Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #3,581
Fainali Tuzo za Kili Machi 26
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 24th January 2011 @ 23:35 Imesomwa na watu: 18; Jumla ya maoni: 0
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), George Kavishe (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mchakato wa tuzo za muziki za kilimanjaro 2011 'Kilimanjaro Music Awards' Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mratibu wa Tuzo za muziki za Kilimanjaro, Angelo Luhala pamoja na Msaidizi wa maandalizi ya Tuzo hizo, Editha Bebwa. (Picha na Fadhili Akida).
FAINALI za tuzo ya muziki ya Kilimanjaro zimepangwa kufanyika Machi 26 mwaka huu
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ndio waandaaji ya tuzo hizo kupitia Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), George Kavishe alisema tuzo za safari hii zitakuwa za aina yake kwani wamedhamiria kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana.
Alisema maandalizi yote yanakwenda vizuri na kwamba Februari 12 na 13 jopo la wadau wa muziki 100 watakutana kupata wanamuziki watakaopendekezwa kuwania vipengele mbalimbali.
Alisema baada ya hapo Februari 16 majina ya waliopendekezwa kuwania tuzo hizo yatatangazwa kabla ya kufanyiwa semina Februari 21.
"Baada ya mambo yote hayo kufanyika mashabiki wa muziki nchini wataanza kupiga kura Machi mosi na majaji watahakiki kura Machi 24 kabla ya siku ya Usiku wa tuzo za muziki za Kilimanjaro,"alisema.
Aidha Kavishe alisema, moja ya maboresho ya tuzo za mwaka huu ni kutokuwa na wasanii kutoka nje ya nchi kama ilivyokuwa kawaida katika tuzo zilizopita.
"Safari hii burudani itatoka kwa wasanii wa hapa hapa nchini kwani lengo letu ni kuufikisha muziki kwenye kilele cha mafanikio… hawa watakuwa kambini ili kuipendezesha siku hiyo.
Pia Kavishe alisema kuna nyimbo maalum kwa ajili ya mashindano ya mwaka huu ulioimbwa na wasanii walioshinda mwaka jana.
"Hizi tutazisambaze kwenye vituo mbalimbali vya runinga na redio tunataka mtu akiusikia tu ajue unaashiria nini, kwa mfano ukisia ooooooh, oooooooh, moja kwa moja unajua ni Kombe la dunia 2010, ndivyo tunavyotaka iwe,"alisema.