Mifumo imara bila watu waadilifu sio suluhisho, jenga watu kwanza

Mahakama ni chombo cha kusimamia haki, ukiona uko kwenye nchi ambayo hauwezi kupata haki yako mahakamani basi, huo mfumo umekuwa compromised
Mahakama ya sasa ina jukumu gani juu ya wale wabunge 19 mpaka isiwe imara ?
 
Utajengaje watu bila kuwa na mfumo imara wa kisheria?

Enzi na enzi popote pale hata katika jamii iliyostaarabika, bila kuwa na mfumo imara wa kisheria, haki haziwezi kuzingatiwa.

Ukitegemea kujenga utashi wa watu ili kufuata sheria bila kuwa na mfumo imara, basi watakapo kengeuka na kuvunja sheria hauwezi kuwabana na kuwawajibisha kwa lolote.
 
Mahakama ni chombo cha kusimamia haki, ukiona uko kwenye nchi ambayo hauwezi kupata haki yako mahakamani basi, huo mfumo umekuwa compromised
Swala lganu sijajibiwaaa..

Nauliza hivii..

Mahakama ina jukumu gani kwa wabunge hawa 19 wa chadema ambao wao bungeni ?

Na spika ana jukumu gani kwa hawa wabunge 19 waliopo bungeni ?

?
 
Nataka nikuize swala moja mkuu.

Kwa mujibu wa sheria wale wabunge 19 wa chadema wanatakiwa kuwepo bungeni ...??
 
Inapendeza zaidi kuwa na mtu mzuri na mwadilifu ndani ya mfumo mzuri. Tusiongozwe tu na uungwana wa mtu, bali uungwana huo uwekwe kwenye mfumo - katiba!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Na huwezi kuwa na mfumo mzuri ambao unafuatwa na watu wasiokuwa waungwana.

Mfano mzuri tuna sheria nzuri tu hapa nchini ambazo zipo.

Lakini hazifuatwi kabisa na zinakeukwa.

Unadhani wanaokeuka ni kwa sababu sheria hizo ni mbaya au ni kwa sababu ya kukosa kwao uungwana na kiburi cha kwamba hakuna anayeweza kunifanya chochote ?
 
Hawatakiwi kuwepo.
Kila mmoja anasema shwria haijafuatwa na ni sheria ambayo ingefuatwa wale pengine wasingekuwa bungeni.

Sasa hii ndo mantiki yangu kwamba wale wabunge 19 wapo pale bungeni sio kwa sababu sheria ni dhaifu.

Sheria ni imara lakini kuna watu ambao pengine wanakosa uungwana wa kufuata shwria hizo eidha kwa kujiona hawawezi kufanywa lolote na yeyote kwa nguvu waliyokuwa nayo.

Na hapa ndo tunarudi pale kwamba uadilifu wa mtu ndo utamfanya afuate sheria na siio sheria kali.

Sasa hapa solution ni hawa watu wawe na moyo wa kufuata sheria sio mutunge masheria kibaaaoo ambayo hayafuatwi.

Ihakikishwe kwamba hizi sheria zilizopo zinafuatwa kwa ukamilifu.
 
Ngoja wapiga dili waje aka wapenda kitonga, walalamishi wakiongozwa na jamaa mwenye ka passo chekundu BAK
😎😎😎
Haaahaa, umenikumbusha mdogo angu alipenda kum describe kaka etu mkubwa....akimwita Kwa kumtukuza "KAKA MWENYE PASSO MJINI"
 
When people waste their time&energy to try to change impossible things.Just live calm life,find your daily bread,do physical exercise.Don't torture your minds in some things.
 
Ni rahisi kuweka sheria za kudhibiti makosa, kuliko kusubiri kwanza tupate watu wasiofanya makosa au walio waadilifu.

Mfumo mzuri unaweza ukaupata kwa muda mfupi na ukaanza kuutumia kudhibiti watu waovu, lakini kupata watu waadilifu hakuna ukomo!

Aidha, tukisema tusiwafunge watu wezi mpaka tutakapopata watu waadilifu itatuchukua vizazi vyote na tusiwapate. Twende na vyote: tujenge mifumo mizuri na bora huku tukisisitiza uungwana na uadilifu.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Ni rahisi kuweka sheria za kudhibiti makosa, kuliko kusubiri kwanza tupate watu wasiofanya makosa au walio waadilifu.
Kuweka sheria za kudhibiti makosa ni jambo moja na pia kudhibiti makosa hayo ni jambo jingine.

Lakini pia naomba utambue kwamba katika mada yangu nimegusia ujumla wa sheria na sio kipengele cha SHERIA ZA KUDHIBITI MAKOSA TU.

Kwa sababu katika sheria ambazo viongozi watafuata sio zile tu za kudhibiti makosa bali kuna sheria watazifuata kama muongozo juu ya nini wafanye katika majukumu yao.

Mfano kama kiongozi sheria inamtaka aweke serikali ya umoja wa kitaifa tuone kweli vigezo vikikidhi anaweka serikali ya umoja wa kitaifa.

Hiyo maana yake ni kuwa anafuata sheria katika jambo ambalo kulitekeleza kwake sio kwa ajili ya kudhibiti kosa fulani bali kutokutekeleza sheria hiyo ndo inakuwa kosa lenyewe.

Tofauti na sheria kwamba mwizi afungwe manake ukitekeleza unatekeleza jukumu la kudhibiti kosa na usipotekeleza ni kosa jingine la pili.

Kwa hiyo katika point hii nasema kuwa lengo sio kudhibiti makosa tu bali lengo kupata watu watakaofuata utaratibu hata katika kanuni ambazo kuzitekeleza kwake hakuwi katika kudhibiti makosa.
Mfumo mzuri unaweza ukaupata kwa muda mfupi na ukaanza kuutumia kudhibiti watu waovu, lakini kupata watu waadilifu hakuna ukomo!
Kama ambavyo huu tulionao tumeupata kwa muda mfupi lakini sio umeona leo unapigiwa kelele ubadilishwe mzee ?

Hata huo ambao mnautaka uje kwa muda mfupi baadae pia watu wataupigia kelele kwa sababu utaratibu wake sio wa kudumu katika kuutekeleza kama unavyosema ni rahisi kuupama.

"Ease come ease go"


Aidha, tukisema tusiwafunge watu wezi mpaka tutakapopata watu waadilifu itatuchukua vizazi vyote na tusiwapate.
Hoja yangu sio kwa wale ambao wanatakiwa kuongozwa na sheria.

Hoja yangu ni wale ambao wasimamizi au viongozi waliowekwa na sheria hizo ili kuwaongoza wengine.

Hoja hapa ni viongozi wa ngazi mbali mbali za serikali akianziwa na raisi mwenyewe hawa ndio ambao nimewakusudia mimi.

Hawa lazima iwe walikuwa well trained katika uadilifu na ustaarabu ili wakiwekwa hapo kuwasimamia wengine wawe wanatenda uadilifu.

Twende na vyote: tujenge mifumo mizuri na bora huku tukisisitiza uungwana na uadilifu.
Tusitegemee kupata watu waadilifu kama msisitizo wa kusisitiza watu wawe waadilifu ni ule ule.

Yani tusitake matokeo mapya kama bado tunatumia njia za zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…