Midahalo ya Katiba Inayopendekezwa inaendelea saa hizi katika kumbi za makanisa kadhaa

President Elect

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
693
Reaction score
212
Midahalo ya Katiba Inayopendekezwa inaendelea saa hizi katika kumbi za makanisa kadhaa! Taarifa zilizonifikia kutoka sharika mbalimbali, vijana wameitisha makongamano kujadili katiba pendekezwa na wamealika wanasheria wasomi kutoa somo na kuwaelewesha yaliyomo!

Kwa uchache wa nakala za katiba pendekezwa zilizombazwa na serikali, hii ni fursa nzuri kwa washarika kuifahamu katiba inayopendekezwa, kabla ya upigaji wa kura ya maoni.

Wito kwa ndugu zetu waislam nao wapate midahalo ya aina hii kama ilivyo kwa wenzao wakirsto!
 
Mungu amenipa nafasi leo nimeenda Kanisani, wakati matangazo ulipofika Waraka wa Maskofu wetu ukasomwa. Halafu Mchungaji wetu akatoa elimu ya bure kuhusu katiba hii pendekezwa. Hatimaye akasema tuipe kura za hapana. Akasisitiza maoni ya msingi ambayo wananchi waliyatoa, wajanja wameyatoa ili kulinda maslahi yao na uroho wao wa madaraka. Kila mwenye kuwaza vizuri na kuitakia mema nchi yetu nzuri yenye kila kitu kilichopo katika uso wa nchi, mwenye kupinga uchumi wa nchi kuhamishwa kijanja kijanja, bila shaka ataungana na viongozi wa dini kusema hapana kwa katiba pendekezwa
 
Midahalo pekee sio suluhisho ndg. President Elect, Waislam ni watu wanaojitambua na wanajua wajibu wao. Kwanini wewe umapenda kuleta tofauti tofauti ndani ya nchi yetu. Hizo ni tabia zenye mwelekeo wa kuwachochea watu wafuate unachotaka wewe.

Hawa ni watu makini wakiambiwa au kukisikiliza jambo ni vema ila changanya na akili zako wasije wakakuburuzwa hawa wasio na nia njema maana kuna wataalamu wa kupotosha Umma. Mtanzania, Uwe na nia ya dhati na utumie muda wako vizuri Kuisoma Katiba Inayopendekezwa ili uwe na uelewa mzuri zaidi kwa manufaa ya taifa lako na vizazi vijavyo.
 
na fursa ya kusoma katiba pendekezwa haipo kwa wengi, nakala zilizopo hazitoshi, na muda uliobaki ni mfupi, hivyo midahalo ni njia sahihi kuelimishana ili kufanya maamuzi sahihi, umenisoma?
 
Mungu amenipa nafasi leo nimeenda Kanisani, wakati matangazo ulipofika Waraka wa Maskofu wetu ukasomwa. Halafu Mchungaji wetu akatoa elimu ya bure kuhusu katiba hii pendekezwa. Hatimaye akasema tuipe kura za hapana. Akasisitiza maoni ya msingi ambayo wananchi waliyatoa, wajanja wameyatoa ili kulinda maslahi yao na uroho wao wa madaraka. Kila mwenye kuwaza vizuri na kuitakia mema nchi yetu nzuri yenye kila kitu kilichopo katika uso wa nchi, mwenye kupinga uchumi wa nchi kuhamishwa kijanja kijanja, bila shaka ataungana na viongozi wa dini kusema hapana kwa katiba pendekezwa

Hongera kwa kwenda kwenye nyumba ya ibada, Mchungaji ni binadamu anaweza kuipelekea nchi yetu na wananchi kupata elimu ya bure ambayo inawaelekeza kwenye mawazo yake. Wanzania tuwe watu wa kuwahoji hawa wanaoleta porojo zao. Watanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu. Tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye mfumo wa demokrasia na misingi ya utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi. Ungana na Watanzania kutimiza azma ya kupa Katiba Mpya.
 
Padri wangu pia alizungumzia kwamba ni wajibu wetu kufanya mema kwa nchi yetu, hivyo kila uamuzi ninaoufanya niufanye kwa busara kwani siasa ni maisha ya binadamu na mwaka huu upo kisiasa zaidi. Lakini mwishoni akasema kila mmoja aisikilize dhamira yake.
 
Hongera kwa kwenda kwenye nyumba ya ibada, Mchungaji ni binadamu anaweza kuipelekea nchi yetu na wananchi kupata elimu ya bure ambayo inawaelekeza kwenye mawazo yake. Wanzania tuwe watu wa kuwahoji hawa wanaoleta porojo zao. Watanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu. Tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye mfumo wa demokrasia na misingi ya utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi. Ungana na Watanzania kutimiza azma ya kupa Katiba Mpya.
umaanisha katiba inayoruhusu uchumi wa nchi kuhujumiwa, ndiyo ipitishwe na wananchi,, sio!!!
unamaanisha wabunge wale wenye sifa ya kujua kusoma na kuandika,, sio!!!!
tena wale ambao wakichaguliwa hawawezi wajibishwa na waliowachagua,, sio!!!
tena wale ambao hawana ukomo wa kukaa madarakani, eti mtu ni mbunge miaka 45,, sio!!!
tena wale ambao wakichaguuliwa wanahamia DSM,, sio!!!
tena wale ambao wanajali matumbo yao, kazi zao anafanya diwani, anayelipwa kiduchu,,,sioo!!!
unamaanisha ile ambayo itaendelea kuruhusu Rais wa nchi kuigeuza mikutano ya serikali kuwa ya chama tawala,, sio!!
KAWADANGANYE WENGINE SIO MIMI,
najitambua
 
Hadanganywi mtu hapa. Nchi isiyo na Katiba ni nchi ya namna gani hiyo? Hivi umesahau hata historia fupi ya uamuzi huu ulianzaje?

Sichoki kuwashirikisha Watanzania kupitia wewe MWAKABOKO namna Mchakato wa kutunga Katiba ya Tanzania ulivyopitia hatua mbalimbali ambapo wananchi sasa wamegawiwa nakala za Katiba Inayopendekezwa, ambayo ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba Mwaka jana Oktoba 4, Bunge hilo likitanguliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa Rasimu ya Kwanza tarehe 3 Juni, 2013 na Rasimu ya Pili ilitolewa tarehe 30 Desemba, 2014 na kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum tarehe 21 Februari, 2014. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, Hatua inayofuata ni yawananchi kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa. Hivyo basi, kwa mujibu wa sheria, wananchi ndiyo wenye uamuzi na kauli ya mwisho juu ya upatikanaji wa Katiba Mpya. Wananchi ni muhimu waisome na kuielewe Katiba Inayopendekezwa ili kufanya uamuzi sahihi wakati wa upigaji kura ya maoni kulingana na ratiba ilivyopangwa.

Hayo yote unayoyasema yanatoka wapi Mwakaboko? Ipende nchi yako au wewe una nchi nyingine?
 
Katiba itatusambaratisha WATZ panahitajika viongozi makini na wenye kujali nchi na watu wake.
 
Na waisilamu nao wakianza midahalo misikitini tutafika?
 
dada Mwasi Mwakenda wewe ni Mtanzania mzalendo na unaipenda sana nchi yetu, swali je unapowashauri wananchi wasome Katiba Pendekezwa ambayo hawajui waipate wapi, nikueleweje?

Serikali imesambaza nakala milioni 2 tu, je watakaopata fursa ya kuisoma watafika hata milioni 3?
 
Katiba itatusambaratisha WATZ panahitajika viongozi makini na wenye kujali nchi na watu wake.

Kwa nini Katiba itusambratishe? Ujasiri wa Watanzania ndiyo msingi wa mafanikio ya upatikanaji wa Katiba Mpya. Wapo wachache wasio na mapenzi mema na nchi yetu ndiyo maana wanawatisha wananchi. Simama imara Mtanzania himahima songa mbele soma na uwe mmoja wa wanaoipa Tanzania Katiba hiyo. Achana na wenye kupotosha jamii kwa maslahi yao binafsi. Watanzania tuungane pamoja kwa umoja wetu na kamwe tusiyumbishwe, tuijali nchi yetu na watu wake.

Simama imara na sema nafsini mwako na mbele ya Mungu wako Nataka kuwa sehemu ya historia njema ya nchi hii.
 
Midahalo pekee sio suluhisho ndg. President Elect, Waislam ni watu wanaojitambua na wanajua wajibu wao. Kwanini wewe umapenda kuleta tofauti tofauti ndani ya nchi yetu. Hizo ni tabia zenye mwelekeo wa kuwachochea watu wafuate unachotaka wewe.
Hawa ni watu makini wakiambiwa au kukisikiliza jambo ni vema ila changanya na akili zako wasije wakakuburuzwa hawa wasio na nia njema maana kuna wataalamu wa kupotosha Umma. Mtanzania, Uwe na nia ya dhati na utumie muda wako vizuri Kuisoma Katiba Inayopendekezwa ili uwe na uelewa mzuri zaidi kwa manufaa ya taifa lako na vizazi vijavyo.

Umakini uko wapi hapo unapandisha jazba! Hamjui kitu, mkishauriwa mnaanza Jihad, mkiachwa nyuma mnalalamika mnaonewa na mfumo kristu, kweli binadamu hatuna jema!!
 
Hongera kwa kwenda kwenye nyumba ya ibada, Mchungaji ni binadamu anaweza kuipelekea nchi yetu na wananchi kupata elimu ya bure ambayo inawaelekeza kwenye mawazo yake. Wanzania tuwe watu wa kuwahoji hawa wanaoleta porojo zao. Watanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu. Tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye mfumo wa demokrasia na misingi ya utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowakilisha wananchi. Ungana na Watanzania kutimiza azma ya kupa Katiba Mpya.

Faiza Foxy hongera sana kwa zao lako. Amekuaa!
 
Hadanganywi mtu hapa. Nchi isiyo na Katiba ni nchi ya namna gani hiyo? Hivi umesahau hata historia fupi ya uamuzi huu ulianzaje?

Sichoki kuwashirikisha Watanzania kupitia wewe MWAKABOKO namna Mchakato wa kutunga Katiba ya Tanzania ulivyopitia hatua mbalimbali ambapo wananchi sasa wamegawiwa nakala za Katiba Inayopendekezwa, ambayo ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba Mwaka jana Oktoba 4, Bunge hilo likitanguliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa Rasimu ya Kwanza tarehe 3 Juni, 2013 na Rasimu ya Pili ilitolewa tarehe 30 Desemba, 2014 na kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum tarehe 21 Februari, 2014. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, Hatua inayofuata ni yawananchi kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa. Hivyo basi, kwa mujibu wa sheria, wananchi ndiyo wenye uamuzi na kauli ya mwisho juu ya upatikanaji wa Katiba Mpya. Wananchi ni muhimu waisome na kuielewe Katiba Inayopendekezwa ili kufanya uamuzi sahihi wakati wa upigaji kura ya maoni kulingana na ratiba ilivyopangwa.

Hayo yote unayoyasema yanatoka wapi Mwakaboko? Ipende nchi yako au wewe una nchi nyingine?
naipenda Tanzania kuliko wewe, ndiyo maana nasema katiba ya chenge ni mbovu tusiunge mkono. Tuemdelee kutumia hii iliyopo. Mpaka pale mafisadi watakapokubali matkwa ya wanazengo
ila wewe sio mzalendo kabisa ,, samahani kama nitakuwa nimekukera ila sina lugha nyinghine rahisi zaidi ya hiyo
 
Faiza Foxy hongera sana kwa zao lako. Amekuaa!
sidhani kama kweli huyo ulimtaja ni zao la FF. wanatofauti kubwa mno lijapo suala la kitaifa ambalo halina mahusiano na dini ya Kiislam, FF hujitahidi kutetea utaifa. Ila huyo uliyemtacomment hapo yy anatetea chama chetu hata kama kimefanya madudu, yuko kama Mzee Mwiru enzi zile aliwahi komaa eti hakuna ufisadi hapa Tanzania, kesho yake asubuhi Dr. Slaa akaja na vielelezo kibao, Mzee Mwiru akabadili kauli na kusema ufisadi uppo ila ni wa mtu binafsi sio wa chama
 
Faiza Foxy hongera sana kwa zao lako. Amekuaa!
nimeipenda avatar yako yenye bendera ya Tanganyika. Awali nilidhani tuko wachache, kumbe tunaotaka Tanganyika irudi katika enzi yake tuko wengi!!!
 
Mungu amenipa nafasi leo nimeenda Kanisani, wakati matangazo ulipofika Waraka wa Maskofu wetu ukasomwa. Halafu Mchungaji wetu akatoa elimu ya bure kuhusu katiba hii pendekezwa. Hatimaye akasema tuipe kura za hapana. Akasisitiza maoni ya msingi ambayo wananchi waliyatoa, wajanja wameyatoa ili kulinda maslahi yao na uroho wao wa madaraka. Kila mwenye kuwaza vizuri na kuitakia mema nchi yetu nzuri yenye kila kitu kilichopo katika uso wa nchi, mwenye kupinga uchumi wa nchi kuhamishwa kijanja kijanja, bila shaka ataungana na viongozi wa dini kusema hapana kwa katiba pendekezwa

Heee kweli hii kali ya mwaka yaani mnashikiwa akili kiasi hicho?mnaamuliwa mambo yenu ya msingi na mtu mmoja?mmeshindwa kusoma mkaamua wenyewe?halafu mnachekelea?nyie kumbe hata mkiambiwa muanze kula majani mpate miujiza mnaweza kula bila woga maana uwezo wenu wa kufikiri umefikia mwisho kweli mwisho wa dunia umekaribia mna masikio lakini hayasikii, mna macho lakini hayaoni mmekua kama wagalatia sio bure mmeshalogwa nyie!!!!!!!

nimebahatika kuisoma,cha msingi tu bado kuna vitu vya kufanyiwa kazi,endeleeni kuisoma muielewe zaidi kabla ya kupigia kura
 
heri yako wewe umebahatika kuisoma, mamilioni ya watanzania hawajaiona wala hawaijui rangi yake, na hawataiona hiyo Katiba pendekezwa hadi siku ya kupiga kura ya maoni, tena si kwa bahati mbaya bali ni mkakati maalum wa watawala kutumia kanuni ya 'wajinga watawale'
 
Back
Top Bottom