Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #261
Daktari wa Kijapani acheza ngoma ya marehemu Mwinamila
Saturday, 11 December 2010 20:57
Habel Chidawali, Dodoma
IMEELEZWA kuwa utamaduni wa Mtanzania unadidimizwa na Watanzania wenyewe kutokupenda ngoma zao na badala yake wanapenda kushabikia utamaduni wa nje.
Hayo yalisemwa jana na Dk Seigo Usami, Mganga wa Kitendo cha Mifupa na viungo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambaye ni msanii katika kikundi cha Sanaa cha Hiari ya Moyo ambacho kiliasisiwa na msanii maarufu marehemu mzee Mwinamila.
Dk Usami (30) alieleza masikitiko yake kuwa hakuna nchi iliyojaliwa kuwana makabila mengi kama Tanzania, lakini ambayo kila kabila linakuwa na utamaduni wake jambo linalofanya nchi hii kuwa na utajiri wa utamaduni.
Usami alisema kuwa kama serikali ya Tanzania pamoja na Watanzania wenyewe wakiamua kuamka na kuanza kuupenda utamaduni wao ni wazi kuwa hakutakuwa na ngoma nyingine itakayotoka nje ya nchi ambayo itapata nafasi katika nchi hii.
Alisema katika nchi zingine ikiwemo Japan, ngoma za asili ni nadra sana kuziona ingawa wamekuwa wakizisoma katika vitabu kwamba zilikuwepo, lakini hivi sasa hakuna kitu na hivyo akashauri ni vema Tanzania ikawa na tahadhari hiyo.
Akizungumzia kuhusu nini kilimsukuma kujiunga na ngoma ya hiari ya Moyo "kwanza napenda utamaduni kuliko kitu kingine na utamaduni ni sehemu ya pili katika maisha yangu kwani sehemu yangu ya kwanza ni kazi yangu"
"Mimi nilikuja Tanzania Januari mwaka jana (2009) na ninafanya kazi ya kujitolea hapa Tanzania (Volunteer) kupitia Shirika JICA kwa muda wa miaka miwili na kwamba mkataba wangu unakwisha Januari mwakani hivyo nitakikosa sana kikundi hiki ambacho nakwenda Japan nikiwa bado nakipenda" alisema Usami.
Kwa upande wake alisema kuwa alijiunga na Hiari ya Moyo Januari Mwaka huu, baada ya kuwaona katika maeneo kadhaa wakitoa burudani ndipo akavutiwa nao na kuamua kuomba nafasi ya kujiunga jambo ambalo alisema lilipokewa kwa mikono miwili na viongozi wa kikundi hicho.
Akizungumzia tofauti ya ngoma za Tanzania na Japan alisema kuwa kwao kuna ngoma zinazotaka kufanana na hizo ambazo hata hivyo alikiri kuwa zilibuniwa kutoka Afrika Mashariki bila ya kutaja ni nchi gani ya Afrika Mashariki zilipobuniwa ngoma hizo.
Alisema haoni shida kucheza ngoma ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya ajabu ambayo hutumiwa na wasanii na mazingira wanayofanyia kazi zao.
Kuhusu vipi anatenga muda wake wa kazi pamoja na mazoezi ya kikundi alisema "Kazini ninaingia saa mbili asubuhi na ninafanya kazi hadi saa tisa, lakini kule ninaingia kwenye mazoezi kuanzia saa 10 hadi saa 12 jioni kila siku hivyo sina shida"
Kuhusu ushirikia katika sherehe alisema pia hakuna shida kwani tangu alipoajiunga na kikundi hicho kila wanapoitwa kwenye michezo huwa anatoa taarifa kwa mkuu wake wa kazi na wanamruhusu bila ya shida.
Alisema ilimchukua muda wa miezi mitatu tangu alipojiunga na kikundi hicho akawa anaweza kucheza kila aina ya mtindo unaochezwa na kikundi hicho pamoja na kuimba nyimbo zao ingawa kwa Kiswahili cha tabu.
"Kinachonifurahisha zaidi ni mtindo wa kukata viuno ambao tunashiriki pamoja na wanawake na wanaume kwa pamoja jambo ambalo si rahisi kwa sisi Wajapani kufanya hivyo na si kwamba hatuwezi ila hatuna ubunifu huo", alifafanua.
Alieleza kuwa iko tofauti kubwa kati ya ngoma aliyowahi kuiona kule Japan na hapa Tanzania, kwani, ile ya Japan ngoma moja inapigwa na watu zaidi ya watatu ilihali hapa Tanzania mtu mmoja anaweza kupiga ngoma zaidi ya tano kwa wakati mmoja kitu alichosema ni ubunifu wa hali ya juu.
Mganga huyo alisema kuwa anasikitishwa sana na kitendo cha ujira mdogo ambao hulipwa wasanii wa Kitanzania kwani alisema kuwa ni kidogo kulinganisha na burudani wanayoitoa jambo alilosema ni lazima serikali iliangalie upya vingine wanawavunja moyo wasanii.
Ngoma nyingine ambazo anazipenda Usami ni pamoja na disko na ngoma za makabila ya Kitanzania ambapo alisema disko huenda kupoteza muda, lakini hafikirii sana kujifunza kuliko ngoma za makabila ambazo alisifia kuwa hata akirudi Japan yuko tayari kutenga muda wake na kuwafundisha raia wa huko huku akiahidi kuwa atakipeleka Japan Kikundi cha Hiari ya Moyo ili wakaimbe na kucheza pamoja.
Akiwa katika kikundi Chake cha Hiari ya Moyo ambacho mwanzilishi wake ni Mwinamila, Usami anajua kucheza,kupiga ngoma pamoja na kuimba na hakuna tofauti yoyote kati yake na wakongwe wa sanaa hao wanapokuwa Jukwaani.
Kwa upande wa madaktari wanaofanya kazi pamoja na msanii huyo wanasema kuwa alichokifanya ndicho ambacho hata wao wanapokuwa nchi za nje huwa wanafanya kwa kuiga ngoma za watu wengine.
"Hata sisi huwa tunaiga ngoma za wenzetu tukiwa huko nje ya nchi kwani si unajua kuwa mtu akitoka Tanzania na kwenda Ulaya huwa anarudi akiwa ameweza kuiga ngoma za kigeni ikiwemo miziki ya Dansi hivyo hata yeye ni haki yake" alisema mmoja wa madaktari ambaye aliomba jina lake lisiandikwe.