Miezi mitatu nimetotolesha vifaranga 500 vya kuku wa kienyeji

Ndio. Humo ndani ya banda kubwa nimeweka vibanda vidogo vidogo kwaajili ya vifaranga
Au huo muongiloano ndo sababu.?..mimi naona ni salama zaidi wakiwa na eneo lao tofauti na ndani ya banda. Kama kuwa na kibanda kingine pembezoni mwa banda
 
Nimewaza pia. Nitafanya kuwatenga mbali kabisa nione matokeo.. thanks.
 
Kuna kuku ambao ni maalumu kwa ajili ya utotoleshaji vifaranga (PARENTAL STOCK) sasa Hawa kuwapata huwa ni issue, kuku wakwanza akishatotoa , nahuyo kifaranga akija kua mkubwa nae akaanza kutaga akitotoa vifaranga mara nyingi huwa haviwi imara, Kinga yao ya mwili inakua dhaifu natural.

Tafuta parental stock ndio wawe maalumu kwa ajili kutaga mayai kisha utotoleshe vifaranga.
Hii hoja huwa siielewi, maana kama ingekuwa hivyo generation ya kuku inge disapear, unless kama kuna sababu za kitaalam, na je hiyo parental stock unaitoa wapi wakati na wao pia walikuwa ni vifaranga, au wao hawakuanguliwa?
 
Mkuu hata mie huwa najiuliza. Utasikia Sungura wamechoka eti wanazaliana wale wale. MbonaWarabu hapa Tanzania wanazaliana wale wale waliokuja miska 500 iliopita. Hakuna makundi mapya ya warabu waneohamia, mbona hawafi na kuwa dhaifu.
Mbona vijijini kabila moja wanaoana wale wale hatujasikia kabila fulani ni dhaifu kwa kuoana.
Labda naweza elewa kuwa vifaranga visizaliane uzao mmoja , ukiviletea jogoo mwingine vinaendekea kuwa vizuri tu.
Hata hivyo nami nitafanya majaribio ndani ya mwaka nione kama uzao utasumbua.
 
Ushajiuliza kwa nini watu wengi hawafugi broiler wakawaruhusu watage mayai kisha wakaenda totolesha mayai ya broiler?.

Na hata kuku wanataga Mayai ya broiler hawajazubaa zubaa kama broiler na Wana utofauti mkubwa sana kwa namna walivyo. Hivi Sababu itakua nini?.
 
Back
Top Bottom