Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mdahalo wa kwanza baina ya Donald Trump na Kamala Harris katika kinyang'anyiro cha urais wa USA umefanyika usiku wa kuamkia leo huko marekani, baadhi yetu tulifanikiwa kuufatilia kwa kina katika kujifunza nk.
Mbali na sera za wagombea kuna vitu vingi mnoo huangaliwa katika midahalo hiyo ili kuwavutia wamerekani wengi ili kuja kuwapigia kura hao wagombea.
Haya machache nitaweka hapa kuhusu mambo ya kiufundi katika mdahalo. Tukianza na upande wa Trump, mtindo wake wa kulumbana katika midahalo ni ule ule, ni mwendo wa kuporomosha mashambulizi mazito dhidi ya mpinzani wake na kusema lolote lile ilimradi litambeba katika mbio zake za urais. Na ndicho hicho hicho alikifanya tena katika mdahalo huo. Ni mtindo wa wanasiasa katika kusaka kura kishabiki. Bahati mbaya sana waendesha mdahalo walikuwa makini na wakali kwake, mara kadhaa walimuonya au kumrekebisha.
Upande wa Kamala Harris alikuja na mtindo wa kujibu mashambulizi papo hapo, kupeleka mashambulizi ya kimkakati kwa ujanja na kusukuma sera zake mbele kwa haraka. Huu ni mtindo wa wanasheria mahiri hupenda kuutumia wakiwa mahakamani.
Kwa kifupi sana mdahalo ule umefanikiwa zaidi kumtambulisha zaidi Kamala Harris kama mgombea urais wa namna gani mbele ya wamerekani. Kwa haraka haraka unaweza ukahisi mdahalo ule uliandaliwa na Democrat ili kumpa jukwaa Kamala Harris.
Kwa style hii ya leo, hata midahalo ikarudiwa mara kumi tena huenda Kamala Harris akaonekana anabebwa au midahalo inambeba.