Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mwishoni mwa juma lililopita nilileta mada hapa jukwaani kuhusu Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Bw. Thabo Mbeki, alivyomkumbuka hayati Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Kwenye bandiko hilo, nami nikatoa maneno mawili matatu kumhusu Rais huyo mstaafu Mkapa, kwa jinsi nilivyomjua mimi, kiumbali.
Moja ya mambo niliyoyakumbuka ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995 ambao ndo ulikuwa uchaguzi wa kwanza katika kurudi kwenye mfumo wa vyama vingi.
Nilisema hivi kuhusu ushiriki wa Rais Mkapa kwenye huo mdahalo:
Hilo bandiko linapatikana hapa.
Siku chache baadaye, mwenzetu Bw. Pascal Mayalla akaleta makala ya January Makamba, ya kumkumbuka marehemu rais huyo mstaafu.
Moja ya mambo ambayo Bw. Makamba aliyazungumzia, ulikuwa ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995, mdahalo ambao nadhani ndiyo uliomtambulisha vizuri Rais Mkapa kwa umma wa Watanzania.
Katika kumbukumbu yangu, mimi nilisema Rais Mkapa alifanya vizuri sana kwenye huo mdahalo. Licha ya kwamba hakuna kipimo sahihi cha kupima na kuona yupi alishinda, kwa maoni yangu, Rais Mkapa alishinda mdahalo ule.
Na kwa maoni ya January Makamba, nadhani ni sahihi pia nikisema hata yeye January aliona kuwa Mkapa alishinda.
Yeye Bw. Makamba alisema hivi:
Kusoma zaidi alichokiandika Bw. Makamba, bofya hapa.
Tokea mwaka huo wa ‘95, nadhani hatujawahi tena kuwa na mdahalo wa kitaifa wa wagombea urais.
Ningependa sana mwaka huu wa uchaguzi tuwe na mdahalo wa wagombea hiyo nafasi. Ila, sitashikilia pumzi yangu kusubiri hilo kutokea.
Lakini pia, nimeona si vibaya kuleta ombi/ wazo hili hapa.
Ombi ama wazo lenyewe ni kuipata video ya mdahalo wa ‘95.
Nimezunguka sana mtandaoni na huko YouTube, lakini nimeambulia patupu.
Pascal Mayalla wewe ni mwandishi wa habari wa muda mrefu. Naamini bado una uhusiano na watu waliomo kwenye vyumba vya habari vya vyombo vya habari hapa.
Sikumbuki vizuri ni stesheni zipi za runinga ambazo zilirusha matangazo ya ule mdahalo. CTN? ITV? DTV? Radio One labda?
Sasa Bw. Mayalla, unaweza kutumia uzoefu na nyenzo zako ulizonazo kututafutia video [au hata audio] ya huo mdahalo?
Mimi si muangaliaji sana wala si mfuatiliaji sana wa stesheni za runinga za hapa Tanzania. Ila kama kuna stesheni ambazo labda zina chaneli huko kwenye YouTube, zinaweza kuipandisha video ya huo mdahalo kwa faida ya umma.
Kama inawezekana, tusaidie Bw. Mayalla...
Shukran jazilan na ahlan wa sahlan.