A
Anonymous
Guest
Wafanyakazi katika Chuo cha Afya Mvumi (Mvumi Institute of Health Sciences – MIHS) kilichopo Mvumi, Dodoma tunaomba msaada na uingiliaji wa mamlaka husika kutokana na changamoto kubwa zinazotukabili kwa muda mrefu.
Kwa sasa baadhi ya wafanyakazi tumekaa takribani miezi 11 bila kulipwa mishahara yetu, hali hii imekuwa ngumu sana kwetu kwa sababu tuna familia na majukumu ya kila siku, lakini tumekuwa tukifanya kazi bila uhakika wa lini tutalipwa.
Mbali na hilo, tunadai kuwa michango ya wafanyakazi katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) haijawasilishwa kwa muda mrefu. Mara ya mwisho tuna taarifa za kuwasilishwa kwa michango hiyo ilikuwa mwezi Machi 2023, hali hii inatupa hofu kuhusu mustakabali wa mafao yetu kama wafanyakazi.
Changamoto nyingine ni kuhusu mazingira ya utoaji wa elimu chuoni. Wanafunzi wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu, huku baadhi yao wakilazimika kupata masomo ya muda mfupi (part-time) hasa kipindi cha kuelekea mitihani ili kuziba mapengo ya masomo yaliyokosekana.
Tunahofia hali hii inaweza kuathiri ubora wa wahitimu, hasa kwa kozi zinazohusiana moja kwa moja na afya kama Optometria, Famasi na Maabara ya Afya.
Pia, baadhi ya wafanyakazi wanaojaribu kuwasilisha malalamiko kuhusu mishahara na haki zao wamekuwa wakihofia vitisho vya kufukuzwa kazi. Hali hii imefanya wengi kukaa kimya licha ya changamoto wanazopitia.
Tunaiomba Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Wizara ya Afya pamoja na viongozi wa Kanisa la Anglikana wanaosimamia chuo hiki kufanya uchunguzi wa kina kuhusu hali ya uendeshaji wa chuo, maslahi ya wafanyakazi na ubora wa mafunzo yanayotolewa.
Lengo letu si kukidhoofisha chuo, bali kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao na wanafunzi wanapata elimu bora itakayowawezesha kutoa huduma salama na yenye viwango kwa wananchi baada ya kuhitimu.