Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Federer atwaa ubingwa wa Qatar Open
Sunday, 09 January 2011 21:04

DOHA, Qatar
ROGER Federer ametwaa ubingwa wa Qatar Open kwa kumchapa mpinzani wake Nikolay Davydenko 6-3, 6-4 katika mchezo uliodumu kwa dakika 79.

Federer amekuwa mchezaji wa kwana kutwaa mara tatu taji la Doha, baada ya kufanya hivyo mwaka 2005 na 2006.

"Ni mwanzo mzuri wa msimu," Federer aliwaambia mashabiki 8,000 waliojitokeza kwenye uwanja wa Khalifa Tennis Complex. "Nimejisikia vizuri wiki zote nilizokuwa hapa. Nilitawala mchezo kuanzia seti ya kwanza hadi ya pili pia."

Wakati alipoulizwa kuhusu nafasi yake kwenye michuano ya Australian Open mwishoni mwa mwezi, Federer alicheka na kusema, "Sipo tayari kwa sasa. Nitakuwa tayari nitakapokuwa pale. Lakini ni wazi ushindi wangu hapa utanisaidia kufanya vizuri Australia."

Davydenko, ambaye alimchapa mchezaji bora Rafael Nadal kwenye nusu fainali, alisema "alicheza vizuri zaidi yangu.Nimekuwa nikichezea naye mara kadha, lakini leo (jana0 alikuwa mwepesi zaidi. Hakunipa nafasi yoyote."

Davydenko alisema. "Kama ningejaribu kucheza kwa kulinda mstari, alikuwa na kasi zaidi. Wakati alipokuwa akianzisha mchezo alikuwa bora zaidi. Nafikiri kama ataendelea kucheza kwa kiwango hiki hakuna shaka kwamba atarudia kuwa namba moja tena.

"Sikucheza vibaya. Kiwango changu kilikuwa juu. Tatizo ni kwamba Federer hakunipa nafasi hata kidogo leo."
 
Federer atwaa ubingwa wa Qatar Open
Sunday, 09 January 2011 21:04

DOHA, Qatar
ROGER Federer ametwaa ubingwa wa Qatar Open kwa kumchapa mpinzani wake Nikolay Davydenko 6-3, 6-4 katika mchezo uliodumu kwa dakika 79.

Federer amekuwa mchezaji wa kwana kutwaa mara tatu taji la Doha, baada ya kufanya hivyo mwaka 2005 na 2006.

“Ni mwanzo mzuri wa msimu,” Federer aliwaambia mashabiki 8,000 waliojitokeza kwenye uwanja wa Khalifa Tennis Complex. “Nimejisikia vizuri wiki zote nilizokuwa hapa. Nilitawala mchezo kuanzia seti ya kwanza hadi ya pili pia.”

Wakati alipoulizwa kuhusu nafasi yake kwenye michuano ya Australian Open mwishoni mwa mwezi, Federer alicheka na kusema, “Sipo tayari kwa sasa. Nitakuwa tayari nitakapokuwa pale. Lakini ni wazi ushindi wangu hapa utanisaidia kufanya vizuri Australia.”

Davydenko, ambaye alimchapa mchezaji bora Rafael Nadal kwenye nusu fainali, alisema “alicheza vizuri zaidi yangu.Nimekuwa nikichezea naye mara kadha, lakini leo (jana0 alikuwa mwepesi zaidi. Hakunipa nafasi yoyote.”

Davydenko alisema. “Kama ningejaribu kucheza kwa kulinda mstari, alikuwa na kasi zaidi. Wakati alipokuwa akianzisha mchezo alikuwa bora zaidi. Nafikiri kama ataendelea kucheza kwa kiwango hiki hakuna shaka kwamba atarudia kuwa namba moja tena.

“Sikucheza vibaya. Kiwango changu kilikuwa juu. Tatizo ni kwamba Federer hakunipa nafasi hata kidogo leo.”
 
Stars bado yadorora Misri
Imeandikwa na Amir Mhando, Cairo; Tarehe: 8th January 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 688; Jumla ya maoni: 0


01_11_5ssh8m.jpg

Kikosi cha Taifa Stars





TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars jana ilibanwa mbavu na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Burundi katika michuano ya Bonde la Mto Nile.

Burundi ilifunga bao la kuongoza katika dakika ya 49 kupitia kwa Tambwe Hamisi aliyefunga kwa kichwa cha chinichini baada ya kuunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Didier Kavumbabo.

Katika kipindi hicho cha pili, Stars ilicheza vibaya na mshambuliaji wake Mrisho Ngassa alionekana ‘kufichwa’ wa Warundi.

Bao la kusawazisha la Stars lilifungwa katika dakika ya 74 kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Shadrack Nsajigwa.

Penalti hiyo ilitolewa baada ya Nizar Khalfani kuchezewa rafu. Kwa ujumla katika mechi hiyo, Stars ilikosa mabao kadhaa hasa lile la dakika ya sita ambapo Athumani Machuppa alikosa baada ya kupiga kichwa kilichopaa juu, alipewa krosi na Shadrack Nsajigwa.

Stars tena nusura ipate bao katika dakika ya tisa kupitia kwa Ngassa lakini akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga, mabeki wa Burundi waliwahi kuokoa mpira.

Dakika ya 31 Stars ililazimika kufanya mabadiliko baada ya Stephano Mwasika kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Idrisa Rashid.

Pia dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili, Stars ilimtoa Machuppa na nafasi yake kuchukuliwa na Jerryson Tegete. Pia alitoka Rashidi Gumbo na kuingia Jabir Azizi.

Kipa Juma Kaseja ilimbidi afanye kazi ya ziada katika dakika ya 65 baada ya kuokoa shuti kali la Tambwe, ambapo dakika ya 68 kocha alimtoa Shaaban Nditi na kumuingiza Saidi Maulidi.

Kwa matokeo hayo, Stars sasa imeendelea kujiweka pabaya katika kundi lake kwani sasa ndio inashika mkia.

Misri inaongoza ikifuatiwa na Uganda zote zikiwa na pointi tatu, Burundi inashika nafasi ya tatu na Stars ni ya nne.

Katika mechi ya kwanza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliifunga Kenya bao 1-0 lililofungwa na Luofo Bongeli katika dakika ya 26.

Kikosi cha Stars: Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika/ Idrisa Rashid, Aggrey Morris, Nadir Haroub, Nurdin Bakari, Nizar Khalfani, Shaaban Nditi/ Saidi Maulidi, Mrisho Ngassa/ Salum Machaku, Athumani Machuppa/Jerryson Tegete, Rashidi Gumbo/ Jabir Azizi.
 

Simba, Zanzibar Ocean View kucheza fainali Mapinduzi


Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 8th January 2011 @ 23:50

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba leo itakuwa uwanjani kumenyana na Zanzibar Ocean View katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Simba ilipata nafasi hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar katika mechi ya robo fainali iliyochezwa kwenye uwanja huo juzi usiku.

Matokeo hayo yaliifanya Simba ishike nafasi ya pili kwenye kundi B na hivyo kukutana na Zanzibar Ocean View iliyoshika nafasi ya kwanza kundi A.

Kwa upande wa Yanga itacheza nusu fainali dhidi ya Mtibwa kesho baada ya kushika nafasi ya pili kundi A huku Mtibwa ikiwa ya kwanza kutoka kundi hilo.

Katika mechi ya juzi, Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 56 likifungwa na Abdulhalim Humoud kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona wa Emmanuel Okwi.

Hata hivyo, bao hilo halikudumu muda mrefu kwani dakika tano baadaye, mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mtibwa Sugar walisawazisha kupitia kwa Masoud Ali Chile.

Akizungumzia mechi ya leo, Kocha wa Simba Patrick Phiri alisema anatarajia itakuwa ngumu kwani wapinzani wake wanaonekana sio wabaya.

Zanzibar Ocean View ilitoka na Yanga katika mechi za kwanza za michuano hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Mapinduzi.

"Ocean View sio timu mbaya ni timu nzuri hivyo ni lazima wachezaji wangu wajue wanacheza
na timu ya aina gani, si unaona ilitoka sare na Yanga, mechi itakuwa ngumu sitarajii kupata urahisi," alisema Phiri.

Fainali za michuano hiyo zitafanyika Jumatano ambayo ndio siku ya kilele cha sherehe za Mapinduzi na mshindi wa kwanza atapata Sh milioni 3, wa pili Sh milioni 2 na watatu Sh milioni moja.
 
Basata kuwaenzi wasanii Friday, 07 January 2011 19:59

basata%20wasanii.jpg
Na Julieth Kulangwa
BASATA baadaye mwaka huu itaandaa tamasha kubwa la wasanii ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka likiwa na jina la Siku ya Msanii wa Tanzania.

Katibu Mtendaji wake, Ghonche Materego alisema kwamba,tamasha hilo ambalo litakuwa likipambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali hapa nchini litakuwa ni maalumu kwa ajili ya kuenzi sanaa na kusisitiza kaulimbiu ya 'Sanaa ni Kazi' kwa vitendo.

"Katika kuhakikisha sanaa inakuwa kazi na ajira kama ilivyo kaulimbiu yetu mwaka huu, tuko katika maandalizi ya kuandaa tamasha la siku ya wasanii ambalo tutawapa taarifa zake hivi karibuni.Katika tamasha hilo wasanii wetu watapata fursa za kuonyesha kazi zao na kushiriki kikamilifu" alisema Materego.

Aliongeza kwamba,tamasha hilo litakuwa ni mwanzo wa kuenzi wasanii wetu na kukuza sekta ya sanaa nchini hasa ikizingatiwa itakuwa ni fursa kwa wasanii kujitangaza na kupanua mwanya wa masoko ya kazi zao.

 
Sita kali za THT hadharani Mlimani City leo


na Khadija Kalili


amka2.gif
MAADHIMISHO ya miaka mitano ya kuasisiwa Nyumba ya Kuvumbua Vipajivya Wasanii Tanzania "˜Tanzania House Of Talent' (THT), yanafanyika leo usiku ukumbi wa Mlimani Cityjijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa tamasha hilo la kihistoria, Kemmy Mutahaba, ambaye pia ni Msemaji wa THT, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika kuona kazi za nyumba hiyo.
Pia albamu sita za wasanii waliovumbuliwa vipaji na nyumba hiyo, zitazinduliwa kwa pamoja.
Kemmy aliwataja wasanii hao watakaozindua kazi zao leo kuwa ni Mwasiti, Amini, Dito, Barnaba, Lina na Mataluma.
Kiingilio katika tamasha hilo ni sh 30,000 ambako mashabiki 400 tu, ndio waliopangwa kushuhudia, hivyo kutakiwa kuchangamkia kununua tiketi ili waweze kupata fursa hiyo.
Mutahaba alizitaja sehemu zinakouzwa tiketi hizo kuwa ni katika maduka ya vipodozi ya Shear Illusions Millennium Tower na Mlimani City, Ofisi za THT Kinondoni na Ofisi za Radio Clouds Mikocheni.
Alisema licha ya wakali hao kuzindua albamu zao pia wataudhihirishia umma kwa kuonyesha shoo ya aina yake siku hiyo.
Kemmy aliwataja wasanii wengine watakaotoa burudani kuwa ni pamoja na Banana Zorro, Maunda Zorro, bendi ya Odama na wanenguaji wa THT.
 
King Majuto apania kuvunja watu mbavu


na Abdallah Menssah


amka2.gif
MWIGIZAJI mkongwe hapa nchini, Amri Athuman,'King Majuto', ameahidi kuvunja mbavu za watakaohudhuria onyesho maalumu la Jahazi Modern Taarab, linalotarajiwa kurindima Januari 15, kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Katika onyesho hilo lililopewa jina la'Usiku wa Mambo ya Pwani', King Majuto atatakuwa ni msanii mwalikwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, King Majuto alisema kuwa, amepanga kuingia ukumbini na mabodigadi wake wawili, ambao ni mbilikimo na kuanza kufanya vitu vyake.
"Nasema hivi, katika onyesho hilo kama atatokea mtu ambaye atastahamili kutokucheka wakati ninavunja mbavu watu, nitampa zawadi" alisema mkongwe huyo mwenye mashabiki wengi.
Mbali ya King Majuto, katika onyesho hilo pia litashirikisha kundi la Ngoma ya Baikoko pamoja na Mkongwe wa taarabu, Mwanahela Salum, atakayepanda jukwaani na kikosi chake cha Gold Star Modern Taarab.
 
TOT Plus yajiimarisha


na Abdallah Menssah


amka2.gif
BENDI ya muziki wa dansi hapa nchini, TOT Plus, juzi Jumapili ilitambulisha rasmi wasanii wake wapya watatu waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni.
Wanamuziki hao na bendi walizotoka kwenye mabano ni mwimbaji, Mhina Panduka'Toto Tundu' (K Mondo Sound), mcharazaji drums, Joseph Waninga (Bwagamoyo Sound), na mnenguaji, Frida Mwanasuka (Mashujaa Musica).
Akizungumza wakati wa utambulisho huo uliofanyika kwenye bonanza la bendi hiyo ukumbi wa Oasis, Kiongozi wa TOT Plus, Badi Bakule, alisema wamewanyakua wanamuziki hao ili kuiongezea nguvu bendi yao.
Aidha, Bakule anayefahamika pia kama "˜Jogoo la Mjini', alieleza kuwa anaamini bendi yake itakuwa katika nafasi nzuri kiushindani baada ya kufanikiwa kuwachukua wanamuziki hao.
"Kiukweli, wapinzani wetu wote wakae vizuri, kwani sasa tuko kamili na nina imani makombora ya burudani tutakayoyafyatua baada ya kuwapata wanamuziki hawa hayatakuwa ya kitoto" alisema Bakule.
Kadhalika, Bakule alisema, kinachofuata sasa baada ya zoezi hilo la kuongeza wanamuziki ndani ya TOT Plus ni kumalizia upakuaji wa albamu yao mpya itakayokwenda kwa jina la'Rikizi na Zengwe'.
 
Mashabiki wahimizwa disko la Igabiro


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MASHABIKI wa burudani wa Mbezi kwa Yussuf jijini Dar es Salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi kwenye disko la aina yake litakalorindima kesho na keshokutwa kwenye ukumbi wa Igabiro Social Centre.
Ombi hilo limetolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkuu wa ukumbi huo, Desderi Tarimo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mbezi kwa Yussuf, jijini Dar es Salaam.
Tarimo alisema, disko hilo alilotamba litakuwa ni la aina yake, litarindimishwa na Ma Dj mashuhuri nchini kuanzia majira ya saa 12:00 jioni na kuendelea hadi majogoo.
"Mbali ya disko hilo ninaloamini kuwa litaacha simulizi kubwa, pia watakaohudhuria watapata fursa ya kushuhudia shoo kabambe kutoka kwa wanenguaji mahiri" alisema Tarimo.
Aidha, alisema kuwa zitakuwapo zawadi mbalimbali kama vile vinywaji baridi pamoja na fulana zenye nembo ya ukumbi huo ambazo zitatolewa kwa mashabiki watakaowahi kufika, watakaokuja wakiwa bibi na bwana, pamoja na wale watakaocheza vema.
 
Stars kusuka ama kunyoa leo


na Mwandishi wetu, Cairo


amka2.gif
NI kusuka ama kunyoa leo kwa Timu ya Taifa ya soka Tanzania "˜Taifa Stars' katika michuano ya nchi za Bonde la Mto Nile wakati itakapovaana na Uganda 'The Cranes' mchezo wa mwisho hatua ya makundi, huku Stars wakitamba wana uwezo wa kumpiga, kwani uwezo wanao na nia wanayo.
Ni mtihani mkubwa kwa Taifa Stars, kama kweli inazihitaji zaidi ya sh milioni 200 za Tanzania, ambazo ni zawadi kwa bingwa wa michuano hii, vinginevyo watabaki kama watalii maana tiketi ya kurudi nyumbani kwa timu zote ni mpaka Januari 17 mwaka huu.
Wachezaji wa Stars wameapa kufa na Uganda, huku wakisisitiza kuwa, makosa waliyoyafanya katika mechi mbili zilizopita hayatajirudia na watahakikisha wanaibuka na ushindi mnono.
Lakini ni kawaida ya Stars kuapa kabla ya mechi kwamba, watafia uwanjani kuhakikisha wanaibuka na ushindi, lakini inapofika siku ya mechi hakuna hata anayekubali kuzimia.
Jana nahodha wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa alisema, wanajua matokeo yetu yamewanyong'onyesha Watanzania, lakini hawatawaangusha tena na wataifunga Uganda na kufuzu nusu fainali.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Polisi mjini hapa kuanzia saa 8:45 za huku sawa na saa 9:45 za Afrika Mashariki kumenyana na Uganda 'The Cranes' mchezo wa mwisho wa michuano ya soka nchi za Bonde la Mto Nile hatua ya makundi.
Kikosi cha Uganda kilichopo mjini hapa, hakina nyota wengi waliokuwa Dar es Salaam mwezi uliopita kwenye michuano ya Chalenji, badala yake walio wengi ni chipukizi lakini walio na uwezo mkubwa wa kusakata soka.
Uganda iliwaduwaza mashabiki wa Misri Jumamosi baada ya kuibana vilivyo Misri'Farao' karibu dakika 89 za mchezo na kufungwa bao pekee dakika ya 90 mfungaji akiwa Ahmed Hassan Gedo.
Hali hiyo imeifanya Uganda sasa kuwa midomoni mwa wadau wa soka mjini hapa kwamba ni timu nzuri na inapewa nafasi kubwa ya kuifunga Stars leo.
Lakini Nsajigwa na wenzake wanasema, watawashangaza wengi na hawaoni kwa nini wasiingie nusu fainali, hivyo kazi yao leo ni moja kumpiga Mganda, kwani nia wanayo, uwezo wanao na sababu pia wanayo.
Kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen alisema, anatarajia mechi itakuwa ngumu, lakini kwa vile wanaingia wakiwa wanajua makosa halitawasumbua sana.
Stars ilifungwa na Misri mabao 5-1, kisha ikatoka 1-1 na Burundi, wakati Uganda iliifunga Burundi 3-1, kisha ikafungwa 1-0 na Misri.
Naye kocha wa Uganda, Bobby Williamson alisema, mechi itakuwa ngumu, lakini ameshajua udhaifu wa Stars na itakuwa si kazi ngumu kushinda.
Misri inayoongoza Kundi A ikiwa na pointi sita, tayari imetinga nusu fainali na leo inamaliza na Burundi mjini Ismailia, ambako hata kama itafungwa haitaathirika.
Ili Stars ifuzu nusu fainali, itabidi iifunge Uganda leo, kisha iombee Misri iifunge Burundi ama itoke nayo sare, vinginevyo kama Burundi itashinda basi itabidi utazamwe uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Mpaka sasa, Stars imefungwa mabao sita na imefunga mawili, hivyo ina deni la mabao manne, wakati Burundi imefungwa manne na imefunga mawili huku nayo ikiwa na deni la mabao mawili.
Uganda ni ya pili ikiwa na pointi tatu na mabao manne ya kufunga, ikiwa imefungwa mawili, huku Burundi ikiwa ya tatu na Stars ya mwisho, zote zina pointi moja.
Kundi B, leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), inacheza na Sudan ambayo mchezo wa kwanza ilifungwa bao 1-0 na Kenya kabla ya DRC kuifunga Kenya bao 1-0, hivyo mchezo huo utaamua timu za kufusu nusu fainali, ingawa DRC ina nafasi kubwa kwani hata sare itakuwa imefuzu.
Michuano hiyo inashirikisha nchi saba zilizogawanywa makundi mawili na timu mbili za juu kila kundi zitacheza nusu fainali, wakati zilizoshika nafasi ya tatu zitacheza kuwania mshindi wa tano.
 
ZESCO kuzinoa Simba, Yanga


na Makuburi Ally


amka2.gif
TIMU ya soka ya ZESCO ya Zambia Januari 15 na 16 inatarajiwa kuzipa mazoezi timu za Simba na Yanga kabla ya michuano yake ya kimataifa, ikichukua nafasi ya Sofapaka ya Kenya.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa ziara ya timu hiyo, George Wakuganda alisema, taratibu za timu hiyo kuja Tanzania zimekamilika, hivyo Januari 13 itawasili hapa nchini kwa ajili ya michezo hiyo.
Wakuganda alisema, wameileta ZESCO kwa sababu wameona wabadilishe ladha ya soka, kwa sababu Desemba mwaka jana waliileta AFC Leopard ya Kenya ambayo ilicheza na Simba, Yanga na Azam, michezo iliyochezwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wakuganda alisema, awali walishafanya mazungumzo na Sofapaka na wakakubaliana, lakini wakaona ni bora wabadilishie ili Simba na Yanga zipate maandalizi bora.
"Kwa sababu tunapenda Simba na Yanga zifanye vizuri katika masindano ya kimataifa, tumeonelea tubadilishe ladha ya soka la Kenya na Zambia kwani Zambia wako juu kisoka" alisema.
Alitoa wito kwa mashabiki wa Simba na Yanga kujitokeza kwa wingi kujionea timu zao zikijiandaa kwa mashindano ya kimataifa, ambako watafahamu mwelekeo kabla ya michezo hiyo.
 
Manji, Mtemvu watia ubani Yanga


na Juma Kasesa


amka2.gif
MFADHILI mkuu wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji na Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu, jana walitembelea kambi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji kufanya vema katika michuano ya Kombe la Mapinduzi na maandalizi ya Ligi Kuu na mashindano ya Kimataifa.
Kwa mujibu Ofisa Habari wa klabu hiyo, Louis Sendeu, ziarahiyo ililenga kuwapa nguvu wachezaji wa timu hiyo kujituma katika mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar, uliotarajiwa kupigwa jana usiku kuamua timu itakayotinga fainali kukumbana na Simba ambayo ilishakata tiketi.
Aidha Sendeu alisema, wamejiandaa vya kutosha ili kutinga fainali, kwa kuwa wanataka kukutana na Simba ili kuendeleza ubabe kwa Simba baada ya kufanya hivyo katika mechi ya Ligi KuuTanzania iliyopigwa Oktoba 16 jijini Mwanza ambako Yanga ilishinda bao 1-0.
 
Kamati ya Uchaguzi ZFA yavunjwa


na Mwandishi wetu


amka2.gif
KAMATI ya uchaguzi ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), imevunjwa ghafla jana, siku chache tangu ilipotengua matokeo ya uchaguzi mkuu yaliyomweka madarakani Rais Ali Ferej Tamim, katika kile kinachodaiwa ilikuwa ikifanya kazi zake kinyume na katiba ya chama hicho.
Azimio la kuvunjwa kwa kamati hiyo limepitishwa jana na Kamati tendaji ya ZFA Taifa, iliyokutana chini ya kikao kilichoendeshwa na Mwenyekiti wake, Mzee Zam Ali katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo katika hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Akizungumza na gazeti hili, mjumbe wa Kamati tendaji ya ZFA taifa, Mussa Soraga alisema, kuanzia sasa kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Ali Suleiman Ali'Shihata' haikuidhinishwa na kamati tendaji ya ZFA taifa, licha ya kuteuliwa na sekreterieti ya chama hicho, wakati huo katika kikao kilichoongozwa na aliyekuwa Rais, Ali Ferej Tamim na msaidizi wake mkuu, Mzee Zam Ali.
Kikao hicho kimepitisha uamuzi wa kuunda kamati mpya itakayokuwa na majukumu ya kusimamia uchaguzi wa marejeo.
Akitoa msimamo baada ya maamuzi hayo, Mwenyekiti wa kamati hiyo ya uchaguzi, Ali Suleiman Ali'Shihata' alisema kamati tendaji ya ZFA taifa, haina uwezo wa kuivunja kamati yao na maamuzi hayo hawayatambui na wataendelea kutekeleza majukumu yao kama yalivyopangwa.
Shihata alisema, maamuzi yaliyofikiwa na kamati tendaji ya ZFA taifa, yanaonyesha baadhi ya wajumbe wameanza kuchanganyikiwa kutokana na mambo ya aibu yanayojitokeza ndani ya chama hicho na kusababisha kupoteza uongozi uliochaguliwa Desemba 31 mwaka jana kisiwani Pemba.
Kufuatia hatua hiyo, Shihata alisema kamati yake leo inatarajiwa kutoa maamuzi mazito, kuhusiana na kurejewa kwa uchaguzi wa ZFA, pamoja msimamo wa kamati hiyo wa kutotambua maamuzi ya kutimuliwa kwao siku chache tangu watengue uongozi mzima wa kitaifa.
 
Msimamizi Uwanja wa Taifa afagilia Chalenji


na Samia Mussa


amka2.gif
MSIMAMIZI wa Uwanja wa Taifa, Rish Moses Urio, amesema kuwa mashindano ya Shirikisho la Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam yamechangia kuinua uchumi wa Tanzania.
Akizungumza na Tanzania Daima Dar es Salaam jana, Urio alisema mashindano hayo yalisababisha hoteli mbalimbali za jijini kujaa na wachezaji na viongozi wengi waliofika katika mashindano walinunua bidhaa mbalimbali kupeleka makwao, jambo lililosaidia kukua kwa uchumi.
Urio alisema, ni jambo la kujivunia kufanyika hapa nchini mashindano ya CECAFA, kwa sababu yana faida kubwa ikiwamo michuano hiyo kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya kimataifa kamaSuper Sport ya Afika Kusini na vinginevyo.
Alisema kuwa uongozi wake umefanya kazi kubwa sana toka mashindano hayo yaanze kwa kuhakikisha uwanja huo unakuwa safi kila baada ya mechi kumalizika, jambo lililowaletea sifa kubwa kutoka kwa wageni hao.
"Kwa kweli mashindano yalikuwa na faida kubwa kwetu, nchi yetu imeweza kufahamika kupitia mashindano haya, nilifuatwa na baadhi ya viongozi wa nchi za kigeni zilizoshiriki na kuisifia nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuwa na uwanja mzuri" alisema Urio.
Aliongeza kuwa kama yataendelea kuandaliwa mashindano kama haya, basi yatazidi kuinua uchumi wetu na kuendelea kuitangaza nchi kupitia michezo hasa soka.


h.sep3.gif

 
Kombe bonde la Nile:Stars yaahidi ushindi leo

Imeandikwa na Na Amir Mhando,Cairo; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 322; Jumla ya maoni: 0


01_11_e6tnbm.jpg

Kikosi cha Taifa Stars





"TUNAJUA matokeo yetu yamewanyong'onyesha Watanzania, hatutawaangusha tena,
tutaifunga Uganda na kufuzu nusu fainai," hiyo ni kauli ya nahodha wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa akizungumzia mchezo wa leo.

Leo timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka kwenye Uwanja wa Polisi mjini hapa kuanzia saa 8:45 za huku sawa na saa 9:45 za Afrika Mashariki kumenyana na Uganda 'The Cranes' mchezo wa mwisho wa michuano ya soka Nchi za Bonde la Mto Nile hatua ya makundi.

Ni mchezo ambao lugha inayotakiwa kwa Stars ni ushindi wakati The Cranes wimbo wao ni 'hata sare' watakuwa wamefuzu nusu fainali.

Kikosi cha Uganda kilichopo mjini hapa hakina nyota wengi waliokuwa Dar es Salaam mwezi uliopita kwenye michuano ya Chalenji, badala yake wachezaji walio wengi ni chipukizi, lakini walio na uwezo mkubwa wa kusakata soka.

Uganda iliwaduwaza mashabiki wa Misri Jumamosi baada ya kuibana vilivyo Misri 'Farao' karibu dakika 89 za mchezo na kufungwa bao pekee dakika ya 90 mfungaji akiwa Ahmed Hassan Gedo.

Hali hiyo imeifanya Uganda sasa kuwa midomoni mwa wadau wa soka mjini hapa kwamba ni timu nzuri na inapewa nafasi kubwa ya kuifunga Stars leo.

Tayari watabiri wameanza kupanga nusu fainali itakavyokuwa kwamba Misri itacheza na Kenya ambayo itashika nafasi ya pili Kundi B, kisha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo 'DRC' itakayoongoza Kundi B itacheza na Uganda itakayoshika nafasi ya pili Kundi A.

Hayo ni matarajio ya mashabiki wengi hapa. Lakini Nsajigwa na wenzake wanasema
watawashangaza wengi na hawaoni kwa nini wasiingie nusu fainali, hivyo kazi yao leo ni moja kumpiga Mganda, kwani nia wanayo, uwezo wanao na sababu pia wanayo.

"Tumedhalilika mechi mbili zilizopita, Uganda itakuwa chakula yetu," alisema Nsajigwa, kauli
pia iliyozungumzwa na Mrisho Ngasa, Jerry Tegete ambao wameahidi kuonesha cheche zao leo wakipata nafasi ya kucheza.

Kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen alisema anatarajia mechi itakuwa ngumu, lakini kwa vile wanaingia wakiwa wanajua makosa halitawasumbua sana.

Alisema amewapa maelekezo ya kutosha washambuliaji wake, pia sehemu ya ulinzi na ana hakika watafanya kile alichowaelekeza kuhakikisha wanapata ushindi mnono.

Kwa upande wake kocha wa Uganda Bobby Williamson naye alisema mechi itakuwa ngumu, lakini ameshajua udhaifu wa Stars itakuwa si kazi ngumu kushinda.

Misri inayoongoza Kundi A ikiwa na pointi sita tayari imetinga nusu fainali na leo inamaliza na Burundi mchezo utakaofanyika mjini Ismailia, ambapo hata kama itafungwa haitaathirika.

Lakini ili Stars ifuzu nusu fainali itabidi iifunge Uganda leo, kisha iombee Misri iifunge Burundi ama itoke nayo sare, vinginevyo kama Burundi itashinda basi itabidi utazamwe uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Mpaka sasa Stars imefungwa mabao sita na imefunga mawili, hivyo ina deni la mabao manne, wakati Burundi imefungwa manne na imefunga mawili huku nayo ikiwa na deni la mabao mawili.

Uganda ni ya pili ikiwa na pointi tatu na mabao manne ya kufunga, ikiwa imefungwa mawili, huku Burundi ikiwa ya tatu na Stars ya mwisho. Zote zina pointi moja.

Kundi B leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), inacheza na Sudani ambayo mchezo wa kwanza ilifungwa bao 1-0 na Kenya kabla ya DRC kuifunga Kenya bao 1-0, hivyo mchezo huo utaamua timu za kufuzu nusu fainali, ingawa DRC ina nafasi kubwa kwani hata sare itakuwa imefuzu.

Michuano hiyo inashirikisha nchi saba zilizogawanywa makundi mawili na timu mbili za juu kila kundi zitacheza nusu fainali, wakati zilizoshika nafasi ya tatu zitacheza kuwania mshindi wa tano.
 
Simba yatinga fainali za Mapinduzi

Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:55 Imesomwa na watu: 470; Jumla ya maoni: 0

WAWAKILISHI wa Tanzania Bara kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba juzi usiku ilitinga fainali za michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Zanzibar Ocean View mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

Simba sasa inasubiri mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili iliyotarajiwa kuchezwa jana usiku kati ya Yanga na bingwa mtetezi Mtibwa Sugar.

Mechi ya juzi usiku ilionesha kuwa na upinzani tangu dakika ya kwanza ya mchezo ambapo Simba ilipata bao la kuongoza katika dakika ya tatu kupitia kwa Emmanuel Okwi aliyefunga bao hilo kwa mkwaju wa penati iliyotolewa na mwamuzi baada ya beki wa Zanzibar Ocean View Aziz Sharif kunawa mpira eneo la hatari.

Kuingia kwa bao hilo kulifanya Zanzibar Ocean View icharuke ambapo washambuliaji wake walikuwa wakilishambulia lango la Simba mara kwa mara na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 44.

Bao hilo lilifungwa na Saidi Ramadhani kwa mpira wa kichwa uliokuwa umetemwa na kipa wa Simba Ally Mustapha ‘Barthez'.

Kipindi cha pili kilikuwa kisichotabirika, baada ya kila upande kuonekana kuimarika na kutaka
kutafuta bao, lakini Simba ndio iliyobahatika katika mashambulizi hayo baada ya mchezaji wake Hilary Echesa kufunga bao la pili katika dakika ya 61.

Echesa alifunga bao hilo kwa shuti kali nje ya eneo la hatari.

Akizungumzia mechi hiyo Kocha wa Simba Patrick Phiri alisema upinzani alioupata katika mechi hiyo aliutarajia lakini anashukuru ameshinda.

"Sasa najua tutacheza fainali na Mtibwa au Yanga, nazijua vizuri timu hizo naziheshimu lakini zisiogopi kwani hata timu yangu ni nzuri," alisema.
 
Yanga kujipima na Zesco

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 140; Jumla ya maoni: 0

TIMU ya soka ya Yanga imepanga kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Zesco ya
Zambia, Januari 16.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya kuipa timu mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho na utachezwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Alisema kuwa Yanga inatambua uwezo wa timu hiyo katika medani ya soka na ndio maana imeamua kuialika katika mechi ya maandalizi na kwamba imechagua timu sahihi ya kujinoa nayo.

Yanga inawakilisha kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo imepangiwa kuanza na
Dedebit ya Ethiopia katika hatua ya awali na ikiiondoa timu hiyo itakutana na Haras El Hadoud ya Misri.

Mechi hizo za hatua ya awali zitachezwa mwishoni mwa Januari na kurudiana wiki mbili baadaye.

Timu hiyo ya El Hadoud iliwahi kuifunga Simba jumla ya mabao 6-3 katika michuano ya kombe la Shirikisho mwaka jana na kuipelekea timu hiyo ya Simba kurudi nyumbani.

Sendeu aliwatoa wasiwasi wapenzi wa klabu ya Yanga juu ya mechi ya timu hiyo na El Hadoud na kuongeza kuwa ushindi iliyoupata kwa Simba sio kigezo kuwa hata Yanga itafungwa.

Mapema baada ya kutangazwa kwa makundi hayo Kocha Kostadin Papic wa Yanga aliwahi sema kuwa kwa upande wake anaona mechi zote ngumu kwa vile haifahamu Dedebit ya Ethiopia na kwamba haelekezi nguvu zake kwa El Hadoud pekee bali kwa timu zote.
 
Michuano ya Afrika U-17: Gambia hoi kwa Kongo

Imeandikwa na Finny Muyeshi wa Cecafa, Kigali; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:45 Imesomwa na watu: 59; Jumla ya maoni: 0

BINGWA mtetezi wa michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 Gambia juzi ilianza vibaya kutetea taji lake baada ya kulamba kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Umuganda mjini Gisenyi katika mpaka wa Rwanda na Kongo.

Matokeo hayo yameiweka Gambia kwenye wakati mgumu kwani sasa ili isonge mbele italazimika kuifunga Mali na Ivory Coast katika mechi zake zilizosalia.

Wakongo walianza kupata bao la kuongoza katika dakika ya saba kupitia kwa Samarange Binguila kabla ya kuongeza bao la pili kupitia kwa Stevy Epako.

Binguila alifunga tena bao la tatu katika dakika ya 51. Katika mechi nyingine, Ivory Coast iliifunga Mali mabao 2-1 katika mechi iliyokuwa ngumu kwa pande zote.

Matokeo ya mechi hizo yanaifanya Kongo na Ivory Coast ziongoze kundi B zikiwa na pointi tatu kila moja lakini zimetofautiana uwiano wa mabao.

Leo michuano hiyo inaendelea baada ya jana kupumzika. Wenyeji Rwanda watakuwa kwenye uwanja wa Amahoro kumenyana na Misri wakati Burkina Faso itacheza na Senegal.

Timu mbili kutoka katika kila kundi zitafuzu nusu fainali za michuano hiyo na pia zitakuwa zimekata tiketi ya kuiwakilisha Afrika kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyopangwa kufanyika Mexico Juni mwaka huu.

 

Nchimbi mgeni rasmi uzinduzi wa THT


Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:40 Imesomwa na watu: 56; Jumla ya maoni: 0
WAZIRI wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Emanuel Nchimbi leo anatarajiwa kubariki albamu sita za wasanii wa Tanzania House of Talent (THT) katika uzinduzi wa albamu ya wasanii sita wa kundi hilo pamoja na hafla yao ya kutimiza miaka mitano.

Akizungumza na HABARILEO, Mkurugenzi Mtendaji wa THT Rugemalila Mutahaba alisema kuwa Waziri Nchimbi pia atazindua mpango maalum wa matumizi ya mtandao katika kuuza kazi za wasanii wa THT.

Akizungumzia zaidi mpango huo, Ruge alisema kwa sasa THT inataka kufanya kazi zake kiteknolojia zaidi kwa kuwasaidia wasanii wake kuongeza kipato pamoja na kuwapatia burudani wananchi.

Alisema katika mpango huo mpya nyimbo za wasanii zitakuwa zikiuzwa kwa shilingi 1,000 kwa kila wimbo na wananchi wanaweza kuununua kwa kupitia simu zao kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno.

Alisema kuwa chini ya mpango huo wasanii wanaweza kujipatia faida zaidi kwa kuwa hakutakuwa na fursa ya kuwadhulumu kwa kupitia njia za kukopi kwa kuwa wananchi wanaweza kupata nyimbo hizo kirahisi.

Akizungumzia mafanikio ya miaka mitano ya THT, Ruge alisema kuwa kwa sasa THT inajiendesha kama kampuni rasmi na sio tena kama Shirika lisilo la kiserikali, hali inayopelekea kampuni hiyo kuaminika na kupewa tenda nyingi.'

"Mimi huwa nawaambia hawa kuwa hii THT ni yao na sasa wajiulize kuwa wanawapatia burudani gani na kwa kiwango gani wapenzi wao wa burudani wanaohudhuria shoo zao," alisema Ruge.

Pia alisema kuwa katika kuwavutia wanunuzi kununua nyimbo za wasanii wao, THT imemtafuta mtaalamu anayetengeneza kava nzuri za wasanii hao kwa kuwatengenezea kava ambazo zinavutia.

Gazeti hili jana lilishuhudia wasanii pamoja na wanenguaji wa THT wakijifua chini ya wataalamu wa kucheza muziki kutoa Chuo cha Sanaa Bagamoyo.

Wasanii wanaotarajia kuzindua albamu zao leo ni Mwasiti, Pipi, Barnaba, Amini, Mataaluma na Linah.

 
Aibuka bingwa kombe la Mwenyekiti

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 10th January 2011 @ 23:35 Imesomwa na watu: 19; Jumla ya maoni: 0


MCHEZAJI gofu chipukizi kutoka Klabu ya Gymkhana Arusha (AGC), Nuru Mollel juzi aliibuka bingwa wa michuano ya Kombe la Mwenyekiti ambayo ilikuwa ni kiporo cha kalenda ya mashindano ya Chama cha Gofu Tanzania (TGU) ya mwaka 2010.

Michuano hiyo ya siku mbili ya viwanja 36 ambayo ilikutanisha wachezaji kutoka klabu mbalimbali nchini ilifanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Gymkhana Moshi, Kilimanjaro.

Nuru, ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita pia alipewa tuzo ya mchezaji mdogo zaidi kwenye timu ya taifa, aliibuka bingwa baada ya kukusanya mikwaju gross 147.

Chipukizi huyo alianza michuano akiwa na mikwaju 72 kabla ya kurejea na 75 siku ya pili na kuondoka na Kombe ambalo alikabidhiwa na mwenyekiti wa TGU, Dioniz Malinzi wakati wa sherehe za kutoa zawadi.

Nafasi ya pili kwenye michuano hiyo ilichukuliwa na Hamis Ally kutoka Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam (DGC) ambaye alikuwa na mikwaju 148.

Ally, ambaye alianza na mikwaju 71 kabla ya kumaliza na 77, amepata mafanikio yake ya kwanza kwa zaidi ya mwaka katika mashindano hayo ya mwisho.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa mchezaji wa DGC pia Adam Mwanyenza ambaye alikusanya mikwaju 150 (75, 75).

Elisante Lembris alishika nafasi ya nne akiwa na ikwaju 151 (77, 74), nafasi ya tano ilikwenda kwa John Saidi 152 (78, 74) na Jimmy Mollel (79, 74) alishika nafasi ya sita 153 wote kutoka AGC.

Mbali na mpambano huo kulikuwa na makundi mengine yaliyoalikwa kwa upande wa wanaume na wanawake na vijana wadogo.

Kwa upande wa wanawake chipukizi Vailet Peter aliibuka mshindi akiwa na mikwaju nett 136 baada ya kupiga kikwaju 65 siku ya kwanza na 71 siku ya mwisho huku Shazi Myombe akishika nafasi ya pili wote kutoka DGC.

Isaac Anania aliibuka mshindi kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18 akiwa na mikwaju gross 163 ( 83,80) na nafasi ya pili kwenda kwa Vincent Gullo (164) 89, 75).

Akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi Mwenyekiti wa TGU, Malinzi aliwataka wachezaji kujenga nidhamu hasa kwa wale watakaochaguliwa timu ya taifa.

Alisema wachezaji wengi hawafahamu umuhimu wa kuchezea timu ya taifa hivyo yeyote atakayekamatwa atakuwa amejiondoa na hakutakuwa na msamaha katika hilo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom