Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Michuano ipi ya World Cup ilikuwa bora sana kuitazama?

Cameroon vs England robo fainali 1990,winga wa cameroon Paul Rose mfede alikosa magoli ya wazi kabisa , England ilisonga mbele kwa goli 3-2 Garry lineker aki ifungia Engand penalty 2 katika muda wa nyongeza. Cameroon ilikua ikiongoza ongoza mbaka dk za 80 na ushee

1990 Cameroon ana mfunga Argentia katika mechi ya ufunguzi 1- 0, Argentina yenye Maradona na Canigia tena wachezaji wawili wa Cameroon wakipewa red card. Ukitaka kujua Africa ilikua na wanasoka wenye vipaji basi unge bahatika kuiona ii mechi. Cameroon wali upiga mpira kama hawachezina kigogo cha dunia Chenye Maradona na Canigia. Wakati uo soka bado haijaanza kuitwa football.
Goli la kichwa la francois omam biyik lilitosha kuwanyamazisha Argentina iliyokuwa na nguli maradona na cannigia achilia mbali sergio goycochea na nery pumpido walinda mlango mahiri hawa kwa hakika miamba imepita jorge burruchaga na Robert sensini chini ya kocha Carlos bilaldo walishindwa kupata matokeo dhidi ya simba wasio fugika
 
Mimi mpaka leo naamini World Cup bora kuiona ni ile ya mwaka 2006. Jinsi Italy walivyopambana mpaka kutwaa taji. Italy ile iliyoundwa na wakongwe kama Luca Toni, Buffon, Pirlo, Materazzi, Del Piero, Canavarro, Zambrotta, Camoranesi na wengineo.

Hayo ni kwa uchache tu, yote kwa yote World Cup ya 2006 ilikuwa bora sana kwa upande wangu.

Wewe unaikubali ipi na kwanini?
Japo sikuziona lakini baada ya kufuatilia nimebaini world cup bora ni ya 1970 iliyofanyika Mexico, ambapo Brazil ilitwaa ubingwa. Hicho ndicho kizazi bora zaidi cha Brazil au duniani kwa upande wa kandanda kuwahi kutokea. Kwa upande wa forward ilikuwa na magwiji wa tano wa kandanda ambao wote kiasili ni no 10 lakini wakapangwa wote na kutengeneza forward isiyo kabika, bora Zaidi kuwahi kutokea duniani. Jairzinho, Pelé, Gérson, Tostão na Rivelino. Pele alikuwa mchezaji bora wa mashindano hayo ambapo alihusika katika mabao 14 kati ya 19 ambayo Brazil walifunga. Alifunga bao 4 na assists 10. Kikosi hicho cha Brazil kilishinda mechi zake zote 6 katika fainali hiyo, na wakati wa ku qualify vilevile kilishinda mechi zake zote 6

World ya cup ya pili kwa ubora kwa upande wangu ni ile ya mwaka 1958, ni world iliyomtambulisha Pele, akiwa na miaka 17 tu. (Siyo umri wa passport bali ni umri halisia), ni world cup ambayo Brazil ilichukua kombe. Pele alicheza sambamba na gwiji wa soka wakati huo Garrincha. Pele alifunga mabao 6 world cup hiyo.
 
Ile mechi ilikuwa moto sana na huenda iliwahamasisha sana Italy mpaka kufikia hatua ya kubeba kombe pamoja na uzee wao
Haikuwa extra tym, bali dakika za mwisho mwisho. Nadhani ilikuwa 86 kabla ya del piero kuwamalizia.

Wachezaji wote wa german walilala chini. Maana hawakujua ni jinsi gani wangeweza kuchomoa goli mbili ndani ya dk 2
 
Mimi mpaka leo naamini World Cup bora kuiona ni ile ya mwaka 2006. Jinsi Italy walivyopambana mpaka kutwaa taji. Italy ile iliyoundwa na wakongwe kama Luca Toni, Buffon, Pirlo, Materazzi, Del Piero, Canavarro, Zambrotta, Camoranesi na wengineo.

Italy njia aliyopitia mpaka kutwaa ubingwa ilikuwa ngumu sana. Mechi kama ya Nusu Fainali dhidi ya wenyeji Ujerumani ni ya kukumbukwa muda wote.

Pia kuna mechi za kukumbukwa kama robo fainali ya Argentina Vs Ujerumani ambao Argentina aliongoza muda mwingi wa mchezo, kocha wa Argentina alikuja kufanya mistake ya kumtoa Requelme jambo ambalo lilipelekea kuwarudisha mchezoni Ujerumani.

Halafu kuna mechi inajulikana kama Battke of Nuremberg, kati ya Uholanzi Vs Ureno ambapo jumla ya kadi za njano 16 na nyekundu 4 zilitoka.

Hayo ni kwa uchache tu, yote kwa yote World Cup ya 2006 ilikuwa bora sana kwa upande wangu.

Wewe unaikubali ipi na kwanini?
2018 ndo bora kwangu,kwa sababu France ambao hakuna aliewadhania watabemba ndoo,mwishowe wakaibeba.
 
Haikuwa extra tym, bali dakika za mwisho mwisho. Nadhani ilikuwa 86 kabla ya del piero kuwamalizia.

Wachezaji wote wa german walilala chini. Maana hawakujua ni jinsi gani wangeweza kuchomoa goli mbili ndani ya dk 2
Germany: Lehmann, Friedrich, Metzelder, Mertesacker, Lahm, Borowski (Schweinsteiger 72), Ballack, Kehl, Schneider (Odonkor 83), Klose (Neuville 111), Podolski.
Subs Not Used: Jansen, Huth, Nowotny, Hanke, Kahn, Asamoah, Hitzlsperger, Hildebrand.
Booked: Borowski, Metzelder.
Italy: Buffon, Zambrotta, Cannavaro, Materazzi, Grosso, Camoranesi (Iaquinta 90), Perrotta (Del Piero 104), Gattuso, Pirlo, Totti, Toni (Gilardino 74).
Subs Not Used: Zaccardo, Barzagli, Peruzzi, Nesta, Amelia, Barone, Inzaghi, Oddo.
Booked: Camoranesi.
Goals: Grosso 119, Del Piero 120.
Att: 65,000
Ref: Benito Archundia Tellez (Mexico).
Fifa man of the match: Andrea Pirlo
 
Back
Top Bottom