Clinton alimshinda Trump kwa kura za wananchi. Ila kundi la watu wasiozidi 300 wakampitisha Trump.
Rais wa Marekani eshajulikna hata kabla ya kura kupigwa
Hapana. Hauko sahihi.
Watu wengi sana hamuelewi jinsi ambavyo Rais wa Marekani anavyochaguliwa.
Hao “watu wasiozidi 300” [btw, Trump alipata electoral votes 306] hawakujiamulia tu ‘wampe’ Trump urais.
Mgombea ni lazima ashinde statewide popular vote ili aweze kuzipata electoral college votes za jimbo.
Wingi wa kura za Clinton zilitokana na yeye kushinda kwa asilimia kubwa kwenye majimbo yenye watu wengi, mfano California na New York, lakini ikija kwenye idadi ya majimbo na electoral votes, hakushinda vya kutosha.
Kusema ukweli, ni mfumo rahisi sana kuuelewa. Siyo rocket science kabisa.
Ila pengine labda Watanzania wengi wana vichwa vigumu tu vya kuelewa hata mambo yaliyo marahisi.
Halafu Trump wala hakuwa wa kwanza kushindwa national popular vote lakini akashinda electoral college votes.
Hiyo ilishatokea kuanzia miaka ya 1800 huko. Ni kiasi cha kujifunza tu.
Halafu kuna scenario ingine ambayo wengi hamuijui.
Jumla ya electoral college votes ni 538.
538 ukiigawanya kwa mbili unapata 269.
Ili mgombea ashinde, anahitaji kupata 270.
Sasa ikitokea wagombea wote wawili wanapata 269, hapo inakuwaje?
Jibu nalijua. Ila naamini wabongo wengi hawajui hata kuwa scenario kama hiyo inaweza kutokea.