Nakupa mbinu
Nirahisi hakikisha unakuwa na kuku kwaajili ya kuatamia tu na wengi kwaajili ya kutaga tu sasa Unafanya vipi 👇🏼
Chukulia mfano wa kuku 30 Tenga 15 wa kutaga na 15 kuatamia Hawa 15 wa kutaga wapatie Kila tete 5 jogoo mmoja hii ni kupata mayai Bora yenye mbegu za kutoa vifaranga Hawa kuku wafungie sehemu Moja baada za zoezi la utagaji kuku wakianza kuatamia wawekee mayai ya kisasa matatu au mawili ili kuwasubirisha wote 15 waanze kuatamia kwa pamoja wakitimia wagawie mayai kulingana na umbo LA kuku hakika mayai haya hayavuki siku Saba Hadi 10 tangu yatagwe utawawekea wote kwa siku moja baada ya zoezi hili hakikiksha kuku wale wengine 15 unawarudisha kwa jogoo baada ya siku 14 wataanza kutaga mayai tena sasa hayo unaweza kuuza kwasababu wale wengine Bado hawajaanza kutotoa ikifika siku ya 7 tangu waanze kuatamia unaweza kwenda kuangalia mayai yenye vifaranga na kutoa yale yasio na vifaranga utatumia kwa Chakula sasa ikifika siku ya 21 kuku wote watakuwa wameanza kutotoa hakikisha kila kifaranga aliyekamilika unamtoa na kupeleka kwenye bluda (sehemu ya joto) ili kuacha nafasi na kumfanya kuku yule aendelee kuatamia akijua Bado hajapata watoto Fanya hivyo kwa kuku wote Hadi mayai uliyowapatia yatotolewe yote kabla ya mayai hayo kuisha muwekee mayai yale ya kisasa ili aendelee kubaki pale kwenye kiota baada ya kuwa mayai yote yametotolewa sasa unaweza chukua mayai mengine kutoka kwa wale kuku 15: wa kutaga na kuwagawia tena kuku hawa waendelee kuatamia kwa mwenzi mwingine hakikiksha mayai hayavuki siku saba tangu yatagwe utarudia zoezi la ukaguzi kama kawaida baada ya siku saba ili kutoa mayai yasiyokuwa na vifaranga unaweza fanya zoezi la kutotolesha kwa namna hii kwa miezi 3 ndio unawatoa wale kuku kwenye viota ili wapumzike kwa mwenzi mmoja tena au miwili kwa namna hii utapata kuku wengi