Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Twanga kuburudisha Mbagala Kuu
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 6th December 2010 @ 21:00 Imesomwa na watu: 25

BENDI ya muziki wa Dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta' Ijumaa inatarajiwa kutoa burudani kwenye Ukumbi wa Nawina Resort Mbagala Kuu Dar es Salaam.

Mratibu wa Onesho hilo Zahor Said, alisema kuwa onesho hilo litakuwa maalumu kwa wakazi wa Mbagala Kuu na vitongoji vyake ikiwa ni pamoja na kuwapa burudani hiyo.

Alisema katika kuhakikisha wanatoa burudani safi kutakuwa na utambulisho wa vikundi vya unenguaji ambavyo vimekuwa vikitamba Tanzania.

Said alisema vikundi hivyo ni Kiduku na Khanga Moja ambapo lengo la kuwaita katika onesho hilo ni kutoa burudani kwa wakazi wa Mbagala.

Bendi inaongozwa na waimbaji mahiri kama Chaz Baba, Kalala Junior, Dogo Rama, Luiza Mbutu, Janeth Isinika na marapa Khalid Chokoraa na Ferguson.

Wakati kwa wapiga vyombo kuna James Kibosho, mpiga ngoma, Soud Mohamed ‘MCD' mpiga tumba, huku solo gitaa likipapaswa na Miraji Shakashia ‘Shakazulu'.
 
Yanga kutumia Mkwakwani ligi kuu
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 6th December 2010 @ 23:50 Imesomwa na watu: 16

TIMU ya Yanga imehama Uwanja wa Jamhuri Morogoro na sasa itatumia Uwanja wa Mkwakwani Tanga katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Januari.

Baada ya Uwanja wa Uhuru uliokuwa ukitumiwa na timu za Dar es Salaam na Pwani katika mechi mbalimbali za ligi kufungwa, timu hizo zilichagua kutumia viwanja vingine katika mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi ambapo nyingi ikiwemo Yanga zilichagua Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Azam ndio iliyokuwa inatumia Uwanja wa Mkwakwani hivyo kitendo cha Yanga kinafanya timu zinazotumia uwanja huo kufika mbili.

Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu hakuwa tayari kulizungumzia hilo lakini habari kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinasema maamuzi hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana mwishoni mwa wiki iliyopita.

"Tumekutana tumeamua tuondoke Morogoro kwenda Tanga maana Uwanja wa Jamhuri unatumika sana kutokana na timu nyingi kuhamia huko, hivyo mzunguko wa pili tutaanza kuutumia Mkwakwani,"alisema kiongozi mmoja wa juu wa Yanga.

Yanga imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kuwa na pointi 25 katika mechi 11 ikiongozwa na Simba yenye pointi 27 na Azam inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20, nafasi ya nne ni Mtibwa Sugar yenye pointi 19 na Kagera Sugar ni ya tano ikiwa na pointi 17.

Wakati Yanga ikibadili uwanja, mahasimu wa jadi Simba, inadaiwa wataendelea kuutumia uwanja uleule wa CCM Kirumba Mwanza.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema uongozi umeamua kutohama uwanja na kwamba maandalizi ya safari ya kurudi Mwanza yanaendelea.

"Timu yetu itakuwa kulekule Mwanza, na timu inatarajiwa kuondoka mwishoni mwa mwezi huu kwenda Mwanza,"alisema mtoa habari wetu.
 
Watakiwa kujitokeza usaili wa vipaji

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 6th December 2010 @ 23:00 Imesomwa na watu: 21

VIJANA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika usaili wa shindano la kusaka vipaji vya muziki wa dansi utakaofanyika Desemba 21 na 22 katika ukumbi wa Africenter uliopo Ilala.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) Suleiman Mathew ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayoandaa shindano hilo, Makukwe Entertainment alisema, fomu za usaili ni Sh 3,000 ambapo wanaotaka fomu za kujiunga wanatakiwa kumuulizia Meneja wa Ukumbi wa Africenter ili awapatie fomu.

Alisema kuwa fainali za shindano hilo ni Machi 6 mwakani ambapo kabla ya hapo washiriki watakaofanikiwa kuingia katika shindano watakaa kwa miezi miwili kambini.

Alisema, wakiwa kambini washiriki watafundishwa muziki na wataalamu wa muziki nchini ambapo wataelekezwa namna ya kutumia vyombo mbalimbali.

Alisema kwa wanaotaka kushiriki kwa vikundi wanatakiwa kujitenga katika makundi ya watu saba ambapo kutakuwa na makundi 12 yatakayoshindanishwa.

" Mimi naona kuwa jamii na Serikali pia inatakiwa kutuunga mkono katika kufanikisha masuala haya muhimu kwa faida ya muziki wetu na vijana kiujumla," alisema Mathew.

Naye mwanamuziki Ally Choki alisema kuwa shindano hilo ni muhimu kwa kuwa linawaandaa vijana mapema kuingia katika fani ya muziki.

Alisema kuwa kupitia mpango huo vijana wanaweza kupata ajira na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuisaidia jamii inayowazunguka.
 
Viingilio robo fainali Chalenji hadi raha

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 6th December 2010 @ 23:59 Imesomwa na watu: 210;

ROBO fainali za michuano ya Kombe la Chalenji zinaanza leo, huku Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwa limetangaza viingilio vidogo vya kushuhudia mechi hizo.

Kwa karibu mechi zote za makundi za michuano hiyo, mashabiki walikuwa wakiingia bure uwanjani kitendo kilichowavutia wengi kwani walikwenda kwa wingi Uwanja wa Taifa.

Hata hivyo bure hiyo imeingia dosari kwani wapo baadhi ambao si wastaabu wameharibu samani za uwanja huo ikiwa ni pamoja na kuvunja masinki ****** na kuchafua kwa vinyesi.

Mechi ya kwanza ya robo fainali leo itakuwa kati ya timu waalikwa Malawi na Ivory Coast zitakazocheza saa nane mchana kabla Zambia haijamenyana na Ethiopia kuanzia saa kumi jioni.

Mechi zote ni kali, kutokana na soka ya ushindani iliyooneshwa na timu hizo tangu kuanza kwa michuano hiyo kwenye mechi za makundi.

Malawi imeingia hatua ya robo fainali ikiwa ya pili Kundi C baada ya kufikisha pointi tano katika mechi tatu ilizocheza na Ivory Coast imepata nafasi hiyo ikiwa kinara wa Kundi B baada ya kufikisha pointi sita.

Na Kwa upande wa Zambia ambayo imeonesha upinzani mkubwa tangu kuanza kwa michuano hii, imefuzu hatua ya robo fainali ikiwa kama kinara wa Kundi A baada ya kufikisha pointi saba huku Ethiopia ikipenya katika hatua hiyo kama ‘best loser' baada ya kushika nafasi ya tatu katika Kundi C ikiwa na pointi nne.

Kwa upande wa viingilio, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Sunday Kayuni alitangaza kwa waandishi wa habari jana kuwa cha juu ni Sh 5,000 na cha chini ni Sh 1,000.

"Kamati ya Mashindano ilikutana jana na kuamua kupanga viingilio vya chini ili kuwawezesha mashabiki kuingia uwanjani kwa wingi,"alisema Kayuni.

Alivitaja viingilio hivyo kuwa ni Sh 1,000 kwa viti vya Kijani na Bluu, Sh 2,000 kwa viti vya machungwa. Sh 3,000 kwa VIP C, Sh 4,000 kwa VIP B na Sh 5,000 kwa VIP A.

Hivyo ni viingilio vya chini zaidi kupangwa kwenye michuano mikubwa hasa inapofanyika katika Uwanja wa Taifa.
 
Zanzibar, Stars visasi leo

Imeandikwa na Zena Chande; Tarehe: 7th December 2010 @ 23:59 Imesomwa na watu: 208

BAADA ya jana Ethiopia kuwaduwaza mashabiki wa soka kwa kuifunga Zambia mabao 2-1, hivyo kutinga nusu fainali ya Kombe la Chalenji, leo mambo yanaendelea ambapo wenyeji Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' na Zanzibar Heroes ni wakati wao wa kulipa visasi kwa Rwanda ‘Amavubi' na Uganda ‘The Cranes'.

Ni mechi za kukata na shoka ambapo ya kwanza itakuwa ni kati ya Zanzibar Heroes na Uganda kabla Kilimanjaro Stars haijamenyana na Amavubi mechi inayofuata.

Uganda imeingia robo fainali ikiwa inaongoza Kundi C kwa kufikisha pointi sita huku mpinzani wake Zanzibar ikipenya kama ‘best loser'.

Mechi ya leo kwa timu hizo ni kama marudio ya michuano ya Kombe la Chalenji ya mwaka jana ambayo ilifanyika Mumias na Nairobi.

Uganda ilikuwa Kundi C pamoja na Zanzibar, Kilimanjaro Stars na Burundi.

Na katika mechi ya makundi Uganda na Zanzibar zilitoka sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Mumias.

Timu hizo zilikutana tena kwenye mechi ya nusu fainali baada ya Zanzibar kuitoa Zambia kwa mikwaju ya penalti 4-3 kwenye robo fainali na Uganda kuiondoa Kenya kwa bao 1-0, mechi hizo zilichezwa kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi.

Hatua ya nusu fainali, Uganda ikaiondoa Zanzibar kwa mabao 2-1 yaliyofungwa na Steven Bengo, na Andy Mwesigwa na lile la Zanzibar likifungwa na Suleiman Kassim.

Kitendo hicho ndicho kitakachoifanya Zanzibar itake kulipa kisasi kwa Uganda leo, na hakuna shaka kwamba timu zote zilizoingia hatua ya robo fainali maombi yao leo kwa Zanzibar iiondoe Uganda kwenye mashindano hayo ili kazi ya kutwaa ubingwa iwe rahisi.

Uganda inafundishwa na kocha Robert Williamson ‘Boby' kutoka Scotland na imetwaa Kombe la Chalenji mara mbili mfululizo, na kwa soka inayoonesha ina nafasi kubwa ya kulitwaa kwa mara ya tatu.

Kwa upande wa mechi ya Kilimanjaro Stars na Amavubi, kazi ipo kwa mahasimu hao wa miaka ya karibuni kwenye michuano hiyo.

Mwaka jana timu hizo zilikutana kwenye nusu fainali baada ya Stars kuitoa Eritrea kwa mabao 4-0 na Rwanda kuitoa Zimbabwe kwa mabao 4-1.

Mechi ya nusu fainali Rwanda iliifunga Kili Stars mabao 2-1 yaliyofungwa na Ndayishimiye J Luc na Mutesa Mafisango huku bao la Kili likifungwa na Mussa Hassa Mgosi ambaye katika kikosi cha mwaka huu kwenye michuano hiyo hayupo.

Mbali na mechi hiyo, Kilimanjaro Stars na Rwanda zimekuwa na upinzani kwa muda mrefu sasa, na mara kadhaa Kili imekuwa ikinyanyaswa na Amavubi, hivyo ni nafasi nyingine ya kuifunga timu hiyo na Tanzania kuingia nusu fainali.

Katika mchezo wa kwanza wa robo fainali jana, Ethiopia ilitinga nusu fainali baada ya kuifunga Zambia mabao 2-1, ambapo Ethiopia haikuwa ikipewa nafasi kubwa na wadau hasa kutokana na Zambia ‘Chipolopolo' kuanza vyema michuano hiyo kwa kuifunga Kilimanjaro Stars bao 1-0 hatua ya makundi hivyo kuonekana ina nguvu kubwa.
 
Nico Bambaga afariki dunia
12_10_5nh4tx.jpg


Bambaga watatu kushoto waliochuchumaa



Imeandikwa na Betram Lengama; Tarehe: 7th December 2010 @ 23:50 Imesomwa na watu: 183

MEDANI ya soka nchini imepata pigo lingine kutokana na kifo cha kiungo mahiri wa zamani wa timu ya taifa ‘Taifa Stars', Nicodemus Bambanga.

Kifo hicho cha Bambaga kimekuja wiki chache baada ya kiungo mahiri wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Juma Mkambi naye kufariki dunia, ambapo kabla ya Mkambi pia aliyepata kuwa kocha mahiri nchini, Syllersaid Mziray naye alifariki dunia.

Kwa mujibu wa mpwa wa marehemu, Marwa Kasuhu, Bambanga alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Lugalo,Dar es Salaam alikokuwa amelazwa tangu Jumamosi iliyopita kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kifua kubana na hali yake ilibadilika juzi saa tano usiku na kuaga dunia.

Bambaga alipata kuchezea Pamba ya Mwanza, Yanga na Simba zote za Dar es Salaam, Malindi na Mlandege za Zanzibar na kung'ara pia na Taifa Stars.

Kwa mujibu wa mpwa huyo, Bambaga ameacha mjane na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 ambaye anasoma shule ya msingi Gilman Rutihinda, Kigogo jijini Dar es Salaam.

Alisema taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu Kigogo na mwili unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda kijijini kwao Mwisenge, Musoma mkoani Mara kwa ajili ya maziko, ambayo yanatarajiwa kufanyika Jumamosi.

"Bambaga kabla ya kufariki, alisema watu wasihangaike kumsafirisha wanaweza kumzika popote, lakini shangazi zake pamoja na mjomba wake wamesisitiza akazikwe nyumbani Mwisenge ambako ndiko asili ya wazazi wake ambao wote wamekwishatangulia mbele za haki," Kasuhu alisema, Bambanga aliyezaliwa mwaka 1964 Mwisenge, baada ya kustaafu soka Nico alikuwa akijishughulisha na biashara mbalimbali.

Wakimzungumzia Bambanga wachezaji ambao wamewahi kucheza naye katika timu mbalimbali, walibainisha kuwa watamkosa kiungo huyo kwa mambo mengine hasa tabia yake ya uungwana pamoja na uongozi wake katika masuala mbalimbali.

Mshambuliaji Edibily Lunyamila ambaye alicheza na marehemu Yanga na Malindi, alisema licha ya kucheza naye waliishi katika nyumbani moja hapo kabla na kusema kuwa Bambanga alikuwa ni mtu makini na mkimya ambaye ukigombana naye basi lazima chanzo cha ugomvi utakuwa wewe.

Na kwa upande wake Bitta John yeye alimtaja Bambanga kama mtu ambaye alimshawishi ajiunge na timu ya Pamba wakati akiichezea, lakini alikuja kujiunga naye wakati akiwa Simba na Taifa Stars ambako alikuwa kiongozi wake katika mambo mbalimbali .

Baadhi ya wachezaji waliokuwepo kwanye msiba huo jana ni pamoja na Abdallah Msamba, Abubakari Kombo, Athumani Jumapili Chama, Robert Damian na Dua Said ambaye ni jirani yake marehemu.
 
Msechu awashukuru Watanzania

12_10_07wavh.jpg

Mshindi wa pili wa shindano la Tusker Project Fame, Peter Msechu akipungia mashabiki (hawapo pichani) waliofika kumpokea baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana akitikea nchini Kenya. (Picha na Fadhili Akida)

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 7th December 2010 @ 23:30 Imesomwa na watu: 66;
MTANZANIA Peter Msechu aliyeshika nafasi ya pili katika shindano la Tusker Project Fame lililomalizika nchini Kenya mwishoni mwa wiki amewashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono.

Msechu aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana, kuwa ushindi huo unatokana na kujituma pamoja na msaada wa Watanzania walioamua kumpigia kuwa awe mshindi na kuwashukuru kwa jitihada zao.

Alisema ni vema vijana wengine wakajitokeza kushiriki katika shindano hilo ambalo limekuwa likiinua vipaji vya vijana wengi kimuziki.

Alisema serikali inatakiwa kuendelea na mkakati wake wa kuwasaidia vijana katika sekta hiyo ya muziki kwa kuwa wengi wao kwa sasa wamejiajiri katika sekta hiyo.

Naye Katibu Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Ghonche Materego aliyekuwepo kwenye mapokezi hayo alisema baraza lake linatambua umuhimu wa sanaa kwa maendeleo na utambulisho wa nchi.
 
Ligi Arusha sasa yaiva

Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 7th December 2010 @ 21:00 Imesomwa na watu: 47

TIMU 16 mkoani Arusha zinashiriki ligi ya Taifa ngazi ya wilaya na zimepangwa katika makundi mawili, ambapo kila kundi litatoa timu tatu zitakazoshiriki hatua ya fainali.

Katika michezo minne ya ufunguzi timu ya Flamingo ilianza ligi hiyo kwa kishindo kwa kuibamiza Olduvai mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kaimu Katibu wa Chama cha Soka cha Wilaya ya Arusha (ADFA), Abdull Kondo alizitaja timu zilizopo Kundi A ni Manna Baptist, Golden Kids, Flamingo, Olduvai, CIDT, Proyota, Pentagon na Banana.

Alizitaja timu zilizo Kundi B ni pamoja na Njiro, Kakakuona, Jamhuri, United Boys, Tacoda, Arusha Talent, Polisi na Bishop Durning.

Katika michezo mingine ya ufunguzi timu ya United Boys ambayo inashiriki ligi hiyo ikiwa imefungiwa miaka miwili na chama cha soka cha mkoa wa Arusha (ARFA) ilifanikiwa kuifunga Jamhuri mabao 3-0.

Michezo mingine ni Manna Baptist ilitoka 0-0 na Golden Kids na timu za Njiro na na Kakakuona zilifungana bao 1-1 katika michezo iliyochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kaimu Katibu huyo alisema kila kundi zitatoka timu tatu ambazo zitashindana katika hatua ya sita bora ambayo itatoa bingwa wa wilaya ya Arusha.
 
Bondia Emilian achiwa huru

Tuesday, 07 December 2010 19:35
Imani Makongoro

MMOJA wa mabondia wa Tanzania waliokamatwa nchini Maurtius, Emilian Patrick, ameachiwa huru baada ya uchunguzi wa awali nchini humo kukamilika na kuonekana hana hatia.

Kabla ya kukamatwa Maurtius, Emilian alikuwa Mtanzania pekee aliyekuwa amefuzu kushiriki michezo ya Olimpiki iliyofanyika jijini Belgiji, China, lakini ndoto hizo zilizimika ghafla baada ya kukamatwa wakati ana kwenda kushiriki mashindano ngumi Afrika kama maaandalizi ya Olimpiki.

Emilian na wenzake watano walikamatwa nchini humo mwaka 2008 na kutuhumiwa kula njama ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine, huku aliyekuwa rais wa Shirikisho la mchezo huo (BFT), Shaban Mintanga naye alikamatwa hapa nchini kwa tuhuma hiyo.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi ulionyesha bondia huyo amewasili hapa nchini wiki iliyopita akitokea Maurtius baada ya kurudishwa na kuambiwa kuwa hana hatia huku wenzake watano wakiendelea kushikiliwa nchini humo kwa uchunguzi zaidi.

Habari hizo za kina kutoka Maurtius zilieleza kuwa watanzania wanaondelea kushikiliwa nchini humo ni pamoja na aliyekuwa kocha, Nassor Michael, bondia Petro Mtagwa na wengine watatu ambao wametwajwa kuwa ni meneja wa timu, daktari na kocha msaidizi.Uchunguzi huo wa kina uliofanywa na Mwananchi ulionyesha kuwa kati ya wachezaji waliokuwa wamefuzu kucheza michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 hapa nchini iliyokuwa ikifanyika mjini Belgiji, Emilian pekee.

Uchunguzi huo ulionyesha kuwa mabondia walibaki nchini Maurtius bado wanaendelea kushikiliwa kama mahabusu nchini humo wakati hapa nchini Mintanga akiendelea kusota mahabusu kusubili uchunguzi wa kesi hiyo kukabiliwa.

Uchunguzi huo ulisema kuwa wakati Emilian na wenzake waliobaki Maurtius wakipelekwa mahakamani kujibu tuhuma hizo Emilian akuwa akijibu chochote kwa kuwa wakati wanakamatwa hakujua wamekamatwa kwa kosa, hivyo baada ya uchunguzi huo kukamilikwa alionekana hana hatia na kupandishwa ndege kurudi nchini kwake kama raia mwema.
 
Tanzania yachapwa

Tuesday, 07 December 2010 19:34
Jessca Nangawe
TANZANIA imeanza vibaya katika mashindano ya kimataifa ya mchezo wa netiboli baada ya kukubali kichapo cha magoli 36-52 kutoka kwa Scotland mchezo uliofanyika jana mjini Singapore.

Kwa mujibu wa mtandao Taifa queens walishindwa kuonyesha uwezo wao katika mchezo huo hivyo hadi wanakwenda mapumziko ya robo ya kwanza walikua nyuma kwa jumla ya magoli 10-7.
Mpaka mapumziko Scotland walizidi kuwa mbele kwa kuinyuka Tanzania kwa magoli 17-26 huku robo ya tatu ikiwa nyuma kwa magoli 28-33.

Katika mchezo huo Scotland walionyesha kujiamini huku wakiwa na kumbukumbu ya kichapo cha magoli 48-29 dhidi ya Malasia katika mchezo wake wa ufunguzi.

Katika mchezo mwingine Taifa queens leo watakua na kibarua kingine dhidi ya Ireland Kaskazini kabla ya kukabiliana na wenyeji Singerpore siku ya Alhamisi.

Mashindano hayo ambayo yanajumuhisha nchi sita ni kwa ajili ya kupandisha timu hizo katika viwango vya kimataifa vya mchezo huo vinavyotambuliwa na Shirikisho la mchezo huo duniani IFNA.
 
Bondia Emilian achiwa huru
Tuesday, 07 December 2010 19:35
Imani Makongoro
MMOJA wa mabondia wa Tanzania waliokamatwa nchini Maurtius, Emilian Patrick, ameachiwa huru baada ya uchunguzi wa awali nchini humo kukamilika na kuonekana hana hatia.

Kabla ya kukamatwa Maurtius, Emilian alikuwa Mtanzania pekee aliyekuwa amefuzu kushiriki michezo ya Olimpiki iliyofanyika jijini Belgiji, China, lakini ndoto hizo zilizimika ghafla baada ya kukamatwa wakati ana kwenda kushiriki mashindano ngumi Afrika kama maaandalizi ya Olimpiki.

Emilian na wenzake watano walikamatwa nchini humo mwaka 2008 na kutuhumiwa kula njama ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine, huku aliyekuwa rais wa Shirikisho la mchezo huo (BFT), Shaban Mintanga naye alikamatwa hapa nchini kwa tuhuma hiyo.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi ulionyesha bondia huyo amewasili hapa nchini wiki iliyopita akitokea Maurtius baada ya kurudishwa na kuambiwa kuwa hana hatia huku wenzake watano wakiendelea kushikiliwa nchini humo kwa uchunguzi zaidi.

Habari hizo za kina kutoka Maurtius zilieleza kuwa watanzania wanaondelea kushikiliwa nchini humo ni pamoja na aliyekuwa kocha, Nassor Michael, bondia Petro Mtagwa na wengine watatu ambao wametwajwa kuwa ni meneja wa timu, daktari na kocha msaidizi.Uchunguzi huo wa kina uliofanywa na Mwananchi ulionyesha kuwa kati ya wachezaji waliokuwa wamefuzu kucheza michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008 hapa nchini iliyokuwa ikifanyika mjini Belgiji, Emilian pekee.

Uchunguzi huo ulionyesha kuwa mabondia walibaki nchini Maurtius bado wanaendelea kushikiliwa kama mahabusu nchini humo wakati hapa nchini Mintanga akiendelea kusota mahabusu kusubili uchunguzi wa kesi hiyo kukabiliwa.

Uchunguzi huo ulisema kuwa wakati Emilian na wenzake waliobaki Maurtius wakipelekwa mahakamani kujibu tuhuma hizo Emilian akuwa akijibu chochote kwa kuwa wakati wanakamatwa hakujua wamekamatwa kwa kosa, hivyo baada ya uchunguzi huo kukamilikwa alionekana hana hatia na kupandishwa ndege kurudi nchini kwake kama raia mwema.
 
Rwanda wapania Ngasa

Tuesday, 07 December 2010 19:33

Calvin Kiwia
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi' Sellas Tetteh ameitaka safu yake ya ulinzi kumweka chini ya ulinzi kiungo mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngasa kwenye mchezo wao wa robo fainali ya Tusker Chalenji utakaofanyika leo kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam alisema kuwa ameifuatilia kwa ukaribu Kili Stars na kugundua kuwa inatengeneza mashambulizi yake kupitia kwa winga wake Ngasa."Nafikiri tukimshika vizuri yule kijana mfupi mwenye mbio anavaa jezi namba 8 (Ngasa) tutaweza kuizuia Kili Stars kutushinda," alisema Tetteh.

Alisema Kilimanjaro Stars imekuwa ikimtumia zaidi Ngasa kutengeneza mashambulizi yake na tayari amewaambia walinzi wake kuwa naye makini ili kuhakikisha haleti madhara kwenye lango lao.

Aliongeza kuwa hata kama timu hizo zitafikia kwenye hatua ya matuta hana wasiwasi kutokana na zoezi hilo la upigaji penati amelifanyia kazi kwa ufanisi mkubwa.

Vile vile aliongeza kuwa anafahamu kuwa mchezo huu utakuwa mgumu kutokana mashabiki wengi watakaojitokeza uwanjani watakuwa wakiwashangilia wenyeji Kili Stars na kuwataka wachezaji wake kuyachukulia kama mambo ya kawaida katika soka.
 
Cecafa yapigwa jeki mil 190

Tuesday, 07 December 2010 19:32
Clara Alphonce
WAKATI Michuano ya Tusker Chalenji yakiwa katika hatua ya robo fainali Kampuni ya simu ya Vodacom imejitosa kudhamini mashindano hayo yanayoendelea hapa nchini kwa Shilingi Milioni 190.

Meneja Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza alisema kuwa wameamua kuingia katika mashindano hayo kwa ajili ya kujenga uhusiano mzuri na TFF, pamoja na CECAFA pia kuongeza msisimko wa mashindano hayo.

Pia, alizitaka timu za Tanzania ambazo zinashiriki michuano hiyo ambayo ni Kilimanjaro Stars na Zanzibar Herous kuakikisha wanafanya vizuri katika mashindano hayo makubwa na kulibakisha kombe hapa nchini.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) na Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya michezo Afrika Mashariki na Kati Leodegar Tenga alisema kuwa wamefurahi kwa kampuni hiyo kusikia kilio chao kwa kutoa udhamini katika mashindano hayo.Alisema CECAFA ilikuwa inaitaji bilioni 1.1 kwa ajili ya kuandaa mashindano hayo makubwa, lakini walikuwa wamepata Shilingi Milioni 650 kutoka kwa SBL na Tusker ambao ndio wadhamini wakuuu wa mashindano hayo.

Alisema kwa sasa wakiongeza na fedha za Vodacom watakuwa wamebaki na deni la 250m ilikutimiza idadi ya fedha ya 1.1 bilioni kitu ambacho kimewafariji sana.

Tenga alisema anatumaini kuwa viingilio walivyoweka vitawakidhi Watanzania wote ambao wamekuwa wakishuhudia michuano hiyo katika ngazi ya makundi.

''Kunakitu kimoja tumejifunza kuwa mashabiki wengi wanapenda mpira hivyo naamini kuwa viingilio tuilivyoweka ni vizuri nia ni kuakikisha watu wanakuja kwa wingi kushuhudia michuano hiyo kwani uwanja bila watu haupendezi watu ndio wanapamba uwanja'' alisema Tenga.

Hata hivyo Tenga aliipongeza Serikali kwa kupitia Waziri wake wa Michezo Ajira na Vijana, John Nchimbi kwa kutoa ushirikiano wao kuakikisha kuwa mashindano hayo yanafanikiwa kwani hapa udhamini huo wa Voda walioupata umechangiwa na yeye.

''Kwa kweli tutakuwa wachoyo wa fadhila tusipo mshukuru Waziri wetu Nchimbi kwani kupitia Wizara yake ametusaidia kufanikisha mashindano hayo kwani yeye ndiye alienda Vodacom kutuombea udhamini baada ya kusikia kilio chetu,'' alisema.

Hata hivyo Tenga aliongeza kuwa kama Mwenyekiti wa CECAFA angependa timu bora na ambayo imefanya vizuri katika mashindano hayo ndio ishinde.
 
Cecafa yapigwa jeki 190?= Mil

Tuesday, 07 December 2010 19:32

Clara Alphonce
WAKATI Michuano ya Tusker Chalenji yakiwa katika hatua ya robo fainali Kampuni ya simu ya Vodacom imejitosa kudhamini mashindano hayo yanayoendelea hapa nchini kwa Shilingi Milioni 190.

Meneja Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza alisema kuwa wameamua kuingia katika mashindano hayo kwa ajili ya kujenga uhusiano mzuri na TFF, pamoja na CECAFA pia kuongeza msisimko wa mashindano hayo.

Pia, alizitaka timu za Tanzania ambazo zinashiriki michuano hiyo ambayo ni Kilimanjaro Stars na Zanzibar Herous kuakikisha wanafanya vizuri katika mashindano hayo makubwa na kulibakisha kombe hapa nchini.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) na Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya michezo Afrika Mashariki na Kati Leodegar Tenga alisema kuwa wamefurahi kwa kampuni hiyo kusikia kilio chao kwa kutoa udhamini katika mashindano hayo.
Alisema CECAFA ilikuwa inaitaji bilioni 1.1 kwa ajili ya kuandaa mashindano hayo makubwa, lakini walikuwa wamepata Shilingi Milioni 650 kutoka kwa SBL na Tusker ambao ndio wadhamini wakuuu wa mashindano hayo.

Alisema kwa sasa wakiongeza na fedha za Vodacom watakuwa wamebaki na deni la 250m ilikutimiza idadi ya fedha ya 1.1 bilioni kitu ambacho kimewafariji sana.

Tenga alisema anatumaini kuwa viingilio walivyoweka vitawakidhi Watanzania wote ambao wamekuwa wakishuhudia michuano hiyo katika ngazi ya makundi.

''Kunakitu kimoja tumejifunza kuwa mashabiki wengi wanapenda mpira hivyo naamini kuwa viingilio tuilivyoweka ni vizuri nia ni kuakikisha watu wanakuja kwa wingi kushuhudia michuano hiyo kwani uwanja bila watu haupendezi watu ndio wanapamba uwanja'' alisema Tenga.

Hata hivyo Tenga aliipongeza Serikali kwa kupitia Waziri wake wa Michezo Ajira na Vijana, John Nchimbi kwa kutoa ushirikiano wao kuakikisha kuwa mashindano hayo yanafanikiwa kwani hapa udhamini huo wa Voda walioupata umechangiwa na yeye.

''Kwa kweli tutakuwa wachoyo wa fadhila tusipo mshukuru Waziri wetu Nchimbi kwani kupitia Wizara yake ametusaidia kufanikisha mashindano hayo kwani yeye ndiye alienda Vodacom kutuombea udhamini baada ya kusikia kilio chetu,'' alisema.

Hata hivyo Tenga aliongeza kuwa kama Mwenyekiti wa CECAFA angependa timu bora na ambayo imefanya vizuri katika mashindano hayo ndio ishinde.
 
Mwape kutua kesho Dar

Wednesday, 08 December 2010 19:10 newsroom




Na Mwandishi Wetu
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga Davies Mwape, anatazamia kurejea nchini kesho kuungana na wenzake tayari kwa vita ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika. kizungumza na Burudani kwa njia ya simu juzi, Ofisa Habari alisema kuwa Mwape ameshakamilisha maandalizi yote ya kuja nchini kucheza katika timu ya Yanga na anarejea kutoka Zambia kuanza jukumu hilo. wape alikwenda kwao kuaga familia na klabu yake ya Konkola Blades anayotaka, baada ya usajili wake Yanga kukamilika mapema mwezi huu.
Mchezaji huyo alisema kuwa alipokuja ëBongoí hakuwa amejiandaa kwa kila kitu kwa sababu alikuwa hajajadiliana na klabu ya Yanga kuhusu usajili wake.
Kwa mujibu wa Sendeu, nyota huyo aliyefanya mazoezi siku chache katika kikosi cha Jangwani na kurejea kwao Zambia, amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.
ìMwape hana wasiwasi ni mali yetu Yanga na tumezungumza naye amesema atakuja Ijumaa (kesho) ilikuwa arudi Jumatano, lakini imeshindikana kwa kuwa amekosa ndege,î alisema Sendeu.
Yanga imesajili wachezaji wawili katika dirisha dogo mbali ya Mwape mwingine ni Salum Seif kutoka Zanzibar.
Kusajiliwa Mwape kumeiongezea makali safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyokuwa inamtegemea zaidi Jerry Tegete na mara nyingine ikipata mabao kupitia kwa Abdi Kassim ëBabií na Nurdin Bakari.
Tegete anaongoza kufunga mabao katika ligi kuu, kwani hadi duru la kwanza linamalizika amefikisha mabao sita sawa na Mussa Hassan ëMgosií.
Katika hatua nyingine, klabu ya Yanga imeamua kuwapima afya wachezaji wake wote kabla ya kuanza mazoezi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.
Sendeu alisema wachezaji walianza kupimwa juzi na ambao wamebainika na matatizo wataanza tiba mapema kabla ya kuingizwa gym kuanza mazoezi.
 
Inter Milan yapigwa, Man United chupuchupu

Wednesday, 08 December 2010 19:13 newsroom




BERLIN, Ujerumani
MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Inter Milan, juzi walipata kipigo cha aina yake baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na Werder Bremen, katika mchezo wa kundi A uliochezwa juzi usiku mjini Bremen, Ujerumani. Matokeo hayo yamezidisha presha kwa kocha Rafael Benitez kufukuzwa Inter Milan. Mhispania huyo alikumbana na adha hiyo baada ya kupumzisha wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza. Timu hiyo imefuzu hatua ya 16 bora na inaongoza kundi hilo ikifuatiwa na Tottenham Hotspurs. Inter Milan imepoteza mechi saba katika michuano msimu huu, matokeo hayo yanalingana na aliyowahi kuyapata kocha wa zamani wa timu hiyo, Jose Mourinho, aliyetua Real Madrid. Sebastian Proedl, Marko Arnautovic na Claudio Pizarro waliifungia Werder Bremen mabao hayo.

Kiungo Mbrazil, Anderson, aliiokoa Manchester United isiadhirike kwa kufunga bao la kusawazisha dakika ya 62 dhidi ya Valencia, ikiwa kwenye uwanja wake Old Trafford. Pablo Hernandez alimpa presha Sir Alex Ferguson baada ya kutangulia kufunga dakika 32 katika mchezo huo wa kundi C.
United ilikosa nafasi nyingi za kufunga kupitia kwa mchezaji Dimitar Berbatov, aliyefunga mabao matano katika mchezo wa ligi dhidi ya Blackburn Rovers, ambao kigogo hicho kilishinda 7-1. Anderson angeweza kufunga bao lingine kama angetumia vyema pasi ya Wayne Rooney.
Nayo Tottenham Hotspurs imekwepa kukutana na vigogo wa Ulaya katika mechi za mtoano, baada ya kulazimisha sare mabao 3-3 dhidi ya FC Twente katika mchezo wa kundi A uliokuwa na upinzani mkali.
Mabao mawili yaliyofungwa na wachezaji, Andreu Fontas na Victor Vazquez yalitosha kuipa ushindi wa mabao 2-0 Barcelona, ilipovaana na Rubin Kazan kwenye Uwanja wa Nou Camp.
Barcelona tayari ilikuwa inaongoza kundi D na hadi sasa haijafungwa msimu huu. Kocha Pep Guardiola aliwatumia wachezaji wa akiba dhidi ya klabu hiyo kutoka Russia. Fantas alifunga bao la kwanza dakika ya 51 baada ya kupokea pasi ya Thiago Alcantara,
na Vazquez aliongeza la pili dakika ya 82.
Katika mchezo mwingine, Rangers ikiwa ugenini ililazimisha sare ya bao 1-1 ilipokwaana na Bursaspor kwenye Uwanja wa Ataturk, Lyon ilipata sare ya 2-2 dhidi ya Hapoel Tel Aviv, wakati Schalke iliipa kipigo Benfica kwa kuilaza mabao 2-1. FC Copenhagen ilitakata baada ya kuibanjua Panathinaikos mabao 3-1.
 
14 kushiriki Kombe la Taifa netiboli

Wednesday, 08 December 2010 19:35 newsroom



NA DEUSDEDIT UNDOLE
TIMU za mikoa 14 zimethibisha kushiriki michuano ijayo ya Kombe la Taifa la mchezo wa netiboli, ambalo litafanyika kati ya Desemba 16 na 23, mwaka huu mkoani Pwani. Michuano hiyo ambayo kwa kawaida hufanyika kila mwaka, msimu huu imepangwa kufanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Filbert Bayi, vilivyoko kijiji cha Mkuza mkoani humo. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Rose Mkisi alisema michuano hiyo itachezwa kwa kuzishirikisha timu za mikoa pekee iliyothibisha.

Alisema hatua hiyo inatokana na ukweli kuwa chama chake kilitoa muda mrefu na wa kutosha, ili viongozi wa mikoa waweze kufanya uteuzi wa wachezaji sambamba na kuthibisha kwa barua kuhusiana na ushiriki wao.
Rose alisema lakini hadi Novemba 30, mwaka huu ambapo ilikuwa mwisho wa mchakato wa kuithibitisha, alisema ni idadi hiyo ya mikoa 14 ambayo ilitekeleza kwa wakati agizo la kutihibisha ushiriki kwa njia ya barua.
"Hatuna tena muda mwingine wa kuwalazimisha viongozi waliosalia wa mikao tisa iliyosalia kufanya hivyo kwa wakati, lakini badala yake tutaendesha michuano kama ilivyopangwa na kuzishindanisha timu za mikoa zilizotibisha ushiriki kwa barua," alisema.
Kaimu Katibu mkuu huyo, alizitaja timu za mikoa zilizothibisha kushiriki kinyang'anyiro hicho kuwa ni Morogoro, Temeke, Kinondoni, Ilala, Mbeya, Tanga, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Arusha, Iringa, Tabora, Lindi na wenyeji wa michuano hiyo Pwani.

Alisema timu za mikoa shiriki kwenye michuano hiyo zinapaswa kuzifanyia maandalizi mazuri timu zao, kwani alisema kwa kufanya hivyo kutaoingeza ushindani na msisimko wa michuano hiyo mikubwa nchini ya netiboli.
"Tunatoa wito tu kwa viongozi wa timu shiriki kuzianda vema timu zao, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuongeza ushindani na msisimko wa kinyang'anyiro hicho ambacho hufanyika mara moja kwa mwaka," alisema.
 
Yani kichwa kimeshindwa kushika hili wala lile

Uwe unaanzia ukurasa wa mwisho yaani kwa hivi sasa ni ukurasa wa 8 ndiyo utakuta habari za leo.....vinginevyo utachoka kabisa..........
 
Stars send Rwanda packing


By ABADALLAH MSUYA, 8th December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 288

HEAVY down pour could not prevent Kilimanjaro Stars from advancing into the semifinals of the Cecafa Tusker Challenge Cup, with a 1-0 hard fought victory over Rwanda's Amavubi in a closely contested quarterfinal clash at National Stadium on Wednesday.

It was a mixed emotion for the country's football as Zanzibar Heroes crashed out of the regional championship after they were beaten 5-3 by the defending champions Uganda Cranes on post match penalty shootouts.

Stars skipper Shadrack Nsajigwa emerged the hero after clinically dispatching a 62nd minute penalty that gave the home lads all the important victory in the match that was nearly disrupted by a heavy rain that poured over the city late in the evening on Wednesday.

Referee Bamla Tessema awarded the penalty after Stars' striker John Bocco who replaced Henry Joseph after the restart, was bundled down by two of the Rwanda's defenders as he powered his way into the 18-yard area.

The Amavubi players protested against the decision claiming that it was a fair challenge,
but Tessema stood by his decision and Nsajigwa kept his cool as stepped up to burry it into the back of the net, sending thousands of home supporters wild.

Jan Poulsen started with the same lineup that played against Burundi, but was forced to make early substitution, when he replaced injured Mohamed Banka by Jabir Aziz after only 33 minutes.

The first half lacked the spark as Stars looked nervous and short of ideas up front, while Rwanda opted for a defensive game, occasionally trying to hit on the counter attacks.

Rwanda had the game's first meaningfully chance after nine minutes, when Jean Iranzi teased Stars Nsajigwa and Juma Nyosso before releasing a nice ball in that narrowly evaded Haruna Niyonzima and Daddy Birori with Stars goalkeeper Juma Kaseja already lost on the way.

Stars could have opened the scoring after 20 minutes, following a good work by Mrisho Ngasa on the right wing, but Nurdini Bakari, scorer of two goals against Burundi missed out as he attempted to head the cross from barely six yards.

Kaseja was called into action and made a heroic save to deny Abouba Sibomana, who had raced clear into the Stars' penalty box.

Poulsen made tactical changes after the restart. Bocco came in to replace Henry, while Bakari moved to the central midfield.

Stars showed resurgence after the changes, with Bakari driving the team to great effect.

In the first quarter final match, defending champions Uganda Cranes advanced to the semi finals after beating Zanzibar 5-3 on penalties after a 2-2 draw in regular time.

Simba's striker Emmanuel Okwi produced a man of the match display, setting up Mike Sserumaga, who clinically gave Uganda the lead after 13 minutes. However, Zanzibar pulled level just before the interval from a free kick, well taken by Khamis Mcha.

After the break, both teams wasted clear goal scoring chances.

However, it was the Cranes who looked more dangerous going in front. The record 11 times champions regained their lead from the penalty spot after former Yanga midfielder Steven Bengo was fouled in the penalty area and the referee was quick to point to the spot.

kwi stepped up and he made no mistake,sending Heroes goalie Mwadini Ali Mwadini the wrong way from the resultant spot kick.

Uganda were left to rue hosts of scoring chances that went begging, when Aggrey Morris made it two all with three minutes remaining only to send the game to penalties.

Cranes custodian Robert Odongkara, saved Agrrey Morris's poorly taken spot kick in the penalty shootout as Uganda Cranes' Isinde Isaac, Sadam Juma, Godfrey Walusimbi, Tonny Mawejje, and Okwi, who capped off a great game by scoring the decisive spot kick.

Heroes' penalties were converted by skipper Nadir Haroub, Wazir Salum and Abdulhalim Humoud.

The Cranes will now play Stars in ton Friday's semifinal, with the other semifinal pitting Ivory Coast against Ethiopia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom