Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

2002 michuano ilikuwa easy.. timu zinashinda ndani ya dakika 90...

World cup ya ukweli niliyoiona ni germany 2006... games zilikuwa za kibabe sana.. yaani kuanzia nusu fainali games zilienda extra time mpaka fainali
1998, 2006, 2018 kwangu zilikuwa finali bora sana.
 
1998 niliumizwa sana na Denmark kuifunga Nigeria 4 - 1, though Taribo West alitoa show moja matata ya chenga ya kupanda juu ya mpira.

Mechi kali kwangu kwenye hayo mashindano: Nigeria 3 - Spain 2, Croatia 3 - German 0 na Brazil 1 - Holland 1 (Patrick Kluivert anarudisha goli la kichwa dakika mbovu Sana, Brazil anapita kwa matuta).
 
Nigeria vs spain mwamba sunday oliseh anatupia kamba ya hatarii
 
1998 niliikubali sana maana enzi hizo ndio tulikuwa na ushamba wa TV ,tambua kwamba miaka ya 90 TV zilikuwa chache sana na waliokuwa wanazo walikuwa watu wenye ukwasi.
 

Sema Denmark ilikuwa na umoto fulani hivi, unawakumbuka The Laudrap brothers?
 
1998 aisee,wachezaji wengi sana walionyesha viwango, kina Davo Suka, Marcelo Salas, Nwanko Kanu, Zinedine Zadane "Zizu", Luis Figo, Dennis Bergkamp, Patrick Kluivert, n.k
Chrisian ziege duuh kama unamkumbuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…