Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vyombo vyote vya habari vilivyoisapoti ccm viko hoi.Kazi kwelikweli hii nchi ina safari ndefu isiyo mithilika. Wanasiasa tatizo, watumishi tatizo, wananchi nao tatizo. Basi ni vurugu tupu.
Mbona itv wengine wana zaidi ya 9?miez 9 hulipwi na bado unakomaa tuu? too good to be true
Aliimiliki kimkakati imsaidie kuingia ikulu baada ya kuukosa urais ameitelekeza...je unamsikia hata kuchangia msikiti au kanisa tena?Radio station inampeleka kasi Tanzania angeiweza!!!
Mungu atuhurumie🤣baada ya kuukosa urais ameitelekeza...je unamsikia hata kuchangia msikiti au kanisa tena?
Siasa za Tz ni chafu, ukiona wapewa msaada ni hongo tu ili kesho umkabidhi nchiMungu atuhurumie🤣
Zile face scrubs na injoface sizikubabaishe kwenye ma-TvHua nikisikia watangazaji wanavyokua wanajigamba kwenye vipindi mbali mbali redioni hua nadhani ni matajiri mno kumbe bora ata mm ninae bangaiza mtaani uku? Hatari sana
YesSiasa za Tz ni chafu, ukiona wapewa msaada ni hongo tu ili kesho umkabidhi nchi
Hahhaa kweli lakiniAliimiliki kimkakati imsaidie kuingia ikulu baada ya kuukosa urais ameitelekeza...je unamsikia hata kuchangia msikiti au kanisa tena?
Ni misukule haswaMiezi tisa bila mshahara na bado mnaenda kazini. Wabongo bana
Na hamna mikataba hiyo haki sijui mtaidai vipi?
Ndio Kwanza walikuwa juu kidomo domo kuomba mapambio , umbwa hawa . Na yasivyo na akili bado yanapigika miezi Tisa bila mishaharaMbowe alikuwa anaonewa hatukuwahi kuwasikia wakipaza sauti acha wanyooshwe wajinga wakubwa
Hahaaaa wanaongeanga Kwa shombo Sana hawa pimbiz as if ni millionaires flani ,kumbe glorified kapukuzHua nikisikia watangazaji wanavyokua wanajigamba kwenye vipindi mbali mbali redioni hua nadhani ni matajiri mno kumbe bora ata mm ninae bangaiza mtaani uku? Hatari sana
Na vitaendelea kufa kutokana na upunguani wao na uchawa ,Kwanza Nani ana muda mchafu WA kusikikiza hao vilaza most of them unprofessional ? Siku nzima kuongea ongea upuuz humuVyombo vyote vya habari vilivyoisapoti ccm viko hoi.
1. Sahara midia
2. Itv hoi mbaya kabisa...watu hawajalipwa mishahara ya nyuma kibao
3. Na sasa R.5
Dah!.. Wafanyakaz wanapata tabu na kuendesha maisha yao binafsi, naamini mamlaka husika zitachukulia uzito swala hili kama inavuotakiwa.."ANDIKO HILI LIMETOLEWA NA WAFANYAKAZI WA RADIO 5 ARUSHA"
"Habari za wakati huu wanahabari wenzetu.
Sisi ni Wafanyakazi wa Radio5 Arusha iliyo chini ya TAN COMMUNICATION MEDIA ambayo inamilikiwa na Familia ya Mzee Edward LOWASSA kwa masikitiko kabisa tunalazimika kuandika ujumbe huu kueleza mateso tusiyostahili ambayo tunayapitia kwa muda mrefu sana. Tunajua kwamba hii si njia ambayo tungetamani kutumia kutatua changamoto zetu, lakini tumeona kwamba ndio njia pekee iliyosalia kufanikisha hili.
Kampuni yetu haitutendei haki na imekuwa ikifanya unyanyasaji kwa wafanyakazi kwa miaka mingi, lakini sasa hali imekuwa mbaya zaidi:-
1. Kampuni hailipi wafanyakazi. Huu ni mwezi wa 9 hawajatulipa wafanyakazi na bado wanatulazimisha kuingia kazini. Ni ngumu kwetu kuendesha maisha bila mshahara. Ni kama hawajiulizi tunakula nini, tunaishi wapi, tukiumwa tunajitibu vipi, tunasafirije kuja kazini, watoto wetu wanasomaje, familia zetu zinazotutegemea tunazimudu vipi, nk.
2. Hatuna Bima ya Afya.
Tangu Radio hii iwe chini ya familia ya Lowassa mwaka 2007, hakuna mfanyakazi amewahi kukatiwa Bima ya Afya ilhali mikataba inasema tutapewa Bima ya Afya. Haijawahi kutokea
3. Makato ya HIFADHI ZA JAMII HAYAFIKI KWENYE MIFUKO HUSIKA NA TUNAKATWA.
Kampuni hii haijawahi kupeleka hata Sh. 10 ya makato wanayotukata wafanyakazi.
Tumekuwa tukilalamika miaka yote, tukaenda Idara ya Kazi na NSSF kulalamika kwenye ofisi zao za Arusha, ila wanakuja ofisini, wanaonana na Uongozi, WANAHONGWA wananyamaza (Kwenye Hili Viongozi wa IDARA YA KAZI na MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII Tunaomba Rais SAMIA SULUHU HASSAN Awawajibishe maana Wana Michezo Hatari sana na ni WALA RUSHWA. Hawajawahi kutusaidia kabisa licha ya kuwa tumepeleka malalamiko mara kwa mara.
4. Kampuni inaingiza Fedha nyingi sana kwa mwezi sababu tuna matangazo makubwa lakini haitujali.
Radio hii haitoi nafasi za wafanyakazi kujindeleza wala haitoi fursa hata za mikopo midogomidogo kwa wafanyakazi
5. Uongozi wa Radio5 ni mbovu kiasi kwamba kila siku tunaona jinsi radio inaelekea kufa. Maelezo mtandaoni yanasema tunasikika mikoa 21, tulikuwa tunasikika mikoa 11, ila sasa tumebaki Arusha na Dar tu, na hata hiyo miwili mara leo tupo hewani kesho haipo. Vipindi havina ubora sababu wafanyakazi wengine wanashindwa kufika kazini SABABU YA KUKOSA NAULI na hata wanaobahatika kuingia kazini wana stress za ugumu wa maisha. Cha Kushangaza tunapiga kelele kila siku lakini Hawasikii
Mfano, Bob Lowassa ambaye ndiye anasimamia Radio ANA MIAKA MITATU (3) Hajakanyaga Radio5!!!!
6. Kampuni haina usafiri
Radio 5. Haina hata GARI BOVU kwa ajili ya wafanyakazi kinyume na mikataba na pia hawatoi nauli japo mkataba unasema kampuni ina gari za usafiri na pia wafanyakazi watakuwa wanapewa NAULI.
Hali hii imepelekea wafanyakazi kufika kazini kwa tabu au kutofika kabisa. Na wengine kulala ofisini hasa wale wenye vipindi vya usiku kwa kukosa namna salama ya kurudi majumbani kwao
7. Uongozi hautaki VIKAO NA WAFANYAKAZI.
Ni zaidi ya miaka mitano sasa wafanyakazi tumekuwa tunaomba kukutana na viongozi wetu haswa MD bila mafanikio.
8.Wafanyakazi hatuna mikataba, tangu ilipomalizika takribani miaka miwili sasa.
MAOMBI YETU:-
1. TUNAMUOMBA WAZIRI WA Habari MH.NAPE NNAUYE Aingilie kati hii kampuni ili wafanyakazi tupate stahiki zetu muhimu (Mishahara ya miezi 9 na mafao ambayo tunakatwa na hayapelekwi kwenye mfuko) kwani mpaka sasa hakuna wa kutusikiliza.
2. Tunaiomba Serikali ya Mama yetu mpendwa MH.SAMIA SULUHU HASSAN kuingilia Kati idara zake muhimu ambazo zinakuwa hazitimizi wajibu wao. Mfano ni kama IDARA YA KAZI na MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII
UJUMBE HUU TUMEANDIKA WAFANYAKAZI WA RADIO5 na hatuwezi kutaja majina yetu kwa kuhofia usalama wetu na familia zetu ila ni uhalisia kwamba tunateseka na uchunguzi mdogo unaweza kuthibitisha madai yetu yote
WANAHABARI TUMEKUWA MSTARI WA MBELE KUPAMBANIA MASLAHI YA WENGINE NA HUKU TUNATEKETEA.
Umefika wakati sasa tupaze sauti pia kwa ajili yetu."
Asante
View attachment 2333508
Una maanisha nini?Are they so sure that the Owner knows everything that happens on Earth?