Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #1,641
Viongozi Yanga katika hili hamna hoja
Mwandishi wetu
Kamaada turejeshane kwa ufupi katika mada yetu iliyopita, ambayo ilikuwa ikisema ‘UMITASHUMTA Taifa mikoa 10? Katika mada hiyo tuliezea kushangazwa na kasi ambayo imekuwa ikihubiriwa na wakubwa ya kurejesha michezo shuleni.
Tulielezea kuwa, licha ya jambo hili kushikiwa bango na hata kupigiwa debe na mkuu wa nchi, Rais Jakaya Kikwete, lakini watendaji wenye dhamana husika huku chini wanasikitisha utadhani hiki ni kitu wanacholazimishwa.
Mfano hai tuliuchukua wa mashindano ya UMITASHUMTA ya taifa ambayo yalimazika hivi karibuni mjini Kibaha, lakini kichekesho licha ya kuitwa mashindano ya taifa lakini mikoa iliyoshiriki ni 10 tu, zaidi ya 2i iliyopo hapa nchini, kimsingi hata nusu tu haikufikia.
Sasa hapo tunajivunia nini, kweli kuibua vipaji kwa namna hiyo, sijuim kama tutafika, hivio hiyo mikoa zaidi 10 hakuna vipaji kweli, tuache porojo inagawaje sipendi kuita ‘Siasa' maana neno hilo naliheshimu sana ingawaje wahusika wenyewe hawalifanyii kazi ipasavyo hivyo kufanya maana yake halisi kwenda ndivyo sivyo.
Baada ya kupena dondoo hizo embu turejee katika mada ya leo. Takribani siku mbili tatu zilizopita lindi la habari ya kugoma kwa wachezaji wa timu kubwa na kongwe hapa nchini lilishamiri hatimaye juzi wachezaji hao hao waligoma rasmi.
Nadhani kitendo cha kipekee kwa klabu hiyo kutokea kwa wachezaji kugoma, ingawa sijui viongozi wa klabu hiyo wanalichukuliaje.
Vyovyote wanavyolichukulia suala hilo, lakini viongozo wa Yanga hawawezi kulikwepa maana ni pigo na limechafua sura nzuri ya klabu hiyo.
Viongozi makini katika hili, lazima wangechukua hatua stahili aidha kwa kujiuzulu ama hatua nyingine sahihi.
Inashangaza klabu hiyo ambayo ina sifa ya kuwa na mfadhili wa kweli ‘Yussuf Manji' ambaye kimsingi amekuwa akiweka uzito mkubwa katika masuala mbalimbali ya klabu Yanga.
Lakini katika kuonyesha Yanga ina udhaifu mkubwa na hata wanachama wanatakiwa kulifanyia kazi hili juu ya viongozi wao, kwa nini viongozi wao wameshindwa kuwajibika katika hili.
Wanachama wanapaswa kuwaweka kiti moto viongozi wao wanafanya nini hadi kushindwa kuwajibika ipasavyo katika hilio na kuitia aibu klabu yao. Sidhani kama kama wanachama wanafurahia hali hii, hapo ndipo pa wanachama kufanya uchunguzi wa kina nani aliyesababisha hali hii.
Kimsingi hapo viongozi wa Yanga hawawezi kulikwepa hili kwamba ni wazembe, kwani ni hivi karibuni tu iliibuliowa hoja ya mtendaji mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, kutoa maelezo juu ya sh milioni 100 zilizotolewa na mfadhili Manji kwa ajili ya usajili.
Katika maelezo yake, Mwalusako alieleza kuwa wametumia sh milioni 20 kwa wachezaji wawili hivyo kubaki milioni takriban 80, hivyo leo ni kitu cha kushangaza wachezaji kudai milioni 75 za mishahara yao na fedha za usajili.
Hivi kwa nini hapo viongozi wasiwajibike katika hili, fedha zipo lakini kumbe wanadaiwa masula ya msingi na wachezaji kama hili lililosababisha kugoma. Wana Yanga chukueni hatua la sivyo ni ndoto kwa soka yetu kufika mbali. Kila la heri tukutane wiki ijayo.