Midahalo ya wagombea urais kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Midahalo ya wagombea urais kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Midahalo ajabu mtu mwingine utasikia Ohhh ifanyike kingereza kwa Nini isiwe kwa kifaransa? Lugha kuu zinazoongoza duniani Ni kingereza na kifaransa kwa Nini wengi wakomae kutaka kingereza tu?

Kiingereza tunajua hakipandi kwa Magufuli, hatutaki huko maana ni kuaibishana kusiko na sababu. Tunataka wa kiswahili ili kila mpiga kura aelewe kinachoongelewa. Uzuri wa midahalo hakuna nafasi ya kudanganya, na hata ukidanganya watu wataelewa.
 
1995 ulikuwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi tukiiga mataifa ya nje kila kitu Mkapa hakuwa na uzoefu

Vyama vingine mkitaka fanyeni Ruksa CCM hatutashiriki

Mdahalo si lazima kila chama kishiriki kiwe CCM au chochote

Binafsi natoa ruksa vyama vyote vinavyotaka mdahalo ruksa nendeni mkafanye ila CCM hatutashiriki . Mdahalo Ni kitu Cha hiari sio amri kuwa utake usitake lazima ushiriki!!

Vyama vingine endeleleeni kuitisha huo mdahalo ila CCM mtutoe nyie ruksa endeleeni as long as mna pesa za kulipia media

Hana uwezo wa kujieleza maana hana uwezo wa urais, mngetaka sana iwapo angekuwa na uwezo huo, ila hana uwezo huo ndio maana mnakimbia. Hata uchaguzi wa 2015 hakukuwa na mdahalo, maana wagombea wote wenye nguvu walikuwa ni wanaccm wasio na uwezo wa urais, bali wategemee mbeleko ya dola kuwa viongozi.
 
CCM tungekuwa hoja hatuna tusingekuwa tunashinda chaguzi!!!

Kwani huwa mnashinda uchaguzi au huwa mnatangazwa washindi? Huenda hujui tofauti ya kushinda, na kutangazwa washindi. Ndio maana mnang'ang'ania mfumo mbovu wa uchaguzi, maana mnajua fika kukiwa na VAR technology, hamuwezi kutangazwa washindi kwa mabavu.
 
CCM huwa hatutaki midahalo ya wagombea Uraisi sababu wapiga kura wengi asilimia 80 wanaishi vijijini na wengi hawana TV Wala Radio Wala mitandao ya kijamii tofauti na ulaya na Marekani hata hao wa mjini Ni wachache Wana TV na Radio na huingia mitandao ya kijamii

Na Ni useless sababu wengi wenye TV na waingia mitandao ya kijamii huwa hawaendi kupiga kura huwa wako tu majumbani wanafuatilia uchaguzi wakiwa kwenye sofa set zao!!

CCM tunaenda waliko wapiga kura ndio maana ofisi za CCM ziko kila Kijiji na kila mtaa na ziko active tofauti na vyama vingine

YEHODAYA,
Acha propaganda za kitoto!
Hivi unajua kwa bandiko lako hili unahatarisha AJIRA YA WAZIRI WA NISHATI Mhe. KALEMANI? Huyu Msukuma wa Watu anatamba kuwa mpaka sasa ameeneza UMEME kwa 80% ya Vijiji vyote Tanzania na vina umeme mpaka wa SUNDAR SOLAR na TV zake....!! Upo??
 
Nyani Ngabu,
Hii hoja yako Ina mashiko.
Mie nashauri mdahalo uwe wa Kiingereza ili kuwapa viewers wote including foreigners kujua Tanzania inaweza kuongoza na mtu mwenye uelewa wa maswala kwa kiwango gani....!!!
1995 nilishuhudia mdahalo huo na kiukweli Marehemu Mkapa was the right candidate.

Mwaka huu wa 2020 nategemea kuona list ifuatayo kwenye Mdahalo huo:
  1. John Pombe Magufuli...CCM.
  2. Bernad Callius Membe....ACT.
  3. Tundu Antipas Lissu-CHADEMA.
  4. Ibrahim Haruna Lipumba- CUF.
Angalizo kwa waandaji :LUGHA NI UNG'ENG'E.
Magufuli ataburuza mkia[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], na hatakuja ng'ooo Kwenye mdahalo
 
Ni mjinga tu ambaye haja muelewa mh JPM na staili yake ya uongozi kama Rais wa nchi katika miaka 5 ya uongozi wake. Eti ahitaji kumuelewa kupitia mdahalo. Tatizo lenu nyie ni kuchukua mambo ya wazungu na kuyakariri badala ya kuyaelewa na kuyafanyia kazi kwa jinsi na namna yenu.

Waraka wa wastaafu na katuni ya nguruwe wa zulia jekundu vimeshindwa mnafikiri mtatoka na mdahalo sio? pathetic!! Karahisha sana tu!
 
Sababu hasa ya ccm kukimbia midahalo ni uwezo duni wa viongozi wao kwenye kujieleza kwa hoja. Kama kweli ccm inamini watu wengi wa vijijini hawapati taarifa kwa njia hizi, ni kwanini Magufuli kila kitu anafanya mubashara kwenye Media zote? Ukijaribu kuangalia kuhusu kuwepo Mubashara, Magufuli ndio kiongozi aliyekuwa mubashara kuliko kiongozi yoyote aliyewahi kuwa rais wa nchi hii. Na iwapo hatatokea kwenye mdahalo wa safari hii, ni kwa sababu hana uwezo wa mijadala, bali anaweza sehemu za kuhubiri na kuamrisha fullstop.
Umemaliza kila kitu mkuu, Magufuli Hana ushawishi na hawezi mdahalo
 
Mwishoni mwa juma lililopita nilileta mada hapa jukwaani kuhusu Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Bw. Thabo Mbeki, alivyomkumbuka hayati Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Kwenye bandiko hilo, nami nikatoa maneno mawili matatu kumhusu Rais huyo mstaafu Mkapa, kwa jinsi nilivyomjua mimi, kiumbali.

Moja ya mambo niliyoyakumbuka ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995 ambapo ndo ulikuwa uchaguzi wa kwanza katika kurudi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Nilisema hivi kuhusu ushiriki wa Rais Mkapa kwenye huo mdahalo:
View attachment 1522615

Hilo bandiko linapatikana hapa.

Siku chache baadaye, mwenzetu Bw. Pascal Mayalla akaleta makala ya January Makamba, ya kumkumbuka marehemu rais huyo mstaafu.

Moja ya mambo ambayo Bw. Makamba aliyazungumzia, ulikuwa ni ule mdahalo wa wagombea urais wa mwaka 1995, mdahalo ambao nadhani ndiyo uliomtambulisha vizuri Rais Mkapa kwa umma wa Watanzania.

Katika kumbukumbu yangu, mimi nilisema Rais Mkapa alifanya vizuri sana kwenye huo mdahalo. Licha ya kwamba hakuna kipimo sahihi cha kupima na kuona yupi alishinda, kwa maoni yangu, Rais Mkapa alishinda mdahalo ule.

Na kwa maoni pia ya January Makamba, nadhani ni sahihi pia nikisema hata yeye January aliona kuwa Mkapa alishinda.

Yeye Bw. Makamba alisema hivi:

View attachment 1522626

Kusoma zaidi alichokiandika Bw. Makamba, bofya hapa.

Tokea mwaka huo wa ‘95, nadhani hatujawahi tena kuwa na mdahalo wa kitaifa wa wagombea urais.

Ningependa sana mwaka huu wa uchaguzi tuwe na mdahalo wa wagombea hiyo nafasi. Ila, sitashikilia pumzi yangu kusubiri hilo kutokea.

Lakini pia, nimeona si vibaya kuleta ombi/ wazo hili hapa.

Ombi ama wazo lenyewe ni kuipata video ya mdahalo wa ‘95.

Nimezunguka sana mtandaoni na huko YouTube, lakini nimeambulia patupu.

Pascal Mayalla wewe ni mwandishi wa habari wa muda mrefu. Naamini bado una uhusiano na watu waliomo kwenye vyumba vya habari vya vyombo vya habari hapa.

Sikumbuki vizuri ni stesheni zipi za runinga ambazo zilirusha matangazo ya ule mdahalo. CTN? ITV? DTV? Radio One labda?

Sasa Bw. Mayalla, unaweza kutumia uzoefu na nyenzo zako ulizonazo kututafutia video [au hata audio] ya huo mdahalo?

Mimi si muangaliaji sana wala si mfuatiliaji sana wa stesheni za runinga za hapa Tanzania. Ila kama kuna stesheni ambazo labda zina chaneli huko kwenye YouTube, zinaweza kuipandisha video ya huo mdahalo kwa faida ya umma.

Kama inawezekana, tusaidie Bw. Mayalla...

Shukran jazilan na ahlan wa sahlan.
Hakika nakwambia kamwe jiwe hawezi na wala hatakubali kusimama kwenye mdahalo na mtu yeyote yule, unataka aumbuke mchana kweupe?
 
Nadhan we Nyani unataka bwana yule aumbuliwe haitokuja tokea hilo kamwe
 
CCM huwa hatutaki midahalo ya wagombea Uraisi sababu wapiga kura wengi asilimia 80 wanaishi vijijini na wengi hawana TV Wala Radio Wala mitandao ya kijamii tofauti na ulaya na Marekani hata hao wa mjini Ni wachache Wana TV na Radio na huingia mitandao ya kijamii

Na Ni useless sababu wengi wenye TV na waingia mitandao ya kijamii huwa hawaendi kupiga kura huwa wako tu majumbani wanafuatilia uchaguzi wakiwa kwenye sofa set zao!!

CCM tunaenda waliko wapiga kura ndio maana ofisi za CCM ziko kila Kijiji na kila mtaa na ziko active tofauti na vyama vingine
Kwahiyo huo umeme wa REA huko vijijini mnapeleka wa kazi gani??
 
Naukumbuka mdahalo wa 1995

Mwamba Benjamin Mkapa na Lipumba walitisha

Mrema hakuwa na sera wakati Mzee Cheyo aliingia kautwika
 
Nyani Nagabu, utaua mtu kwa presha. CCM hupenda kuuzia Watanzania mbuzi kwenye gunia. Hivi unategemea Mgombea wa Sasa wa CCM akubali kushindanishwa kwenye mdahalo ambao kwa dhahiri anajua ataaibika!?
Hata kama mdahalo huo ufanyike kwa kiswahili, na wataalamu wote nchi nzima wakusanyike kuelekeza bado Mgombea wa CCM atashindwa vibaya.
Nasema ninachokijua. Ikiwa Kuna Mwananchi amepotezwa kwa kuhoji elimu ya mtu, ije kuwa aibu ya mdahalo!!
Hata hivyo mdahalo ndiyo njia sahihi ya kuelewa uwezo wa kiongozi, japo CCM huuona ni adui kwa chaguzi zao dhaifu.
 
Naukumbuka mdahalo wa 1995

Mwamba Benjamin Mkapa na Lipumba walitisha

Mrema hakuwa na sera wakati Mzee Cheyo aliingia kautwika
Kabla ya hapo watu wengi walikuwa wanadhani Mkapa ni ‘lightweight’ kwa sababu bungeni hakuwa mchangiaji machachari wa hoja.
 
Back
Top Bottom