Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Habarini wadau na wazazi wote katika jukwaa hili...
Ukizungumza na watoto wadogo waliopo madarasa ya awali, utakutana na wengi wao wakiwa na hulka au ushawishi wa kujua mambo mengi ya kisayansi na mazingira.
Na wanauliza maswali muhimu, wanauliza " ndoto ni nini, kwanini tunalala usingizi, kwanini mwezi unawaka taa, Mungu anaishi wapi, kwanini majani yana rangi ya kijani" Haya ni maswali yanayo sisimua ambayo wanauliza kila mara.
Ukienda kuzungumza na watoto waliofika madarasa ya juu, mfano la sita au saba, hutaona wala kusikia maswali ya aina hiyo, wamekuwa hawana uwezo wa kuhoji zaidi ya kutii kile wanacho ambiwa.
Nini kimetokea katika kipindi hicho kati ya darasa la awali mpaka kufikia madarasa ya juu? Kwanini hawawezi tena kuuliza na kuhoji mambo ya msingi?
Jibu ni kwamba tayari wamepitia Brainwashing au indoctrination kwa kufundishwa mambo na kulazimishwa kuyaamini pasipokuwa na uwezo au ruhusa ya kuhoji.
Wote tunafahamu mifumo ya elimu zetu haimuandai mtoto kuwa na uwezo wa kuuliza na kuhoji, kabla mtoto hajaanza elimu anakuwa na uwezo wa kuuliza kwa uhuru, lakini baada ya kupata elimu anakuwa hawezi tena kuhoji zaidi ya kutii na kuamini kile anacho fundishwa. Haijalishi anafundishwa yaliyo ya kweli au uwongo, hana ruhusa ya kuhoji au kupinga chochote.
Elimu inayotolewa hapa duniani lengo lake sio kuongeza uwezo wa akili za watoto wetu bali ni kupunguza uwezo wao na kuwafanya wawe kama maroboti, wasiweze kuwaza au kufikiri kwa akili zao za asili.
Lengo ni kupunguza au kudhoofisha akili ya mwanadamu ( mtoto), kumfanya awe na majibu ambayo ameaminishwa ni ya ukweli, kutii na kuamini mambo pasipo kutafakari na kupata maana asilia.
ANGALIZO: Ni muhimu kufahamu kwamba akili ya mwanadamu ndyo silaha kuu aliyopewa na Mungu, kuidhohofisha na kuidumaza ni lengo kuu la shetani, na mifumo yote ya Elimu ipo chini ya tawala za dunia, tawala za shetani.