Midahalo hata irudiwe mara kumi, kiufundi Trump hataweza kumshinda Harris katika mdahalo!

Midahalo hata irudiwe mara kumi, kiufundi Trump hataweza kumshinda Harris katika mdahalo!

Trump ndio mwamba.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mdahalo Trump kwenye mdahalo amedanganya mara 30+ na almost wamesema ni kila sentensi aliyoitamka alikuwa anachomeka uongo
 
Wenzako tuna taarifa za "ndani" kuwa Rais ajaye wa Marekani ni Donald Trump.

Kama unabisha subiri uchaguzi ukamilike. Usisahau kuja kunikumbusha!
Hakuna tatizo.
Mimi nipo hapa JF, tutakuja kukumbushana.
Kwa jicho la kiuchambuzi, mwelekeo wa siasa za USA kwa sasa ni kama vile unambeba Kamala kwa speed kubwa. Kama hali itaendelea hivi hivi kwa wiki zingine tatu zijazo, basi hii game Trump atakuwa ameipoteza kirahisi kama. Mwanamama inaonekana kama anajimudu na amejipanga vizuri.
 
Wapo wachambuzi kadhaa wanasema kama inawezekana basi Trump na mgombea mwenza wake wasishiriki midahalo mingine ijayo maana huenda ikawadidimiza.
 
Hakuna tatizo.
Mimi nipo hapa JF, tutakuja kukumbushana.
Kwa jicho la kiuchambuzi, mwelekeo wa siasa za USA kwa sasa ni kama vile unambeba Kamala kwa speed kubwa. Kama hali itaendelea hivi hivi kwa wiki zingine tatu zijazo, basi hii game Trump atakuwa ameipoteza kirahisi kama. Mwanamama inaonekana kama anajimudu na amejipanga vizuri.
Mpira ni dakika tisini mkuu! Muda tutasema.

Wengine hatuna hata haja ya kumfuatilia nidahalo. Tayari tunajua kuwa Rais wa Marekani ni Donald Trump!
 
Mpira ni dakika tisini mkuu! Muda tutasema.

Wengine hatuna hata haja ya kumfuatilia nidahalo. Tayari tunajua kuwa Rais wa Marekani ni Donald Trump!
Fuatilia midahalo ya waliokutangulia ujifunze kitu na kufurahia minyukano mizuri ya viunga vya siasa. Ni raha sana.
 
Kushinda mdahalo Haina shida mkuu! Kama umesoma nilochoandika, utakumbuka kuwa hata mimi nimelubali kuwa Harris kashinda mdahalo I gawa sijauangalia ila Urais ni w Trump! Mbona hilo wengi tushalifahamu? Rais ajaye wa USA ni Trump!
Haya ni maneno ya kijinga
 
Mdahalo wa kwanza baina ya Donald Trump na Kamala Harris katika kinyang'anyiro cha urais wa USA umefanyika usiku wa kuamkia leo huko marekani, baadhi yetu tulifanikiwa kuufatilia kwa kina katika kujifunza nk.

Mbali na sera za wagombea kuna vitu vingi mnoo huangaliwa katika midahalo hiyo ili kuwavutia wamerekani wengi ili kuja kuwapigia kura hao wagombea.

Haya machache nitaweka hapa kuhusu mambo ya kiufundi katika mdahalo. Tukianza na upande wa Trump, mtindo wake wa kulumbana katika midahalo ni ule ule, ni mwendo wa kuporomosha mashambulizi mazito dhidi ya mpinzani wake na kusema lolote lile ilimradi litambeba katika mbio zake za urais. Na ndicho hicho hicho alikifanya tena katika mdahalo huo. Ni mtindo wa wanasiasa katika kusaka kura kishabiki. Bahati mbaya sana waendesha mdahalo walikuwa makini na wakali kwake, mara kadhaa walimuonya au kumrekebisha.

Upande wa Kamala Harris alikuja na mtindo wa kujibu mashambulizi papo hapo, kupeleka mashambulizi ya kimkakati kwa ujanja na kusukuma sera zake mbele kwa haraka. Huu ni mtindo wa wanasheria mahiri hupenda kuutumia wakiwa mahakamani.

Kwa kifupi sana mdahalo ule umefanikiwa zaidi kumtambulisha zaidi Kamala Harris kama mgombea urais wa namna gani mbele ya wamerekani. Kwa haraka haraka unaweza ukahisi mdahalo ule uliandaliwa na Democrat ili kumpa jukwaa Kamala Harris.

Kwa style hii ya leo, hata midahalo ikarudiwa mara kumi tena huenda Kamala Harris akaonekana anabebwa au midahalo inambeba.
naskai bibiye kamala kamkimbiza kikongwe jana
 
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mdahalo Trump kwenye mdahalo amedanganya mara 30+ na almost wamesema ni kila sentensi aliyoitamka alikuwa anachomeka uongo
hakuna mwanasiasa mkweli duniani labda mwanaharakati.
 
Unarudia kuandika propaganda zile zile za Trump.

Unapozungumzia wahamiaji huko USA unazungumzia mamilioni ya watu, sio vibaka wawili watatu kwenye kijiji fulani huko USA. Sasa mgombea unapopewa jukwaa la kusikilizwa na watu zaidi ya milioni 300 halafu analipuka na hoja kuwa wahamiaji huko USA wanalaumiwa kwa kupukutisha paka na mbwa wa wenyeji, hapo unapaswa hata kupimwa akili.
Unajua Kwann taifa let’s haliendelei?
Kwa sababu y unafki…

Sasa trump kakataa kuwa mnafki, wahamiaji wanaoingia USA kila leo wanaimpact kubwa sn kwa wenyeji, na ndo maana mataifa mengi yalioendelea yameanza kuchukua hatua
 
Hakuna tatizo.
Mimi nipo hapa JF, tutakuja kukumbushana.
Kwa jicho la kiuchambuzi, mwelekeo wa siasa za USA kwa sasa ni kama vile unambeba Kamala kwa speed kubwa. Kama hali itaendelea hivi hivi kwa wiki zingine tatu zijazo, basi hii game Trump atakuwa ameipoteza kirahisi kama. Mwanamama inaonekana kama anajimudu na amejipanga vizuri.
Kama trump aliweza kumuangusha hirrary mbobezi wa siasa za marekani, alie olewa na kuishi ikulu kipnd mumewe akiwa rais…

Huyo karani wa mahakama n m2 mdogo sn
 
Sawa....

Tunataka sasa mdahalo wa marais wa kwenye uchaguzi wa Tanzania pia

Ova
Tujikite kwenye uchaguzi wa Marekani kwani inakubalika wazi kwamba Tanzania hakuna uchaguzi. Uchaguzi gani chama kinachoshiriki kwenye uchaguzi eti ndicho kinachoandaa, kusimamia, kuratibu na kisha kutangaza matokeo ya uchaguzi. Bure kabisa.
 
Clinton alimshinda Trump kwa kura za wananchi. Ila kundi la watu wasiozidi 300 wakampitisha Trump.

Rais wa Marekani eshajulikna hata kabla ya kura kupigwa
Ndio walewale wa vijiweni hata hujui uchaguzi wa Marekani ulivyo ni kazi ngumu sana kuwaelewesha mazao ya St Kayumba wakichanganyikana na wa madrasa.
 
Tujikite kwenye uchaguzi wa Marekani kwani inakubalika wazi kwamba Tanzania hakuna uchaguzi. Uchaguzi gani chama kinachoshiriki kwenye uchaguzi eti ndicho kinachoandaa, kusimamia, kuratibu na kisha kutangaza matokeo ya uchaguzi. Bure kabisa.
😄 hatuna uchaguzi
Tuna zekomedi shw tu

Ova
 
Back
Top Bottom