Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #2,821
Kanda Kabongo mbabe kickboxing
na Andrew Chale
BONDIA wa Kickboxing Kanda Kabongo ameibuka mbabe wa mchezo huo baada ya kumchapa mpinzani wake Moses Gololo wa Uganda mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Katika pambano hilo kali lililojaa kila aina ya ushindani ulioteka hisia za mashabiki wengi waliofurika kushuhudia, Kabongo aliweza kuonyesha umahiri wake wa kutumia mateke na ngumi nzito, ambazo zilimchanganya Gololo kiasi cha kwenda chini mara kwa mara.
Hadi raundi ya tatu na ya mwisho inamalizika, Kabongo aliweza kumshinda mshindani wake huyo kwa pointi, lakini kwa kipigo alichokitoa kilimfanya Gololo kutoka uwanjani hapo akiwa hoi na alishuka akichechemea, hali iliyomfanya kushindwa kupanda jukwaani kuchukua zawadi yake ya mshindi wa pili.
Hata hivyo, pambano hilo la fainali nusura livunjike baada ya kuingia dosari kadhaa, ikiwemo kukatika kwa kamba za ulingo mara mbili na kusababisha pambano kusimama mara kwa mara na wakati mwingine mabondia kuangushana hadi nje ya ulingo.
Kwa ushindi huo, Kabongo alizawadiwa ngao yake ya ubingwa na televisheni kutoka kwa Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Katika mapambano ya awali, Mtanzania Rajabu Mrisho, alipigwa na Mkenya Kevin Onyango, huku Miraji Madiwa naye akichapwa na Abdul Nasser wa Uganda wakati Hamis Mwikinyo wa Tanzania alimsambaratisha Mkenya Alphonce Kakaa na katika uzito wa juu Alphonce Mchumiatumbo alimchapa kwa KO, Eddie Dyle.