Mifumo ya Elimu inavyo wafanya watoto kupoteza uwezo wa kuuliza na kuhoji

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Habarini wadau na wazazi wote katika jukwaa hili...

Ukizungumza na watoto wadogo waliopo madarasa ya awali, utakutana na wengi wao wakiwa na hulka au ushawishi wa kujua mambo mengi ya kisayansi na mazingira.

Na wanauliza maswali muhimu, wanauliza " ndoto ni nini, kwanini tunalala usingizi, kwanini mwezi unawaka taa, Mungu anaishi wapi, kwanini majani yana rangi ya kijani" Haya ni maswali yanayo sisimua ambayo wanauliza kila mara.

Ukienda kuzungumza na watoto waliofika madarasa ya juu, mfano la sita au saba, hutaona wala kusikia maswali ya aina hiyo, wamekuwa hawana uwezo wa kuhoji zaidi ya kutii kile wanacho ambiwa.

Nini kimetokea katika kipindi hicho kati ya darasa la awali mpaka kufikia madarasa ya juu? Kwanini hawawezi tena kuuliza na kuhoji mambo ya msingi?

Jibu ni kwamba tayari wamepitia Brainwashing au indoctrination kwa kufundishwa mambo na kulazimishwa kuyaamini pasipokuwa na uwezo au ruhusa ya kuhoji.

Wote tunafahamu mifumo ya elimu zetu haimuandai mtoto kuwa na uwezo wa kuuliza na kuhoji, kabla mtoto hajaanza elimu anakuwa na uwezo wa kuuliza kwa uhuru, lakini baada ya kupata elimu anakuwa hawezi tena kuhoji zaidi ya kutii na kuamini kile anacho fundishwa. Haijalishi anafundishwa yaliyo ya kweli au uwongo, hana ruhusa ya kuhoji au kupinga chochote.

Elimu inayotolewa hapa duniani lengo lake sio kuongeza uwezo wa akili za watoto wetu bali ni kupunguza uwezo wao na kuwafanya wawe kama maroboti, wasiweze kuwaza au kufikiri kwa akili zao za asili.

Lengo ni kupunguza au kudhoofisha akili ya mwanadamu ( mtoto), kumfanya awe na majibu ambayo ameaminishwa ni ya ukweli, kutii na kuamini mambo pasipo kutafakari na kupata maana asilia.

ANGALIZO: Ni muhimu kufahamu kwamba akili ya mwanadamu ndyo silaha kuu aliyopewa na Mungu, kuidhohofisha na kuidumaza ni lengo kuu la shetani, na mifumo yote ya Elimu ipo chini ya tawala za dunia, tawala za shetani.
 
Ukizungumza na watoto wadogo waliopo madarasa ya awali, utakutana na wengi wao wakiwa na hulka au ushawishi wa kujua mambo mengi ya kisayansi na mazingira...
Hamna watu wanao haribu reasoning ya watoto kama sunday school za RC, majibu wanao toa wana indoctorinate watoto vibaya majibu hayana hata logic ni dogma tupu.....
 
Hamna watu wanao haribu reasoning ya watoto kama sunday school za RC, majibu wanai indoctorinate watoto hayana hata logic ni dogma......
Ndyomaana watu wanajiuliza kwanini wasomi wengi hawawezi kuigeuza elimu yao na kupata manufaa, jibu ni kwamba akili zao haziwezi tena kubuni na kudadisi.
 
Nimekumbuka mdogo wetu wa mwsho alivyokuwa akimuuliza dada ake kila kitu anachokiona hasa wakiwa wametoka out,hadi dada mtu akawa anamind akawa anamrusha dogo kwa ukali hadi dogo ikabid awe kimya tu
 
Hasa wasomi wa Tanzania ni bure kabisa hawana "critical thinking" katika siasa majibu ni obvious kwenye uchumi hamna jipya zaidi yale walio kalilishwa kwenye jamii ndo wameganda kibisa hamna creayivity na initiatives mpya, elimu yetu ni ya hovyo kabisa......
 
Huyo dogo naamini kwa sasa hana tena uwezo wa kuuliza maswali kama hayo, tayari amepewa majibu shuleni na amejengewa mtazamo mpya.
 
Hasa wasomi wa Tanzania ni bure kabisa hawana "critical thinking" katika siasa majibu ni obvious kwenye uchumi hamna jipya zaidi yale walio kalilishwa kwenye jamii ndo wameganda kibisa hamna creayivity na initiatives mpya, elimu yetu ni ya hovyo kabisa......
Kwa maana hiyo wasomi wa sasa ndyo wanapaswa kuelimishwa upya ili kuendana na uhalisia wa mazingira ya sasa.
 
Mfumo wa elimu ni mbovu, kabisa ndo shida kubwa hausaidii wstoto kua na independent thinking capacity, nikupe mfano wanafudisha darasa la nne vitendawali, na majibu yake ni yale yale hata ukileta tafauti na hile umekosa kwa mfano "nina nyumba yangu haina mlago" jibu ni yai.... wakati hata begu ya parachichi haina mlago pia.
 
Elimu inaanzia kwenye familia yako ndgu.
Mtoto anakua na uoga wa kuhoji tangu nyumbani anakotoka.

Mengine anadangamywa, mengine ataambiwa hana nidhamu, mengine ataambiwa ni mwiko, mengine ataambiwa anakufuru, wengine wataenda mbali zaidi na kumwambia akawaulize walimu wake yeye analipa ada ili walimu wamfundishe sio kujibujibu maswali ya kijinga.

Mtoto akipewa homework ambayo anatakiwa kipata uangalizi au msaada wa mzazi, mzazi atamwambia nishalipa ada nimemaliza.

Baba/mama mkali kama pilipili mbuzi, nani amuulize haogopi kupigwa.
 
Elimu inaanzia kwenye familia yako ndgu.
Mtoto anakua na uoga wa kuhoji tangu nyumbani anakotoka...
Mada inahusu kupotea kwa uwezo wa watoto kuhoji na kuuliza maswali, wazazi wana jukumu la kusimamia mienendo ya watoto na jukumu la kuwafundisha wamewaachia walimu mashuleni.

Jiulize, leo hii wazazi wanatumia muda kiasi gani na watoto wao zaidi ya weekend tu. Watoto wanaondoka asubuhi na kurudi usiku, nafasi kubwa ya muda wanaitumia shuleni, na huko ndipo wanapojazwa mambo mengi kichwani bila kupewa nafasi ya kuhoji.
 
Mfumo wa elimu ni mbovu, kabisa ndo shida kubwa hausaidii wstoto kua na independent thinking capacity, nikupe mfano wanafudisha darasa la nne vitendawali, na majibu yake ni yale yale hata ukileta tafauti na hile umekosa kwa mfano "nina nyumba yangu haina mlago" jibu ni yai.... wakati hata begu ya parachichi haina mlago pia.
Nimekuelewa vyema mkuu, mambo ya shuleni ni yale yale miaka yote, dunia inabadilika na kuwa na kasi kubwa, lakini shuleni bado watoto wanafundishwa vitendawili na hadithi za sungura na fisi.
 
Wakati kwa sasa ni generation ya digital waves technology, sisi tunakomaa na hadith za kijinga etu usipo ziba ufaa........wakati kuna nyumba za mbao na asbestos ubora wao ni kuweka nyufa kwenye joints.......mtoto wa kitanzania unampotasha angali mdogo.
 
Unadhani nini kifanyike ili kukuza uwezo wa watoto kuhoji na kudadisi?
 
Habarini wadau na wazazi wote katika jukwaa hili...

Ukizungumza na watoto wadogo waliopo madarasa ya awali, utakutana na wengi wao wakiwa na hulka au ushawishi wa kujua mambo mengi ya kisayansi na mazingira.

Na wanauliza maswali muhimu, wanauliza " ndoto ni nini, kwanini tunalala usingizi, kwanini mwezi unawaka taa, Mungu anaishi wapi, kwanini majani yana rangi ya kijani" Haya ni maswali yanayo sisimua ambayo wanauliza kila mara.

Ukienda kuzungumza na watoto waliofika madarasa ya juu, mfano la sita au saba, hutaona wala kusikia maswali ya aina hiyo, wamekuwa hawana uwezo wa kuhoji zaidi ya kutii kile wanacho ambiwa.

Nini kimetokea katika kipindi hicho kati ya darasa la awali mpaka kufikia madarasa ya juu? Kwanini hawawezi tena kuuliza na kuhoji mambo ya msingi?

Jibu ni kwamba tayari wamepitia Brainwashing au indoctrination kwa kufundishwa mambo na kulazimishwa kuyaamini pasipokuwa na uwezo au ruhusa ya kuhoji.

Wote tunafahamu mifumo ya elimu zetu haimuandai mtoto kuwa na uwezo wa kuuliza na kuhoji, kabla mtoto hajaanza elimu anakuwa na uwezo wa kuuliza kwa uhuru, lakini baada ya kupata elimu anakuwa hawezi tena kuhoji zaidi ya kutii na kuamini kile anacho fundishwa. Haijalishi anafundishwa yaliyo ya kweli au uwongo, hana ruhusa ya kuhoji au kupinga chochote.

Elimu inayotolewa hapa duniani lengo lake sio kuongeza uwezo wa akili za watoto wetu bali ni kupunguza uwezo wao na kuwafanya wawe kama maroboti, wasiweze kuwaza au kufikiri kwa akili zao za asili.

Lengo ni kupunguza au kudhoofisha akili ya mwanadamu ( mtoto), kumfanya awe na majibu ambayo ameaminishwa ni ya ukweli, kutii na kuamini mambo pasipo kutafakari na kupata maana asilia.

ANGALIZO: Ni muhimu kufahamu kwamba akili ya mwanadamu ndyo silaha kuu aliyopewa na Mungu, kuidhohofisha na kuidumaza ni lengo kuu la shetani, na mifumo yote ya Elimu ipo chini ya tawala za dunia, tawala za shetani.
Mifumo uchwara hii tumebeba mizigo mikubwa mpk akili Zina float🤣🤣
 
Tati

tatizo fimbo...
 
Mada inahusu kupotea kwa uwezo wa watoto kuhoji na kuuliza maswali, wazazi wana jukumu la kusimamia mienendo ya watoto na jukumu la kuwafundisha wamewaachia walimu mashuleni.

Jiulize, leo hii wazazi wanatumia muda kiasi gani na watoto wao zaidi ya weekend tu. Watoto wanaondoka asubuhi na kurudi usiku, nafasi kubwa ya muda wanaitumia shuleni, na huko ndipo wanapojazwa mambo mengi kichwani bila kupewa nafasi ya kuhoji.
Bado mzazi una nafasi yako aisee, shule haijamzaa mwanao..

Huwezi kuwachia walimu wakulelee mwanao..
Kwani huko uliposoma hujawahi kukutana na kina "Joni kisomo" wanaopenda kuwachallenge walimu?? Wanaopenda kukibu maswali hata kama hajui na hana idea nacho yeye atanyoosha mkono kujibu.
Na vipi wale wakula ngumu hata kama swali analijua ila anaogopa kujibu?

My concern ni kuwajengea uwezo wa kuhoji watoto ingali bado wadogo, wakuhoji wewe na yeyote wanayehitaji ingali bado wadogo.
Shida ni kua wazazi hatupendi maswali ya watoto na hapo ndipo tunapowajengea uoga wa kuuliza anapopata utata.
 
Mfumo wa elimu ni mbovu, kabisa ndo shida kubwa hausaidii wstoto kua na independent thinking capacity, nikupe mfano wanafudisha darasa la nne vitendawali, na majibu yake ni yale yale hata ukileta tafauti na hile umekosa kwa mfano "nina nyumba yangu haina mlago" jibu ni yai.... wakati hata begu ya parachichi haina mlago pia.
😅😂😅😂Mkuu Covax umeua.
 
Back
Top Bottom