Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Mimi mpaka leo naamini World Cup bora kuiona ni ile ya mwaka 2006. Jinsi Italy walivyopambana mpaka kutwaa taji. Italy ile iliyoundwa na wakongwe kama Luca Toni, Buffon, Pirlo, Materazzi, Del Piero, Canavarro, Zambrotta, Camoranesi na wengineo.

Italy njia aliyopitia mpaka kutwaa ubingwa ilikuwa ngumu sana. Mechi kama ya Nusu Fainali dhidi ya wenyeji Ujerumani ni ya kukumbukwa muda wote.

Pia kuna mechi za kukumbukwa kama robo fainali ya Argentina Vs Ujerumani ambao Argentina aliongoza muda mwingi wa mchezo, kocha wa Argentina alikuja kufanya mistake ya kumtoa Requelme jambo ambalo lilipelekea kuwarudisha mchezoni Ujerumani.

Halafu kuna mechi inajulikana kama Battke of Nuremberg, kati ya Uholanzi Vs Ureno ambapo jumla ya kadi za njano 16 na nyekundu 4 zilitoka.

Hayo ni kwa uchache tu, yote kwa yote World Cup ya 2006 ilikuwa bora sana kwa upande wangu.

Wewe unaikubali ipi na kwanini?
Cameroon vs England robo fainali 1990,winga wa cameroon Paul Rose mfede alikosa magoli ya wazi kabisa , England ilisonga mbele kwa goli 3-2 Garry lineker aki ifungia Engand penalty 2 katika muda wa nyongeza. Cameroon ilikua ikiongoza ongoza mbaka dk za 80 na ushee

1990 Cameroon ana mfunga Argentia katika mechi ya ufunguzi 1- 0, Argentina yenye Maradona na Canigia tena wachezaji wawili wa Cameroon wakipewa red card. Ukitaka kujua Africa ilikua na wanasoka wenye vipaji basi unge bahatika kuiona ii mechi. Cameroon wali upiga mpira kama hawachezina kigogo cha dunia Chenye Maradona na Canigia. Wakati uo soka bado haijaanza kuitwa football.
 
Uzi mzuri sana huu!

Kombe la Dunia bora kabisa kulishuhudia ni 1998 pale Ufaransa. Kulikuwa na vipaji maridhawa vya hali ya juu sana. Wachezaji walionyesha ubora wao wa hali ya juu.

Ufaransa katika ardhi ya nyumbani walikuwa na kikosi bora kabisa kilichoongozwa na mchanyato wa waarabu wa Algeria Zidane na Youri Djokaeff, pia akina Vieira, Karembeu, Lizarazu, Desailly na akina Petit.

Pia siwezi kusahau Croatia ya akina Davor Suker, fundi wa mpira Zvonomir Boban walivyopambana mpaka wakatwaa nafasi ya 3.

Kizazi cha dhahabu cha Uholanzi pia kilichagiza michuano ile. Wengi wa wadachi wale wakitokea katika akademi ya Ajax Fc. Moja ya magoli ya kukumbukwa ni Denis Bergkamp alivyoifunga Argentina katika robo fainali bila shaka baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa beki wake, akakontroo, akageuka akaweka kambani. Bao maridadi sana.

Vilevile mechi bora kwa mtazamo wangu ni ile ya nusu fainali ya Brazil Vs Uholanzi, ulipigwa mpira mwingi sana, dakika 120 1-1, Brazil anashinda 4-2 kwa penati. Zamani kulikuwa na ufundi.

Kilichotokea katika mechi ya fainali, Ufaransa Vs Brazil, ni degedege alilopata Ronaldo De Lima mpaka leo hakieleweki ni nini kilimsibu inawezekana ni fitna za Wafaransa.

Mwisho kabisa, michuano hii ilipambwa sana na ule wimbo wa mashindano (go, go, go ale ale ale) ulioimbwa na msanii nguli Ricky Martin. Hakika kwangu mimi ule ni wimbo bora wa Kombe la Dunia wa wakati wote.

Hakika kombe la dunia la 1998 ilikuwa ni michuano ya aina yake.
 
1571721573109.png

Mimi mpaka leo naamini World Cup bora kuiona ni ile ya mwaka 2006. Jinsi Italy walivyopambana mpaka kutwaa taji. Italy ile iliyoundwa na wakongwe kama Luca Toni, Buffon, Pirlo, Materazzi, Del Piero, Canavarro, Zambrotta, Camoranesi na wengineo.

Italy njia aliyopitia mpaka kutwaa ubingwa ilikuwa ngumu sana. Mechi kama ya Nusu Fainali dhidi ya wenyeji Ujerumani ni ya kukumbukwa muda wote.

Pia kuna mechi za kukumbukwa kama robo fainali ya Argentina Vs Ujerumani ambao Argentina aliongoza muda mwingi wa mchezo, kocha wa Argentina alikuja kufanya mistake ya kumtoa Requelme jambo ambalo lilipelekea kuwarudisha mchezoni Ujerumani.

Halafu kuna mechi inajulikana kama Battke of Nuremberg, kati ya Uholanzi Vs Ureno ambapo jumla ya kadi za njano 16 na nyekundu 4 zilitoka.

Hayo ni kwa uchache tu, yote kwa yote World Cup ya 2006 ilikuwa bora sana kwa upande wangu.

Wewe unaikubali ipi na kwanini?
umeangalia world cup ngapi had ufikie hitimisho hilo?
 
Nashangaa hakuna anae isifu ile ya 2002 wakati haiji kutokea Kali Kama ile
Hata mi nashangaa , mpira ulipigwa sana aisee 2002 ni funga kazi inaonekana wengi humu walikuwa watoto au hawakuwa na exposure , Mimi nilikuwa siendi shule sa mbili asubuh nipo kwenye banda....ukiona wengi wanasifia 2006 na 2010 ujue ndo fainali zao za kwanza kuchek, mpak leo namkumbuka Oliver Kahn akichukua kiatu cha dhahabu , golikeeper pekee in football history kufanya hvyo...
 
world cup 2002 (korea and japan)
nilikuwa nawapenda spain kuliko wakatalunya.

fernando hierro alikuwa ndiye shujaa wangu.
ruben baraja
gaizka mendietta
fernando morientes
gonzalez raul
ivan helguera.
carles puyol

wanafungwa kwa mikwaju ya penalty dhidi ya korea ya kusini.
Korea Kusini walikuwa na ngekewa flani hivi. Waliwatoa Italy kisha baadae wakawatoa Spain.
 
Mimi mpaka leo naamini World Cup bora kuiona ni ile ya mwaka 2006. Jinsi Italy walivyopambana mpaka kutwaa taji. Italy ile iliyoundwa na wakongwe kama Luca Toni, Buffon, Pirlo, Materazzi, Del Piero, Canavarro, Zambrotta, Camoranesi na wengineo.

Italy njia aliyopitia mpaka kutwaa ubingwa ilikuwa ngumu sana. Mechi kama ya Nusu Fainali dhidi ya wenyeji Ujerumani ni ya kukumbukwa muda wote.

Pia kuna mechi za kukumbukwa kama robo fainali ya Argentina Vs Ujerumani ambao Argentina aliongoza muda mwingi wa mchezo, kocha wa Argentina alikuja kufanya mistake ya kumtoa Requelme jambo ambalo lilipelekea kuwarudisha mchezoni Ujerumani.

Halafu kuna mechi inajulikana kama Battke of Nuremberg, kati ya Uholanzi Vs Ureno ambapo jumla ya kadi za njano 16 na nyekundu 4 zilitoka.

Hayo ni kwa uchache tu, yote kwa yote World Cup ya 2006 ilikuwa bora sana kwa upande wangu.

Wewe unaikubali ipi na kwanini?
Naikubali ya mwaka 2002. Brazil akichukua kombe akiwa na Triple R,,,Ronaldo,,Ronadihno,,,Rivaldo ,,germanya wakiwa na kipa wao Oliver kahn wakisema ana mikona elfu moja..
 
Back
Top Bottom