KERO Mifuko ya Hifadhi za Jamii NSSF na PSSSF kwanini mnatesa wastaafu kuwalipa Pesa zao?

KERO Mifuko ya Hifadhi za Jamii NSSF na PSSSF kwanini mnatesa wastaafu kuwalipa Pesa zao?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2018
Posts
881
Reaction score
2,569
Mazoea yamekuwa desturi, baada ya kuchangia kwa miaka mingi mifuko hiyo hadi kustaafu sasa wastaafu ndio wana kumbana na adha ya kupewa pesa zao utadhani wanaomba kazi upya.

Kwanza wanacheleweshewa wakati mifumo ya kustaafu inaeleweka mwezi mmoja kabla mtu hajastaafu.

Sasa kesha toka kazini na hana mshahara tena mnajua anaishije? Moja ya taasisi zinazoifanya serikali hii ya CCM ionekane ya hovyo kabisa ni hii mifuko ya jamii inavyo watenda wenye pesa zao yaani WASTAAFU
 
Ukiwa umeajiriwa unabidi kujiwekea akiba yako pembeni maana kuna wakati ukitegemea hii mifuko ya wanasiasa unaweza kufa bila kupenda

Hela zinaibiwa na kuchezewa vibaya mno
 
Mimi ilinichukuwa miaka miwili ndiyo nikapata fedha zangu.

Hata huruma hawana hawa jamaa.
 
Sina ham na hayo mamifuko, yanatuumiza sana. Ila ukipata usisahau na kujiwekea akiba binafsi.
 
Mkuu hii mifuko ni chaka la wezi la wanasiasa na ccm yao!
ndio wanakomba hizi hela na kuwafanya wastaafu kutaabika mno!
Mifano hai i[po ya wanasiasa wengi walikopa fedha huko na hakuna kurudisha!
Kibaya zaidi sio wanachama wa mifuko hii!
 
Back
Top Bottom