Ni rahisi kuweka sheria za kudhibiti makosa, kuliko kusubiri kwanza tupate watu wasiofanya makosa au walio waadilifu.
Kuweka sheria za kudhibiti makosa ni jambo moja na pia kudhibiti makosa hayo ni jambo jingine.
Lakini pia naomba utambue kwamba katika mada yangu nimegusia ujumla wa sheria na sio kipengele cha SHERIA ZA KUDHIBITI MAKOSA TU.
Kwa sababu katika sheria ambazo viongozi watafuata sio zile tu za kudhibiti makosa bali kuna sheria watazifuata kama muongozo juu ya nini wafanye katika majukumu yao.
Mfano kama kiongozi sheria inamtaka aweke serikali ya umoja wa kitaifa tuone kweli vigezo vikikidhi anaweka serikali ya umoja wa kitaifa.
Hiyo maana yake ni kuwa anafuata sheria katika jambo ambalo kulitekeleza kwake sio kwa ajili ya kudhibiti kosa fulani bali kutokutekeleza sheria hiyo ndo inakuwa kosa lenyewe.
Tofauti na sheria kwamba mwizi afungwe manake ukitekeleza unatekeleza jukumu la kudhibiti kosa na usipotekeleza ni kosa jingine la pili.
Kwa hiyo katika point hii nasema kuwa lengo sio kudhibiti makosa tu bali lengo kupata watu watakaofuata utaratibu hata katika kanuni ambazo kuzitekeleza kwake hakuwi katika kudhibiti makosa.
Mfumo mzuri unaweza ukaupata kwa muda mfupi na ukaanza kuutumia kudhibiti watu waovu, lakini kupata watu waadilifu hakuna ukomo!
Kama ambavyo huu tulionao tumeupata kwa muda mfupi lakini sio umeona leo unapigiwa kelele ubadilishwe mzee ?
Hata huo ambao mnautaka uje kwa muda mfupi baadae pia watu wataupigia kelele kwa sababu utaratibu wake sio wa kudumu katika kuutekeleza kama unavyosema ni rahisi kuupama.
"Ease come ease go"
Aidha, tukisema tusiwafunge watu wezi mpaka tutakapopata watu waadilifu itatuchukua vizazi vyote na tusiwapate.
Hoja yangu sio kwa wale ambao wanatakiwa kuongozwa na sheria.
Hoja yangu ni wale ambao wasimamizi au viongozi waliowekwa na sheria hizo ili kuwaongoza wengine.
Hoja hapa ni viongozi wa ngazi mbali mbali za serikali akianziwa na raisi mwenyewe hawa ndio ambao nimewakusudia mimi.
Hawa lazima iwe walikuwa well trained katika uadilifu na ustaarabu ili wakiwekwa hapo kuwasimamia wengine wawe wanatenda uadilifu.
Twende na vyote: tujenge mifumo mizuri na bora huku tukisisitiza uungwana na uadilifu.
Tusitegemee kupata watu waadilifu kama msisitizo wa kusisitiza watu wawe waadilifu ni ule ule.
Yani tusitake matokeo mapya kama bado tunatumia njia za zamani.