Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Daktari wa Kijapani acheza ngoma ya marehemu Mwinamila
Saturday, 11 December 2010 20:57

Habel Chidawali, Dodoma

IMEELEZWA kuwa utamaduni wa Mtanzania unadidimizwa na Watanzania wenyewe kutokupenda ngoma zao na badala yake wanapenda kushabikia utamaduni wa nje.

Hayo yalisemwa jana na Dk Seigo Usami, Mganga wa Kitendo cha Mifupa na viungo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambaye ni msanii katika kikundi cha Sanaa cha Hiari ya Moyo ambacho kiliasisiwa na msanii maarufu marehemu mzee Mwinamila.
Dk Usami (30) alieleza masikitiko yake kuwa hakuna nchi iliyojaliwa kuwana makabila mengi kama Tanzania, lakini ambayo kila kabila linakuwa na utamaduni wake jambo linalofanya nchi hii kuwa na utajiri wa utamaduni.

Usami alisema kuwa kama serikali ya Tanzania pamoja na Watanzania wenyewe wakiamua kuamka na kuanza kuupenda utamaduni wao ni wazi kuwa hakutakuwa na ngoma nyingine itakayotoka nje ya nchi ambayo itapata nafasi katika nchi hii.
Alisema katika nchi zingine ikiwemo Japan, ngoma za asili ni nadra sana kuziona ingawa wamekuwa wakizisoma katika vitabu kwamba zilikuwepo, lakini hivi sasa hakuna kitu na hivyo akashauri ni vema Tanzania ikawa na tahadhari hiyo.
Akizungumzia kuhusu nini kilimsukuma kujiunga na ngoma ya hiari ya Moyo "kwanza napenda utamaduni kuliko kitu kingine na utamaduni ni sehemu ya pili katika maisha yangu kwani sehemu yangu ya kwanza ni kazi yangu"
"Mimi nilikuja Tanzania Januari mwaka jana (2009) na ninafanya kazi ya kujitolea hapa Tanzania (Volunteer) kupitia Shirika JICA kwa muda wa miaka miwili na kwamba mkataba wangu unakwisha Januari mwakani hivyo nitakikosa sana kikundi hiki ambacho nakwenda Japan nikiwa bado nakipenda" alisema Usami.

Kwa upande wake alisema kuwa alijiunga na Hiari ya Moyo Januari Mwaka huu, baada ya kuwaona katika maeneo kadhaa wakitoa burudani ndipo akavutiwa nao na kuamua kuomba nafasi ya kujiunga jambo ambalo alisema lilipokewa kwa mikono miwili na viongozi wa kikundi hicho.

Akizungumzia tofauti ya ngoma za Tanzania na Japan alisema kuwa kwao kuna ngoma zinazotaka kufanana na hizo ambazo hata hivyo alikiri kuwa zilibuniwa kutoka Afrika Mashariki bila ya kutaja ni nchi gani ya Afrika Mashariki zilipobuniwa ngoma hizo.

Alisema haoni shida kucheza ngoma ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya ajabu ambayo hutumiwa na wasanii na mazingira wanayofanyia kazi zao.

Kuhusu vipi anatenga muda wake wa kazi pamoja na mazoezi ya kikundi alisema "Kazini ninaingia saa mbili asubuhi na ninafanya kazi hadi saa tisa, lakini kule ninaingia kwenye mazoezi kuanzia saa 10 hadi saa 12 jioni kila siku hivyo sina shida"
Kuhusu ushirikia katika sherehe alisema pia hakuna shida kwani tangu alipoajiunga na kikundi hicho kila wanapoitwa kwenye michezo huwa anatoa taarifa kwa mkuu wake wa kazi na wanamruhusu bila ya shida.

Alisema ilimchukua muda wa miezi mitatu tangu alipojiunga na kikundi hicho akawa anaweza kucheza kila aina ya mtindo unaochezwa na kikundi hicho pamoja na kuimba nyimbo zao ingawa kwa Kiswahili cha tabu.
"Kinachonifurahisha zaidi ni mtindo wa kukata viuno ambao tunashiriki pamoja na wanawake na wanaume kwa pamoja jambo ambalo si rahisi kwa sisi Wajapani kufanya hivyo na si kwamba hatuwezi ila hatuna ubunifu huo", alifafanua.
Alieleza kuwa iko tofauti kubwa kati ya ngoma aliyowahi kuiona kule Japan na hapa Tanzania, kwani, ile ya Japan ngoma moja inapigwa na watu zaidi ya watatu ilihali hapa Tanzania mtu mmoja anaweza kupiga ngoma zaidi ya tano kwa wakati mmoja kitu alichosema ni ubunifu wa hali ya juu.

Mganga huyo alisema kuwa anasikitishwa sana na kitendo cha ujira mdogo ambao hulipwa wasanii wa Kitanzania kwani alisema kuwa ni kidogo kulinganisha na burudani wanayoitoa jambo alilosema ni lazima serikali iliangalie upya vingine wanawavunja moyo wasanii.

Ngoma nyingine ambazo anazipenda Usami ni pamoja na disko na ngoma za makabila ya Kitanzania ambapo alisema disko huenda kupoteza muda, lakini hafikirii sana kujifunza kuliko ngoma za makabila ambazo alisifia kuwa hata akirudi Japan yuko tayari kutenga muda wake na kuwafundisha raia wa huko huku akiahidi kuwa atakipeleka Japan Kikundi cha Hiari ya Moyo ili wakaimbe na kucheza pamoja.

Akiwa katika kikundi Chake cha Hiari ya Moyo ambacho mwanzilishi wake ni Mwinamila, Usami anajua kucheza,kupiga ngoma pamoja na kuimba na hakuna tofauti yoyote kati yake na wakongwe wa sanaa hao wanapokuwa Jukwaani.
Kwa upande wa madaktari wanaofanya kazi pamoja na msanii huyo wanasema kuwa alichokifanya ndicho ambacho hata wao wanapokuwa nchi za nje huwa wanafanya kwa kuiga ngoma za watu wengine.

"Hata sisi huwa tunaiga ngoma za wenzetu tukiwa huko nje ya nchi kwani si unajua kuwa mtu akitoka Tanzania na kwenda Ulaya huwa anarudi akiwa ameweza kuiga ngoma za kigeni ikiwemo miziki ya Dansi hivyo hata yeye ni haki yake" alisema mmoja wa madaktari ambaye aliomba jina lake lisiandikwe.
 
Kili Stars tupeni raha
• Ngassa, Banka nje, Poulsen atamba ushindi

na Dina Ismail


amka2.gif
KAMA kuna kitu kitakachowaumiza, kuwaliza ama kulidhalilisha Taifa la Tanzania ni pale leo timu ya Taifa ya Bara ‘Kilimanjaro Stars' ikishindwa kutwaa kwa mara ya tatu ndani ya miaka 74 ya uhai wa Kombe la CECAFA Chalenji ambalo ni kongwe kabisa barani Afrika.
Stars inashuka dimbani kukwaana na Ivory Coast ambapo ilikata tiketi hiyo juzi baada ya kuivua ubingwa Uganda katika nusu fainali kwa matuta 5-4.
Kombe la Chalenji lilianzishwa rasmi mwaka 1926 wakati huo likiitwa Gossage Cup, ambapo Tanzania Bara imefanikiwa kulitwaa mara mbili tu mwaka 1974 na 1994, hivyo leo kuna kiu kubwa kwa Watanzania kuona kombe hilo linabaki katika ardhi ya nyumbani.
Kiu hiyo ni kutokana na ukame wa muda mrefu wa mataji katika medani ya soka hapa nchini ambapo juzi morali ya Watanzania ilipanda na imebaki katika kiwango cha juu baada ya kushuhudia timu yao Kili Stars ikiwaondosha waliokuwa mabingwa watetezi wa kihistoria Uganda ‘The Cranes' kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 5-4.
The Cranes ndiyo inayoongoza kwa kulitwaa kombe hilo ikiwa imefanya hivyo mara 11, hivyo ushindi huo wa nusu fainali hakika umewaweka Watanzania katika mkao wa kushangalia kombe, wakiamini ng'ombe kishaliwa kila kitu kilichobaki ni mkia tu.
Kutokana na mazingira hayo yaliyojengeka hivi sasa, hakika wachezaji wa Stars wajue mzigo mkubwa walionao kutokana na kazi nzuri waliyoifanya hadi leo, itakuwa haina maana endapo watashindwa kutwaa taji hilo dhidi ya Tembo wa Ivory Coast na kunogesha furaha ya Watanzania waliokuwa nayo toka juzi.
Hivi sasa karibu kila shabiki anaamini kuwa leo ni furaha kwa Watanzania, hivyo hali ikitokea kinyume chake itakuwa ni pigo kubwa kwa Watanzania hasa ukizingatia wanacheza ardhi ya nyumbani.
Akizungumzia mechi ya leo, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, Jan Poulsen, amesema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao kuwa imara sambamba na kusheheni vijana mahiri, lakini amejipanga kukabiliana nao, bila ya mshambuliaji wake Mrisho Ngassa mwenye kadi mbili za njano.
Poulsen alisema Ivory Coast ni timu iliyojipanga vilivyo kimchezo ambapo inaitumia michuano hii kama maandalizi ya michuano ya kimataifa na hasa ile inayoshirikisha nyota wanaocheza ligi za ndani (CHAN).
Alisema pamoja na ubora wa Ivory Coast kikosi chake kiko katika hali bora ya ushindani kwa sababu kutokana na mazoezi aliyowapa vijana wake wako katika hali nzuri ya ushindani, huku mmoja wa wachezaji wake Mohamed Banka pia akiukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa majeruhi aliyoyapata katika mashindano hayo.
Poulsen alisema kiungo, Henry Joseph, ambaye alikuwa akisumbuliwa na malaria amepata nafuu na leo atakuwa mmoja ya wachezaji ambao watavaa jezi za timu hiyo katika kusaka ubingwa.
Naye nahodha wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa alisema wanashukuru kutinga fainali za mashindano hayo ingawa mchezo wa nusu fainali kati yao na Uganda ulikuwa ni mgumu sana kwa sababu walicheza na bingwa mtetezi.
Alisema ugumu huo walipambana nao ipasavyo na kuibuka a ushindi huo wa matuta ambao uliwakatia tiketi ya fainali.
Nsajigwa alitoa wito kwa Watanzania kuwapa sapoti kwa kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa leo ambao utakuwa ni wa vuta nikuvute.
Mbali na mechi hiyo ya fainali, pia kutakuwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu ambapo Uganda itakwaana na Ethiopia huku baraza la vyama vya soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) likisema maandalizi yamekamilika.
 
Azam Fc yamdaka kocha wa Znz Heroes
• Kusaini mkataba leo

na Dina Ismail


amka2.gif
BAADA ya mchakako wa muda mrefu wa kusaka kocha, hatimaye klabu ya soka ya Azam imemnasa kocha wa timu Zanzibar ‘Zanzibar Heroes' Muingereza Stewart Hall na leo anatarajiwa kuingia mkataba wa kuinoa timu hiyo.
Hall anamaliza mchakato wa muda mrefu wa klabu hiyo kusaka kocha atakayerithi mikoba ya aliyekuwa kocha wake Mbrazil Itamar Amorin aliyetupiwa virago kutokana na kushindwa kuipatia mafanikio timu hiyo.
Habari kutoka ndani ya uongozi wa Azam zinasema kwamba pamoja na kuwepo kwa makocha wengi waliotuma maombi kutoka ndani na nje ya nchi lakini waliachana nao na kuamua kuzungumza na Hall.
Kiongozi mmoja wa Azam aliliambia Tanzania Daima kuwa kutua kwa Hall kunafuatia mazungumzo baina yao na Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kabla ya kuridhia kumuachia kocha huyo kwa makubaliano maalum.
Alisema, kilichowafanya waridhie ni kutokana na Zanzibar Heroes kutokabiliwa na mashindano katika siku za usoni na kama yatatokea atakwenda kuwasaidia kwani itakuwa ni kwa kipindi kifupi.
"Unajua sasa hivi Zanzibar Heroes haina mashindano itakayoshiriki sana ni timu ya Taifa ya Vijana ambapo hata hivyo ZFA imesema anaweza kuwa mshauri wa ufundi," alisema kiongozi huyo.
Aidha, kiongozi huyo aliongeza kuwa pamoja na kocha huyo kutua Azam lakini atashirikiana na ZFA katika kutafuta kocha atakayerithi mikoba yake.
 
Azam Fc yamdaka kocha wa Znz Heroes
• Kusaini mkataba leo

na Dina Ismail


amka2.gif
BAADA ya mchakako wa muda mrefu wa kusaka kocha, hatimaye klabu ya soka ya Azam imemnasa kocha wa timu Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ Muingereza Stewart Hall na leo anatarajiwa kuingia mkataba wa kuinoa timu hiyo.
Hall anamaliza mchakato wa muda mrefu wa klabu hiyo kusaka kocha atakayerithi mikoba ya aliyekuwa kocha wake Mbrazil Itamar Amorin aliyetupiwa virago kutokana na kushindwa kuipatia mafanikio timu hiyo.
Habari kutoka ndani ya uongozi wa Azam zinasema kwamba pamoja na kuwepo kwa makocha wengi waliotuma maombi kutoka ndani na nje ya nchi lakini waliachana nao na kuamua kuzungumza na Hall.
Kiongozi mmoja wa Azam aliliambia Tanzania Daima kuwa kutua kwa Hall kunafuatia mazungumzo baina yao na Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kabla ya kuridhia kumuachia kocha huyo kwa makubaliano maalum.
Alisema, kilichowafanya waridhie ni kutokana na Zanzibar Heroes kutokabiliwa na mashindano katika siku za usoni na kama yatatokea atakwenda kuwasaidia kwani itakuwa ni kwa kipindi kifupi.
“Unajua sasa hivi Zanzibar Heroes haina mashindano itakayoshiriki sana ni timu ya Taifa ya Vijana ambapo hata hivyo ZFA imesema anaweza kuwa mshauri wa ufundi,” alisema kiongozi huyo.
Aidha, kiongozi huyo aliongeza kuwa pamoja na kocha huyo kutua Azam lakini atashirikiana na ZFA katika kutafuta kocha atakayerithi mikoba yake.
 
Cecafa yaongeza zawadi za washindi


na Dina Ismail


amka2.gif
WAKATI leo michuano ya Chalenji inafikia tamati, Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeongeza zawadi kwa washindi wa michuano ya mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholaus Musonye, alisema jana kwamba maandalizi kwa ajili ya fainali ya leo yamekamlika na hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.
Alisema mbali na zawadi za mshindi wa kwanza hadi wa tatu, pia kutakuwa na zawadi ya mfungaji bora, kipa bora, timu yenye nidhamu na mchezaji bora ‘best fair player'.
Hata hivyo Musonye hakutaka kuziweka wazi zawadi hizo zaidi ya kutaja zile za mshindi wa kwanza (dola 30,000), mshindi wa pili (dola 20,000) na mshindi wa tatu (dola 10,000), huku pia washindi hao wakikabidhiwa medali.
Aidha, Musonye ameishukuru serikali, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na makampuni yaliyojitokeza kudhamini mashindano hayo ikiwemo Vodacom, Serengeti Breweries (SBL), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Airtel na wengineo.
Musonye pia amewapongeza Watanzania kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi chote cha mashindano na sambamba na amani waliyoonyesha.
 
JK kuzindua UMITASHUMTA


na Juma Kasesa


amka2.gif
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuzindua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Desemba 14 mjini Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya Elimu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa, alisema, serikali imeamua kurudisha michezo hiyo kwa lengo la kusaka vijana wenye vipaji katika michezo mbalimbali.
Alisema michezo hiyo ambayo ilifanyika mara mwisho mwaka 2000, itakuwa msaada mkubwa katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo kwa kuwa vijana wengi wenye vipaji wako mashuleni wakihitaji kuendelezwa ili kulisaidia taifa katika sekta hiyo.
Majaliwa alisema uwepo wa mashindano hayo utapanua soko la ajira kwa wachezaji watakaofanya vyema na kuinua uchumi pamoja na hadhi ya wachezaji binafsi, klabu zao na Taifa kwa ujumla.
"Michezo ni sekta ambayo inaweza kuajiri vijana katika michezo mbalimbali ambapo pia itawawezesha kuweka miili yao kuwa na afya njema kukabiliana na lolote," alisema Majaliwa.
Alisema Mikoa 10 imeshathibitisha kushiriki ambayo ni Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Mbeya, Iringa, Dodoma na Singida na kufafanua kuwa mwakani mikoa yote ya Tanzania itashiriki.
Aidha alisema kila mkoa unatarajia kushirikisha wanafunzi 60 ambao watashindana katika soka, netiboli, na riadha ambapo kwa mwaka huu mikoa ya Dar es Salaam na Tabora imepata bahati ya kutoa wanafunzi wenye uhitaji maalum katika michezo hiyo.
Alitoa wito kwa walimu katika shule mbalimbali nchini kuanza kuwatumia kikamilifu walimu wa michezo ili kufanikisha mkakati huo Serikali katika kuibua vipaji vya wachezaji katika shule.
 
Mathew amsifia Nsajigwa


na Makuburi Ally


amka2.gif
ALIYEKUWA mchezaji wa timu ya soka Tanzania ‘Taifa Stars', Suleiman Mathew, amemmwagia sifa beki wa kulia wa timu ya Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa, kwa kuonyesha umahiri katika mashindano ya CECAFA Tusker yanayofikia tamati leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mathew alisema Nsajigwa ameonyesha umahiri kwa kulibeba jahazi la timu ya taifa ambalo leo linafikia tamati.
Mathew alisema kiwango kilichoonyeshwa na Nsajigwa kinapaswa kupambwa na Watanzania wengi kutokana na kwamba amekubali kazi aliyopewa ambayo ni kuwaongoza wenzake wawapo uwanjani.
"Nsajigwa kwa kweli amekubali kazi aliyopewa na kocha Mkuu Jan Poulsen ambayo matunda yake yanaonekana kwa Stars kucheza fainali baada ya kuwatoa mabingwa watetezi, Uganda," alisema Mathew.
Mathew alisema Nsajigwa alikubali jahazi alilopewa hata wakati wa upigaji wa mikwaju ya penati ambapo alifanikiwa kufunga bao.
 
Sunday December 12, 2010 Sports
Stars inches closer to trophy

By SUNDAY NEWS Reporter, 11th December 2010 @ 16:00, Total Comments: 0, Hits: 38

MAINLAND Tanzania could end their 16 years drought by winning the Cecafa Tusker Challenge Cup on Sunday, if they beat guest side Ivory Coast in the final match at the National Stadium in Dar es Salaam.

Kilimanjaro Stars Coach Jan Poulsen has said it is not going to be easy against the young Ivory Coast side, who have surprised many by reaching this far, especially after their low key start into the tournament.

However, he remained optimistic that his team will be buoyed by their Friday's big semifinal win against the then favourites Uganda Cranes to give Tanzanians a perfect Christmas gift.

"Facing Ivory Coast will be tough because they are just as physical and tough as Uganda. We have few hours to prepare before the match but we will pick ourselves up and get ready for the final," said Poulsen.

Stars edged out defending champions Uganda Cranes 5-4 on post match penalties to qualify for today's final.

After a barren stalemate in regulation and extra time, Juma Kasseja's save off a Tony Maweije penalty sparked off huge party as close to 50,000 strong crowd celebrated a momentous win for Kilimanjaro Stars who made it to their first final in eight years.

Poulsen was delighted with the win, "It was very even because the first half was not so good but we dominated the second half creating many chances. Our problem remains the same; we are not able to put the ball in the back of the net."

He added that the crowd had played its part in the team's win, "The crowd was really the 12th man on Friday as they rallied behind the boys and gave them energy throughout the match.''

In today's final, Stars will have to do without influential wing wizard Mrisho Ngasa, who is serving a match ban after picking two yellow cards.

Stylish midfielder Mohamed Banka is also certainly out of the clash due to injury but there is a slight hope that Norway based Henry Joseph could return in the team on Sunday, after missing the match against Uganda due to injuries.

Uganda coach Bobby Williamson whose team suffered its first defeat in 16 Cecafa matches stretching back to 2008 during which they have won it two years in a row is confident that Kilimanjaro Stars will go all the way to win the trophy.

"We played well but the referee had a bad game. He should have sent off a Tanzanian player just before halftime but he didn't and I think he was poor. But congratulations to Tanzania, they worked hard and deserve to go through," Williamson said.

He added: "Hopeful Kilimanjaro Stars will win the trophy and keep it in the region.
 
Msola warns Stars players

By SUNDAY NEWS Reporter, 11th December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 146

FORMER Mainland and Taifa Stars Coach Mshindo Msola, has warned Kilimanjaro Stars players that they may languish in obscurity playing at home, if they are not on their guard.

Kilimanjaro Stars desperately want a win to end their under achiever's tag in the regional championships and here comes the scary part for them, when they face Ivory Coast in the Cecafa Tusker Challenge Cup final at the National Stadium in Dar es Salaam.

And Msola believe that Kilimanjaro Stars are favourites to win the trophy today, if they stick to the nitty-gritty of playing football. He said the team should learn to limit wasting passes and scoring chances.

Msola is still staggering from the memory of losing the 2002 final match to Kenya's Harambee Stars when he was the Kilimanjaro Stars coach. The match played at the CCM Kirumba Stadium in Mwanza saw Kenya lifting the trophy in front of packed stadium after posting a shocking 2-1 win.

"Players should be reminded that there are disadvantages of playing at home. They would be put to a lot of pressure by pregnant fans, who are eager to see their team lifting the trophy after many years of daydreaming.

"Fans will be pushing the players to deliver and sometimes this could affect them psychologically. Players just need to be focused and keep their concentration…they should control their emotions and fears," said Msola, who is a respected local coach.
 
Sunday December 12, 2010 Sports

Taifa Queens beat Namibia in Singapore meet



By SUNDAY NEWS Reporter/Agencies, 11th December 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 71

THE national netball team is reaping from excellent tactics by their Australian coach Simone McKinnis, beating Namibia 45-37 at the ongoing Six Nations Cup in Singapore.

It was the third consecutive victory for the Taifa Queens of Tanzania ladies in the championships that saw them settling third on the table. Both teams started well with Tanzania beginning to pull ahead at the end of the first quarter leading 12 – 7.

The Namibian’s failed to make up the point deficit entering half time 26 – 18 and trailed by a similar margin for the rest of the match to lose 45 – 37. The introduction of Namibian Wing Attacker (WA), Rhuu Hengua in the final quarter shook things up with Namibia winning the quarter 10-11.

Unfortunately it was too little too late as Tanzanian Goal Shooter (GS), Mwanaidi Hassan used her height in the circle to convert 96 per cent of attempts to retain the lead. Namibia is now firmly in a bottom two play off position having lost four out of four games so far.

Following their third win in a row, Tanzanian Head Coach Simone McKinnis, said: “I am happy to have the win but I don’t think it is as good a performance as we should have put out there.'' Taifa Queens were set to play against second placed Wales in the decisive match late on Saturday and McKinnis promised to lift her team’s game.

“We will be turning out to win that match and get ourselves into the final,” she said on Friday. In previous matches Taifa Queens beat Singapore 52-36, thumping India 60-27. They only lost their first match against Scotland, the highest ranked team in the competition at 16th, by 46-33.

Hosts Singapore fell 39-49 to Wales to leave them with two wins and two losses. Singapore are now out of the running for the final.
 
Tanzania have no fear for Ivorians



By CHARLES NYENDE in DAR ES SALAAM cnyende@ke.nationmedia.comPosted Saturday, December 11 2010 at 20:31




Sunday's final between Tanzania and Cote d'Ivoire at the National Stadium has nothing to do with Ethiopia but their coach Ifem Onuora pretty much summed up the prospects the hosts were facing.

"They (Cote d'Ivoire) will take some stopping," Onuora said of the West Africans.





Indeed, Cote d'Ivoire's progress to the final has resembled a snowball gathering mass and pace at it rolls down the hill.

After losing 2-1 to Rwanda in their opening match the Elephants won their next four games, scoring six goals in the process to stand on the brink of winning the title in their first appearance as guests.



Their coach, Georges Kouadio, has confidently talked about his country playing beautiful football to win matches and how they will plot to snatch the title from the hosts.



Tanzania coach Jan Poulsen pushed up the psychological duel a notch higher, saying their tough 5-4 post-match penalty semi-final win over Uganda after 120 minutes of open play had drained his team.



Play their hearts out


"We played for two hours in the semi-finals two days after playing in the quarters and two days later we will play in the final. You may see tired legs out there," he said.



Whatever their physical state, Kilimanjaro Stars have scented blood and will, just like they did in the semi-finals, play their hearts out to reclaim the trophy they last won in 1994.



Curiously, despite hosting the championship six times, Tanzania have only won it once at home, way back in 1974.



"Other teams have gotten used to beating us at home. But now we have refused. The cup will remain here," Godfrey Mwambugu, a hotel worker in Dar es Salaam, said.



Kili Stars' genuine quality is the diminutive Mrisho Ngasa, who has tormented defences with his pace. The home team has also demonstrated tonnes of sheer determination backed by a partisan crowd of some 60,000 fans that will be a key factor in the game.

Poulsen has also shown a fluid tactical mind, switching players and positions with each game, and is bound to have a card up his sleeve on Sunday.



Cote d'Ivoire certainly have that extra class in Kipre twins Bolou and Tchetche, Marc Goua and Co. but you feel this match will be decided by the team with the strongest desire to win.



Winners will walk away with $30,000 (Sh2.4 million), runners-up $20,000 (Sh1.6 million) and second runners-up $10,000 (Sh800,000)
.

Sunday matches – Final: Tanzania v Cote d'Ivoire (3.30 pm); Third-place play-off: Uganda v Ethiopia (1.30 pm)
 
Tomorrow's final brought forward


Published on 10/12/2010


The kick-off for the final of this year's Cecafa Tusker Cup has been brought forward to 3.30pm tomorrow and will be aired live by SuperSport, which has been screening live all the matches since the tournament kicked off two weeks ago.


The third-place match is expected to kick off at 1.30pm, and will also be aired live.
Winners of this year's event are expected to pocket Sh2.4 million (30, 000 dollars), while runners-up will go home with Sh1.6 million (20, 000 dollars) and third-placed team will go home with Sh800, 000 (10, 000 dollars).


Meanwhile, with almost two 10 months to go before Harambee Stars face arch rivals Uganda in a crucial Africa Cup of Nations qualifier in Kampala, Cranes players have already started plotting for the match and their skipper at the ongoing Cecafa Tusker Cup. Andrew Mweisigwa has told Stars not to expect any point in Namboole.
Uganda beat Kenya 2-0 to knock out Stars from the regional event and Mweisigwa believes they will give Kenya a similar treatment in Kampala on October 9.


"We have never lost a match in Nambole since 2002, when we were lost to South Africa. Teams like Nigeria and Angola have lost there and Kenya should not expect any point there," said Mweisigwa.
 
Crack the whip on errant bodies, VP urges Sports Minister Otuoma


Updated 11 hr(s) 57 min(s) ago


By Oscar Pilipili



The Government has issued a stern warning and declared it would no longer entertain leaders of non-performing sports federations.


In reference to embattled football administration, Vice President Kalonzo Musyoka urged his Sports counterpart Paul Otuoma to "crack the whip" and ensure Kenya qualifies for 2014 Fifa World Cup in Brazil.


Kalonzo told Otuoma that he posseses full authority to streamline federations that don't develop sports.
The Vice President congratulated athletes who excelled at Soya and urged them to maintain the standards for their own benefits.
"Sports is no longer a hobby but a big socia-economic activity," Kalonzo said during the ceremony at Kenyatta International Conference Centre Friday night.
Otuoma told the Soya gathering that the Government was moving fast to restore sanity in football.


"We've put Fifa on notice and we're not going to allow a limited company run football. Football is run by federation," Otuoma said in reference to Kenya Football Limited which claim authority over local football.


Otuoma was categorical that football elections must be conducted by March and asked all stakeholders to support the cause.
Otuoma?s reaction on football was expected after Soya chairman Chris Mbaisi wondered why administrators were left to mess up the sport in the country.


"Are these Kenya Football Federation and Football Kenya Limited untouchable, Mr Minister?" Mbaisi asked in his key speech.
Safaricom Managing Director Bob Collymore said the company has a long standing relationship with sports in the country.
This, he said, has seen the company invest heavily in the sponsorship of sporting disciplines among them: athletics, rugby, lawn tennis and football.



"Our sponsorship and effort to relaunch Kenya's premier rugby tournament as a wholesome family under the Safaricom Sevens brand was recently recognised by the Public Relations Society of Kenya (PRSK) winning the 2010 Sponsorship Campaign of the Year Award," he said.


Collymore said Safaricom was keen on developing local talent through sponsorship of sports events which helps in tapping talent which goes on to conquer on the global arena.
 
Kili Stars wee acha tu...


na Makuburi Ally na Juma Kasesa


amka2.gif
TIMU ya soka ya Tanzania Bara, Kilamanjaro Stars, jana ilifanikiwa kunyakua taji la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA Tusker Chalenji Cup' baada ya kuiadhibu Ivory Coast kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kilimanjaro imeandika historia kwa mara ya tatu kunyakua ubingwa huo baada ya kufanya hivyo kwa mara mwisho mwaka 1994 ikiwa chini ya kocha marehemu Syllersaid Mziray na Charles Boniface baada ya kuandaliwa na Sunday Kayuni, ambao walifanikisha ubingwa huo walipoiadhibu Uganda kwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti.
Kabla ya ubingwa huo, Kilimanjaro ililitwaa kwa mara ya kwanza mwaka 1974 na mwaka huu imeunyakuwa ubingwa ikiwa chini ya kocha Mdenish, Jan Poulsen, ambaye alichukua nafasi ya Mbrazil Marcio Maximo aliyemaliza muda wake, Juni 21, mwaka huu.
Stars jana iliibuka bingwa wa michuano hiyo kwa mkwaju wa penalti katika dakika 42 uliopigwa na nahodha Shadrack Nsajigwa baada ya beki wa Ivory Coast, N'goran Kouassi, kulinawa shuti lililopigwa na Salum Machaku.
Awali kabla ya mchezo huo, mashabiki wapatao 60,000 na wapenzi wa soka wa Tanzania walikuwa wakiishangilia timu hata kabla ya mchezo na kuipongeza huku wakiizomea Ivory Coast kwamba ilikuwa ni siku yao ya kufungwa.
Katika mchezo huo, pengo la mshambuliaji Mrisho Ngassa lilionekana kwa sababu timu haikucheza soka la kueleweka na badala yake, mabeki Kelvin Yondan na Juma Nyosso walifanya kazi ya ziada kuokoa hatari zilizoelekea lengoni kwao, huku nahodha Shadrack Nsajigwa akisaidia mashambulizi langoni kwa Ivory Coast, akisaidiana na Machaku Salum na Jabir Aziz.
Uchezaji uliotumiwa na Stars ulisababisha mabeki kuokoa hatari nyingi langoni kwa Stars.
Katika dakika ya nane ya mchezo, Idrissa Rajab wa Stars alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumizwa vibaya kifuani na beki Bile Georges Eric ambaye alipewa kadi ya njano na mwamuzi wa mchezo huo, Bamlak Tessama wa Ethiopia.
Baada ya kutoka, nafasi yake ilichukuliwa na Kigi Makasi, lakini katika kipindi cha kwanza pengo la mshambuliaji Mrisho Ngassa lilionekana kwa sababu ya timu kutoelewana katika nafasi ya ushambuliaji.
John Bocco alipata taabu kwa mabeki wa Ivory Coast ambao walikuwa wanacheza wanavyotaka.
Pamoja na Stars kucheza chini ya kiwango, bao la Nsajigwa lilidumu hadi mwamuzi Bamlak anapuliza filimbi ya mapumziko, Stars ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Stars ilirejea uwanjani ikiwa na badiliko la Makasi pekee ambaye baada ya dakika chache alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhan Shamte lengo likiwa ni kuongeza ulinzi katika timu hiyo.
Mabadiliko hayo hayakuishia hapo, Poulsen alimtoa, John Bocco, ambaye mashabiki walimzomea mara kadhaa kutokana na kushindwa kumudu mchezo na nafasi yake ilichukuliwa na Henry Joseph ambaye siku chache zilizopita alikuwa akisumbuliwa na malaria.
Katika dakika ya 87, shabiki wa Stars aliingia uwanjani akiwa na jezi ya Stars mkononi na kukimbilia langoni mwa Stars na kumkabidhi kipa Juma Kaseja kabla ya kutolewa nje na polisi waliokuwemo uwanjani hapo.
Ukuta ulioongozwa na Juma Nyosso na Kelvin Yondan ulikuwa imara kwa kuwadhibiti mapacha Kipre Tchetche na Kipre Bolou ambao ndio mwiba wa Ivory Coast.
Aidha kukosekana kwa vituo vya kuuzia tiketi kulionekana kuwakera maelfu ya mashabiki nje ya uwanja na kulazimika kuzinunua kwa baadhi ya watu kwa bei ya kulangua.
Mashabiki mbalimbali waliozungumza na Tanzania Daima waliwalaani waandaji wa mashindano kwa kuwasababishia usumbufu kwa jambo lililokuwa linaweza kuepukika.
Kabla ya mchezo huo, mchezo wa kuwania mshindi wa tatu, Uganda iliiadhibu Ethiopia kwa mabao 4-3, mchezo uliochezwa kabla ya fainali hiyo.
Mabao ya Uganda yalifungwa na Emmanuel Okwi, Kiseka Henry, Matovu Sula na Tony Maweje huku ya Ethiopia yakifungwa na Omod Okwury aliyefunga mawili na Tesfaye Alebachew.
Baada ya mechi kumalizika, kocha Msaidizi wa Stars, Marsh Sylvester, alisema Stars katika michuano hiyo imeonekana ni timu bora kutokana na kufungwa mara moja.
Marsh alisema pamoja na ushindi huo, pengo la Ngassa lilionekana na kuongeza kwamba changamoto hiyo wataifanyia kazi kwa kusaka vipaji zaidi.
Alisema Stars ina upungufu wa sehemu mbalimbali ikiwemo safu ya ushambuliaji ambayo ilionekana kutokuwa na mfungaji.
Kwa upande wake, nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa, alisema uelewano na upendo katika timu yao umesababisha kuibuka na ubingwa huo.
Nsajigwa alisema pamoja na kuibuka na ushindi hawakucheza vizuri lakini walistahili ushindi.
Naye kipa wa Kilimanjaro Stars, Juma Kaseja, alisema tangu wanaanza mashindano hayo walikuwa katika hali nzuri, ingawa maandalizi hayakuwa mazuri sana.
Kuhusu kupewa jezi na shabiki wakati mchezo ukiendelea, alisema hiyo inaonyesha ni jinsi gani mashabiki wanavyomkubali hadi wanamfuata uwanjani na kumtunza jezi.
Bingwa wa mashindano hayo, Kilimanjaro Stars, walikabidhiwa kombe na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, sambamba na medali za dhahabu na dola 30,000 za Marekani kutoka kwa wadhamini kampuni ya bia ya East Africa Breweries Ltd (EABL).
Washindi wa pili, Ivory Coast, walikabidhiwa dola za Marekani 20,000, medali za fedha huku Uganda wakikabidhiwa medali za shaba na dola za Marekani 10,000, huku mchezaji bora wa mashindano hayo, Shadrack Nsajigwa akikabidhiwa nishani sambamba na kipa bora, Juma Kaseja, aliyekabidhiwa nishani.
Wakati shamrashamra hizo zinaendelea, aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni, alikumbatiana na Kaseja, akionyesha kufurahishwa na umahiri wake langoni huku rais wa shirikisho hilo Leodegar Tenga akipatwa na kigugumizi cha furaha kutokana ushindi huo.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Waziri Nchimbi alisema, ubingwa huo ni zawadi kwa Watanzania na Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni mdau namba moja katika masuala ya michezo.
Aliwapongeza Kilimanjaro Stars kwa ushindi huo huku akisema hiyo ni hatua ya kwanza ya Tanzania kutaka kufika mbali katika medani ya kimataifa akisisitiza kuelekezwa nguvu kwa Taifa Stars ili iweze kufuzu kucheza fainali za CHAN.
Aidha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo, alikuwa kivutio mara alipoingia uwanjani na kushangiliwa na mashabiki kwa kibwagizo cha ‘haki sawa kwa wote' jambo lililoleta hamasa ya mchezo huo.
Mashindano ya 34 ya CECAFA yalishirikisha timu 12 zilizo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zikiwemo timu waalikwa, Ivory Coast, Malawi na Zambia huku Cameroon ambayo ilikuwa nayo ishiriki haikutokea.
Timu nyingine ambazo zilishiriki ni pamoja na Ethiopia, Zanzibar, Uganda, Kenya, Kilimanjaro Stars, Somalia, Burundi, Rwanda na Sudan.
Stars iliwakilishwa na Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasyika, Kelvin Yondani, Juma Nyosso, Jabir Aziz, Shaban Nditi, Nurdin Bakari, Idrissa Rajab/Kigi Makasi/ Haruna Shamte na John Bocco/Henry Joseph.
Ivory Coast iliwakilishwa na Sangare Badra, Goua Mahan/Kouadio Konan, Wawa Serge, Kouame Desire, Bile Georges, N'goran Kouassi, Coulibaly Tiecoura, Kone Mahamadou/Kipre Tchetche, Kipre Balou na Dion Sede/Guy Herve
 
Nyota Ensamble kurudi kivingine


na Chile Kasoga


amka2.gif
KUNDI la maigizo la Nyota Ensemble ambalo lilisambaratika baada ya wasanii wake kujiondoa katika kundi hilo lipo mbioni kurejea.
Msanii Michael Sangu (Mike) alisema kuwa maandalizi ya kulirudisha kundi hilo yanaenda vizuri ambapo hadi sasa wasanii wengi wamekubali kurudi katika kundi.
Msanii huyo alisema kurudi kwa kundi hilo anaamini kutaleta upinzani kwa makundi mengine kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya wasanii wengi kujiengua ndani ya kundi hilo.
"Tegemea ujio wa mapinduzi na si porojo, asilimia kubwa ya wasanii wapo tayari kuanza kazi, wasanii hao ni Anna Costantine (Waridi), Abdul, Mama Abdul, Baba Abdul, mimi mwenyewe Mike, Mashaka Matongo ‘Abiola', Husna Posh ‘Dotnata'," alisema.
Mike alisema ujio wa Mambo Hayo utakuwa tofauti kama ilivyokuwa awali ambapo itakuwa ni kampuni ambayo itawawezesha kufanya kazi mbalimbali zinazohusu sekta ya filamu.
Msanii huyo alibainisha kuwa katika uanzishwaji wa kundi hilo wanataarajia kuja na filamu ambayo itawashirikisha wasanii wote waliokuwepo enzi hizo wakati wakisubiri hatua ya kurudisha vipindi vyao katika runinga.
 
Baba Haji atoa ofa Bagamoyo


na Abdallah Menssah, Bagamoyo


amka2.gif
MWIGIZAJI mahiri, Haji Adam ‘Baba Haji' ametoa ofa kwa wakazi wa Bagamoyo, Pwani wenye vipaji vya sanaa kujitokeza kwa wingi katika kushiriki filamu zake mpya.
Baba Haji aliyasema hayo jana, katika mazungumzo maalum na Tanzania Daima yaliyofanyika katika Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TASUBA) anakosomea Uigizaji na Ujuzi wa Jukwaa (Acting and Stage Technology).
Alisema, ameamua kutoa ofa hiyo baada ya kubaini kuwa Bagamoyo imekusanya wakazi wengi wenye kiu ya kuwa wasanii ambapo kwa namna moja ama nyingine, wamekosa sapoti ya kutosha katika kuwanyanyua na kuwaendeleza.
"Watakaokuwa tayari wawasiliane nami kwa kufika moja kwa moja chuoni Bagamoyo, ambako nitaanza kuwapa mazoezi ya hapa na pale kabla ya kuwapatia muongozo wa filamu nilizolenga kuwashirikisha," alisema Baba Haji.
 
Profesa Ngedele kugeukia miondoko ya reggae


na Andrew Chale


amka2.gif
MSANII wa miondoko ya dansi na kiongozi wa bendi ya Misituz nchini John Peter ‘Prof. Ngedele' amesema anataka kung'arisha nyota yake katika miondoko ya muziki wa reggae.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kutoka Moshi, Prof. Ngedele alisema amekaa muda mrefu kimya akiwa ‘chimbo' ili kujiweka fiti kwa lengo la kuipua albam ambayo anasema itakuwa mwangaza kwake kimuziki huku akigeukia miondoko ya reggae.
"Mpaka sasa nimeshamaliza kufanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya kukamilisha mpango wa albamu ambao nina hakika itakuwa ni ya hali ya juu kutokana na kuwa nitachanganya miondoko ya dansi, zouk, reggae na reggae dansi," alisema Prof.Ngedele.
Aidha, Prof. Ngedele kugeukia miondoko ya reggae ni baada ya kupewa mawazo mbalimbali ya wadau wa muziki hapa Bongo ambapo ameyapokea na kuyafanyia kazi.
Prof. Ngedele anatamba na staili yake ya kuhamasisha pindi awapo jukwaani kwa kibwagizo chake cha ‘Haaaaaaaaaaaayaah' ambayo inapendwa na wadau wengi wa burudani anapokuwa anapiga shoo kwenye kumbi mbalimbali hapa nchini.
Prof. Ngedele aliwaomba wadau wa muziki watakao kuwa tayari kujitokeza kumuunga mkono ili kusuka gurudumu hilo la kuendeleza muziki hapa nchi. Mkali huyo alianza muziki tangu mwaka 1994, katika kundi la Dozee Muzika-(Arusha), kabla ya kuhamia kundi la la Super Melody la Dodoma na kisha kuhamia bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) na baadaye alijiunga na bendi ya Bambino Sound.
 
Kagera Sugar kambini wiki ijayo


na Mwandishi wetu


amka2.gif
TIMU ya Kagera Sugar, inatarajiwa kuingia kambini Jumatatu ijayo kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya soka Tanzania Bara inayotarajia kuanza Januari mwakani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, kwa njia ya simu kutoka Bukoba jana, Meneja na msemaji wa timu hiyo Mohammed Hussein alisema wachezaji wataanza kuripoti Desemba 18 na 19.
Alisema Kocha wao Mkuu Jackson Mayanja, raia wa Uganda ndiye aliyependekeza timu hiyo kuanza mazoezi Jumatatu ya Desemba 20, yatakayofanyika kwa wiki mbili mfululizo, kabla ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki.
Alisema, kocha huyo kwa sasa anafanya mazungumzo na timu kadhaa za Uganda ambazo amepanga kucheza nazo kwa nia ya kupata mazoezi ya kutosha kabla ya kuanza mzunguko wa pili.
"Kagera Sugar tutaanza mazoezi Jumatatu Desemba 20, tutafanya kwa wiki mbili kisha kwenda Uganda kucheza na timu za huko," alisema Hussein.
Aliongeza kwamba dhamira yao ni kuhakikisha katika mzunguko wa pili wanazinduka na kupanda juu katika msimamo wa Ligi hiyo.
 
Super D aita mabondia ufukweni


na Ruhazi Ruhazi


amka2.gif
KOCHA wa ngumi wa klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajab Mhamila ‘Super D', amewataka mabondia wa ngumi za ridhaa wasio na klabu kuhudhuria mafunzo ya mchezo huo bure siku za mwisho wa wiki.
Akizungumza Tanzania Daima jana, Super D alisema amekuwa akitoa mafunzo hayo kila Jumamosi na Jumapili, kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Klabu ya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa sasa amepata vifaa vya kutosha kuendeshea mafunzo hayo hivyo mabondia wajitokeze kwa wingi kuanzia saa mbili asubuhi.
"Ninapenda kuwatangazia mabondia wasio na timu wanaotaka kujifunza waje Gymkhana kila siku za Jumamosi na Jumapili, kuanzia saa mbili asubuhi ninatoa mafunzo bure, tunavyo vifaa vya kutosha," alisema Super D.
Alisema mafunzo ya ngumi yatawasaidia vijana hao kujijenga kimchezo na hata katika kujiweka fiti, kwa ajili ya afya zao.



h.sep3.gif

 
Angetile Osiah amrithi Mwakalebela TFF
• Wambura msemaji mpya, Jimmy Kabwe Ofisa Masoko

na Dina Ismail


amka2.gif
BAADA ya mchakato wa kujaza nafasai za Katibu Mkuu na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania hatimaye watendaji hao wamepatikana.
Nafasi ya Katibu Mkuu ilikuwa ikishikiliwa na Fredrick Mwakalebela ambaye mkataba wake ulikwisha na kuamua kwenda kwenye shughuli za kisiasa na Ofisa Habari, Florian Kaijage ambaye naye muda wa mkataba wake ulikuwa umekwisha kabla ya kusimamishwa kutokana na sakata la kugoma ‘CD' ya Wimbo wa Taifa, siku ya mechi ya Taifa Stars na Morocco mbele ya mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete.
Baada ya kupitiwa kwa maombi mengi yaliyotumwa na wadau mbalimbali kuomba nafasi hizo, waliopenya kwenye kinyang'anyiro hicho ni wanahabari waandamizi, Angetile Osiah ambaye atakuwa Katibu Mkuu na Boniface Wambura atakayekuwa Ofisa Habari.
Kabla ya uteuzi huo, Osiah alikuwa mmoja wa wahariri wa michezo wa gazeti la Mwananchi huku Wambura akitokea gazeti la Jambo Leo alikokuwa Mhariri Mkuu.
Aidha, TFF imemuajiri mtangazaji wa kituo cha Radio cha East Africa, Jimmy Kabwe kuwa Ofisa Masoko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom