Midahalo ya wagombea urais kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Midahalo ajabu mtu mwingine utasikia Ohhh ifanyike kingereza kwa Nini isiwe kwa kifaransa? Lugha kuu zinazoongoza duniani Ni kingereza na kifaransa kwa Nini wengi wakomae kutaka kingereza tu?

Kiingereza tunajua hakipandi kwa Magufuli, hatutaki huko maana ni kuaibishana kusiko na sababu. Tunataka wa kiswahili ili kila mpiga kura aelewe kinachoongelewa. Uzuri wa midahalo hakuna nafasi ya kudanganya, na hata ukidanganya watu wataelewa.
 

Hana uwezo wa kujieleza maana hana uwezo wa urais, mngetaka sana iwapo angekuwa na uwezo huo, ila hana uwezo huo ndio maana mnakimbia. Hata uchaguzi wa 2015 hakukuwa na mdahalo, maana wagombea wote wenye nguvu walikuwa ni wanaccm wasio na uwezo wa urais, bali wategemee mbeleko ya dola kuwa viongozi.
 
CCM tungekuwa hoja hatuna tusingekuwa tunashinda chaguzi!!!

Kwani huwa mnashinda uchaguzi au huwa mnatangazwa washindi? Huenda hujui tofauti ya kushinda, na kutangazwa washindi. Ndio maana mnang'ang'ania mfumo mbovu wa uchaguzi, maana mnajua fika kukiwa na VAR technology, hamuwezi kutangazwa washindi kwa mabavu.
 

YEHODAYA,
Acha propaganda za kitoto!
Hivi unajua kwa bandiko lako hili unahatarisha AJIRA YA WAZIRI WA NISHATI Mhe. KALEMANI? Huyu Msukuma wa Watu anatamba kuwa mpaka sasa ameeneza UMEME kwa 80% ya Vijiji vyote Tanzania na vina umeme mpaka wa SUNDAR SOLAR na TV zake....!! Upo??
 
Magufuli ataburuza mkia[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], na hatakuja ng'ooo Kwenye mdahalo
 
Ni mjinga tu ambaye haja muelewa mh JPM na staili yake ya uongozi kama Rais wa nchi katika miaka 5 ya uongozi wake. Eti ahitaji kumuelewa kupitia mdahalo. Tatizo lenu nyie ni kuchukua mambo ya wazungu na kuyakariri badala ya kuyaelewa na kuyafanyia kazi kwa jinsi na namna yenu.

Waraka wa wastaafu na katuni ya nguruwe wa zulia jekundu vimeshindwa mnafikiri mtatoka na mdahalo sio? pathetic!! Karahisha sana tu!
 
Umemaliza kila kitu mkuu, Magufuli Hana ushawishi na hawezi mdahalo
 
Hakika nakwambia kamwe jiwe hawezi na wala hatakubali kusimama kwenye mdahalo na mtu yeyote yule, unataka aumbuke mchana kweupe?
 
Nadhan we Nyani unataka bwana yule aumbuliwe haitokuja tokea hilo kamwe
 
Kwahiyo huo umeme wa REA huko vijijini mnapeleka wa kazi gani??
 
Naukumbuka mdahalo wa 1995

Mwamba Benjamin Mkapa na Lipumba walitisha

Mrema hakuwa na sera wakati Mzee Cheyo aliingia kautwika
 
Nyani Nagabu, utaua mtu kwa presha. CCM hupenda kuuzia Watanzania mbuzi kwenye gunia. Hivi unategemea Mgombea wa Sasa wa CCM akubali kushindanishwa kwenye mdahalo ambao kwa dhahiri anajua ataaibika!?
Hata kama mdahalo huo ufanyike kwa kiswahili, na wataalamu wote nchi nzima wakusanyike kuelekeza bado Mgombea wa CCM atashindwa vibaya.
Nasema ninachokijua. Ikiwa Kuna Mwananchi amepotezwa kwa kuhoji elimu ya mtu, ije kuwa aibu ya mdahalo!!
Hata hivyo mdahalo ndiyo njia sahihi ya kuelewa uwezo wa kiongozi, japo CCM huuona ni adui kwa chaguzi zao dhaifu.
 
Naukumbuka mdahalo wa 1995

Mwamba Benjamin Mkapa na Lipumba walitisha

Mrema hakuwa na sera wakati Mzee Cheyo aliingia kautwika
Kabla ya hapo watu wengi walikuwa wanadhani Mkapa ni ‘lightweight’ kwa sababu bungeni hakuwa mchangiaji machachari wa hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…