Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Kanda Kabongo mbabe kickboxing


na Andrew Chale


amka2.gif
BONDIA wa Kickboxing Kanda Kabongo ameibuka mbabe wa mchezo huo baada ya kumchapa mpinzani wake Moses Gololo wa Uganda mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Katika pambano hilo kali lililojaa kila aina ya ushindani ulioteka hisia za mashabiki wengi waliofurika kushuhudia, Kabongo aliweza kuonyesha umahiri wake wa kutumia mateke na ngumi nzito, ambazo zilimchanganya Gololo kiasi cha kwenda chini mara kwa mara.
Hadi raundi ya tatu na ya mwisho inamalizika, Kabongo aliweza kumshinda mshindani wake huyo kwa pointi, lakini kwa kipigo alichokitoa kilimfanya Gololo kutoka uwanjani hapo akiwa hoi na alishuka akichechemea, hali iliyomfanya kushindwa kupanda jukwaani kuchukua zawadi yake ya mshindi wa pili.
Hata hivyo, pambano hilo la fainali nusura livunjike baada ya kuingia dosari kadhaa, ikiwemo kukatika kwa kamba za ulingo mara mbili na kusababisha pambano kusimama mara kwa mara na wakati mwingine mabondia kuangushana hadi nje ya ulingo.
Kwa ushindi huo, Kabongo alizawadiwa ngao yake ya ubingwa na televisheni kutoka kwa Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Katika mapambano ya awali, Mtanzania Rajabu Mrisho, alipigwa na Mkenya Kevin Onyango, huku Miraji Madiwa naye akichapwa na Abdul Nasser wa Uganda wakati Hamis Mwikinyo wa Tanzania alimsambaratisha Mkenya Alphonce Kakaa na katika uzito wa juu Alphonce Mchumiatumbo alimchapa kwa KO, Eddie Dyle.
 
Mtambo wa Gongo naye ataka kujaribu kwa Cheka


na Makuburi Ally


amka2.gif
BONDIA mkongwe, Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo' ametoa wito kwa wadhamini wa mchezo huo nchini kumuandalia pambano kati yake na Francis Cheka ili amfundishe zaidi mchezo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Oswald alisema, Cheka ni bondia bora ambaye akicheza naye ana hakika atamdunda kutokana na kuwa yeye ni mmoja wa mabondia bora Tanzania.
Oswald alisema, bondia anayemsumbua ni Rashid Matumla ‘Snake Man', lakini wengine wote hana wasiwasi nao kwa sababu ya ubora aliokuwa nao katika mchezo huo.
Alisema, anamtaka Cheka kwa sababu ni bondia ambaye anaonekana ana muelekeo wa mchezo huo hapa nchini, hivyo atampa ushindani.
Aidha Oswald alisema, Mada Maugo si bondia, kwa sababu hana sifa za kuwa bondia kwani anapoteza malengo ya mabondia mahiri kutokana kukumbatia katika mchezo wake dhidi ya Cheka.
Alitoa wito kwa Maugo, kuendelea kujifunza ngumi zaidi ili kuachana na masuala ya kukumbatia awapo ulingoni na kubwabwaja.
 
TFF yazionya klabu

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 11th January 2011 @ 23:00

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezionya klabu ambazo zinachezea usajili wa wachezaji
wake kwa kukiuka mikataba bila ya kufuata taratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za TFF kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi kwa wachezaji wa Shirikisho hilo, Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osia 'Ngeta' alisema kuwa TFF inatambua kuwa wachezaji ndio soka kutokana na mchango wao kuwa mkubwa katika tasnia hiyo.

Alisema kuwa TFF imegundua kuwa baadhi ya klabu hushindwa kutimiza matakwa ya wachezaji na nyingine hushindwa kulipa malipo yanayostahili kitendo ambacho kinawakatisha tamaa wachezaji.

Akisoma maamuzi ya kamati hiyo alisema kuwa kamati imeiamuru klabu ya African Lyon kuwalipa wachezaji Geofrey Komba na Abdul Masenga Sh milioni 4.3 kila mmoja na kama ikishindwa kufanya hivyo haitoruhusiwa kusajili au kuuza mchezaji yeyote kwa msimu mpya wa 2011 na 2012.

Alisema kuwa maamuzi mengine ni kuhusu mchezaji wake Yusuf Soka aliyekuwa hajajiunga na klabu hiyo tangu msimu uanze na baada ya kusuluhishwa na kamati kwa sasa uongozi wa klabu hiyo umemruhusu aende nchini Sweden kwa majaribio.

Wachezaji Wisdom Ndlovu, Steven Marashi na John Njoroge hoja yao ya kutaka kulipwa na Yanga imetupiliwa mbali na kamati hiyo kwa kuwa wachezaji hao hawakuwahi kufika katika vikao vya kamati hiyo.
 
Stars nje Kombe la Nile

Tuesday, 11 January 2011 19:56 newsroom


Na Mwandishi Maalum, Cairo
TAIFA Stars imetupwa nje ya michuano ya kuwania Kombe la Nile inayoendela mjini hapa, baada ya kushindwa kutinga nusu fainali
kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Uganda. Stars ilianza mechi hiyo kwa matumaini makubwa ambapo katika dakika za mwanzo ilifanya mashambulizi makali langoni kwa Uganda, ambayo ilionekana kubabaika kutokana na kasi ya Stars.
Mashambulizi hayo yalizaa matunda katika dakika ya 24 ambapo Athumani Machuppa anayecheza soka ya kulipwa nchini Sweden,
aliandika bao la kuongoza kwa shuti kali.Bao hilo lilijenga matumaini kuwa Stars ingeweza kuwamudu Waganda na kushinda mchezo huo, lakini hali iligeuka katika dakika ya 71, wakati Yudah Mugalu wa Uganda, alipoisawazishia timu yake alipofunga kwa kichwa kufuatia mpira wa kona. Mapema katika kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu, ambapo Daniel Wagaluka nusura aipatie Uganda bao katika dakika ya 10, alipowatoka mabeki wa Stars na kupiga shuti kali lililoishia mikononi mwa kipa wa Stars, Juma Kaseja. Dakika mbili baadae, Kaseja aliokoa hatari katika lango la Tanzania kutokana na shuti jingine la Derick Walulya.
Baada ya Uganda kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao moja, kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu hiyo ililisakama lango la Stars kwa dakika 10 za mwanzo, lakini washambuliaji wake walishindwa kulenga lango la Stars. Kocha Jan Poulsen kuona hivyo, alifanya mabadiliko kunusuru jahazi lake kwa kuwatoa Salum Machaku na Saidi Maulidi, na nafasi zao kuchukuliwa na Mrisho Ngasa na Idrissa Rajabu.
Mabadiliko hayo hayakuisaidia Stars, ambayo ilicheza vibaya na kuifanya Uganda kutawala karibu sehemu kubwa ya kipindi hicho,
hali iliyomlazimisha Poulsen kufanya mabadiliko mengine ya kuwatoa Machuppa na Shaaban Nditi, na nafasi zao kuchukuliwa na Jabir
Azizi na Ally Ahmed ëShibolií, lakini hakukuwa na mafanikio ya kupata bao la ushindi. Matokeo hayo yanaifanya Uganda iungane na Misri kucheza nusu fainali, wakati Stars ikisubiri Burundi ifungwe na Misri, ili ipate fursa ya kuwani nafasi ya tano. Lakini matumaini hayo yatapotea ikiwa Burundi itashinda kwani itakuwa imeshika mkia katika kundi lake.
Stars: Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Nurdin Bakari, Salum Machaku/Mrisho Ngasa, Shaaban Nditi/ Ally Ahmed ëShibolií, Nizar Khalfani, Athumani Machuppa/Jabir Azizi, Saidi Maulidi/Idrissa Rajabu.
 
Ni Simba au Yanga Kombe la Mapinduzi leo

Tuesday, 11 January 2011 19:55 newsroom



NA SOPHIA ASHERY
NI fainali ya kihistoria ambayo inazikutanisha Simba na Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, katika mchezo utakaofanyika leo Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, ambapo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye uwanja huo katika fainali ya Kombe la Kagame mwaka 1992, Simba iliibuka na ushindi wa
penalti 5-4, na kutwaa kombe hilo. Mchezo huo ambao unavuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini, kwa vyo vyote utakuwa mkali na wa kusisimua kutokana na kila timu kuupania, jambo ambalo litaufanya uwe na upinzani mkali kutokana na timu hizo kuwa na upinzani wa jadi.

Licha ya mchezo huo kutokuwa na tambo, timu zote zitashuka dimbani zikiwa hazina baadhi ya wachezaji wake muhimu ambao wako katika kikosi cha timu ya taifa kinachoshiriki mashindano ya kuwania Kombe la Nile yanayofanyika nchini Misri. Akizungumzia mchezo huo jana, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, alisema mchezo huo licha ya kuwa mgumu, kikosi chake kinatarajia kufanya vizuri na kuibuka na ubingwa wa mashindano hayo. Phiri alisema hana wasiwasi na timu yake ambayo ina mazoezi ya kutosha, ikiwa na kiwango kizuri cha soka, na kusema ni lazima timu yake ishinde ili imuharibie kibarua kocha wa Yanga, Kostadin Papic.
"Nina kila sababu ya kujiamini kwa sababu nina timu nzuri ambayo haina wasiwasi na timu yoyote, na tunajua tutawakabili wapinzani wetu tukiwa na uhakika wa kushinda," alisema Phiri. Alisema katika mchezo wa leo wachezaji watakaoongoza mashambulizi watakuwa Mussa Hassan 'Mgosi', Emmanuel Okwi na Hilary Echesa, wakati safu ya ulinzi itasimamiwa vizuri na Kevin Yondan, Meshack Abel na Juma Nyoso. Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic, alisema hana wasiwasi kwa kuwa ubingwa ni wao baada ya kuwavua ubingwa mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar. Papic alisema fainali ya mashindano hayo ilikwishamalizika, hivyo mchezo wake na Simba ni wa kukamilisha ratiba ya mashindano hayo pamoja na kuchukua zawadi za ushindi.
"Simba haina ubavu wa kuifunga Yanga, hilo liko wazi na tutahakikisha tunaendeleza rekodi ya kuwafunga na hilo halina wasiwasi," alisema Papic.
Simba ilianza michuano hiyo kwa kutoa sare ya bao 1-1 na Jamhuri, kabla ya kuifunga KMKM mabao 3-0, kisha kuifunga Mtibwa 2-1 na kutinga fainali hizo.
Yanga nayo ilianza kwa kutoka sare ya bao 1-1, kabla ya kutoka suluhu na Chuoni na kisha kuifunga Mtibwa mabao 2-1, kabla ya kukata tiketi ya kucheza na watani wao hao wa jadi.
Bingwa wa mashindano hayo atajinyakulia kombe lenye thamani ya sh. milioni tatu na fedha taslimu sh. milioni tano, wakati mshindi wa pili atajipatia sh. milioni tatu.


 
Ashley Cole moves Kayla Collins into marital home as ex-missus Cheryl finally moves out


  • transparent.gif
  • transparent.gif
by Sarah Tetteh, Daily Mirror 12/01/2011
image-1-for-paper-pics-12-jan-2011-gallery-446779236.jpg

CHELSEA ace Ashley Cole is moving back into the marital home – while also moving on from his ex-missus...
As Cheryl finally moves out of the lavish Surrey mansion, five months after their divorce, footballer Ashley, 30, plans to play house there with new girlfriend, 24-year-old blonde Kayla Collins.
Less than a month after they started dating, he is bringing Kayla from the States to stay on an "indefinite" basis.
The I'm a Celebrity... star and Playboy Bunny – yep, she's a right minger – is flying in this weekend.
An excited Kayla, who is leaving the Playboy mansion with Hugh Hefner's blessing, has already said to pals about Ashley: "It's the real deal." And she tweeted yesterday: "Hello. Good morning. So many errands to run and things to do before back to the UK."
What better way to settle into life in Blighty than in the sprawling £3.5million, nine-bedroom mansion complete with private gym, jacuzzi, swimming pool and home entertainment room?
Advertisement - article continues below »



A source close to the couple tells me: "Ashley and Kayla are totally loved-up.
"She never thought she'd fall so hard, so quickly for someone but they get on really well. Kayla was gutted when she had to go back to LA for Christmas without him – they were in touch throughout the festive period.
"Ashley thinks she is so down-to-earth and is looking forward to just chilling with her at home. After training, they can just hang out, be together and have a laugh.
"Cheryl is moving out and Ashley will go back home. So it's a new start for everyone."
It's been a whirlwind romance for Ashley and Kayla. He fell in love/lust with the model when she appeared in an assortment of bikinis in the I'm A Celebrity... jungle. He then wooed her with dinners and flowers before finally introducing her to his Chelsea team-mates at his 30th birthday bash last month, where she gave Ash a football made of cupcakes.
While Kayla is heading over here to live with Ashley, Girls Aloud beauty Cheryl is off to Los Angeles to stay with dancer boyfriend Derek Hough.
Derek stayed in the Surrey mansion when Chezza was recovering from malaria. So if Kayla needs to know where the clean towels are kept...



 
Ben Foster error gives West Ham Carling Cup edge over Birmingham





Carling Cup Semi-Final L1

West Ham United 2
  • Noble 13,
  • Cole 78
Birmingham City 1
  • Ridgewell 56


  • David Hytner at Upton Park
  • guardian.co.uk, Tuesday 11 January 2011 21.56 GMT <li class="history">Article history
    West-Hams-Carlton-Cole-ce-007.jpg
    West Ham's Carlton Cole celebrates his first-leg winner with Zavon Hines. Photograph: Clive Rose/Getty Images If Avram Grant does survive as the manager of West Ham United, and goodness knows the jury remains out, he will know who he has to thank. His 10-man team was heading for a damaging draw in this first leg, and Grant for almost certain dismissal in what was a must-win fixture for him when Jonathan Spector cut a low ball back for the substitute Carlton Cole in pretty much West Ham's only forward thrust of the second half.
    It was the 78th minute and the ball was there to be smashed home yet the striker failed to make proper contact and his shot dribbled towards the Birmingham City goalkeeper Ben Foster. The crowd cleared their throats to groan only for Fate to click her fingers. Almost in slow motion, Foster tumbled off balance and Cole's tame effort crawled through his legs and over the line. Upon such moments can careers hinge. Had Grant enjoyed his Mark Robbins moment?
    That will become clearer today when to discuss the best way forward and, specifically, whether it ought to feature Grant at the helm. In one sense, he has done all he can. An excellent first-half performance here was followed by a desperately disappointing second-half one, which was scarred by Victor Obinna's reckless red card, but his team somehow got the result, which extended a reasonably positive recent run.
    In seven matches, Grant's team have lost only once, albeit dismally at Newcastle United in the Premier League, and it is a fact that this is their best sequence of the season. And it has been fashioned against all the difficulties; the injuries, the backstabbing and the intrigue.
    A first Wembley final in 30 years is within reach for West Ham. Grant has a flawless semi-final record with English clubs, having previously played three and won three but the big question is whether he will have the opportunity to lead the team in the second leg at St Andrew's in two weeks' time. Even this most laconic of men must feel his pulse hammering.
    Typically, the tie that had been billed as the one that Grant had to win to save his skin was a roller-coaster affair. The whole thing could conceivably have been over by the interval were it not for Foster who, ironically, had performed heroics to repel West Ham in the first half. He made reaction saves from Matthew Upson's early crack at the near post and Obinna's 30th-minute blast while he was also required to tip over from both Spector's rasping drive and James Tomkins' header from Scott Parker's corner.
    West Ham's goal had been all about Mark Noble. Having surged past two blue shirts to cross, he found the ball heading back his way after a heart-stopping scramble. The angle was tight but he sized up the shooting opportunity and let fly first-time. His right-footed connection was sweet and with Scott Dann obscuring Foster's command of the near post, the ball crashed through both of them.
    Birmingham were a shadow, in the first half, of the competitive force that their supporters have come to expect and Alex McLeish, the manager, fumed on the touchline. Yet by full-time, he could talk with some justification about an "opportunity missed".
    His team's improvement immediately after the restart was marked. Rather abruptly, there was drive and urgency, particularly from his three central midfielders. The equaliser almost came from one Sebastian Larsson corner, when Cameron Jerome's header was smuggled off the line by Freddie Sears and then it did come from another, Larsson's delivery again dangerous and Liam Ridgewell getting in front of Winston Reid to thump a header home.
    The turnaround illustrated just how fragile confidence is at West Ham and the feeling was compounded when Obinna lost his head completely. The on-loan Internazionale forward tangled with Larsson at a throw-in and flicked his studs up and back into his opponents' nether regions.
    The stupidity was almost surreal and it took a while to realise that he had indeed got himself sent off. Birmingham sought to turn the screw and Upson was mightily fortunate to escape the concession of a penalty when he shoved Barry Ferguson inside the area. "It was a stonewaller," McLeish said. "He did not just impede him, it was a barge in the back."
    "The goal was a monstrosity," said McLeish, who added that Foster had apologised to his team-mates.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom