Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Yanga wabariki Mwalusako kubwaga manyanga
• Papic, Mpangala nao kuiacha timu Shamba la Bibi leo

na Juma Kasesa


amka2.gif
BAADA ya Kamati ya Utendaji ya Yanga jana kubariki kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako, mzimu huo utarajiwa leo kuliandama benchi la ufundi.
Habari za uhakika zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam, zilieleza kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Mserbia Kostadin Papic na Meneja Emmanuel Mpangala nao wamedhamiria kufuata nyayo za katibu huyo.
Inadaiwa kuwa Papic na Mpangala wamekerwa na hujuma dhidi Mwalusako zilizomfanya abwage manyanga, hivyo nao wanatarajiwa kuwasilisha barua zao leo kwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Llyod Nchunga, baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi jana kubariki kuachia ngazi kwa Katibu Mkuu huyo ambaye hajatimiza hata mwaka tangu akabidhiwe mikoba hiyo mwaka jana.
Mwalusako alilithibitishia gazeti hili kuhusu kuwasilisha kwake barua ya kujiuzulu, huku akigoma kufafanua sababu za kufanya hivyo na kuahidi kuzungumza na vyombo vya habari leo.
Lakini habari za uhakika kutoka kwa mmoja wa watu wa karibu na Mwalusako zilisema, uamuzi huo wa kujiuzulu umetokana na kushinikizwa na mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, kutokana na kitendo chake cha kumkana mwenyekiti wake Nchunga, kuwa hakushirikishwa katika barua iliyoandikwa kwenda kwa mmoja ya wadhamini wa klabu hiyo, Francis Kifukwe.
Imeelezwa, kitendo cha Mwalusako kukana kufahamu barua ya mwenyekiti wake ikimuagiza Kifukwe kutafuta wakurugenzi 10 wenye uwezo wa kutoa shilingi milioni 50 kila mmoja ili kuunda kampuni itakayokuwa ikitengeneza bidhaa za Yanga, kimemkera mdhamini huyo na kuona kuwa katibu huyo hafai kuendelea kuingoza klabu hiyo.
Barua hiyo ya Nchunga kwa Kifukwe ni kati ya sababu zilizosababisha mwishoni mwa wiki iliyopita, viongozi wa matawi ya Yanga kuitisha mkutano wa dharura kumjadili mwenyekiti huyo kwa kitendo hicho, ambacho walikiita ni ukiukwaji wa katiba uliofanywa kwa makusudi, ikiwemo suala la uteuzi wa kiholela wa Mbunge wa Temeke, Abass Mtemvu, kuwa mmoja ya wadhamini wa klabu hiyo.
Katika mkutano huo wa viongozi wa matawi, Mwalusako na mjumbe wa Kamati ya Utendaji Mohamed Binda walihudhuria kwa niaba ya uongozi ambapo alikana kulifahamu suala hilo na kwamba hakushiriki kubariki uanzishwaji wa kusaka wakurugenzi hao, hivyo kumtupia msala mwenyekiti wake, jambo lililomkera mdhamini.
Aidha chanzo hicho kimefafanua, sababu nyingine ya kujiuzulu kwa Mwalusako, ni kufahamu njama za muda mrefu za kundi moja la wanachama, kupania kumng'oa yeye na meneja wa timu hiyo Emmanuel Mpangala kutokana na kutofautiana na baadhi ya viongozi wake.
Imeelezwa, Mwalusako amesoma alama za nyakati kwani hali ya amani imeanza kutoweka ndani ya klabu hiyo, kutokana na kundi hilo la wanachama kumfanyia fujo, Mpangala mara baada ya mechi baina ya Yanga na AFC ya Arusha, mchezo uliopigwa jijini Dar es Salaam na kulazimika meneja huyo kuondoka uwanjani saa 2:00 usiku chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Chanzo hicho kilibainisha kuwa katibu huyo amechukua uamuzi huo mzito, baada ya kuona akielemewa na mzigo wa utendaji wa majukumu ya Yanga kutokana na ukata wa fedha uliotanda klabuni hapo, hivyo kulazimika kufanya kazi ya ziada kuhakikisha timu hiyo inasonga mbele katika Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
"Hivi ninavyozungumza, Yanga haina fedha za kuwagharamia waamuzi na timu ya Dedebit ya Ethiopia kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho na huyo aliyeshinikiza ajiuzulu, amesema atatoa fedha hizo mara baada ya Mwalusako, Mpangala na Papic kuondoka, hivyo ndiyo ujue Yanga inaelekea kubaya, kwani mtu mwenye pesa akiwa hakutaki atafanya kila hila uondoke," kilisema chanzo hicho.
Imeelezwa kuwa Kocha Papic ambaye ameishatafutiwa msaidizi wake Fred Felex Minziro ‘Majeshi' anatarajiwa kuicha Yanga leo katika dimba la Uhuru wakati Yanga itakaposhuka dimbani kuumana na polisi Dodoma, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
 
Simba wautafuta mpira kwa tochi Dar


na Makuburi Ally


amka2.gif
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, jana walianza mzunguko wa pili Ligi Kuu bara vibaya baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2 mbele ya ‘Watengeneza Koni' Azam Fc kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Simba waliuanza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kufunga bao lao la kwanza katika dakika ya tisa, mfungaji akiwa Nico Nyagawa baada ya kazi nzuri ya Mussa Mgosi.
Baada ya bao hilo, Azam nao walibadilika na kuanza kulisakama lango la Simba na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 14 kupitia kwa John Bocco baada ya kuvunja mtego wa kuotea.
Azam waliendelea kulisakama lango la Simba na kufanikiwa kufunga bao la pili katika dakika ya 24 lililowekwa wavuni na Mrisho Ngassa aliyemlamba chenga kipa Juma Kaseja na kudumu hadi mapumziko. Kipindi cha pili, Simba walirejea uwanjani wakiwa na nguvu mpya baada ya kutolewa Nyagawa na nafasi yake kuchukuliwa na Ali Ahmed Shiboli ambaye alipiga mashuti mengi langoni mwa Azam, lakini umahiri wa kipa Vladimir Niyonkuru, uliokoa jahazi.
Azam walifunga bao la tatu dakika ya 54 kupitia kwa Bocco aliyemzidi ujanja beki Juma Nyosso na kipa Kaseja na kuukwamisha mpira wavuni.
Baada ya bao hilo Azam waliendelea kulisakama lango la Simba, kwa kugonga zaidi ya pasi 20 ambazo ziliwafanya Simba ‘wausake mpira kwa tochi', lakini kucheza huko hakukuisaidia Azam kuongeza bao.
Simba ilipata bao la pili la Simba likifungwa na Hilary Echesa dakika ya 87 akitumia vema pasi ya Mohammed Banka; bao lililowaongezea nguvu kutaka kusawazisha, lakini hadi mwamuzi Ibrahim Kidiwa Mdudu anamaliza mpira, Azam 3 Simba 2 hivyo kulipa kisasi cha kichapo cha 2-1 mzunguko wa kwanza.
Kocha Simba, Patrick Phiri, alisema kipigo hicho kimesababishwa na mawasiliano mabaya kati ya mabeki na kipa Kaseja huku Stewart Hall akisema ingawa wameshinda wapinzani wao ni wazuri.
Simba iliwakilishwa na Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah/Juma Jabu, Meshack Abel, Juma Nyoso, Jerry Santo, Rashid Gumbo/Mohamed Banka, Hillary Echesa, Patrick Ochan, Mussa Mgosi na Nico Nyagawa/Ally Ahmed Shiboli.
Azam iliwakilishwa na Vladimir Niyonkuru, Ibarahim Shikanda, Mutesa Patrick, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Obrahim Mwaipopo, Jamal Mnyate/Himid Mao, Salum Abubakar, John Bocco/Ssenyonjo Peter, Ramadhani Chombo na Mrisho Ngassa.
 
IRFA yasikitishwa kifo cha shabiki uwanjani


na Francis Godwin, Iringa


amka2.gif
CHAMA cha soka mkoani Iringa (IRFA) kimeeleza kusikitishwa na kifo cha shabiki wa timu ya Njombe Mji, Geofrey Mwalongo, ambaye aliuawa kwa kuchomwa kisu juzi katika Uwanja wa Amani Makambako, wilaya ya Njombe, wakati wa mchezo wa ligi daraja ya tatu ngazi ya taifa kati ya mji wa Njombe na Mbeya Road. Pamoja na kumlilia shabiki huyo bado IRFA inajiandaa kufanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo la mauaji katika mchezo huo pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wa chama cha soka wilaya ya Njombe kwa kukiuka maagizo ya kuufungia uwanja huo.
Katibu Mtendaji wa IRFA, Eliud Mvella 'Wamahanji' aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na kifo cha shabiki huyo na mikakati ya chama hicho katika kuendeleza michezo mkoani hapa.
 
Rwanda waifagilia Taifa Stars


na Method Millanzi, Bagamoyo


amka2.gif
BALOZI wa Rwanda hapa nchini, Fatma Ndangiza, amewataka wasomi hapa nchini kuupanga muda wao katika kushiriki michezo mbalimbali, hatimaye waweze kung'ara kimataifa.
Akizungumza kwenye mahafali ya kidato cha sita katika shule ya Boabab iliyopo Mapinga Wilayani Bagamoyo juzi, Ndangiza alimpongeza mkurugenzi wa shule hiyo, Khalfan Swai kwa kujenga viwanja vya michezo ambavyo vinatumika kwa michezo ya soka, netiboli, wavu na mpira wa kikapu inayochangia kuwaandaa nyota wa taifa wa baadaye.
Balozi huyo ambaye kitaaluma ni mwalim alifika mbali zaidi kwa kupongeza mafanikio ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kuwataka wasomi hao na Watanzania kuunga mkono juhudi hizo kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia inapocheza michuano ya kimataifa.
Ndangiza aliweka bayana timu ya Arsenal ya Uingereza na wahitimu walipendekeza pia kuipenda na Yanga, alisema nchi yake inathamini changamoto wanapokumbana na klabu za Tanzania hususani Yanga na Simba.
 
TASWA yaiadhibu Tanzania Stars


na Juma Kasesa


amka2.gif
MABAO mawili yaliyotiwa kimiani na mshambuliaji Said Seif wa timu ya Waandishi wa Habari za Michezo Taswa FC jana yalitosha kuiangamiza timu ya wachezaji wa zamani ‘Tanzania Stars', katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ulioandaliwa na Kampuni ya Popular Sports Entertainment ya jijini Dar es Salaam, Taswa FC ndio walikuwa wa kwanza kulishambulia lango la Tanzania Stars dakika 16 ya mchezo kupitia Julius Kihampa baada ya kumegewa pasi safi na Wilbert Molandi, lakini akababaika kuzitikisa nyavu za wapinzani wao kwa kunyang'anywa mpira na mabeki kabla ya kukosa bao lingine dakika ya 22 akiwa na kipa.
Tanzania Stars walijibu mashambulizi hayo dakika 24 kupitia Abubakar Kombo ambaye alifanikiwa kuitoka ngome ya Taswa FC na kubakia na kipa Mohamed Abdalah lakini akababaika kufunga na kujikuta akipoteza mpira.
Dakika ya 26 Abdalah Kaburu alikosa bao la wazi baada ya kushindwa kuitumia krosi aliyomiminiwa na Lawrence Mwalusako lakini shuti lake lilitoka nje na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa Taswa kulishambulia lango la Tanzania Stars ambapo shuti la chinichini lililopigwa na Majuto Omary lilitoka mita chache ya lango, kabla ya Said Seifu kuifungia timu yake bao la kuongoza dakika 47 kwa kuwapiga chenga mabeki na kipa wa Maveteran hao na mpira kutinga wavuni.
Seifu aliihakikishia ushindi timu yake dakika 67 kwa kupachika bao la pili akiunganisha krosi ya Wilbert Molandi na kufanya mechi hiyo kumalizika kwa Taswa kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0.
 
Manji atoa sababu za kumteua Mtemvu Sunday, 23 January 2011 20:59

manjii.jpg
Yusuf Manji

Vicky Kimaro
MFADHILI wa Yanga, Yusuf Manji ameibuka na kutoa sababu za yeye kumteua Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kuingia kwenye bodi ya wadhamini wa klabu hiyo.

Akizungumza na kituo cha Televisheni cha TBC, Manji alisema kabla ya Mtemvu kutangazwa kuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya wadhamini aliwasilisha hoja ya kutaka aongezwe mbunge mmoja na mfanyabiashara mmoja kwenye bodi ya wadhamini ya klabu hiyo katika kikao cha kamati ya utendaji kilichokaa Novemba 30, mwaka jana kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam

"Hayo yalikuwa ni maoni yangu baada ya kuona wenzetu wa Simba tayari wana watu wa kuwatetea na kuwatatulia matatizo yao kwa haraka pale watakapokwama, mwenyekiti wao Rage ni mbunge, wana watu wengi bungeni kama Mohamed Dewji, Idd Azan, Musa Hassan ‘Zungu' Makongoro Mahanga, wote ni wa hapa Dar es Salaam Yanga wana nani?"alisema kwa kuhoji.

"Ndio maana nilimpendekeza Mtemvu kwa vile niliona ana vigezo vinavyostahili, Halima Mdee ni mpya sijui ana mapenzi na timu gani kati ya Simba au Yanga, kuna hati za kufuatilia ardhi kwa ajili ya ujenzi wa ule uwanja wetu umekwama kuendelea kujengwa kwa vile kuna watu wamevamia pale wanatakiwa waondolewa sasa nani atafuatilia ardhi.

"Yanga imekuwa ikihangaikia uwanja kila kukicha, lakini kama tuna mtu Mbunge akiungana na Mbunge wa Simba ni rahisi kukaa na Waziri mhusika wakatatuliwa tatizo lao kwa urahisi tofauti na mimi, lakini wao kama wanaona Mtemvu hafai basi watafute mbadala mimi simng'ang'anii,"alisisitiza.

"Mimi kumteua Mtemvu si kwa utashi wangu ni baada ya mwenyekiti Lloyd Nchunga kunipa idhini hiyo ya kumtafuta mtu ambaye namuona anafaa, lakini kwa vile hawamtaki tusilumbane kwa ajili ya masuala haya tukaipeleka Yanga kwenye migogoro isiyokuwa na maana mimi nawaomba watafute mbadala na hata kama wanataka na mimi niondoke nipo tayari kukaa pembeni na kuwaachia Yanga yao."

Wakati huo huo; Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimedai kuwa Manji amemshinikiza Katibu Mkuu Lawrance Mwalusako kujiudhuru kwa kuhuma za kikiuka maagizo.

Juzi Mwalusako aliandika barua kwa mwenyekiti Nchunga ya kujiudhuru kuendelea kuitumikia klabu hiyo akiwa kama katibu wa kuajiliwa.

Habari za uhakika zilizotolewa na mmoja wa Viongozi wa Yanga aliimbia Mwananchi kuwa Mwalusako kajiudhuru baada ya kukutana na Manji na kumtaka afanye hivyo kwa sababu hataki kufuata anayoagizwa na mdhamini huyo.

Kiongozi huyo alisema mdhamini huyo alichukizwa na Mwalusako kwenda kwenye mkutano wa Viongozi wa Matawi ambao ulimtaka Nchunga asimamishwe kutokana na kutaka kuiuza Yanga kinyemela bila kushirikisha kamati ya Utendaji.

Alisema kosa jingine lililomtoa Mwalusako ni kuikana barua ambayo ilikuwa imeandikwa na Nchunga na Francis Kifukwe ya kumtaka atafute watu kumi watakatoa milioni 50 kwa Mwaka na kufikisha milioni 500 ambazo zitakuwa kama mtaji wa kuanzisha Yanga Kampuni.

Mbali na hayo pia Manji alimwambia kuwa astahili kubaki Yanga kutokana na ubadilifu wa fedha alioufanya ambazo zilikuwa ni fedha za usajili 100 milioni ambazo Mwalusako alishazitolea ufafanuzi.

Kiongozi huyo alidai kuwa Manji amekuwa akitumia fedha zake kwa ajili ya kuwapa wanachama kitu kidogo na kuendeleza migogoro inayoendelea hivi sasa.

 
Pazi aongelea umuhimu wa soka la vijana
Sunday, 23 January 2011 20:47

Sweetbert Lukonge
KIPA wa zamani wa Simba na timu ya taifa,'Taifa Stars', Idd Pazi 'Father'amezitaka klabu mbalimbali hapa nchini kutengeneza mazingira mazuri katika kuinua soka la vijana kama zinataka kupata mafaniko ya kweli.

Kipa huyo wa zamani wa Simba ya miaka ya tisini hivi sasa anafundisha klabu ya Seeb inayoshiriki Ligi Kuu nchini Oman.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa njia ya simu, Pazi alisema kuwa klabu za Tanzania zinatakiwa kubadilika na kujikita zaidi katika kuendeleza soka la vijana ambao hapo baadaye watakuwa hazina kubwa na chachu ya mafanikio katika timu hizo.

Alisema kukosekana kwa mipango madhubuti kwa klabu za hapa nchini katika kukuza soka la vijana ndiyo sababu iliyoifanya Ligi Kuu ionekane kuwa ni ya Simba na Yanga pekee.

"Umefika wakati wa klabu zetu kubadilika na kujikita zaidi katika kuinua soka la vijana na kuachana na tabia ya kusajili wachezaji ambao hawana msaada wowote zaidi ya kuziongezea matatizo.

"Katika dunia ya sasa vijana ndiyo wana soko kubwa katika soka hii ni kutokana na mabadiliko makubwa ya soka yanayotekea kila kukicha, hivyo klabu zetu zinatakiwa kwenda sambamba na mabadiliko hayo ikiwa ni pamoja na kujitengenezea faida kubwa ya kuuza wachezaji nje kama zinavyofanya timu nyingine za mataifa ya magharibi," alisema Pazi.

Katika hatua nyingine Pazi amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini kuhakikisha linatengeneza mfumo mzuri kwa vijana utakaosaidia kuwa chachu ya kuibua vipaji mbalimbali vilivyojificha.

Alisema Tanzania sasa inahitajika kuwepo na ligi ndefu ya timu za vijana kama ilivyo ile ya Ligi Kuu ili kuhakikisha timu za vijana zinakuwa katika mashindano kwa muda mrefu hali itayosaidia kuwajenga na kuwapa uzoefu zaidi kabla ya kupandishwa na klabu zao.

Alisema mfumo wa sasa wa mashindano ya wiki moja kwa mwaka mzima kama yaliyomalizika hivi karibuni na Ruvu Shooting kuibuka mabingwa hausaidii isipokuwa unachangia kuua vipaji hivyo vya soka nchini.

 
Mwakalebela:Timu hazijishughulishi kupata wadhamini
Sunday, 23 January 2011 20:48

Allan Goshashy

KATIBU Mkuu wa zamani wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Frederick Mwakalebela amesema klabu za soka zinazoshiriki Ligi Kuu zinashindwa kupata udhamini kwa sababu hazijishughulishi kuhakikisha zinapata wadhamini.

Amesema viongozi wa klabu zinazoshiriki ligi kuu hawawezi kuandika mapendekezo (proposal) ya kutafuta wadhamini kwa sababu hazina uwezo wa kuwashawishi wadhamini.

Mwakalebela alisema hayo baada ya kufanya mahojiano maalum na Mwananchi, huku akisisitiza hata klabu za Simba na Yanga zilipata udhamini wa TBL baada ya kusaidiwa na TFF.

"Mdhamini anataka taarifa za benki(bank statement), kanuni za fedha (financial regulations), akaunti zilizokaguliwa (audited account),Mipango ya biashara (Business plans), lakini mimi sijawahi kusikia klabu yoyote inajitokeza kifua mbele kudai mahesabu yao yamepitiwa na kampuni ya ukaguzi ambayo inaheshimika,"alisema Mwakalebela.

Alisema,"Pia klabu za soka za ligi kuu zimejaa migogoro hivyo wadhamini wanaogopa kuweka fedha zao kwa sababu wanaona hakuna viongozi bora na utawala bora."

Mwakalebela alisema baada ya TFF kugundua tatizo hilo waliamua kuzisaidia klabu za ligi kuu na kurahisisha kazi zao ambapo mwaka 2008 waliamua yafanyike marekebisho ya katiba zote za klabu za soka zilizo Ligi Kuu.

Alisema baada ya klabu kufanya marekebisho ya katiba, mwaka 2009, TFF iliamua wachezaji na makocha wote wa Ligi Kuu lazima wawe na mikataba jambo ambalo lilifanyika pia.

Katibu huyo wa zamani wa TFF alisema mwaka 2010 TFF iliamua klabu zote za Ligi Kuu ziwe na watendaji wa kuajiriwa kwa sababu walifahamu klabu ikiajiri katibu mwenye shahada atasaidia zaidi masuala ya utawala na pia klabu ikiwa na mweka hazina ambaye ana shahada atasaidia katika masuala ya fedha ya klabu.

Mwakalebela alisema TFF iliamua mwaka 2011 kila klabu kuhakikisha inakuwa na akaunti ambayo imekaguliwa (audited account) kwa sababu zinao waweka hazina wataalamu, pia kila klabu iwe na ofisi na sehemu maalum ya kufanyia mazoezi siyo kuhama hama.

"Klabu za soka nchini zinahitaji sana wadhamini kwa sababu hazina fedha za kuwaandaa wachezaji wake wawe wazuri na kuwaweka kambini kwa sababu kufanya hivyo ni gharama,"alisema Mwakalebela.

Alisema,"TFF ikisema ligi kuu imekwisha na kambi za klabu zote za soka zinazoshiriki ligi kuu zinavunjwa, suala hilo la kuvunja kambi mapema kwa klabu zinazoshiriki ligi kuu linachangia kudumaza soka ya Tanzania.

Mwakalebela alisema pia ukosefu wa fedha kwa klabu zinazoshiriki ligi pia unasababisha klabu za ligi kuu kushindwa kuanzisha timu za vijana.

"klabu nyingi zimekuwa zikiunda tu timu za kushiriki mashindano ya Uhai ambapo mashindano hayo ya vijana yakimalizika na timu za vijana zinakuwa hazipo tena mpaka mashindano yajayo wanatafutwa wachezaji wengine na ndio maana ni vigumu kusikia klabu imepandisha wachezaji wake wa timu ya vijana kucheza ligi kuu,"alisema Mwakalebela.

Mwakalebela pia amezishauri klabu za Ligi Kuu kuhakikisha zinakuwa na viwanja vya kufanyia mazoezi kama ilivyo klabu ya Mtibwa huku akisisitiza klabu hizo kuwa na umoja ili kuwa na sauti.

Pia alizishauri klabu ziache tabia ya kushirikiana na waamuzi kufanya rushwa katika soka kwa sababu kitendo hicho kinasababisha timu inayoshinda inakuwa haistahili.

 
Yanga out to consolidate league lead Sunday, 23 January 2011 21:22 By Majuto Omary
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Red-hot Yanga swing back into action today when they entertain relegation threatened Police Tanzania at Uhuru Stadium.

The Jangwani Street boys embarked on the second round of the Mainland Premier League on a high note following their resounding 6-1 win over minnows AFC on Saturday.

Yanga, now relishing at the summit of the league, will bank on Davies Mwape who is firing on both cylinders. The Zambian bagged a superb hat-trick against strugglers AFC of Arusha.

The former champions, however, will not expect an easy ride since Police Tanzania would be all out as they fight to avoid relegation.

Police Tanzania have been struggling in the league since their promotion last year. They lost their last two matches to Mtibwa Sugar (1-0) and Toto Africa (2-0).

The Dodoma-based team has accumulated 13 points while their opponents lead the league with 28 points.

In today's match, newly hired Yanga assistant coach Fred Felix Minziro is expected to be on the technical bench for the first time.

Recently, Yanga head coach Kosta Papic went on record as refusing to work with Minziro, claiming that club leaders overstepped their authority to hire their former defender.

"Leaders do not have the power to choose my assistant coach, at least, they should have consulted me, but what they did is unacceptable," the Serbian was quoted as saying.

It remains to be seen whether the two will work together since Papic had even threatened to resign should the Yanga leaders hold on with their decision to keep Minziro as his assistant.

Meanwhile, Yanga secretary general Lawrence Mwalusako has tendered a letter of resignation to the club. Mwalusako said yesterday that he decided to resign because of health issues.

However, some insiders linked his resignation with the ongoing wrangles at the club.

 
TFF yatafuta mrithi wa Rodrigo Sunday, 23 January 2011 20:46

Sosthenes Nyoni
KAMATI ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeiagiza kamati ya ufundi na ile ya soka la vijana kukutana na kujadili suala la kocha atakayezinoa timu za taifa za vijana, Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys baada ya mkataba wa kocha wa sasa Rodrigo Stockler kumalizika mwezi Aprili.


Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah aliliambia Mwananchi jana kuwa hatua hiyo inatokana na kocha wa sasa Rodrigo Stockler kumaliza mkataba wake.

"Kwa kuzingatia Rodrigo anamaliza mkataba wake Aprili tayari kamati ya utendaji imeiagiza kamati ya ufundi na ile ya soka la vijana kukutana na kujadili suala hilo.

"Kimsingi wao ndio watajua nini cha kufanya kama ni kusaka kocha mwingine ama vinginevyo," alisema Osiah.

Rogrigo aliondoka nchini mwishoni mwa mwaka jana kuelekea mapumzikoni Brazil na alishindwa kurejea kwa wakati licha muda wake wa likizo kuisha na hivyo kuilazimu TFF kumtangaza Jamhuri Kihwelo kuwa kocha wa muda wa timu za vijana.

Hata hivyo vyanzo vingine vya habari vimekuwa vikimhusisha Rodrigo na mpango wa kujiunga na moja kati ya klabu kubwa nchini Brazil.
 
Cranes stars seal deals to St. George Sunday, 23 January 2011 21:21

Kampala. The Uganda Cranes stars have been issued with International Transfer Certificates (ITC's) to join Ethiopian giants St. George.

All three players were part of Uganda's squad that finished third in the Council for East and Central Football Associations (Cecafa) Senior Challenge Cup held in Dar es Salaam year.

Odongkara and Isinde, passed their trials and were given two-year contracts. The club, handled by new Italian coach Giuseppe Dossena, paid $20,000 for the pair who pocket $2,000 per month each.

The left winger who was the first to arrive at St George on a six-month development contract with a view of joining a European club was also granted a temporary ITC.

"Giuseppe Dossena is a personal friend and we needed to work with a coach of that calibre whose aim is to train Malouda for European football," Proline's football director Mujib Kasule told Sunday Monitor.

He added that Matovu will get the chance to play in the Confederation of African Football (Caf) Champions League first leg encounter against Angola's Petro Altletico next week.

"He needs to gain experience for a move to Europe next season," added Kasule.

Elsewhere, reigning African club champions TP Mazembe will begin their quest to defend the title for a record third consecutive time against Tanzanian or Comorian opposition.

The runners-up at the 2010 Club World Cup were spared the first-round in a three-round qualifying draw for the 2011 competition. The Congolese could either face Elan Club Mitsoudje from Comoros Islands or the Tanzania Mainland champions, Simba Sports Club in the second round with Mazembe.(The Citizen Correspondent)

 
Federer aweka rekodi Sunday, 23 January 2011 20:45

MELBOURNE, Australia
BINGWA mtetezi Roger Federer amefikia rekodi ya Jimmy Connors baada ya kufuzu kwa robo fainali kwa kumfunga Tommy Robredo 6-3, 3-6, 6-3, 6-2 kwenye michuano ya Australian Open.

Federer amefuzu kwa fainali hiyo akiwa ameshinda michezo 27 mfululizo tangu alipotolewa kwenye hatua ya tatu mwaka 2004 mchuano ya French Open na kuifikia rekodi ya Connors.

Mshindi huyo wa mataji 16, hakupoteza pointi kuanzisha mchezo katika seti ya kwanza, lakini alizidiwa kwenye raundi ya pili wakati Robredo alipotawala na kulazimisha Federer kubadilika katika seti ya tatu na nne.

"Nilipoteza dira kwa muda kila nilichofanya kilikataa kabisa," alisema Federer. "Sikuwa kwenye kiwango kizuri cha mchezo nilipokuwa nyuma kwa 4-3." Federer alirudi mchezo katika seti ya tatu baada ya kuongoza kwa 2-0.

Federer anatafuta kuwa mchezaji wa pili kwa wanaume kushinda mataji matano ya Australian Open.

Mchezaji namba tatu kwa ubora Djokovic anasaka taji la pili la Australian.
Bingwa huyo wa mwaka 2008, amefuzu kwa robo fainali kwa ushindi wake wa 6-3, 6-4, 6-0 dhidi ya Nicolas Almagro. Sasa atakuna na mshindi wa pili wa michuano ya Wimbledon 2010, Tomas Berdych, aliyemshinda Fernando Verdasco 6-4, 6-2, 6-3.

Caroline Wozniacki amefuzu kwa robo fainali kwa wanawake baada ya kupata ushindi wa 6-3, 6-4 dhidi ya Anastasija Sevastova.

Naye Li Na, nyota wa China mwenye mafanikio zaidi amefuzu kwa robo fainali kwa ushindi wa 6-3, 6-3 dhidi ya Victoria Azarenka wa Belarus.

 
Burkina Faso yatwaa ubingwa U17, Afrika
Sunday, 23 January 2011 20:45

KIGALI, Rwanda
VIJANA Burkina Faso walizima kelele zote za mshabiki waliofurika uwanjani baada ya kuwachapa wenyeji Rwanda 2-1 na kutangazwa kuwa mabingwa wa fainali za tisa za Mataifa ya Afrika CAF kwa vijana U17 kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali.

Pamoja na kadi za njano na nyekundu kutolewa Burkina walionekana kutulia zaidi kiufundi na mwisho walifanikiwa kupata bao kupitia mshambuliaji wao mahiri Kabore Aziz aliyempiga shuti lilomshinda kipa wa Rwanda, Marcel Nzarora na kunyamazisha mashabiki wote uwanjani hapo.

Nzarora hakuwanyamazisha mashabiki uwanjani hapo, ila aliwaumuza mamilioni ya Rwanda waliokuwa wakisikiliza redia na kuangalia televisheni nchi nzima wakishudia Burkina wakatangazwa kuwa mabingwa wapya.

Chipukizi hao wa Burkina walisimama vifua mbele wakati walipopanda kuchuwa medali zao na kombe walilokabidhi na Rais Kagame pamoja na Rais wa CAF, Issa Hayatou.

Kocha wa Rwanda, Tardy Richard alisema; "Nawapongeza Burkina Faso na ususani kocha Rui Vierra Manuel kwa mchezo mzuri. Tumefungwa kwa sababu mbili kubwa. Tulichoka na pili, tulicheza mechi kabla ya kuingia uwanjani. Kulikuwa na shindikizo kubwa na mategemeo mengi kutoka kwa wachezaji jambo lililowaathiri kwa namna furani. Warwanda wameumia kwa matokeo haya, lakini mimi nimelizika kwa sababu tumecheza fainali kwa mara ya kwanza na tumefuzu kwa Kombe la Dunia."

"Tunatakiwa kufanya kazi zaidi kwa ajili ya maandalizi yetu ya Kombe la Dunia. Tumemaliza mashindano haya kwa heshima kubwa," alisema Tardy.

Katika mchezo huo Burkina walipata bao la kuongoza kupitia kwa Sanou Zaniou alipotumia vizuri uzembe wa nahodha wa Usengimana Faustin kuipa Stallions goli la kuongoza dakika ya 59. Hata hivyo bao hilo lilidumu kwa muda mchache kabla ya Mwesigye Tibingana kusawazisha kwa shuti la mbali dakika ya 67.

Matokeo yakiwa 1-1, mwamuzi kutoka Angola, Martins De Carvalho Helder alitoa zawadi kwa kumpa kadi nyekundu beki Kanazoe Bassirou dakika ya 60, Rwanda walijaribu kutumia nafasi hiyo kwa kufanya mashambulizi mengi na kucheza pasi nyingi, lakini ngome ya Burkina ilikuwa makini kuokoa hatari zote.

"Rwanda ni timu nzuri walitulizimisha tubadilishe mbinu za uchezaji. Tumezoea kushambulia zaidi, lakini leo tulijaribu kaa sana nyuma na kujilinda zaidi katikati ya uwanja," alisema Vierra Manuel na kuongeza: "Ulikuwa mchezo mzuri na tumepata mabao mazuri. Jambo la huzuni pekee ni kadi nyekundu ya beki wetu Kanazoe Bassirou. Ni jambo zuri tumetwaa ubingwa huu wakati tulipoondoka Burkina Faso hatukuahidi mtu yoyote kwamba tutarudi na ubingwa. Nimefurahi sana tumetwaa ubingwa huu."
 
Barca thrash Racing to stretch lead Sunday, 23 January 2011 21:16

Barcelona. Barcelona won its 14th straight Spanish league game with a comfortable 3-0 victory over Racing Santander on Saturday.
Pedro Rodriguez and Lionel Messi scored in the first half and Andres Iniesta added another after the restart to send the league leaders seven points clear of Real Madrid ahead of its match against Mallorca late yesterday.

Pep Guardiola's team showed no signs of its midweek defeat to Betis in the Copa del Rey, which ended its run of 28 games without a loss, and continued its dominating play that led it to the midway point of the season with a record points haul of 52.

Racing did what it could to withstand Barcelona's barrage, but the Catalan side's trademark combination of short, quick passes was too much for the visitors to handle.

Rodriguez opened the scoring in the second minute chesting a lob pass from Messi across the goal line after the Argentina star combined with David Villa and penetrated the area on the left side.

Messi made it 2-0 from the penalty spot in the 33rd after Villa was fouled in the area by Racing defender Henrique, and Iniesta fired a pass from Rodriguez that took a friendly deflection off a defender before landing in the net to cap the win in the 56th.

Barcelona's league-winning run matched a club record from 2005-06, and was just one victory shy of equaling the league record of consecutive wins set by Real Madrid in 1960-61.

"There are no easy games," Villa said. "But we went ahead in the second minute and that took the pressure off.
"Now we have to see if we are lucky tomorrow and Madrid doesn't win."(AFP)

 
Tunaamini Simba na Yanga zimejiandaa vya kutosha Sunday, 23 January 2011 20:55

papic.jpg
Kocha wa Timu ya Yanga Kostan Papic

MWISHONI mwa wiki hii klabu za Simba na Yanga zitaingia uwanjani kuanza harakati zao za kuliwakilisha taifa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Klabu ya Simba italiwakilisha taifa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza na Elan Club de Mitsoudje nchini Comoro wakati klabu ya Yanga itacheza na Dedebit ya Ethiopia mjini Dar es Salaam.

Tumekuwa tukizikumbusha timu hizi mara kwa mara kuzingatia maandalizi kabla ya kushiriki mashindano yoyote kwa sababu huwa tunaamini ni vigumu kupata ushindi katika mchezo wowote bila kujiandaa vizuri.

Mara baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu wachezaji wa klabu za Simba na Yanga waliendelea kucheza mashindano mbalimbali, wale waliokuwa kwenye timu ya taifa walicheza mashindano ya Chalenji na Bonde la Mto Nile na wale ambao hawakuwa katika timu ya taifa walicheza mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Pia, wiki iliyopita klabu za Simba na Yanga zilipata nafasi ya kucheza mechi ya kirafiki na timu kutoka Brazil ya Atletico Paranaense vilevile Simba ilicheza mechi ya kirafiki na mabingwa wa soka wa Zambia, Zesco.

Tunaamini klabu hizi mbili kubwa nchini zimejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mashindano hayo makubwa ya soka kwa upande wa klabu barani Afrika na wataipeperusha vizuri bendera ya Taifa letu.

Tunasema hivyo kwa sababu hatutapenda kuona klabu hizo zikiondolewa mapema badala yake tunapenda kuona klabu hizo zikifika mbali jambo ambalo pia litasaidia kuongeza changamoto katika maendeleo ya soka nchini na kuiweka Tanzania katika ramani nzuri ya soka barani Afrika.

Tunaelewa yapo baadhi ya mapungufu kwa wachezaji wa klabu za Simba na Yanga yakiwemo ya saikolojia na akili ya mchezo wa soka, lakini tunaamini makocha Kostadin Papic na Patrick Phiri watakuwa wameyafanyia kazi mapungufu hayo.

Pia, tunaamini kabla ya kuanza ligi kuu ya msimu huu klabu za Simba na Yanga zilifanya usajili sahihi kwa sababu zilikuwa zikifahamu zinaliwakilisha taifa katika mashindano makubwa Afrika.

Tunaamini kama klabu za Simba na Yanga zitashinda mechi zao za awali, macho na masikio ya mashabiki wa soka yatakuwa kwao kutokana na timu wakazokutana nazo huko mbele, hivyo tunaamini wamejiandaa kwa nguvu,hatutarajii visingizio.

 
Dortmund held as Gomez hat-trick helps lift Bayern Sunday, 23 January 2011 21:15

Berlin. Bundesliga leaders Borussia Dortmund went 13 points clear at the top after a 1-1 draw with VfB Stuttgart while Mario Gomez hit a hat-trick as Bayern Munich crushed Kaiserslautern 5-1 on Saturday.

Russian Pavel Pogrebnyak stunned Dortmund with an unstoppable shot from the edge of the box five minutes from time to cancel out Mario Goetze's goal in the first half.

The draw lifted Dortmund to 47 points from 19 games, with Hanover 96 second on 34 points after they lost 1-0 to Schalke 04 thanks to Spanish striker Raul's 10th goal of the season.

"We should have decided the game much earlier," said Dortmund coach Juergen Klopp, whose team missed several chances.
"A 2-0 or 3-0 would have been deserved. We just were not clever enough and in the end we did not defend as we should have done. But we are still top of the table."

Gomez struck three times for Bayern in the second half and Dutch winger Arjen Robben scored his first goal for the club since May last year as the champions moved into third place with 33 points, their highest position this season.

Robben returned to action last week after aggravating a muscle injury at the World Cup in South Africa last July.(AFP)
 
Viwanja hivyo vitakuwa chachu ya mpira wa kikapu
Sunday, 23 January 2011 20:51

CHAMA cha mpira wa kikapu mkoani Dar es Salaam kinatarajia kujenga viwanja 10 kwa ajili ya kuendeleza na kukuza mchezo huo jijini.

Chama hicho kinatarajia kukamilisha ujenzi wa viwanja hivyo mwezi wa tano ili kuhamasisha mchezo huo kwa vijana wanaokuwa ili kukuza vipaji vyao.

Tunakipongeza chama hicho cha mchezo wa kikapu kwa kufiria kujenga viwanja hivyo kwa sababu tunaamini hiyo ni njia mojawapo ya kutatua matatizo ya maendeleo ya mchezo huo nchini.

Tunasema hivyo kwa sababu kukosekana miundombinu bora kama viwanja vya mchezo wa kikapu jijini Dar es Salaam na nchi nzima kumechangia kukatisha tamaa vijana wengi kujifunza na kucheza mchezo huo.

Ni wazi viwanja vya mchezo wa kikapu vilivyopo jijini Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla ni vichache mno kiasi kwamba kijana anaweza akatembea kilomita nyingi asione uwanja wa mchezo wa kikapu.

Tukiacha suala la kukosekana udhamini mkubwa katika mchezo wa kikapu nchini, tunaamini kabisa viongozi wa mchezo huo ndiyo tatizo kubwa kwa sababu hawana nia ya dhati ya kusaidia wachezaji na miundombinu ya mchezo huo.

Tunaamini kama chama cha mchezo wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam kitajenga viwanja hivyo 10 wataongeza idadi ya wachezaji wa mchezo huo mkoani Dar es Salaam, lakini tunawasisitiza pia viongozi wa mchezo huo mikoani wajenge viwanja vya mchezo wa kikapu.
 
Valencia edge out Malaga in a thriller
Sunday, 23 January 2011 21:14

Madrid. Aritz Aduriz's late strike settled an amazing La Liga seven-goal-thriller in UEFA Champions League-chasing Valencia's favour on Saturday against a spirited nine-man Malaga side, with the game ending 4-3.

Salomon Rondon opened the scoring for the visitors after ten minutes and netted again ten minutes before the break after Juan Mata had equalised from a penalty - an incident which had seen Malaga defender Martin Demichelis sent off.

Half-time substitutes Roberto Soldado and Ever Banega had the desired effect with goals either side of Malaga's second red card - this time for Demichelis' central-defensive partner Helder Rosario.

Malaga refused to give up, though, and got back on level terms through Julio Baptista - only for Aduriz to have the last word.

The relegation-threatened visitors made a lively start, Baptista's deflected effort stinging the hands of Vicente Guaita within the first minute.

There was no flag, much to the hosts' dismay, when Apono escaped down the right and the midfielder produced the perfect low cross for Rondon to slot home.

However, the game looked to have swung dramatically in Valencia's favour just six minutes later. Demichelis was shown a straight red card after his trailing leg caught Mata, who blasted the spot-kick into the bottom corner. Defender Manolo was then immediately introduced in place of Enzo Maresca as Malaga reshuffled to cope with their numerical disadvantage.

Guaita was beaten for a second time in the 35th minute. The home defence failed to deal with Sergio Duda's floated free-kick from the left and it fell kindly for Rondon, who lashed high into the net from six yards.

Malaga's numbers were further depleted when Rosario was sent off, seemingly for foul and abusive language after a decision went against him.

The Mestalla erupted two minutes later when Banega fired into the bottom-left of Sergio Asenjo's net following a corner. Not to be outdone, Baptista stunned the hosts by curling a fine equaliser into the bottom-right corner with 11 minutes remaining. (AFP)

 
Katibu Angetile ratiba bora, wingi wa mashindano ndio dawa Friday, 21 January 2011 20:00
osiah.jpg
Andrew Kingamkono
WAKATI Katibu mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Angetile Osiah aliposema hatambui mechi za kirafiki zilizoandaliwa na DRFA kati ya Yanga, Simba dhidi ya Zesco ya Zambia nilijua kazi imeanza.

Kauli hiyo ya Osiah haikunishangaza kwa sababu najua vizuri msimamo wake kuwa ni moja ya kitu alichokuwa akikipinga siku zote hivyo sasa ulikuwa ni kutekeleza na kuthibisha kwa vitendo.

Kwa bahati mbaya DRFA waliweza kutumia busara zao wakafanikisha kuchezwa kwa mechi hizo huku Yanga wakiingia mitini kucheza na mabingwa hao wa Zambia.

Nadhani walichomshinda 'Ngeta' ndugu zake wa DRFA ni kuwa tayari wameileta timu hiyo pia walikuwa na kisingizo kizuri cha kutaka kuziandaa Simba na Yanga kwa ajili ya mechi zao za Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho baadaye mwezi huu.

Hivyo kitendo cha yeye kung'ang'ania msimamo wake kingefanya mashabiki wa timu hizi mbili kumshutumu zaidi kuliko ambavyo alivyokubali zicheze na Yanga kuingia mitini.

Ukiacha hilo pia, Taifa Stars ilikwenda Misri kwenye michuano ambayo haikuwepo katika ratiba, lakini TFF ilikubali kuzilazimisha klabu za Simba, Yanga, Azam na Mtibwa Sugar kuwatoa wachezaji wake wakaitumikie timu ya taifa.

Nadhani ili Katibu Osiah atimize ndoto yake ya kuondoa mechi hizi za kirafiki za kuibuka tu ili wajanja kujipatia ulaji usiokuwa na msingi ni kupitisha kanuni ambayo itakuwa wazi kwa klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu kuhusu jambo hili.

Lakini bora zaidi ni kwamba kuanzia sasa TFF wanapaswa kutumia kipindi hiki kuandaa ratiba makini na yeye kuchukua matukio yote pamoja na kujumuisha mechi hizo za kirafiki.

Kwa sababu itakuwa vigumu kwa klabu kuingia kwenye mapumziko ya katikati ya msimu kwa miezi miwili bila ya kutafuta japo mechi mbili tatu za kuwaandaa wachezaji wao kama kweli imedhamiria kufanya vizuri na kuwaweka fiti nyota wake.

Hiyo ndiyo nafasi wale wajanja wanaojua kusaka fedha wanapotumia kwa kutafuta timu za hovyo hovyo na kuja kucheza mechi kama zile za FC Leopards ya Kenya iliyocheza mechi tatu za kirafiki kwa siku tatu mfululizo.

Nakumbuka kocha Dusan Kondic aliwahi kusema,"hatuna uwezo wa kuifunga Al Ahly hata kama tutafanya kila kitu kwa sababu ya kiwango cha wachezaji wangu, hawalingani hata kidogo na nyota wa mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika."

Nao viongozi wa Yanga, Februari 13 mwaka jana, waliomba kwa TFF kusogeza mbele mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar ili wajiandae na mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Lumpopo.

Viongozi wa klabu zetu na makocha wanapaswa kuwa wawazi kuhusu kiwango cha wachezaji wao na si kutafuta sababu zisizo na msingi kwamba TFF imewanyima muda wa kutosha wa kufanya mazoezi.

Jambo la kwanza ambalo Ngeta na timu yake wanaweza kufanya ni kukutana na wenzao wa ZFA ili kujadiliana jinsi ya kuyaingiza mashindano ya Kombe la Mapinduzi kwenye ratiba na kushirikisha timu zote zinazoshiki Ligi Kuu Bara na Visiwani.

Michuano hii itakuwa ikianza Agosti na kumalizika Januari 12, na siku ya mwisho atakuwa akikabidhi kombe rais wa Zanzibar kama vile England wanavyofanya kwa Kombe la FA au Kombe la Carling ambao bingwa wake ukabidhiwa kombe na Malkia.

Michuano hii inaweza kuendeshwa kwa namna mbili, moja ni kuzishirikisha timu za bara pekee na visiwani pekee mwisho kupata timu nne zitazoingia kwenye hatua ya nusu fainali na fainali kufanyika Zanzibar.

Mbili inaweza kuchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini kwa timu za Z'bar na Bara zote, lakini fainali yake itachezwa Amaan na rais ndiye atayekuwa mgeni ikiwa ni moja ya shughuli zake za kusheherekea siku kuu ya Mapinduzi.

Kukiwa na ratiba ngumu ya aina hii itazisaidia klabu zetu kujiweka vizuri na kupata timu bora ambazo zitakuwa zikishiriki michuano ya Afrika, pia itaondoa hizi mechi za kirafiki zisizokuwa na macho wala masikio.

Jambo lingine ni kutimiza ndoto ya Rais Leodegar Tenga ya kurudisha michuano ya Kombe la FA ambalo hili nalo litakuwa likijumuisha timu zote za Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Kuu, lakini mashindano hayo yote ni lazima yaende sambasamba na ratiba ya ligi kuu.

Najua ni gharama kusafirisha timu kila wiki, lakini hiyo ndio kazi kubwa ya kitengo cha masoko kuhakikisha inatafuta wadhamini wa kutosha kutoka kwa makampuni mbalimbali hapa nchini.

Nadhani itakuwa fursa sahihi ya kutengeneza wadhamini kwani wafanya biashara watajua wataweza kutangaza bidhaa zote sehemu mbalimbali za Tanzania kuliko ilivyokuwa sasa.

Nayo TFF ikiwa na wajibu wa kutengeneza ratiba na kuheshimu kama jicho sio mara wamechakachua hivi mara vile hatutaweza kutimiza malengo.

Tukiwa na aina ya mashindano mengi ya kiasi hiki hakutakuwa na sababu ya timu kutafuta mechi za kirafiki kwa lengo la kujiandaa na michezo ya Afrika au timu ya taifa kuandaliwa kwa wiki tatu kwa ajili ya mechi ya siku moja.

 
La Liga title not yet won, says Guardiola Sunday, 23 January 2011 21:13

Madrid. Pep Guardiola expects Real Madrid to push Barcelona all the way this season, despite seeing his side move provisionally seven points clear at La Liga's summit with a 3-0 win over Racing Santander tonight.

Goals from Pedro, Lionel Messi - from the penalty spot - and Andres Iniesta gave Barça a 14th consecutive triumph in La Liga ahead of second-placed Madrid's 20th-round match at home to Real Mallorca yesterday.

And Guardiola fully expects the difference at the top to be reduced to four points again following that clash. "Madrid are a very good team and their coach (Mourinho) is the best," he said after tonight's game. "I imagine they will win tomorrow; I think they will be four points behind us again."

I imagine they will win tomorrow; I think they will be four points behind us again.Barcelona coach Pep Guardiola on their seven point lead over Real Madrid

Guardiola believes Mourinho is a great competitor, but says Madrid have always been strong - regardless of personnel. "Mourinho is a very good coach. He's a very smart guy and he's motivated," the Barça boss said. "Madrid are a strong team this year, but they have always been a strong team.

"When I was a player and now, as coach, Madrid have always been strong, no matter who is the president and no matter who is the coach - every season they play they are competitive. Last season they ended up with 96 points (Barça won the league with 99) and this season will be close again - they will be up there at the end of the season."

And Guardiola reckons the title will go down to the wire once more.
"Five, six or seven points is nothing at this stage of the league," he said.

"The league will be decided in the last few rounds of the championship."(AFP)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom