Miezi mitatu nimetotolesha vifaranga 500 vya kuku wa kienyeji

Miezi mitatu nimetotolesha vifaranga 500 vya kuku wa kienyeji

Acha kukatisha tamaa! Kama huna taarifa, usisema HAKUNA au haiwezekani
Shida ya sisi watu weusi tuna negativity sana, wazungu wamepambana kufanya uvumbuzi wa vitu mbalimbali mpaka wamefanikiwa. Lakini njoo huku kwetu sasa hata vitu vya kawaida ambavyo ni asili ya mwanadamu utaambiwa huwezi.

Mimi nashauri kama mtu una passion na hivi vitu viwili kilimo na ufugaji fanya bila kuchoka hata kama unafeli kuna wakati utakuja kufanikiwa na utawashangaza watu.
 
mara nyingi huwa ni kuku jamii ya saso ndio hutaga mayai haya ni mazuri sana kibiashara lakini kwa mfugaji unapaswa kupata elimu juu ya uchaguzi wa mayai yake kwajili ya vifaranga kwani huwa hawatagi yote yenye viini viwili
Nikweli hata Mimi ni sasso ndo wanataga hivo na ninayajua.

Halafu Sasa Hivi sasso wanapatikana wapi nilikuwa na chukulia silver pale iringa Kwa Sasa oda una subiri sana Kwa muda mrefu.

Hata kroiler nilikuwa nachukulia AKM Dar Sasahivi hta no Yao haipo hewani naweza pata wapi hizi kuku aina mbili na ziwe og (F1)
 
makampuni mengi yanabadilisha mitetea wazazi FALCON wako vizuri japo wanaanza kutoa tena mwezi ujao mwezi huu hawana
 
Njoo nikupeleke Kwa mama mdogo wangu. Siyo kuku hata kanga anao zaidi ya 200!

Ukishindwa wewe na mkeo siyo wote Mimi ninao357 Hadi Sasa njoo dmna hiyo laki yako
Na ajue kuwa watu hawafugi ili kutambiana, na kila mtu ana mbinu zake.
Hata akienda pale Interchick na kuuliza, je mna kuku wangapi? Hatopata jibu sahihi.
 
Kuku wa kienyeji hawakai wengi kwa pamoja.
Wakifika 100 tu, wanaanza kufa kwa mdondo. Fuga wa kisasa.
Au kuuza tu
Tatizo la ufugaji unakuwa na tamaa na unataka idadi iongezeka tu
Wakifika 200 unasema wafike 500 wakifika 500 unawaza 1000 mwisho wanakufa wote unaanza kulia na kusema ooh kuna dawa feki nimeuziwa
Mara kuna mama alipita na kuku mgonjwa mradi sababu tu

Wafugaji wengi ndio tabia zetu unataka kufurahisha macho wanakuwa kama wanao 😄 🤣 😂
Jamani unafuga kwa faida uza pindi wanapofika umri wa kuuza
Tena uza wengi tu hata nusu
Jitangaze kaangalie masoko
Leta Canter jaza kauze
Ila ukiwalea kusafisha macho kila asubuhi mwisho machozi fact
 
eLimu nzuri
ILa yai likisha laliwa kwa siku kumi linafaa kwa kula kweli??
Yanaliwa saana tu!...tena hata na ww itakua ushawahi kula sema haukujua tu!
Iko hiv, yai likiwa halina mbegu ya jogoo hata lilaliwe hadi siku kumi lina liwa kama kawaida. Na watumiaji wengi wa mayai design hio ni waoka KEKI! Sasa jiulize keki unazokulaga hua unajua mayai wanayotumia!!
 
Kuku wa kienyeji hawakai wengi kwa pamoja.
Wakifika 100 tu, wanaanza kufa kwa mdondo. Fuga wa kisasa.
Kwa asili kuku ni ndege pori. Hiyo ni nature.
Pili. Kadiri ya mfumo wao wa maisha wanaposogamana huongeza hatari ya kuzuka magonjwa.
Je unadhani ni rahisi, kwa mfano kundi la kware wa porini kukaa wengi pamoja?
 
N
Kheri kwenu wapendwa nimeamini kila kitu ni nia na kujituma.

Mwezi wa saba nilinunua tetea 30 na jogoo 3 wanaotetea mwezi wa nane nikapata vifaranga 280 na mwezi huu wa tisa 220.

Na bado naendelea kuatamishiae. Lengo kufika mwezi wa kumi na mbili niwe na kuku 1000 wa kienyeji pure.

NJIA NAZOTUMIA KUFANIKISHA MALENGO HAYA
1: Mimi mwenyewe ndiyo msimamizi mkuu naamka saa11 alfajili kuosha makopo na kulisha chakula.

2: Nimetenga kuku 15 wanaoatamia na wengine15 wanataga tu.

3: Vifaranga navilea kwa joto la mkaa.

4: Kwenye mabanda ya vifaranga kwa siku nafanya ukaguzi Mara 4.

5: Eneo la kufugia ni kubwa na nimezungushia fesi.

6: Dawa za kuku zipo za kutosha za maji na unga.

Karibuni
Naona unatafuta mbinu ya kuwapiga wapuuuzi?
 
Kuku wa kienyeji hawakai wengi kwa pamoja.
Wakifika 100 tu, wanaanza kufa kwa mdondo. Fuga wa kisasa.
Shule tu! Huku kwetu watu wana kuku mamia kwa maelfu ya kienyeji.
Gonjwa ulilotaja ni la kukingwa kwa chanjo+ kuzingatia kanuni za ufugaji.
Soma historia ya eneo unalofugia tEmbea na chanjo kwa wakati+ zingatia kanuni tatu za muhimu katika ufugaji. Kudhibiti muingiliano, kutenga & Usafi. Ndani ya kanuni hizo kuna mambo meeengi meengi sasa.
Narudia tena TAFUTA SHULE YA UFUGAJI USIKARIRI.
 
Na ajue kuwa watu hawafugi ili kutambiana, na kila mtu ana mbinu zake.
Hata akienda pale Interchick na kuuliza, je mna kuku wangapi? Hatopata jibu sahihi.
Uko sawa mkuu. Pale Kenya Kuna jamaa ana kuku kienyeji zaidi ya6000 ukiwaona unaweza usiamini.

Watu Wana Nia na wanathubutu sio kama yeye anashangaa kuku500
 
Back
Top Bottom