwa pointi 14 kwa vinara wa ligi Borussia Dortmund.

"Hii ni kazi yangu, najua hili ndio jukumu langu hapa," alisema Gomez mwenye miaka 25.

Mshambulaji wa Brazil, Fabiano alifunga mabao matatu waliposhinda 4-1 dhidi ya timu ya mkiano Levante na kumfanya afikishe mabao nane msimu huu.

Fabiano, ambaye mwanzoni mwa mwezi huu alikuwa mchezaji wa tano wa Sevilla kufunga mabao100 akiwa na klabu hiyo.

Kasi yake ya ufungaji inaifanya timu yake kuwa kwenye wakati mzuri zaidi hapo kesho wataposhuka kwenye nusu fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Real Madrid.

"Kila mchezo kwa sasa ni kama fainali tunataka kuendelea kucheza kama hivi," alisema Fabiano.

"Utakuwa ni mchezo wa kuvutia dhidi ya Real Madrid, tunataka kwenda kwenye mechi hiyo na kupata ushindi ili tuweze kutetea ubingwa wetu.

"Ni timu bora, lakini tutawafunga na kuwaacha Madrid msimu mwingine wakiwa mikono."
 
Roger Federer crushes Stanislas Wawrinka in Melbourne


Australian Open, Melbourne
Venue: Melbourne Park Dates: 17-30 January
Coverage: Watch on BBC TV, Red Button, BBC Sport website (UK only) & Eurosport; listen on BBC 5 live sports extra and online; text commentary online; full details

_50933927_011105153-1.jpg
Federer has now won seven of his eight meetings with Wawrinka


Defending champion Roger Federer marched into the Australian Open semi-finals with an emphatic 6-1 6-3 6-3 win over fellow Swiss Stanislas Wawrinka.
Federer broke the underwhelming Wawrinka in his first service game and took the opener inside 30 minutes.
Nineteenth seed Wawrinka squandered a chance to break in the sixth game of the second and was soon made to pay.
Federer claimed the next three games before making a solitary breakthrough in the third game of the final set.
The world number two will face either Tomas Berdych or Novak Djokovic in his eighth appearance in the final four of the tournament, and if he serves as well as he did in the quarter-final he will be a hard man to stop.
o.gif
JONATHAN OVEREND'S BLOG
There was an exhibition element to much of this performance, which, while not perfect, was clearly Federer's best of the tournament.


"The scoreline suggests maybe it was easier than it looked like. I thought it was a pretty tough match," said Federer
"He really got into the match, especially in the second set. But I was able to mix it up well and just keep him on his toes.
"I've been in so many quarterfinals, in this situation so many times before, that I have the experience and I have the game to be tricky for him."
Before the match neither second-seeded Federer, winner of the Qatar Open, nor Wawrinka, the Chennai Open champion, had tasted defeat this season.
But in dropping three sets in his previous four rounds Federer, who is hunting a 17th Grand Slam title, had invited suggestions that he may be vulnerable to an upset.
Wawrinka had given his supporters hope with straight-sets wins over Gael Monfils and Andy Roddick in the previous rounds, but struggled to reproduce that form as his serve particularly failed to fire.
Federer immediately took an assured grip on the match and, after delivering the first game to love, a deft backhand volley handed the 29-year-old two break points in the second.
Wawrinka sprayed wide to surrender the first and, after coming off worse in an exchange on his favoured backhand side in the next game, the younger Swiss found himself 3-0 down in only seven minutes.
A pair of backhand winners down the line in the fourth and fifth games hinted at the skills that could trouble the four-time champion, but the set was gone once he was broken in the sixth by a stinging Federer return on his toes.
o.gif
Roger always had an answer today. He was just too good for me


Stanislas Wawrinka

With the opener consigned to history, Wawrinka posed more of an obstacle in the second but will rue his wastefulness when he appeared to have the Federer serve at his mercy.
With a clear chance to move 4-2 in the lead and Federer rooted on the baseline, Wawrinka planted an over-eager backhand between the tramlines.
Instead, it was Wawrinka's service that fell as the next game ended with a clumsy forehand volley into midcourt that allowed Federer to coax a shot down the line and edge ahead.
A disguised drop shot from Federer brought up break point in the ninth and Wawrinka strayed long to drop two sets behind.
Federer duly took a third successive service game from his compatriot with a drilled forehand and, pinned back by a first serve that landed 77% of the time, Wawrinka rarely threatened a response.
The 25-year-old had powered down 24 aces in victory over Roddick but managed just one as he failed to find any sort of foothold in the match.
Wawrinka briefly suggested he may prolong his defeat as he rallied to 0-30 in the final game, but Federer was not to be denied.
"Roger always had an answer today," reflected Wawrinka.
"He was just too good for me. Roger is always the same - you know he can win this tournament."
 
Bolton 0 - 4 Chelsea


_50932738_011103524-1.jpg
Ramires scored Chelsea's fourth as they moved to within seven points of top spot


By Catherine Etoe
999999.gif


Fourth-place Chelsea boosted their title defence with an emphatic victory over Bolton at the Reebok Stadium.
Didier Drogba gave the visitors an early lead against the run of play with an audacious shot from 30 yards out.
Matt Taylor almost levelled with a bullet header but Petr Cech saved well before Florent Malouda scored at the other end from a tight angle.
Nicolas Anelka hit a third with a left-foot shot in the corner and Ramires finished it with a side-foot volley.
It was a night to forget for Bolton, who failed to draw inspiration from the tributes paid before the match to club legend Nat Lofthouse, who died aged 85 on 16 January.
The west Londoners arrived at the Reebok looking to continue an unbeaten away run against Bolton that stretched back 13 years.
Perhaps more importantly, the reigning champions were seeking to reverse a loss of form that has seen them fall behind in the Premier League title race.
_50934776_ancelotti_640.jpg
Please turn on JavaScript. Media requires JavaScript to play.
</p>
_50934776_ancelotti_640.jpg
Click to play


Click to play




We have turned corner - Ancelotti

With not only leaders Manchester United, but second-place Arsenal and Manchester City sitting above them in the table, and with the advantage over fifth-placed Tottenham based on goal difference only, Chelsea needed all three points to stay in touch.
Bolton boss Owen Coyle's side are without a win in 2011, but the Trotters dominated the opening exchanges.
Bulgarian midfielder Martin Petrov found Johan Elmander with a high cross in the box for the hosts' best early chance but as the Swede flicked on to Kevin Davies, the captain failed to test Blues goalkeper Cech.
Central defensive duo Branislav Ivanovic and John Terry, who was playing after suffering a rib injury, looked jittery as Coyle's men continued to threaten.
o.gif
606: DEBATE
Thought Nat's sad passing might have inspired us, but again we looked devoid of ideas and creativity


onegamein

Until this match, Bolton had suffered only one home defeat all season, while Chelsea had lost five league games away this term, but the form book was torn up by Drogba.
Having nicked the ball off defender Gretar Steinsson, Malouda found the Ivorian striker whose blistering shot dipped into the top of keeper Jussi Jaaskelainen's net from around 30 yards out.
Trotters old boy Anelka then had a chance to extend the visitors' lead, but defender Zat Knight made a fine saving tackle to thwart the France international.
The home side were denied moments later when Petrov provided a teasing cross from the left which Matt Taylor met with a bullet header, but Cech acrobatically pushed his effort around the post.
But it was Chelsea who found the back of the net next, this time after Malouda, who was standing almost on the byeline, slammed the ball against the legs of Gary Cahill before slotting the rebound in from a tight angle.
It was 3-0 to the Blues just after the break, Michael Essien pulling the ball back into the area from the line and though Knight was able to prevent Drogba from getting a shot off, the ball fell to Anelka who made no mistake.
_50934834_owencoyle640.jpg
Please turn on JavaScript. Media requires JavaScript to play.
</p>
_50934834_owencoyle640.jpg
Click to play


Click to play




We gifted goals to Chelsea - Coyle

Bolton's Mark Davies entered the fray just after the hour, and the midfielder almost netted after a smart one-two with Elmander, but the advancing Cech bravely grabbed the ball off his toe.
Any hopes of a Trotters revival were ended, though, when Essien turned another decent ball into the penalty area and Brazilian midfielder Ramires hit a side-footed shot beyond Jaaskelainen to make it 4-0 - mirroring the scoreline in this fixture last season.
Mark Davies continued to probe the visitors' goal but Cech was quick to extinguish the 22-year-old's efforts and Bolton survived a late penalty appeal as Paul Robinson looked to have caught Anelka in the area, but referee Chris Foy waved play on.
Chelsea now sit seven points behind leaders Manchester United, who have a game in hand but travel to Blackpool on Tuesday, while Bolton drop to tenth below Stoke on goal difference.
 
We have turned corner says Chelsea boss Carlo Ancelotti





Chelsea boss Carlo Ancelotti is delighted with his team's display in the 4-0 win at Bolton and says it ends the club's "difficult moment.
 
We gifted goals to Chelsea, says Bolton boss Owen Coyle


Bolton boss Owen Coyle says his team shot themselves in the foot by "gifting Chelsea all their goals" in their 4-0 home defeat to Chelsea.
 
Bolton 0-4 Chelsea




13 comments »

Updated Jan 24, 2011 7:29 PM ET
Chelsea found its old ruthless streak as the Blues dispatched Bolton 4-0 at The Reebok on Monday night.
The Blues banished their away-day blues and narrowed the gap on Premier League leaders Manchester United to seven points with this emphatic victory.

Sat., Jan. 22
Wolves 0-3 Liverpool |Recap
Arsenal 3-0 Wigan | Recap
Everton 2-2 West Ham | Recap
Man Utd 5-0 Birmingham | Recap
Newcastle 1-1 Tottenham | Recap
Fulham 2-0 Stoke City | Recap
Blackpool 1-2 Sunderland | Recap
Aston Villa 1-0 Man City | Recap
Sun., Jan. 23
Blackburn 2-0 West Brom | Recap
Mon., Jan. 24
Bolton 0-4 Chelsea | Recap
Tue., Jan. 25
Blackpool vs. Man Utd
Wigan vs. Aston Villa
Wed., Jan. 26
Liverpool vs. Fulham BPL Scores | Table | Fixtures

Goals from Didier Drogba, Florent Malouda, Nicolas Anelka and Ramires gave manager Carlo Ancelotti the result he craved.
It was Chelsea's first win on the road since October and even though United have a game in hand Ancelotti must have renewed hope they can go on and retain their crown.
Certainly they have terrific attacking options and managed to secure the win without Frank Lampard, who had suffered a recent calf injury.
The match was preceded by an immaculately observed minute's silence for Bolton legend Nat Lofthouse, who died earlier this month, and it was the hosts who threatened first when a miscued clearance from John Terry, who had shrugged off a back problem, landed at the feet of Stuart Holden in the second minute. However, the American failed to test goalkeeper Petr Cech from a good position.
The home side kept up the momentum and Kevin Davies headed into the arms of the goalkeeper following a flick-on from Johan Elmander.
Chelsea, however, opened the scoring in the 10th minute with a magnificent effort from Drogba.
Malouda won the ball from Gretar Steinsson and released Drogba 30 yards out. He caught the ball sweetly and thumped a swerving shot past Jussi Jaaskelainen and into the net to gasps around the ground.
It was Drogba's 10th goal of the season in all competitions and just the boost Ancelotti was looking for.
Play switched back down the other end and a minute later Cech kept his side on level terms, getting a great touch to turn a Matt Taylor header around the post following a cross from Martin Petrov.
Chelsea then extended their lead in the 41st minute with defender Gary Cahill cursing his luck. He managed to block Malouda's cross but it rebounded to the Frenchman who scored at the second attempt, his shot beating Jaaskelainen from a narrow angle at the goalkeeper's near post. That strike took him equal with Drogba on 10 goals.
Bolton almost pulled a goal back a minute before the break with Cech doing well to push away Elmander's clever flick.


Davies, though, was back doing some defensive work in the 52nd minute, heading away an inswinging free-kick from Drogba.
Taylor had been penalised for a challenge on the Chelsea striker which incensed the home supporters.
Bolton, however, suffered another blow in the 56th minute when Chelsea went 3-0 ahead.
Michael Essien delivered a cross from the right and Zat Knight seemed to be distracted by Drogba. The ball broke to Anelka, who swept it home for his 13th goal of the season.
Bolton boss Owen Coyle decided to switch things around and brought on Rodrigo Moreno and Mark Davies for Petrov and Fabrice Muamba, and Davies came close in the 67th minute after latching on to a through-ball from Elmander.
The midfielder tried to lob the ball over Cech but the goalkeeper stood tall and made the save.
Bolton could not handle the speed of Chelsea's counter-attacks and it was becoming a rout.
Ramires made it 4-0 in the 74th minute with his first goal for the club after arriving from Benfica in the summer.
Essien was again instrumental in the build-up, finding Anelka in the area. When his shot was blocked, the Brazil midfielder sidefooted home the rebound.
Anelka almost got his second of the night in stoppage time but Jaaskelainen somehow managed to turn his close range effort around the post.
It was a disappointing night for Bolton, who paid proper homage to the late, great Lofthouse, and they have now taken only eight points from 10 games.
 
Mashindano ya gofu Nahodha kusogezwa mbele

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 24th January 2011 @ 23:45

MASHINDNO ya gofu ya Mwezi Januari ambayo yameshindwa kufanyika mwezi huu yamesogeza mbele mashindano ya Nahodha kwenye klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu wa gofu klabuni hapo Lawrence Pangani mashindano ya mwezi Januari sasa yamepangwa kufanyika Februari 12 ambayo awali ilikuwa yafanyike mashindano ya Nahodha.

Kutokana na mabadiliko hayo mashindano ya Nahodha ambayo awali yalikuwa yafanyike tarehe hiyo yamesogezwa mbele kwa wiki moja.

Pangani alisema kusogezwa mbele kwa mashindano ya Januari kuna lengo la kuwapa muda wa kutosha kujiandaa wadhamini wa mashindano hayo kampuni ya Zantel.

Itakuwa ni mwezi wa tatu kwa Zantel tangu kuanza kudhamini mashindano hayo ya kila mwezi baada ya kufanya hivyo mwezi Novemba na Desemba mwaka jana na washindi kuzoa zawadi nono ikiwa pamoja na simu za mkononi aina ya blackberry.

Pangani alisema mashindano ya Nahodha yatafanyika kwa siku mbili Februari 19 na 20 kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa viongozi wa gofu klabuni hapo Februari 23.

Mashindano ya nahodha yanafanyika kwa heshima ya nahodha anayemaliza muda wake
ambaye kwa sasa ni Joseph Tango.

Tango alisema mabadiliko hayo ni mazuri kwani ni vema kufanya mashindano yake siku ya mwisho kabla ya uchaguzi ili kufunga vema utawala wake.

Uchaguzi mkuu wa kamati ya gofu klabuni hapo hufanyika kila baada ya mwaka mmoja.

 
Mshindi Miss Utalii kupewa zawadi nono

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 24th January 2011 @ 23:40

FAINALI za shindano la Miss Utalii Tanzania zimepangwa kufanyika Februari 5, mwaka huu na mrembo atakayenyakua taji hilo ataondoka na faida kubwa ya zawadi ya mkataba wenye thamani ya Sh milioni 150.

Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo ilieleza kuwa, shindano la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya Kiromo View Resort mjini Bagamoyo.

Alisema pia warembo wengine watajitwalia mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA).

"Pia kutakuwa na tuzo zingine toka baadhi ya kampuni na taasisi zilizodhamini shindano hili ili kuyawakilisha katika suala zima la kuutangaza utalii kupitia hifadhi za taifa na utamaduni wa Mtanzania na hivyo kuongeza hamasa zaidi kwa washiriki ambao nao wameonesha kujawa shauku ya kufanya vema.

"Fainali za taifa za Miss Utalii zitakuwa tukio kubwa zaidi la kitaifa la kitamaduni na urembo nchini, ambalo kishindo chake kitaleta mageuzi makubwa katika sanaa ya urembo nchini, barani Afrika na duniani kwa ujumla," alisema.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom