Miezi mitatu nimetotolesha vifaranga 500 vya kuku wa kienyeji

Kheri kwenu wapendwa nimeamini kila kitu ni nia na kujituma.

Mwezi wa saba nilinunua tetea 30 na jogoo 3 wanaotetea mwezi wa nane nikapata vifaranga 280 na mwezi huu wa tisa 220.

Na bado naendelea kuatamishiae. Lengo kufika mwezi wa kumi na mbili niwe na kuku 1000 wa kienyeji pure.

NJIA NAZOTUMIA KUFANIKISHA MALENGO HAYA
1: Mimi mwenyewe ndiyo msimamizi mkuu naamka saa11 alfajili kuosha makopo na kulisha chakula.

2: Nimetenga kuku 15 wanaoatamia na wengine15 wanataga tu.

3: Vifaranga navilea kwa joto la mkaa.

4: Kwenye mabanda ya vifaranga kwa siku nafanya ukaguzi Mara 4.

5: Eneo la kufugia ni kubwa na nimezungushia fesi.

6: Dawa za kuku zipo za kutosha za maji na unga.

Karibuni
Hongera aisee, mm ninao wa kienyeji wanaweza pitisha hata miezi 2 nisione mayai, wanakuwa wanene tu.
 
Huwa napata maswali mengi juu ya mtu anayeanzisha mada, yupo online na hajibu maswali ya msingi.
 
K
Kheri kwenu wapendwa nimeamini kila kitu ni nia na kujituma.

Mwezi wa saba nilinunua tetea 30 na jogoo 3 wanaotetea mwezi wa nane nikapata vifaranga 280 na mwezi huu wa tisa 220.

Na bado naendelea kuatamishiae. Lengo kufika mwezi wa kumi na mbili niwe na kuku 1000 wa kienyeji pure.

NJIA NAZOTUMIA KUFANIKISHA MALENGO HAYA
1: Mimi mwenyewe ndiyo msimamizi mkuu naamka saa11 alfajili kuosha makopo na kulisha chakula.

2: Nimetenga kuku 15 wanaoatamia na wengine15 wanataga tu.

3: Vifaranga navilea kwa joto la mkaa.

4: Kwenye mabanda ya vifaranga kwa siku nafanya ukaguzi Mara 4.

5: Eneo la kufugia ni kubwa na nimezungushia fesi.

6: Dawa za kuku zipo za kutosha za maji na unga.

Karibuni
kwanini haujamwandika Samia Suluhu kwa kukuwezesha uwe na kuku wengi?
 
Itakuwa unawapa pumba tupu mfululizo, zisizochanganywa na vyakula vingine. Hivyo zinawafanya wawe na mafuta mengi sana mwilini na kushindwa kutaga. Badilisha namna unavowalisha.
Cha ajabu mkuu chakula nachowapa ni cha formula ya layers, na hao layers wanataga tu kawaida ila hawa kienyeji ndo shida japo hata si wazee. Je, banda likiwa na mwanga mwingi inaweza kuwa shida pia? Maana banda lao liko na dirisha kubwa sana la kupitisha hewa.
 
Labda ni tasa! Fanya uwapime.......vidole vitatu weka kati ya mifupa ya nyonga....vikibana, inamaanisha kuku ni TASA.
 
una passion ya kufuga, unahitaji mtu mwenye ujuzi mzuri wa biashara akufungue mahali.

Garama ya chakula, madawa, huduma zote unazowapa hao kuku wa kienyeji pure ungezihamishia kwenye chotara F1 ungepiga hatua kubwa sana. Bei ya mayai ya chotara na ya kienyeji bei zinaachana kwa 2000 hadi 1000 kwa trey, ukuaji wa chotara hadi kufaa kwa nyama ni ndani ya miezi 3 tofauti na kienyeji hadi miezi 6.

Kazi njema mkuu
 
Kheri kwenu wapendwa nimeamini kila kitu ni nia na kujituma.

Mwezi wa saba nilinunua tetea 30 na jogoo 3 wanaotetea mwezi wa nane nikapata vifaranga 280 na mwezi huu wa tisa 220.

Na bado naendelea kuatamishiae. Lengo kufika mwezi wa kumi na mbili niwe na kuku 1000 wa kienyeji pure.

NJIA NAZOTUMIA KUFANIKISHA MALENGO HAYA
1: Mimi mwenyewe ndiyo msimamizi mkuu naamka saa11 alfajili kuosha makopo na kulisha chakula.

2: Nimetenga kuku 15 wanaoatamia na wengine15 wanataga tu.

3: Vifaranga navilea kwa joto la mkaa.

4: Kwenye mabanda ya vifaranga kwa siku nafanya ukaguzi Mara 4.

5: Eneo la kufugia ni kubwa na nimezungushia fesi.

6: Dawa za kuku zipo za kutosha za maji na unga.

Karibuni
Hongera sana mkuu
 
Mkuu hongera Sana naitwa Bwana masawe nipo mkoa wa pwani wilaya ya Chalinze eneo la mbwewe ningependa nijifunze kwako huu mradi manake nimejaribu mara 2 zote nimeangukia pua Nina Shamba Zaid ya hekari 20+ mabanda yapo Ila kila nikijaribu chali Post yako imenipa natumaini kuwa kumbe inawezekana naomba nikucheki WhatsApp kama hutajali natanguliza shukurani
 
Mkuu habari ya asubuhi?..... Sorry, nimeona comment yako kwenye post ya jamaa anayetotolesha kuku na kwamba upo mbwewe....Nilikuwa naomba kuuliza kwa mbwewe ardhi inauzwaje?

Kumradhi kwa kuchelewa kujibu mihangaiko ya hapa na pale Huku inategemea na eneo Yani umbali toka lami na pia aina ya shamba Yani ubora Wa shamba bei NI 200k,170k,150k, kwa HEKARI
 
Nakupa mbinu
🤣🤣🤣Tusaidiane mbinu bila ya kutumia mashine
Nirahisi hakikisha unakuwa na kuku kwaajili ya kuatamia tu na wengi kwaajili ya kutaga tu sasa Unafanya vipi 👇🏼
Chukulia mfano wa kuku 30 Tenga 15 wa kutaga na 15 kuatamia Hawa 15 wa kutaga wapatie Kila tete 5 jogoo mmoja hii ni kupata mayai Bora yenye mbegu za kutoa vifaranga Hawa kuku wafungie sehemu Moja baada za zoezi la utagaji kuku wakianza kuatamia wawekee mayai ya kisasa matatu au mawili ili kuwasubirisha wote 15 waanze kuatamia kwa pamoja wakitimia wagawie mayai kulingana na umbo LA kuku hakika mayai haya hayavuki siku Saba Hadi 10 tangu yatagwe utawawekea wote kwa siku moja baada ya zoezi hili hakikiksha kuku wale wengine 15 unawarudisha kwa jogoo baada ya siku 14 wataanza kutaga mayai tena sasa hayo unaweza kuuza kwasababu wale wengine Bado hawajaanza kutotoa ikifika siku ya 7 tangu waanze kuatamia unaweza kwenda kuangalia mayai yenye vifaranga na kutoa yale yasio na vifaranga utatumia kwa Chakula sasa ikifika siku ya 21 kuku wote watakuwa wameanza kutotoa hakikisha kila kifaranga aliyekamilika unamtoa na kupeleka kwenye bluda (sehemu ya joto) ili kuacha nafasi na kumfanya kuku yule aendelee kuatamia akijua Bado hajapata watoto Fanya hivyo kwa kuku wote Hadi mayai uliyowapatia yatotolewe yote kabla ya mayai hayo kuisha muwekee mayai yale ya kisasa ili aendelee kubaki pale kwenye kiota baada ya kuwa mayai yote yametotolewa sasa unaweza chukua mayai mengine kutoka kwa wale kuku 15: wa kutaga na kuwagawia tena kuku hawa waendelee kuatamia kwa mwenzi mwingine hakikiksha mayai hayavuki siku saba tangu yatagwe utarudia zoezi la ukaguzi kama kawaida baada ya siku saba ili kutoa mayai yasiyokuwa na vifaranga unaweza fanya zoezi la kutotolesha kwa namna hii kwa miezi 3 ndio unawatoa wale kuku kwenye viota ili wapumzike kwa mwenzi mmoja tena au miwili kwa namna hii utapata kuku wengi
 
Back
Top Bottom