Miezi 30 ya Rais Samia madarakani: Pamoja na kujikwaa kwenye Bandari, bado ni Rais mwenye record bora ya kukuza uchumi wa Tanzania kwa kipindi kifupi

Akili kisoda
 
Vitu vingi Samia alivyofanya alikuwa anamalizia pale alipoishia hayati, kwahiyo hamna jipya atoke tu MADARAKANI.
Acheni campaign ya kijinga. Huyu hafai urais kabisa sema ni katiba imefanya kazi. Yafaa kumsaidia tu kwa kupinga yasiyofaa hadi amalize urithi wake.. Kuna wanamuingiza mkenge kusudi aharibu na kuna wanamtumia kwa maslahi yao. Pia mwenyewe onaonekana anahangaika na maslahi binafsi
 
Lord denning Faizafoxy njooni huku huyu jamaa anamsema Rais eti kajikwaa kweny bandariii!! Wahini haraka...
 
Ssmaki Akishaoza, Hata Umuunge na viungo Gani Haliki
Kuoza ni kuoza tuu
Na kufa ni kuoza Utumbo.
 
Tuambie asilimia ya watu wanaoweza kula Milo mitatu kwa siku imeongezeka au imepungua?Hatuli tarakimu angalia maisha ya watanzania Wengi wa kawaida yameboreka?au hata Milo miwili ni tabu.
 
Dollar imefika 2640 mbaya zaidi hata haipatikani, nimeenda sheli leo nimekosa mafuta ,hizo recod unazozisfia zipo wapi ,huwezi tu kuona maisha ya mtu mmoja mmoja yalivyo magumu ukiachia nyie wabunge mnaolipwa 17m baada ya kuongezewa
 
Uko sawa mkuu. Sijui nani alimziba huyu mama ufahamu wake ktk hij issue ya bandari
 
Dollar imefika 2640 mbaya zaidi hata haipatikani, nimeenda sheli leo nimekosa mafuta ,hizo recod unazozisfia zipo wapi ,huwezi tu kuona maisha ya mtu mmoja mmoja yalivyo magumu ukiachia nyie wabunge mnaolipwa 17m baada ya kuongezewa
Ngara mafuta yapo,shell Yako ipi ambayo Haina mafuta?
 
Ukuaji wa uchumi ambao hauakishi hali halisi za wananchi walio wengi ni uchumi hewa wa data za kwenye makaratasi.unaweza kuita uchumi propaganda.
 
Samia anafanya mengi makubwa lakini anaangushwa na mitazamo mingi inayoongozwa na akili za mfumo dume.

Hata akifanya mema kumi na baya moja litatazamwa baya na hayo kumi yatasahauliwa,

Nilisoma mahali kwamba barabara za lami za urefu wa kilomita 15,500 zinajengwa muda huu nchi nzima, na ametulia kabisa utadhani hakuna kinachofanyika. Hatafuti sifa binafsi yeye kama yeye, ni wapambe wake wanaoweka mabango njiani.
 
Sijakataa kuhusu mafuta kupanda bei

Ndio akiba ya dola inapungua, na nimegusia sababu na mwarobaini.

Unasema ajira hakuna, jiulize je unaajirika? Una vigezoo? Sawa hakuna za kutosha ila huwezi fananisha na kipindi kile cha uchumi kilema...

Yeye mwenyewe Samia kwa mdomo wake niliwahi kusikia akikili wazi kuwa uchumi umeshuka baada ya mtangulizi wake kufariki, kwasababu WB na IFM waliipeleka tanzania uchumi wa kati, lakini mda mfupi baada ya kifo cha Magufuli waliiondoa.Sasa kama rais mwenyewe akikili adharani inamaana Wewe unapingana nae,tokea hapo sijawahi sikia akisimama akisema uchumi wetu umetengamaa tena, Wewe unatuletea takwimu za Kkoo Lumumba eti uchumi umekua,ujinga mtupu,ameingia kakuta sh imesima juu ya dollar, Sasahivi sh yetu iko hoi,unga ulikuwa unauza sh 800, Sasahivi 1800,naniwakati wa mavuno,kakuta mchele 1000, Sasahivi 2500,mafuta ya ndio usiseme,ukiuliza unaambiwa vita ya Ukreen,labda uchumi umekua kwa mafisadi na watoto wao,juzi hapo tumeona mtoto wa Samia akiwa na Mseveni akitafuta chaka la upigaji,huyo akisema uchumi umekua hapo sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…