Michezo ya utotoni, ni hatari katika ukuaji wa mtoto.

Michezo ya utotoni, ni hatari katika ukuaji wa mtoto.

Michezo niliyocheza utotoni;

1. Sarakasi(mkono uliteguka mara 2 na shingo mara 1),

2. Kuogelea mto ngerengere na ziwa Victoria,

3. Komborela,

4. Kula mbakshie Baba,

5. Kibaba baba,

6. Kiooo kiooo,

7. Ukuti ukuti,

8. Tobo,

9. Safa(kutafuta mpira)

10. Mpira(dana dana),

11. Kidalipo,

12. Mizani (See saw),

13. Bembea,

14. Karata (makwenzi & Stika),

15. Shabaha ya betrii,

16. Kutengeneza na kuendesha magari,

17. Simbi(kwenda mbinguni)kupitia maharagwe,

18. Kubashiri mkono alipoficha mwenzio jiwe au mbegu kwa jedwali la X.

19. Boksi lenye pembe 8 kwa kuoanisha mbegu 3 au visoda vi3 kwenye mstari mmoja,

20. Kuruka kamba,

21. Soro,

22. Kuvutana kwa kamba,

23. Kukimbia kwa kupokezana vijiti.
 
Nimewahi lala chini ya tairi ya gari najifanya fundi nikapitiwa na usingzi ndinga ikawashwa.. ...akaja kuniona maza flani akapga kelele mnauuua mtoto ndio dereva kusikia akazima ndinga ilikuwa nusu nifanywe gogo siku ile.
 
Nakumbuka nilipokuwa mdogo, shule ya msingi nilikwenda kumtembelea ndugu yangu mmoja, alikuwa anafanya kazi kijiji kimoja huko kanda ya ziwa, miaka hiyo.

Baada ya kufika kule kijijini, nikakutana na marafiki wa rika langu; wakawa wananitembeza mtaa kwa mtaa, ili niweze kufahamu mazingira ya huko kijijini.

Siku iliyofuata, tukapanga tuende tukawinde ndege; tukatafuta mapila yale ya kuvutika, pamoja na waya. Tukachukua vipande vidogo vitatu (3) vya miti; vile vipande, tukavigongelea chini vikatengeneza umbo la pembe tatu.

Vipande viwili tukavifunga mapila, na kile cha tatu kikawa ni kiegemeo cha mpira, ili tutakapofyatua mtego uweze kupiga ndege.

Baada ya kuweka mtego vizuri, tukamwagia pumba na tukaunganisha na kamba ndefu, ili ndege wakifika tuweze kufyatua mtego.

Baada ya lisaa kama limoja hivi, walikuja ndege wengi wakaanza kula pumba. Ndipo mmoja wetu, akasema sasa ni muda muafaka wa kufyatua mtego; baada ya kufyatua mtego, ndege kama saba hivi walipigwa, wakashindwa kupaa, na tukaenda kuwakamata.

Baada ya hapo, tukaanza kuseti tena mtego; wakati tunarudishia kijiti cha pili; kile cha kwanza kilifyatuka na kikaja kunipiga kwenye korodani moja; hapo niliona giza ghafla pamoja na maumivu makali, nikasema hapa roho ndio inaanza kuchomoka nini!

Nilijigeuza geuza huku nikisikilizia maumivu kwa muda mrefu kidogo; baada ya maumivu kupungua, nikawaambia marafiki zangu tuondoke, hapa sio mahali salama.

Katika ukuaji wangu, nikajua hapa uzazi ulishaharibika. Lakini, Mungu mkubwa, baada ya miaka kwenda hakukuwa na tatizo; na hatimaye nakimbilia kuja kulea wajukuu.

Ila michezo ya utotoni, ni hatari katika ukuaji wa mtoto.
Aiseee,Pole na hongera
 
Nakumbuka enzi ya utoto tulikuwa na mchezo wa kuingiza punje ya maharage puani ilikuwa ukiweka puani unafanya kama unapenga kamasi and then inatoka, Basi bwana mchezo ukaendelea nikaweka punje puani ile kupenga wapi punje haitoki Imeng'ang'ania huku macho yamenitoka watoto wote wakakimbia nikabaki nalia ilikuwa noma sana Mama anakuja kila wakijaribu kuitoa haitoki masaa kama matatu wanaangaika, kwa bahati nzuri alikuwepo mzee wa kimakonde ikabidi atafute Ugolo akaniwekea puani ile kupiga chafya ile punje ikatoka asee siwezi kusahau ile siku ilikuwa atari sana

[emoji23][emoji23][emoji23] nacheka km mazuri ila pole mkuu sipati picha iyo hekaheka ya kutoa iyo punje
 
Mi kuna siku na wanangu tulikua tunalina asali mchana picha linaanza baada ya ugunduzi wa asali kuna jamaa angu alichovya kijiti kwenye asali sasa akataka aonje aisee kumbe kulikua na nyuki nyuki akamuuma mdomo na ulimi basi tukacheka kwel kwel sasa baadae kidogo tukawasha moto mkal hapo ndo balaa likaanza nyuki walitibuka aisee wanangu wakakimbilia ndan asa mimi kuwafuata wakafunga mlango wa chumba cha kwanza kwenda cha pil wakawa wamejaa nikaanza kukimbia hovyo hovyo dk za mwisho nikatokomea chooni ndo ikawa pona pona yani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom