Midahalo hata irudiwe mara kumi, kiufundi Trump hataweza kumshinda Harris katika mdahalo!

Chonde chonde mwaka 2025 mdahalo kama huo pia ufanyike hapa Tanzania baina ya wagombea kiti cha Urais.
 
Na baada ya hapo nini kitatokea,, dunia itakubali mwanamke awe head off the state? Au watamuwahisha mapema
Kumbuka issue ya Obama ilivyokuwa.
Wakati ule wa kinyang'anyiro swali kuu lilikuwa, hivi itatokea mtu mweusi anaweza kuongoza USA? Ikitokea, itakuwaje?

Hivyo la kuhoji kuhusu mwanamke ni fear of unknown tu hususani kwa sisi huku kwetu Afrika. Kuhusu Rais mwanamke USA, kiujumla wamarekani hawana shida kabisa na hilo, and after all feminist movement ni kubwa mnoo huko Marekani kiasi cha kupelekea kuwepo hatari ya Female dominant culture.
 
Clinton alimshinda Trump kwa kura za wananchi. Ila kundi la watu wasiozidi 300 wakampitisha Trump.

Rais wa Marekani eshajulikna hata kabla ya kura kupigwa
 
Uchambuzi wako umekaa kinafki sn, Mdahalo nimeuckiliza mwanzo mwisho umebalance…

Bt km credit bac nampa trump cz kulikuwa na unfair treatment kutoka kwa waendesha mdahalo… na design km harris alipewa nondo kabla ya kuingia kwny chumba cha mtihani

Unapogombea na chama kilichopo madarakani tegemea figisu figisu
 
Mdahalo wa kwanza baina ya Donald Trump na Kamala Harris katika kinyang'anyiro cha urais wa USA umefanyika usiku wa kuamkia leo huko marekani, baadhi yetu tulifanikiwa kuufatilia kwa kina katika kujifunza nk.

Mbali na sera za wagombea kuna vitu vingi mnoo huangaliwa katika midahalo hiyo ili kuwavutia wamerekani wengi ili kuja kuwapigia kura hao wagombea.

Haya machache nitaweka hapa kuhusu mambo ya kiufundi katika mdahalo. Tukianza na upande wa Trump, mtindo wake wa kulumbana katika midahalo ni ule ule, ni mwendo wa kuporomosha mashambulizi mazito dhidi ya mpinzani wake na kusema lolote lile ilimradi litambeba katika mbio zake za urais. Na ndicho hicho hicho alikifanya tena katika mdahalo huo. Ni mtindo wa wanasiasa katika kusaka kura kishabiki. Bahati mbaya sana waendesha mdahalo walikuwa makini na wakali kwake, mara kadhaa walimuonya au kumrekebisha.

Upande wa Kamala Harris alikuja na mtindo wa kujibu mashambulizi papo hapo, kupeleka mashambulizi ya kimkakati kwa ujanja na kusukuma sera zake mbele kwa haraka. Huu ni mtindo wa wanasheria mahiri hupenda kuutumia wakiwa mahakamani.

Kwa kifupi sana mdahalo ule umefanikiwa zaidi kumtambulisha zaidi Kamala Harris kama mgombea urais wa namna gani mbele ya wamerekani. Kwa haraka haraka unaweza ukahisi mdahalo ule uliandaliwa na Democrat ili kumpa jukwaa Kamala Harris.

Kwa style hii ya leo, hata midahalo ikarudiwa mara kumi tena huenda Kamala Harris akaonekana anabebwa au midahalo inambeba.
Swali la kwanza tu Kamala Harris ameulizwa na ameshindwa kujibu, are Americans better off now Economically than they were four years ago? Baada ya kukwepa hilo swali sikuona hata haja yakuendelea kufuatilia huu mdahalo.
 
Hisia zako kuhusu upendeleo kwa uhakika zimetokana na namna Kamala Harris alivyomudu mjadala mzima na kwa jinsi Trump alivyohenyeshwa pasipo kutegemea. Na hii ni kwa sababu moja kuu, mwanamama ni mahiri mnoo kwenye hiyo mijadala ya one to one, fuatilia hayo hata uchaguzi uliopita alivyoweza kumbeba Biden kupitia hizo Debate.

Ndio maana nakwambia, hiyo mijadala ikirudiwa hata mara kumi, huenda Trump hataweza kutoboa mbele ya Harris kwenye debate.
 
Swali la kwanza tu Kamala Harris ameulizwa na ameshindwa kujibu, are Americans better off now Economically than they were four years ago? Baada ya kukwepa hilo swali sikuona hata haja yakuendelea kufuatilia huu mdahalo.
Mimi sikuona shida sana katika hilo swali namna alivyojibu Harris, issue ingekuwa kubwa kama Trump angeweza kumvuta Harris kwenye kona ya hilo swali na mwanamama kujichanganya. Na karibu mara zote Harris alipobanwa kwenye hilo swali alikimbilia kutoa comparison figures za uchumi mbovu zaidi aliourithi kutoka kwa Trump (Republican) dhidi ya uchumi bora wa sasa wa utawala wa Biden (Democrat), na hapo hapo akamweka kwenye kona Trump kwa kumwambia alirithi uchumi bora wa Obama (Democrat) na kwenda kuua!
 
Mshindi ni Trump na ni Mtu sahihi.

Acha ainyoooshe Marekani. Kila mtu arudi kwao ku practice anachoamini sio kuleta tamaduni zisizoihusu nchi ya wenyewe.
Kwa ulichokiandika, nadhani hii mada ni nzito sana kwako. Kwa nia njema sana nakushauru, jaribu kwanza kuufuatilia uchaguzi wa USA, ukiweza kapitie Youtube hii Debate ya kuamkia leo, kisha utakuja kuandika kitu kikubwa sana hapa JF na sote tutakuelewa vizuri sana.

Kwa kukusaidia tu, Trump amepanga kuinyoosha vizuri Africa na kuibeba USA tu. Hivyo ushindi wowote wa Trump unaweza kuja kuwa ni kilio kikubwa sana kwa Afrika.
 
Mdahalo wa kwanza baina ya Donald Trump na Kamala Harris katika kinyang'anyiro cha urais wa USA umefanyika usiku wa kuamkia leo huko marekani, baadhi yetu tulifanikiwa kuufatilia kwa kina katika kujifunza nk.

Mbali na sera za wagombea kuna vitu vingi mnoo huangaliwa katika midahalo hiyo ili kuwavutia wamerekani wengi ili kuja kuwapigia kura hao wagombea.

Haya machache nitaweka hapa kuhusu mambo ya kiufundi katika mdahalo. Tukianza na upande wa Trump, mtindo wake wa kulumbana katika midahalo ni ule ule, ni mwendo wa kuporomosha mashambulizi mazito dhidi ya mpinzani wake na kusema lolote lile ilimradi litambeba katika mbio zake za urais. Na ndicho hicho hicho alikifanya tena katika mdahalo huo. Ni mtindo wa wanasiasa katika kusaka kura kishabiki. Bahati mbaya sana waendesha mdahalo walikuwa makini na wakali kwake, mara kadhaa walimuonya au kumrekebisha.

Upande wa Kamala Harris alikuja na mtindo wa kujibu mashambulizi papo hapo, kupeleka mashambulizi ya kimkakati kwa ujanja na kusukuma sera zake mbele kwa haraka. Huu ni mtindo wa wanasheria mahiri hupenda kuutumia wakiwa mahakamani.

Kwa kifupi sana mdahalo ule umefanikiwa zaidi kumtambulisha zaidi Kamala Harris kama mgombea urais wa namna gani mbele ya wamerekani. Kwa haraka haraka unaweza ukahisi mdahalo ule uliandaliwa na Democrat ili kumpa jukwaa Kamala Harris.

Kwa style hii ya leo, hata midahalo ikarudiwa mara kumi tena huenda Kamala Harris akaonekana anabebwa au midahalo inambeba.
Haina shida! Kika mmoja ameshinda kwenye eneo alilo na uwezo nalo:
1. Mdahalo - Harris
2. Urais - Trump
 
Clinton alimshinda Trump kwa kura za wananchi. Ila kundi la watu wasiozidi 300 wakampitisha Trump.

Rais wa Marekani eshajulikna hata kabla ya kura kupigwa
Kwa namna ulivyoandika inaonekana uchaguzi wa USA namna unavyofanyika ni darasa gumu sana kwako kuweza kuuelewa.
 
Kwa ulichokiandika, nadhani hii mada ni nzito sana kwako. Kwa nia njema sana nakushauru, jaribu kwanza kuufuatilia uchaguzi wa USA, ukiweza kapitie Youtube hii Debate ya kuamkia leo, kisha utakuja kuandika kitu kikubwa sana hapa JF na sote tutakuelewa vizuri sana.

Kwa kukusaidia tu, Trump amepanga kuinyoosha vizuri Africa na kuibeba USA tu. Hivyo ushindi wowote wa Trump unaweza kuja kuwa ni kilio kikubwa sana kwa Afrika.
Acha tu ainyooshe! Sasa afanyeje kama haitaki kujinyoosha yenyewe?
 
Mdahalo wa kwanza baina ya Donald Trump na Kamala Harris katika kinyang'anyiro cha urais wa USA umefanyika usiku wa kuamkia leo huko marekani, baadhi yetu tulifanikiwa kuufatilia kwa kina katika kujifunza nk.

Mbali na sera za wagombea kuna vitu vingi mnoo huangaliwa katika midahalo hiyo ili kuwavutia wamerekani wengi ili kuja kuwapigia kura hao wagombea.

Haya machache nitaweka hapa kuhusu mambo ya kiufundi katika mdahalo. Tukianza na upande wa Trump, mtindo wake wa kulumbana katika midahalo ni ule ule, ni mwendo wa kuporomosha mashambulizi mazito dhidi ya mpinzani wake na kusema lolote lile ilimradi litambeba katika mbio zake za urais. Na ndicho hicho hicho alikifanya tena katika mdahalo huo. Ni mtindo wa wanasiasa katika kusaka kura kishabiki. Bahati mbaya sana waendesha mdahalo walikuwa makini na wakali kwake, mara kadhaa walimuonya au kumrekebisha.

Upande wa Kamala Harris alikuja na mtindo wa kujibu mashambulizi papo hapo, kupeleka mashambulizi ya kimkakati kwa ujanja na kusukuma sera zake mbele kwa haraka. Huu ni mtindo wa wanasheria mahiri hupenda kuutumia wakiwa mahakamani.

Kwa kifupi sana mdahalo ule umefanikiwa zaidi kumtambulisha zaidi Kamala Harris kama mgombea urais wa namna gani mbele ya wamerekani. Kwa haraka haraka unaweza ukahisi mdahalo ule uliandaliwa na Democrat ili kumpa jukwaa Kamala Harris.

Kwa style hii ya leo, hata midahalo ikarudiwa mara kumi tena huenda Kamala Harris akaonekana anabebwa au midahalo inambeba.
Trump anaweza akashinda, ingawaje atakumbana na ushindani mkali sana.
 
Back
Top Bottom